Dr Slaa atingisha Kigoma Kaskazini

Dr Slaa atingisha Kigoma Kaskazini

Wachawi utawajua tu,wanapenda heshima kwenye mazishi

Next time chagua maneno vizuri unapochangia mijadala kwenye public arena.

Kuna wachawi leo uwanja mzima wa mpira huko SA wameenda kwenye mazishi ya Madiba kutoka kila pembe ya dunia. Huwaoni?
 
Mkuu Molemo tunashukuru kwa taarifa muhimu hii ya kuelekea ukombozi wa fikra!

Big up kwa kamanda Tumaini Makene anayetufanya tuonekane tupo eneo la tukio
 
Last edited by a moderator:
Kuna wachawi leo uwanja mzima wa mpira huko SA wameenda kwenye mazishi ya Madiba kutoka kila pembe ya dunia. Huwaoni?

Poleni kwa kushindwa kusherekea sikukuu ya uhuru. Sherehe ilionekana kama watu waliopo jandoni
 
No photoz/videoz no right for propaganda!
Msafara wa Gwiji wa siasa Tanzania na Katibu mkuu CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa ndo unakatiza hapa Kigoma mjini, ishara ya vidole viwili inatanda kila mahali na maneno ya ''Dkt. Slaa huyo huyo...Chademaaaa....Chademaaaa''.

Msafara unaelekea Jimbo la Kigoma Kaskazini Mkutano wa Kwanza utakuwa Nyarubanga, kisha utaelekea mkutano wa pili.

Updates.....

Ndo twawasili Nyarubanga hapa. Akina mama wamejipanga barabarani pembeni kdg ya uwanja wanaimba kumpokea Katibu Mkuu Dkt. Slaa. Msafara umeshaingia uwanjani.

Red Brigade wako imara kweli kweli leo hapa. Wananchi wanasogea sogea. Naona ngoma hapa inachezwa na akina mama.

Updates No 2:

Dkt. Slaa anaingia kucheza ngoma na wenyeji hapa. Ngoma hii inachezwa na kikundi cha ngoma cha akina mama wa CHADEMA kuhamasisha wananchi kujiunga na CHADEMA hasa akina mama na vijana.

Naambiwa inaitwa Denga. Wananchi wanashangilia kumuona Dokta anaungana na akina mama kucheza Denga!

Updates No 3.....

Mkutano umeshafunguliwa na Mkiti Issa Kibaba. Waitara amemkaribisha Mratibu wa Kanda ambaye amezungumzia namna Kanda inavyojipanga kuhudumia wanachama na wananchi kwa ujumla.

Sasa anapanda Mkiti wa Kanda Shaaban Mambo, anazungumza kidogo kwa sbb ya dalili ya mvua kubwa. Sasa amepanda Dkt. Slaa.

Mvua imekuwa kubwa hapa. Wav wamevumilia kumsikiliza Dkt, ambaye ameamua kubadili kubadili mbinu ya mkutano badala ya kuendelea kuhutubia, anatoa nafasi ya maswali kwa wananchi ili wasiende mbali

Updates No 4.....

Watu 4 hadi sasa wameshauliza maswali na Dkt. Slaa anaendelea kujibu maswali yote 5, 3 yanayuhusu maamuzi ya Kamati Kuu kuwavua madaraka Zitto, Kitila na Mwigamba

Mengine 2 yanayuhusu Chadema na misingi yake. Dkt, anaendelea kufafanua, masuala yote yaliyoulizwa.

Mvua inazidi kuwa kubwa hapa. Dkt. Slaa anawauliza wananchi aendelee au afunge mkutano, wananchi wanasema aendelee. Anaendelea hapa.

Mvua kubwa iliyotanguliwa na ukungu mkubwa sana ktk eneo la mkutano imezidi kuongezeka.

Sehemu ya umati wa wananchi wametafuta miamvuli na kubaki karibu na jukwaa. Wengine wako jukwaa kuu, wengine wamekimbilia upenuni mwa nyumba kuendelea kusikiliza.

Mvua ktk eneo hili la mkutano ni kubwa sana, ingawa mbali kdg tu kutoka hapa hakuna ukungu wala mvua.

Updates No 5....

