Mmejitahidi sana sana kumtetea BABU (Dr. Slaa), lakini...

Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
Wakuu,
Nazitambua juhudi za wafuasi wa babu na mashabiki wake katika kujaribu kumtetea ionekane ni jambo la kawaida sana kwa Dr. W. Slaa kuwa na kadi ya CCM mpaka leo! Juhudi za kutumia social media na magazeti mengine hasa gazeti la M4C(TanzaniaDaima) kujaribu kumtetea Slaa na wakati huo kunikejeli na kunitukana japo kuwa kwa matusi ambayo lazima nikiri si mapya, yalishawahi kutumiwa dhidi yangu au watu wengine duniani. Hapa nitajibu hoja moja baada ya nyingine( wenye matusi mapya wanakaribishwa wakijisikia kunitukana tena).

1. Katika matamshi yangu hakuna mahali nilipohusisha kuwa na kadi na uanachama wa mtu.....hivyo wanaojaribu kubwabwaja kuwa sijui Katiba ya CCM wanakurupuka kwasababu ndogo sana..kukairishwa lazima kumtukana Nape hata bila kupima kwa makini hoja....nilichosema Dr. Slaa na baadhi ya vigogo wa CDM wana kadi za CCM na baadhi yao wanazilipia mpaka leo. Sijazungumzia uanachama wao...najua kuwa kwa katiba ya CCM ukisha kuwa mwanachama wa chama kingine uanachama wako CCM unakufa hapohapo.

2.Ni kweli kuwa hakuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya kuwa na kadi ya CCM kwa babu na maendeleo ya wananchi masikini, lakini babu anatafuta kuwa kiongozi wa nchi ANAPASWA KUISHI YALE ANAYOYASEMA NA KUWA MWAMINIFU KWA NAFSI YAKE MWENYEWE. Ni Dr. huyu ambaye huhamasisha wananchi wengine warudishe kadi za CCM anapofanya mikutano ya hadhara wakati yeye kabaki nayo bila kuanza yeye kuongoza kwa kuonyesha njia kwa kuirudisha yake kwanza...USIPOKUWA MWAMINIFU KWA KIDOGO HUWEZI KUWA MWAMINIFU KWA KIKUBWA PIA....si ajabu alishindwa kutii kiapo chako na nadhiri yake kwa Mungu aliyoapa akiwa padri..leo nitashangaa akiwa mwaminifu kwa binadamu mwenzake kama kashindwa kumweshimu Mungu.

3.Lakini ni siku chache sana zimepita babu aliwatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema Kigamboni kuwa ni mapandikizi ya CCM kwa chama chake...nikashangaa sana, babu anawatuhumu wenzake ambao hawana hata kadi za CCM kama yeye kuwa ni mapandikizi ya CCM huku yeye ambaye kwa tafsiri hii ni pandikizi namba moja akijifanya ni msafi sana..nilichofanya ni kumkumbusha kuwa yeye ndio "pandikizi" namba moja kwahiyo aanze kujifukuza yeye.

Endeleeni kumtetea nianike mtiririko wa kulipia kwake kadi yake ya CCM.

attachment.php
 

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,974
3,104
Nafahamu unatumia neno BABU kuonyesha dharau zako kwa Dr. lakini twende kwa mifano kama ni umri.

1. Hivi wasira kachoka vile naye mmempa uwaziri je ni kijana si ni nyanya yule.
2. Samweli Sitta je?
3. hao akina Mangula AKA Chichi Dodo ni vijana?
4. Kumbuka kingunge katoka lini kwenye uwaziri (mshauri wa mambo ya siasa ikulu) na ndani ya ccm je nikijana?
hao ni wachache tu, kiufupi kama ni vibabu CCM ni vingi mno wengine walishaacha kula nyama siku nyingi, kimsingi uwe na heshima Dr. kiumri hata kisiasa yupo mbali mno kwako, jeuri ya dola na ccm yako inakupa nguvu lakini hunalolote.

