Dr Slaa Apinga Matokeo Yanayoendelea Kutangazwa na Tume

Dr Slaa Apinga Matokeo Yanayoendelea Kutangazwa na Tume

Porojo tupige lakini kwenye ukweli tuwekane sawa, u-rais kwa slaa mwaka huu hakuna alichoibiwa, alihitaji kujitangaza zaidi, katika majimbo yote ~238 hata nusu ya majimbo Slaa hakuwa na watu bado, kule alipokuwa na watu pameonekana, na kura za watu wake hao hazitomfanya kuwa rais. ajiweke sawa 2015.

WHAT ABOUT EUROPEAN UNION ELECTION OBSEVOR REPORT? CAN YOU EXPLAIN THAT?

EU: CCM imebebwa na vyombo vya dola Send to a friend Wednesday, 03 November 2010 04:53 0diggsdigg

Elias Msuya
MWANGALIZI mkuu wa wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Ulaya, David Martin amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya kubebwa na vyombo vya dola, ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Akitoa taarifa ya awali ya waangalizi hao jana jijini Dar es Salaam, Martin alisema uchaguzi huo, uligubikwa na kasoro nyingi licha kuendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari wa gazeti hili kuhusu muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama inatenda haki, Martin alisema hilo ameshaligusia katika taarifa yake.

"Hilo nimelisema kama umesoma kipengele cha nne cha taarifa yetu utaona kinasema, chama tawala kilinufaishwa na muundo wa utawala thabiti wa vyombo vya serikali ambao kiliurithi kutoka kwenye mfumo wa chama cha CCM enzi za chama kimoja ambao wakati mwingine ulikuwa hautambuliki vizuri," alisema.

Alisema kimsingi idadi kubwa ya viongozi wanaoteuliwa katika vyombo hivyo, wamekuwa wakiteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni mgombea katika uchaguzi, jambo ambalo linazua maswali kuhusu uhuru wa vyombo vya dola kukisaidia chama tawala.

Alisema CCM kilisaidiwa na vyombo vya dola katika kuendesha kampeni ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.

Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi, alitaja kitendo cha kutishiwa kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi kutokana na kutoa taarifa hasi za serikali, alisema ilikwenda kinyume na uhuru wa kujieleza.

"Ujumbe wa Ulaya wa kufuatilia kwa kina uchaguzi mkuu nchini unadhania kwamba vitisho kama hivyo dhidi ya vyombo vya habari ni jaribio la kuuwekea mipaka uhuru wa kujieleza" alisema Martins.

Mapungufu mengine kwa mujibu wa Martin ni kuwalazimisha watu kugombea kupitia vyama bila kutumia chama ni kinyume na kanuni za kimataifa.

"Sharti hilo, linawanyima watu haki na fursa ya kusimama kugombea hasa wale ambao wangependa kushiriki katika uchaguzi kama wagombea binafsi. Matokeo yake linaiwekea mipaka ridhaa ya wapiga kura,"alisema.
Alisema tume hiyo, imesikitishwa na tabia yake ya kuchelewesha matokeo huku akitilia shaka uwazi katika kazi ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi.

"Ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo ni jambo lililotusikitisha kwasababu jambo hilo, limesabisha mashaka miongoni mwa wapiga kura na wagombea. Pia tuna mashaka na uwazi katika shughuli ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi," alisema.

Naye kiongozi wa ujumbe kutoka Bunge la Ulaya, Maria Ndelcheva alishangazwa na kutojitokeza kwa wanawake kugombea urais licha ya wanawake hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

"Japo tunaikaribisha hatua ya idadi ya viti vilivyotengwa katika Bunge la Taifa na katika Baraza la Mapinduzi, bado tunasikitishwa kutoona wanawake katika vyombo vya kusimia kazi nzima ya uchaguzi wala mgombea urais," alisema Ndelcheva.
 
akapinge matokeo mahakamani sio ktk itv!!!

Rais akishatangazwa ni final..hakuna cha kwenda mahakamani eti!
Anachokifanya Slaa hapa ni ku protest... kuonyesha kutokuridhika na haina maana kuwa malalamiko hayo yatabadilisha matokeo kama majumlisho yameshakamilika na tume ya uchaguzi kuamua kutangaza matokeo.
 
yamechakachuliwa mpaka basi yani..............slaa amekuwa kama mtu ambaye hakubaliki kabisa.....na huu sio uchechezi tunamuonea huruma huyu anayetangazwa kushindwa kwa sababu atatendaje kazi kama jamii haijamkubali?
 
