Dr Slaa Apinga Matokeo Yanayoendelea Kutangazwa na Tume

Dr Slaa Apinga Matokeo Yanayoendelea Kutangazwa na Tume

Kama sikosei, matokeo ya urais yakitangazwa KISHERIA hayawezi kuhojiwa tena. Kwa hili, Slaa amepoteza.

Pili, kwa wale wanaosema amejishushia credibility, si ametumia haki yake kama Kinana?

Muhimu: Chaguzi zote tangu 1995 zinatukumbusha mambo mawili ya kuweka sawa nchi hii ili matatizo yaishe katika uchaguzi.

1. Katiba na Sheria za Uchaguzi zisizopendelea upande wowote.
2. Tume Huru ya uchaguzi isiyoweza kuingiliwa mipaka yake.

Hayo yakifanikiwa, wananchi watapiga kura na kwenda kulala nyumbani kusubiri matokeo, wakiamini kura yao imehesabiwa na kutangazwa KIHALALI.
 
si rajisi nec/ccm kukubali

hata kama lakini itampa Mkwere taabu kutawala watu wasiokutaka. NI sawa na Idi Amin. Kupora kile kisicho kuwa chako maanake Dictator.
 
Tusiishie kulalamika katika TV, amesema hatua zitazochukuliwa? we need do something, kusubiri 2015 is not the option!
 
WATANZANIA walijitolea kwa hali na mali kuleta mapinduzi hakuna haki inayopatikana kwa njia amani isipokuwa kwa njia ya UPANGA ikiwa watu wanajaribu kuichukua kwa nguvu haki hiyo................wote tuseme NO kwa NEC na matokeo yao watutangazie yale yaliyo halali.
 
Bora Useme ukweli ndugu yangu, Kwanzi mawakala kazi yao ni nini????????????? Wanataka kutuharibia Nchi yetu bure. Mshindwe na mlegeeeee

EU: CCM imebebwa na vyombo vya dola Send to a friend Wednesday, 03 November 2010 04:53 0diggsdigg

Elias Msuya
MWANGALIZI mkuu wa wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Ulaya, David Martin amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya kubebwa na vyombo vya dola, ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Akitoa taarifa ya awali ya waangalizi hao jana jijini Dar es Salaam, Martin alisema uchaguzi huo, uligubikwa na kasoro nyingi licha kuendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari wa gazeti hili kuhusu muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama inatenda haki, Martin alisema hilo ameshaligusia katika taarifa yake.

"Hilo nimelisema kama umesoma kipengele cha nne cha taarifa yetu utaona kinasema, chama tawala kilinufaishwa na muundo wa utawala thabiti wa vyombo vya serikali ambao kiliurithi kutoka kwenye mfumo wa chama cha CCM enzi za chama kimoja ambao wakati mwingine ulikuwa hautambuliki vizuri," alisema.

Alisema kimsingi idadi kubwa ya viongozi wanaoteuliwa katika vyombo hivyo, wamekuwa wakiteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni mgombea katika uchaguzi, jambo ambalo linazua maswali kuhusu uhuru wa vyombo vya dola kukisaidia chama tawala.

Alisema CCM kilisaidiwa na vyombo vya dola katika kuendesha kampeni ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.

Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi, alitaja kitendo cha kutishiwa kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi kutokana na kutoa taarifa hasi za serikali, alisema ilikwenda kinyume na uhuru wa kujieleza.

"Ujumbe wa Ulaya wa kufuatilia kwa kina uchaguzi mkuu nchini unadhania kwamba vitisho kama hivyo dhidi ya vyombo vya habari ni jaribio la kuuwekea mipaka uhuru wa kujieleza" alisema Martins.

Mapungufu mengine kwa mujibu wa Martin ni kuwalazimisha watu kugombea kupitia vyama bila kutumia chama ni kinyume na kanuni za kimataifa.

"Sharti hilo, linawanyima watu haki na fursa ya kusimama kugombea hasa wale ambao wangependa kushiriki katika uchaguzi kama wagombea binafsi. Matokeo yake linaiwekea mipaka ridhaa ya wapiga kura,"alisema.
Alisema tume hiyo, imesikitishwa na tabia yake ya kuchelewesha matokeo huku akitilia shaka uwazi katika kazi ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi.

"Ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo ni jambo lililotusikitisha kwasababu jambo hilo, limesabisha mashaka miongoni mwa wapiga kura na wagombea. Pia tuna mashaka na uwazi katika shughuli ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi," alisema.

Naye kiongozi wa ujumbe kutoka Bunge la Ulaya, Maria Ndelcheva alishangazwa na kutojitokeza kwa wanawake kugombea urais licha ya wanawake hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

"Japo tunaikaribisha hatua ya idadi ya viti vilivyotengwa katika Bunge la Taifa na katika Baraza la Mapinduzi, bado tunasikitishwa kutoona wanawake katika vyombo vya kusimia kazi nzima ya uchaguzi wala mgombea urais," alisema Ndelcheva.
 