Kutokana na mvua kuzidi kuwa kubwa Wananchi wamemruhusu Dkt. Slaa ashuke jukwaani baada ya kuhutubia kama dkk 45.

Msafara unalazimika kuondoka kwenda mkutano wa pili.

Kuna utani unazungumzwa na baadhi ya wananchi kwamba ''wameshindwa njia zote sasa wameamua kujaribu hii...''.

Lakini Dkt. Slaa kabla hajaondoka jukwaani, aliwaambia wananchi kuwa mvua ni baraka, hivyo wasilaumu!

Source: Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene
 
Last edited by a moderator:
Hii ni Habari njema sana kwa watatzania wema wanaopenda ukweli na waelewa kwa hila wasiokitakia meme Chadema na wengine wenaopigania haki ya watanzania kwamuda mrefu. nitakumbuka sana msemo huu kuwa walio wema wanaisikia saidi ya CHADEMA kupitia DR Slaa na Wanamfuata kwa nia njema iliyo ndani ya Mioyo yao na kwa furaha wanaimba kudhihirisha furaha yao. Mungu ni mwema na hii ni miujiza anaifanya kuonesha Dunia kuwa japo kuna wasaliti lakini chadema ni imara sana na kitatukuka kwa harakati za wenye nia njema na sio wasaliti wanaopanga mipango ovu gizani kwa manufaa yao binafsi na sio kwa taifa letu. VIVA VIVA DR, VIVA CHADEMA, VIVA MBOWE na TEAM nzima ya USHINDI na ya Mabadiliko chanya kwa CHADEMA. wabakio wanoouza dignity zao kwa vijisent huku wakiwa watumwa wa kufikiri na vipofu wasioona jinsi CCM inavyozidi kuongeza kutu ua umaskini Tanzania. CCM yaani ni majanga majanga matupu. Bila Chadema tutaangamia Tanzania. Mungu Mpe Maisha Marefu DR.

...

....Mungu ni mwema!!
 
Jamani mwenye sifa tumpe sifa yake wakuu, Mimi toka nimefatilia kwa karibu hekima, maarifa na siasa za Dr.Slaa, ninathubutu kusema huyu Mzee ni miongoni mwa Simba(Wakombozi) wa Africa, Dr.Slaa ni mwanasiasa hasa, Ni jemedari na Kamanda mpiganaji aliye jasiri mithili ya Steve Biko na mwenye muono mithili Cout Camilo cavour wa Italy.

Mungu ampe maisha marefu sana Kamanda wetu na hakika Historia itakuandika na kukumbuka kama shujaa wa haki mwenye ujasiri na kweli aliyeshuka zama hizi.

Umenena Mkuu. Tunatakiwa sasa tujipange kikomandoo kwa kila hatua ya mabadiliko chanya na tupeane nyenzo za kutosha kuweza kuangamiza huu ukoo wa panya na baadhi ya mende wa siasa, ili tuwe na taifa la watu wenye akili timamu, wenye hofu ya Mungu, wanaoenzi maisha ya kila Mtanzania katika nyanja za elimu, umiliki wa uchumi wetu, rasilimali, nidhamu, uwazi na uwajibikaji. tupo pamoja wanamageuzi tumeshajiweka tayari,na sasa ni kwamba, 'LET US WALK TOGETHER FOR THE LIBERATION OF ALL TANZANIANS who are in need of improved livelihoosS.
 
Huyu molemo ni muongo tena ni muongo kweli hakuna msafara wowote uliopita kigoma mjini hivi uongo huo uwongo unakisaidia nini chama kwanza hakuna barabara yoyote inayotoka wilaya yoyote ianaingilia kigoma mjini, mods futa hii thread
Dr. Amelala kigoma mjini, so mida ya saa sita katoka mjini kwenda Nyarubanda na msafara wa magari machache including police. Ni kweli watu wamemshangilia kwa alama ya Victory.
 
zitto akiwa mwenyekiti wa chadema hatimaye rais wa nchi hii utahamia nchi gani?

Mbona tayari ni Mwenyekiti wa CDM masalia a.k.a CDM Wasaliti, na bado Ben anadunda tu kwa raha zake...
 
Back
Top Bottom