Sasa kama anafanya utani. Kwa trend ilivyokuwa hata kwa kujumlisha jimbo kwa jimbo bado Dr. Slaa kura zake ni chache ukilinganisha na za JK. Kwa hiyo anapotoa hilo tamko ambalo ni batili nadhani anachochea machafuko yasiyo ya lazima. Mtoa mada pale juu anatamani kuwe na machafuko kama ilivyokuwa Kenya. Je kwa faida ya nani? Damu zinapomwagika, je ni za akina nani? Si ni watanzania hao? Mimi nadhani hayo ni mawazo hasi. Kwa sasa mimi nadhani sisi wana CHADEMA tuanze mikakati ya ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Huo ndiyo utakuwa ustaarabu mkubwa na sio kuchochea machafuko kama mtoa mada hapo juu anavyopendelea.

Tatizo watu humu wanaushabiki usio kuwa na maana yeyote, matokeo tangu mwanzo wanayaona Slaa hajashinda, sasa mnachobisha ni nini? Mna uhakika gani kwamba watu walimpigia kura Dr Slaa, Mimi ni mmoja wapo niyepigia kura wabunge Chama pinzani na Rais nilimpigia Kikwete, sasa mnadhani ni wangapi waliofanya hivyo.... CHADEMA bado sana kupewa Nchi, nendeni mkajipange tena mrudi 2015 sio kuchochea machafuko yasiyokuwa na maana.
Mnalazimisha ushindi, ushindi haulazimishwi. Kajipangeni upya mtashinda tu muda ukifika.
 
Mtu wa Kwanza kulipa huu udhalimu ni huyu anayejiita Jaji sijui wa wapi Makame na huyo sijui KIRAVU hawa watu ni kuwakamata na kuwachapa viboko tuuu hadharani

Teh...tehe..tehhee...kweli bana huyu Makame na Kiravu ni kuwakamata na kuwacharaza fimbo tu. Nyambaaf sana hawa!
 
Mwaka 2005 Lipumba aliposema kaibiwa kura na bila ya tume huru ya uchaguzi na katiba mpya CCM watatawala milele Chadema wakawa wakwanza kumpongeza Kikwete na Mbowe kumkumbatia kabisa kwenye uapishaji na kumpongeza kwa ushindi sasa Slaa analalamika nini?
 
WAANGALIZI wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 31,kutoka Jumuiya ya Ulaya ( EU EOM) na Umoja wa Afrika wamesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki, utulivu na amani.

Waangalizi hao walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti wakati walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana(leo) kuhusu taarifa ya awali ya uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwangalizi Mkuu wa EU EOM, David Martin alisema uchaguzi huo ambao ni wa nne kufanyika nchini tangu mfumo wa vyama vingi kuanzishwa Tanzania, hadi sasa kwa ujumla umefanyika kwa amani na mpangilio mzuri.

" Siku ya Uchaguzi Mkuu ilijitokeza kwa utulivu mkubwa na kwa ujuml a waangalizi wa uchaguzi wa Ujumbe Maaalumu wa Jumuiya ya Ulaya(EU EOM) ulikadria mchakato mzima wa uchaguzi huo kuwa ama ulikuwa ‘mzuri' au ' kuridhisha' katika asilimia 95 ya vituo vyote vya kupigia kura walivyovitembelea upande wa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar," alisema Martin.

Aliongeza kuwa kwa ujumla taratibu muhimu katika vituo vya kupigia kura zilitumwa kwa ulinganifu kwa kila kituo cha kupigia kura nchini kote, licha kuwepo mapungufu machache.

Martin alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) zilisimamia chaguzi kwa namna ya kitaalamu, hivyo kwa sehemu kubwa ziliwapatia watu watu wote haki ya kupiga kura.

Aliongeza kuwa ujumbe huo utabakia nchini kuzidi kufuatilia kwa karibu zaidi zoezi la kuhesabu matokeo ya uchaguzi, utangazaji wa matokeo na matukio yoyote yatakayojitokeza baada ya uchaguzi.

"Taarifa hii ni ya awali .Taarifa ya kina ya mwisho itatolewa baina ya miezi miwili na miezi mitatu baada ya mchakato mzima wa uchaguzi kukamilika," alisema.

Kwa upande wake Kiongozi wa waangalizi hao, kutoka AU, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Sierra Leone, Dk. Ahmad Tejan Kabbah alisema uchaguzi huo umefanyika wa amani na umefanyika kwa mujibu wa sheria za uchaguzi wa Tanzania .

