Nani kakuambia CHADEMA ni mali ya Watanzania wote??? CHADEMA ni mali ya Mtei ambaye na yeye ameshamuuzia Fisadi Lowassa. Sasa hivi CHADEMA ni mali ya Lowassa na marafiki zake. CHADEMA ishauzwa tayari. Wewe endelea kujidanganya eti CHADEMA ni mali ya Watanzania. Kalaga baho!
Ukikatwa ccm unaenda chadema ukikatwa chadema unaenda act huko nako wakikukata unaenda wapi..? Hizi ndiyo siasa za bongo..Mungu ibariki afrika na ibarikie Tanzania kuvuka kwa Amani mwaka huu wa uchaguzi 2015
Jamani mjue kuwa yule ni Padre do kaweka mfungo na kajifungia. Kuna ule mfungo wenyewe wakatoliki huwa ukifungu huruhusiwi kuongea na mtu
Mumekaribishwa tu jana leo mnajifanya kuanza mihemuko yenu,si ajabu ndio sababu mlishindwa huko mlikotoka nyie ni watu wa kuja tu,sidhani kama umesoma hata ukurasa mmoja wa katiba ya Chadema.Mambo yenu myaache huko huko mlikokuwa huku ni sehemu nyingine,kumbuka nyie mumeomba hifadhi bado ni wakimbizi tu.Wana JF.
Kesho vikao vya Kamati Kuu ya Chadema vinaendelea ili kupanga mikakati ya kuhakikisha Ukawa inapata ushindi wa kishindo October .
Ili mikakati ya ushindi kwenye uchaguzi mkuu october iende vizuri, wajumbe wote wanatakiwa wawepo akiwemo Katibu Mkuu wa Chama Dr. Wilbroad Slaa ambae mpaka sasa hivi hajulikani alipo, endapo Dr. Slaa hatahudhuria kikao kesho naomba Kamati ya Maadili imchukulie hatua kali za kinidhamu ili kulinda kanuni na maadili ya chama.
Chadema sio mali ya mtu binafsi ,ni mali ya watanzania wote, na hakuna mtu mkubwa kupita Chama.
Asietaka ukombozi wa nchi October atupishe.
Nyie wakimbizi ebu acheni upuuzi wenu ,mumekaribishwa tu jana tena kwa mlango wa uani leo ndio mumekuwa na mihemuko,hiyo mihemuko mbona hukuitoa kwa katibu wenu huko mlikotoka.Mzee Slaa apumzike sasa, kama amefikia hatua ya kufichwa na Mchumba wake, hafai huyo!
WanaJF na hasa wana CHADEMA wenzangu tuwe makini sana na maandishi yetu hapa jukwaani kuhusu huu ukimya wa DR SLAA, tafadhalini sana, DR ni kiongozi mkubwa sana anastahili kuheshimiwa, wale wenye uchungu na CHADEMA na tunaofahamu tulipotoka hatuwezi kumkashifu huyu mtu, kwa lipi hasa ? Acheni kabisa jambo hilo, sikupenda kuandika jambo hili maana linaweza kuendeleza malumbano zaidi lakini nimelazimika kuliweka kama angalizo.
de slaa na familia yake waheshimiwe hakuna sababu ya kumtukana yeye wala mkewe jamani wanachadema tuhakikishe hatusahau kazi iliyotukukaWanaJF na hasa wana CHADEMA wenzangu tuwe makini sana na maandishi yetu hapa jukwaani kuhusu huu ukimya wa DR SLAA, tafadhalini sana, DR ni kiongozi mkubwa sana anastahili kuheshimiwa, wale wenye uchungu na CHADEMA na tunaofahamu tulipotoka hatuwezi kumkashifu huyu mtu, kwa lipi hasa ? Acheni kabisa jambo hilo, sikupenda kuandika jambo hili maana linaweza kuendeleza malumbano zaidi lakini nimelazimika kuliweka kama angalizo.