Binafsi ungeyaondoa magamba mliyoyapa siku 90 ningekuona wa maana lakin hamjamaliza hilo mnarukia mengine halafu tabia ya kuleta eti watumishi wa serikali wajewatoe maelezo kwenu mkome kabisa hawajaajiliwa na CCM elewa hapo, nyie ikabeni serikali inayoongozwa na chama chemu (mawaziri, wabunge na Madiwani ) wasimamie vizuri mipango ya maaendelao basi, waje kutoa maelezo kwako au kwa chama kwa mlango upi wa katiba punguani kabisa yie na kiama 2015 we ngoja tu.
 

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,852
9,391
Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba chadema mmepigwa na dhoruba kali ambalo mtahangaika nalo kwa muda sana na kupoteza muda mwingi wa kutumikia wananchi na pia kujenga imani ya Chama chenu na viongozi wenu mbele ya Umma; Lakini yote ni sehemu ya siasa za ushindani katika demokrasia ya uliberali, kote, marekani n.k; Personal attacks ni sehemu ya mchezo wa kisiasa, ndio maana unaitwa mchezo mchafu, kwahiyo msilaumu CCM kwa hilo, kwani hata Chadema ni mabingwa wa personal attacks, kama sehemu ya mchezo huu mchafu;

Bila uangalifu, jambo hili litaipelekesha Chadema kwa muda mrefu sana, miezi sita, mwaka, huku Dr. Slaa akijikuta akitumia muda mwingi kujibu hoja hii badala ya kujadili masuala muhimu huko majukwaani; Ukichanganya na tetesi kwamba pia anataka kumsimamisha Josephine Jimbo La Kawe kwa nguvu, licha ya uwepo wa Mbunge mahiri Halima Mdee pale, there is a big chance kwamba Dr. Slaa's popularity itaporomoka kwa kasi ya ajabu, na pengine jina lake kuwa irrelevant katika political landscape of the country ifikapo 2015;

Vinginevyo yote ni katika kutumikia wananchi, Vyama ni njia tu; Hata Wassira, ambae ni moja ya nguzo kuu ya chama chetu cha mapinduzi leo, huko nyuma alihama chama na kuwa Mbunge wa Bunda kupitia NCCR mageuzi, akikishambulia Chama Chetu kwa hoja nzito majukwaani, leo hii wajumbe wa Mkutano mkuu wetu wa taifa (CCM), wanampa Wassira kura nyingi kuliko hata majina yanayotajwa kuwa na uwezo wa kubeba tiketi ya chama chetu ngazi ya Urais 2015; Sisi sote ni watanzania, vyama huja baadae;

Wanachadema, hizi ndio siasa za zama za leo, jipangeni;
 

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,872
4,536
Mwanangu Nnauye Jr if you really are the same CCM's mad dog, shame on you. Wewe una kadi ya CCJ. Ila hukujua kuwa tunakujua kuwa wewe ni CCJ. Ungejinyamazia huyu babu humuwezi wala siyo saizi yako. Baba yako Njaa Kaya anamgwaya kuliko hata miwaya utamuweza wewe? Ziko wapi tambo zako kuwa mtawavua akina Lowassa gamba? Si mmeishia kuyavaa magamba tena mazito. We kaa ule bure na upige mdomo lakini babu siyo saizi yako. Tumemshauri asibweke atakapobwekewa nawe. Tia akilini basi mwanangu bado u mchanga. Ningekuwa wewe ningetafuta mke nikaoa ili nijifunze kuongoza kabla ya kudandia milima tena ya volcano.
 

SHEMGUNGA

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
666
147
Kaka, hunaa jipyaa watu wanataka hojaaa na ufumbuzii kuhusu ajira kwa watoto wa mkulima hasa wale wanomaliza vyuo vikuuu sasa wewe kama umepata hako kanafasii katumiee vizurii mshukuruu mzeee wako kwa kujitumaa dats why unalipwa fadhilaa umeshindwa kumtoa fisadi mkubwa ndugu EL leoo unatakaa kubishanaa na dr wa ukweliiii tafadhalii tunahitji maendeleoo sio manenooo tumechokaaa na bwabwanyaaa zako
 

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,667
Wakuu,
Nazitambua juhudi za wafuasi wa babu na mashabiki wake katika kujaribu kumtetea ionekane ni jambo la kawaida sana kwa Dr. W. Slaa kuwa na kadi ya CCM mpaka leo! Juhudi za kutumia social media na magazeti mengine hasa gazeti la M4C(TanzaniaDaima) kujaribu kumtetea Slaa na wakati huo kunikejeli na kunitukana japo kuwa kwa matusi ambayo lazima nikiri si mapya, yalishawahi kutumiwa dhidi yangu au watu wengine duniani. Hapa nitajibu hoja moja baada ya nyingine( wenye matusi mapya wanakaribishwa wakijisikia kunitukana tena).