Tume inasema haitaweza kifanyia kazi hayo maombi kwani hawajayapokea kwa maandishi. Kwa nini hayakupelekwa NEC halafu waandishi waarifiwe kwamba malalamuko yamepelekwa?
 
eti nini?! Mnaogopa machafuko? Kum**nina zenu!! Yaani tukae kimya haki zetu zinaporwa?
hongera dr. Slaa kukataa matokeo ya kipuuzi haya. Kama noma na iwe noma.

ni bora kufa nimesimama kuliko kuendelea kuishi huku nimepiga magoti. Kama vipi tuzame mstuni au mwasemaje wabongo?

Matusi ya nini tena, Halafu mnataka mpewe Nchi na midomo yenu michafu hivyo, nendeni mkajifunze heshima kwanza ndio mje kuomba kura zetu.
 
Ikiwa MKE/MMEO atachukuliwa na rafiki yako utasema unakubaliana nae na utatafuta mwingine...AMKA fikiria mara ya pili.
 
Watanzania wasikubali matokeo haya yaliyochakachuliwa na CCM, hii ni hatari sana, CHADEMA wanachukua hatua gani?
 
hata akipinga Kikwete atakuwa raisi tu.
aende Vatcan akapinge
 
Kama ushahidi wake ni mzuri na mahakama zikizingua na jumuiya za kimataifa zikikaa kimya itabidi ile amani tuliyoizoea Watanzania tuiweke pembeni! Haiingii akilini CHADEMA ishinde majimbo mengi ya ubunge uchaguzi halaf tume ya uchaguzi itangaze kuwa ktk baadhi ya majimbo hayo kura za urais zimeenda kwa JK na pia CUF iwe na kura nyingi za urais kuliko Dr Slaa majimbo ya bara wakati kwenye ubunge hawakufanya vizuri kuliko CHADEMA! Moja jumlisha moja unapata mbili! Kura zimechakachuliwa na CUF wameingizwa kijanja ili waonekane wanapendwa zaidi ya CHADEMA! Aluuu! Patakuwa padogo sana TZ, mpaka kieleweke! Na ndo maana tume ilikuwa inasita kutangaza matokeo ktk majimbo yenye upinzani mkubwa toka CHADEMA! Mawakala wapo na evidence zote zipo, hivyo nasisi tutajumlisha kivyetu na tutangaza serikali yetu hata ikiwa ya msituni! Someni Mwanahalisi ya leo, inasemekana Dr Slaa ameshinda kwa kura 61.6% kwa matokeo yaliyopatikana hadi juzi.
 
Kama ushahidi wake ni mzuri na mahakama zikizingua na jumuiya za kimataifa zikikaa kimya itabidi ile amani tuliyoizoea Watanzania tuiweke pembeni! Haiingii akilini CHADEMA ishinde majimbo mengi ya ubunge uchaguzi halaf tume ya uchaguzi itangaze kuwa ktk baadhi ya majimbo hayo kura za urais zimeenda kwa JK na pia CUF iwe na kura nyingi za urais kuliko Dr Slaa majimbo ya bara wakati kwenye ubunge hawakufanya vizuri kuliko CHADEMA! Moja jumlisha moja unapata mbili! Kura zimechakachuliwa na CUF wameingizwa kijanja ili waonekane wanapendwa zaidi ya CHADEMA! Aluuu! Patakuwa padogo sana TZ, mpaka kieleweke! Na ndo maana tume ilikuwa inasita kutangaza matokeo ktk majimbo yenye upinzani mkubwa toka CHADEMA! Mawakala wapo na evidence zote zipo, hivyo nasisi tutajumlisha kivyetu na tutangaza serikali yetu hata ikiwa ya msituni! Someni Mwanahalisi ya leo, inasemekana Dr Slaa ameshinda kwa kura 61.6% kwa matokeo yaliyopatikana hadi juzi.

Your message can not be read precisely, change font!
 
jamani KENYA leo hii watu wanaheshimiana baada ya kibaki na wenzake kutaka kuwaletea wakenya utani na nchi yao. ZIMBABWE ikatokea kitu kile kile. kwanini sisi tufanywe ngamia wa kusikiliza kile anachosema bwana wake.......Dr. Slaa toa TAMKO kwa wananchi wako nini kifanyike watu hatuwezi kukubali kura zetu ziende bure ili kuwaneemesha wachache
 
MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema, atayakataa matokeo ya urais yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa kumefanyika wizi mkubwa wa kura.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema, kama NEC inaitakia mema nchi hii, ifute matokeo yote ya urais na uchaguzi urudiwe upya.

Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema wamekuwa wakifuatilia matokeo ya nchi nzima kwa umakini mkubwa na wamegundua kuna wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.

"Kuna uchakachuaji mkubwa wa kura na kazi hiyo inafanywa na usalama wa taifa,"alisema Dk Slaa.

Chanzo Gazeti la Mwananchi
 
watanzania wasikubali matokeo haya yaliyochakachuliwa na ccm, hii ni hatari sana, chadema wanachukua hatua gani?

sio chadema wanachukua hatua gani, sisi tuliopiga kura halafu wajinga wakawa na kura zao tufanye nini!!??
 
nyie mnaotetea mafisadi hamjui ni kiasi gani watu wameichoka ccm endeleeni kujifariji lkn ukweli utabaki palepale tofauti ya wasio nacho na wenye nacho inapozidi matokeo yake yanajulika na halitakuwa kosa la apinzani bali mafisadi.
 
Back
Top Bottom