Aliongeza kuwa umefanyika kwa kuzingatia Azimia la Durban Demorasia katika Chaguzi za Afrika la Julai mwaka 2002.

" Waangalizi wa Umoja wa Afrika wamesema uchaguzi umefanyika kwa huru, haki , uwazi na uadilifu(Credible) .



​
Naye Katibu Mtendaji wa International Conference of the Great Lakes Region (ICGLR) Balozi Liberata Mulamula amesema wiki hii kwamba wameridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi mkuu Tanzania na kwamba ukiondoa matatizo madogo madogo yaliyojitokeza sehemu mbili tatu, ulikuwa huru na wa haki.
Balozi Mulamula amesema uchaguzi wa Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa nchi wanachama wa ICGLR ambao wengi watakuwa na uchaguzi katika kipindi hiki. Ameisifu serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa na kuruhusu kila mwananchi aliejiandikisha kupiga kura bila wasiwasi.

Waangalizi hao ,waliwapongeza wananchi wa Tanzania, Vyama vya Siasa, wagombea , NEC, ZEC na vyombo vya usalama kwa kuwezesha uchaguzi huo ufanyike kwa amani na kuwashauri wagombea kukubali matokeo yanayotangazwa na NEC.

Wewe ni fisadi mkubwa sana na una self-deception, soma hii taarifa
EU: CCM imebebwa na vyombo vya dola Send to a friend Wednesday, 03 November 2010 04:53 0diggsdigg

Elias Msuya
MWANGALIZI mkuu wa wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Ulaya, David Martin amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya kubebwa na vyombo vya dola, ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Akitoa taarifa ya awali ya waangalizi hao jana jijini Dar es Salaam, Martin alisema uchaguzi huo, uligubikwa na kasoro nyingi licha kuendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari wa gazeti hili kuhusu muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama inatenda haki, Martin alisema hilo ameshaligusia katika taarifa yake.

"Hilo nimelisema kama umesoma kipengele cha nne cha taarifa yetu utaona kinasema, chama tawala kilinufaishwa na muundo wa utawala thabiti wa vyombo vya serikali ambao kiliurithi kutoka kwenye mfumo wa chama cha CCM enzi za chama kimoja ambao wakati mwingine ulikuwa hautambuliki vizuri," alisema.

Alisema kimsingi idadi kubwa ya viongozi wanaoteuliwa katika vyombo hivyo, wamekuwa wakiteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni mgombea katika uchaguzi, jambo ambalo linazua maswali kuhusu uhuru wa vyombo vya dola kukisaidia chama tawala.

Alisema CCM kilisaidiwa na vyombo vya dola katika kuendesha kampeni ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.

Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi, alitaja kitendo cha kutishiwa kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi kutokana na kutoa taarifa hasi za serikali, alisema ilikwenda kinyume na uhuru wa kujieleza.

"Ujumbe wa Ulaya wa kufuatilia kwa kina uchaguzi mkuu nchini unadhania kwamba vitisho kama hivyo dhidi ya vyombo vya habari ni jaribio la kuuwekea mipaka uhuru wa kujieleza" alisema Martins.

Mapungufu mengine kwa mujibu wa Martin ni kuwalazimisha watu kugombea kupitia vyama bila kutumia chama ni kinyume na kanuni za kimataifa.

"Sharti hilo, linawanyima watu haki na fursa ya kusimama kugombea hasa wale ambao wangependa kushiriki katika uchaguzi kama wagombea binafsi. Matokeo yake linaiwekea mipaka ridhaa ya wapiga kura,"alisema.
Alisema tume hiyo, imesikitishwa na tabia yake ya kuchelewesha matokeo huku akitilia shaka uwazi katika kazi ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi.

"Ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo ni jambo lililotusikitisha kwasababu jambo hilo, limesabisha mashaka miongoni mwa wapiga kura na wagombea. Pia tuna mashaka na uwazi katika shughuli ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi," alisema.

Naye kiongozi wa ujumbe kutoka Bunge la Ulaya, Maria Ndelcheva alishangazwa na kutojitokeza kwa wanawake kugombea urais licha ya wanawake hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

"Japo tunaikaribisha hatua ya idadi ya viti vilivyotengwa katika Bunge la Taifa na katika Baraza la Mapinduzi, bado tunasikitishwa kutoona wanawake katika vyombo vya kusimia kazi nzima ya uchaguzi wala mgombea urais," alisema Ndelcheva.
 