Nape na declare Interest kuwa mimi ni MTAIFA siko hapa kuchangia thread yako kwa mapenzi ya kichama bali nachangia upande wa ujenzi kwangu CCM,CUF ama CDM wote wana tiketi moja katika mwelekeo wa kuwa sote tuko kwa ajili ya TAIFA letu.Niliko bold kwa rangi nyekundu ndizo sahemu nitakazo zingatia kwa mujibu wa thread yako ni kejeli na matusi !!!!

Neno Kejeli
Nikianza na neno kejeli hili si neno zuri lakini kwa nyie wanasiasa wa pande zote mbili walioko madarakani na wasioko madarakani mmelihalalisha kwa ujumla wenu kiasi kuwa, kuna wanasiasa pande zote wamekuwa wakitumia maneno ambayo ni dhahiri shaili kuwa uwa ni kejeli dhidi ya wengine.Kiasi kuwa umma nao umegeuza baadhi ya maneno kutoka kutumia nick name ambazo si kosa mpaka matumizi ya maneno ya kejeli kama tabia.Nikitizama jinsi ulivyojieleza hapa,binafsi naona neno kejeli na matusi umelitumia katika kusisitiza kuonyesha upendezwi lakini kwa kuwa ndiko tulipofika unaona ni sawa.Lakini hapo hapo unakemea kejeli lakin nawe WEWE pia umetumia Kejeli kumuita DK SLAA babu.

Vipi imekaaje hiyo ukizingatia kuwa DK SLAA ni hadhi ya marehem baba yako, na kiafrika mtu yoyote anae kuzidi umri tuna amini anastahiki heshima aijalishi mnatofauti wa kabila au utaifa.Umeonyesha kukelwa na matumizi ya kejeli lakini umeshindwa kukumbuka kuwa wanasiasa mmeshindwa kuweka maadili nyie wenyewe.Nimezingatia kwa ulikuwa na sababu zote za kuanzisha threa hii lakini pasiwepo na matumizi ya neno babu kumaanisha Mzee SLAA pamoja na tofauti zenu za kiasiasa, otherwise nisichokijua wewe na yeye mna utani ulio dhahiri kwa maana wa sura ya kisiasa yeye akikuita mjukuu nawe ukimuita babu.I hope utalitoloe ufafanuzi.Kwa kuwa wewe ni kioo na una wafuasi, na yeye unae muita babu ni kioo na anawafuasi wengi sana.

Neno Matusi
Binafsi sipendezwi na hili jambao lakini nyie wote kama kama wanasiasa mmegeuza kuwa ni maisha na kwamba kila kitu kiko sawa.Ebu angalieni nape mimi na wewe leo vijana nyie mkiendekeza matusi katika majukwaa tukijaliwa umri mlefu itakapofika miaka 75 pata picha aina ya lugha itakayokuwa imehalalishwa kutumiwa na wanasiasa kwenye majukwaa na hata kwenye forum kama hizi.

Kupitia cheo chako ebu anza kupaza sauti si lazima kutumia matusi ili jamii ikuelewe kuwa unacho kizungumza kuhusu CDM au CUF kina maanisha hivi kisipokwenda na tusi.Na hata kama CDM au CUD au mwingineyo anapotumia matusi basi nao CCM watumie matusi kujibu mapigo je,tofauti tutaiona wapi!!!Ebu CCM jipangeni manake matusi nayo yamegeuka sera, pambana na unazi,ondoeni mbumbu katika shughuri za kujenga chama chenu kwa kuwa CCM sio CDM na CDM sio CUF wala CCM,lazima tuone tofauti.

1. Katika matamshi yangu hakuna mahali nilipohusisha kuwa na kadi na uanachama wa mtu.....hivyo wanaojaribu kubwabwaja kuwa sijui Katiba ya CCM wanakurupuka kwasababu ndogo sana..kukairishwa lazima kumtukana Nape hata bila kupima kwa makini hoja....nilichosema Dr. Slaa na baadhi ya vigogo wa CDM wana kadi za CCM na baadhi yao wanazilipia mpaka leo. Sijazungumzia uanachama wao...najua kuwa kwa katiba ya CCM ukisha kuwa mwanachama wa chama kingine uanachama wako CCM unakufa hapohapo.

Hapa tena natumaini DK Slaa atakuja na majibu kwa kuwa najua ni mtu makini!!!Kuna mdau kasema hii ni sawa na kwenda na funguo za ziada za nyumba uliyokuwa umepanga baada ya kuama.Hakika ili neno ukiondoka na funguo za mwenye nyumba kwa bahati mbaya ukajisahau, kisha ikatokea mpangaji mpya akaibiwa katika mazingira ya kutatanisha basi si ajabu ukashangaa mapolisi na hodi nyumbani kwako,baada ya source zao akiwemo mwenye nyumba kuwaambia kuna funguo za ziada aliondoka nazo mpangaji aliyekuwa anaishi chumba husika kabla hajaingia mpangaji mgeni alieibiwa.

DK SlAA anapaswa kuludisha funguo hizo kama kweli zipo na kama ni Political strategy manipulation awaambie wafuasi wake kwa kuweka wazi,kwa kuwa hata Obama aliaambiwa sio rais wa USA,kwa gadhabu akawaletee vyeti vya kuzaliwa.Ebu fikilia wewe ushakuwa RAIS wa TAIFA lakini kuna wajomba wanaibuka wanasema wewe sio raia wa TAIFA husika.Hayo yote uwa ni vimbwanga katika kuchemshana na ukikosea kweli unakwenda.Kwa hili hapa Nape umempa muda najua nae atakujibu kuondoa sintofahamu.


2.
Ni kweli kuwa hakuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya kuwa na kadi ya CCM kwa babu na maendeleo ya wananchi masikini, lakini babu anatafuta kuwa kiongozi wa nchi ANAPASWA KUISHI YALE ANAYOYASEMA NA KUWA MWAMINIFU KWA NAFSI YAKE MWENYEWE. Ni Dr. huyu ambaye huhamasisha wananchi wengine warudishe kadi za CCM anapofanya mikutano ya hadhara wakati yeye kabaki nayo bila kuanza yeye kuongoza kwa kuonyesha njia kwa kuirudisha yake kwanza...USIPOKUWA MWAMINIFU KWA KIDOGO HUWEZI KUWA MWAMINIFU KWA KIKUBWA PIA....si ajabu alishindwa kutii kiapo chako na nadhiri yake kwa Mungu aliyoapa akiwa padri..leo nitashangaa akiwa mwaminifu kwa binadamu mwenzake kama kashindwa kumweshimu Mungu.

Ili nalo umeendekeza kejeli usiyoipenda mwenyewe,kwa kiapo cha nadhiri hapa kidogo unaitaji kujua kanisa kiimani kuna viapo vya aina nyingi,kuna ubatizo, ndoa, upadrisho na vingine muhimu katika ngazi tofauti tofauti,na kuna nadhiri ya maisha.Binafsi uwa sipendi kucheza na swala la imani.I hope utaomba msamaha kwa ili na utampa nafasi ya wewe kusimama kwenye hoja ya msingi kuwa uko kwenye utetezi wako wa yeye kumilki kadi ya CCM.

3.Lakini ni siku chache sana zimepita babu aliwatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema Kigamboni kuwa ni mapandikizi ya CCM kwa chama chake...nikashangaa sana, babu anawatuhumu wenzake ambao hawana hata kadi za CCM kama yeye kuwa ni mapandikizi ya CCM huku yeye ambaye kwa tafsiri hii ni pandikizi namba moja akijifanya ni msafi sana..nilichofanya ni kumkumbusha kuwa yeye ndio "pandikizi" namba moja kwahiyo aanze kujifukuza yeye.

Nakubaliana na wewe kama hiki ndicho chanzo cha wewe kuibua swala lako!!!Lakini kifuatacho hapo chini ndio kwenye bomu lenyewe!!!


Endeleeni kumtetea nianike mtiririko wa kulipia kwake kadi yake ya CCM.