Amedhulumiwa mali gani? na nani? hakuwa na mawakala wa kuthibitisha! Tatizo mlikuwa mkikampeni kewnye mtandao watanzania wengi vijijini wanaikubali CCM MSITUHARIBIE NCHI YETU:nono:

Bora Useme ukweli ndugu yangu, Kwanzi mawakala kazi yao ni nini????????????? Wanataka kutuharibia Nchi yetu bure. Mshindwe na mlegeeeee
 
yani NEC hawana hata aibu, wametuzuga wananchi kwa kututolea kwanza matokeo ya ubunge kumbe wao wamejichimbia wakichakachua matokeo ya urais, hii ni dhambi isiyosameheka.. Dr songa mbele mahakamani tupo nyuma wananchi wako tunakusupport kwa kila hali.
 
eti nini?! Mnaogopa machafuko? Kum**nina zenu!! Yaani tukae kimya haki zetu zinaporwa?
hongera dr. Slaa kukataa matokeo ya kipuuzi haya. Kama noma na iwe noma.

ni bora kufa nimesimama kuliko kuendelea kuishi huku nimepiga magoti. Kama vipi tuzame mstuni au mwasemaje wabongo?

List me number one Bro! siwezio kutawaliwa na CCm ndo maana ninapoishi diwani na mbunge wote ni wa Chadema. Sasa ndo najua kwa nini watu wanajilipua
 
Tatizo watu humu wanaushabiki usio kuwa na maana yeyote, matokeo tangu mwanzo wanayaona Slaa hajashinda, sasa mnachobisha ni nini? Mna uhakika gani kwamba watu walimpigia kura Dr Slaa, Mimi ni mmoja wapo niyepigia kura wabunge Chama pinzani na Rais nilimpigia Kikwete, sasa mnadhani ni wangapi waliofanya hivyo.... CHADEMA bado sana kupewa Nchi, nendeni mkajipange tena mrudi 2015 sio kuchochea machafuko yasiyokuwa na maana.
Mnalazimisha ushindi, ushindi haulazimishwi. Kajipangeni upya mtashinda tu muda ukifika.

Self-deception
 
Nafikiri hakuna haja ya kutafuta sifa. Kama ameshinda si watoe matokeo halali? Kwanini tume isihusishe wahusika kabla ya kutangaza? Tuondolee balaa hizi. Kura mbona zimepigwa kwa amani?
 
Dr Slaa Apinga Matokeo Yanayoendelea Kutangazwa na Tume, akidai kuwa yamechakachuliwa
Source ITV
 
ni uchochezi rasmi, uchu wa madaraka, kutojiamini, na kutoitakia salama nchi hii. sijali watu kuchukia juu ya hilo. ila alie msafi na awe wa kwanza kutupa jiwe😎

Wewe unaelewa maana ya uchochezi? Nchi zote zinazominya demokrasia hupenda sana kutumia hili neno la kijinga 'UCHOCHEZI' ili kulinda uovu wa watawala na mibaka uchumi. Neno hilo pia lilitumiwa na wale wapuuzi wenzako wa MAELEZO wakiyatisha magazeti yanayoandika ukweli kuhusu uozo uliopo ndani ya CCM - yaani Mwananchi na Mwanahalisi. Gazeti la Kulikoni pia lilipata kufungiwa kwa kile kilichodaiwa kuwa uchochezi. Lazima tukomeshe ujinga huu.
 
Kukaa kimya bila tamko lolote sasa akisubiri ati aende mahakamani ni sawa na mbumbumbu kwamba yote sawa tu, tushinde tusishindwe hamna tofauti. Njia nzuri kukabili tatizo ni papo hapo linapotokea au linakaribia kutokea (unachukua mitigative measures and not after a disarter)
 
Tatizo watu humu wanaushabiki usio kuwa na maana yeyote, matokeo tangu mwanzo wanayaona Slaa hajashinda, sasa mnachobisha ni nini? Mna uhakika gani kwamba watu walimpigia kura Dr Slaa, Mimi ni mmoja wapo niyepigia kura wabunge Chama pinzani na Rais nilimpigia Kikwete, sasa mnadhani ni wangapi waliofanya hivyo.... CHADEMA bado sana kupewa Nchi, nendeni mkajipange tena mrudi 2015 sio kuchochea machafuko yasiyokuwa na maana.
Mnalazimisha ushindi, ushindi haulazimishwi. Kajipangeni upya mtashinda tu muda ukifika.

Kweli wewe ni DOMOKAYA huna maana
 
Hafadhali kuna mahala pa kuanzia na ana data za uhakika. Tume holela.
 
Back
Top Bottom