Kwa hili hapa ndipo mchezo ulipo lala,kwa hili nape kama DK hatofikisha utetezi wake makini na binafsi naamini Mzee yule ni makini atakuja na ushahidi makini na ufafanuzi makini,kujibu hoja yako,nawe pia ujiandae kututhibitishia uyasemayo [Wenzetu wanasema walk to your talk]. Tufike sehemu Nape tubadilike kama TAIFA visiwe vitu vya kuzusha bila strategy ,vitu vya namna hiyo uzaa matatizo yasiyo ya msingi kwa jamii.

Na kama nyie baada ya kuchokwozwa nae na swala la mapandizi,iwe kweli mmejipanga kujibu mapigo kwa njia zinazokubalika kisiasa ulimwenguni,yani kutoka na angle ambayo inaonekana ni weekness yenye dalili za ukweli kwa kosa la gharama ya muhusika.Ndio maana waliotaka kutoka na boss wa CIA waliingia na angle ya Email elfu 30,000 kwa kuonekana zinamlenga mwanamke,ingawa si kosa lakini dhamira inaleta hoja je ni za kikazi au za mapenzi.Kama ni za mapenzi unapima uzito kama ni za kazi utapima uzito na kuleta utetezi.

Tunasubilia jibu la DK na baada ya hapo tutapa feedback ya ushahidi toka kwako.Hizi ndizo siasa HASA!!!lakini napenda ziwe na STRATEGY zisizo mpa hofu wala mashaka mwanachi wa kawaida, bali mwananchi huyo amini kwa kupima kila upande ya wote mtuhumiwa na mtoa tuhuma!!!!!


Na hakika game ndio linaanza mpka 2015 mengi yatakuja
 

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,225
869
Mi nadhani hakuna haja kusubiri waendelee kumtetea ndiyo uanike mtiririko huo, hebu mwaga tu mara moja hapa itawafanya hao unaowaita kwamba wanamtetea waache mara moja kumtetea,lakini mimi niseme tu kidogo kwamba sitaki kukubaliana na wewe moja kwa moja ama kupingana na wewe katika hoja hii kuhusiana na kadi ya 'Babu' kama unavyomuita kwa sababu hay mambo ya kisiasa yamejaa usanii usanii fulani hivi,lakini yote ka yote mkuu Nnauye mwaga hayo mdokomenti humu mbona unaogopa?!.
 

majebere

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
4,799
1,595
SHEMGUNGA

Sasa wewe nani alikwambia kazi ya Nape ni kutafutia watu kazi? Halafu unataka akatoe hela za urithi akuletee maendeleo, mbona mnakuwa hamuelewi kazi za watu.
 
Last edited by a moderator:

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,655
944
Nnauye Jr

- Duh! Kamanda inaitwa kujulikana mbichi na mbivu, tena mchana kweupeee! ha! ha1 ha! ha! hapa leo mtoto hatumwi sokoni! neno aibu halitoshi kuelezea duh!!

Es!
 
Last edited by a moderator:

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,655
944
Mbona wewe unajichanganya?
Umeshasema kwa katiba ya CCM,mtu akiwa mwanachama wa chama kingine,uanachama wake wa CCM unakufa mara moja.

Sasa hapa hoja ya Dr Slaa kuwa pandikizi inakujaje?

Kweli mfa maji haishi kutapatapa.

- So brother naomba kukuelewa, unamtetea Slaa kwa kuwa na Kadi ya CCM na kulipia kila mwezi huku akiwa Kiongozi wa Chadema or what?

Es!
 

Prisoner 46664

JF-Expert Member
Dec 18, 2010
1,948
1,234
CCM hizi ngonjera mtaacha lini?..badala ya kuzungumza jinsi huu uongozi wenu mpya(ingawa viongozi ni wa zamani)utakavyojenga mazingira ya watanzania kupata maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii mmekazania hizi propaganda za ngonjera..nadhani umefika wakati muelewe kuwa mtanzania wa sasa ana uelewa na busara tosha ya kutofautisha mambo muhimu na vituko kama hivi vya nani ana kadi ya wapi na kwa nini
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,204
25,655
Dr Slaa rudisha kadi ya CCM yaishe. Ni sawa sawa umeama katika nyumba uliyokuwa umepanga umeondoka na funguo za akiba.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

29 Reactions
Reply
Top Bottom