Ngoja niwatag akina Heche na Lema na
CHADEMA
Tume hawakupaswa kukanusha tuhuma za Polepole badala yake walipaswa kutangaza kusimamisha chaguzi hadi Auditing ya Vyama na waangalizi wa Uchaguzi kukamilisha uchunguzi.
Ngoja nitoe brief details kuongeza nyama kwenye watakachojadili na wadau wengine wengi wakiwemo wananchi hata wakiwa wanamuelezea Lissu nini kimetokea wiki hii.
Anayeweza ku share na Viongozi wa Chadema kwenye mkutano wao ujao kujadili Kauli za Polepole na Watanzania na Mabalozi/Diplomats wa Mataifa washirika.
1. Katiba, hapa kuna element ya Uhaini (Lissu na Mawakili wa Chadema wanajua sheria kunizidi)
2. Data protection act, Cybercrime act
Sheria za bunge zinazohusu uhifadhi na uchakataji wa taarifa binafsi.
Kwa sheria zetu CCM anakuwa Data processor, kwa sababu anakusanya taarifa, ambaye anatakiwa awe compliance na Sheria zote za Data za Tanzania.
Katika website ya CCM ambayo mtu anaweza kujisajili kidijitali hakuna sehemu yoyote ambayo inamtaka mtu afanye consent, hakuna page au maelezo yoyote yanayosema kwa nini wanakusanya Taarifa binafsi(ikiwemo Number ya NIDA) na kama watakaa nazo milele au kwa Muda gani, hili ni kosa kisheria chini ya Sheria zetu za chini ya data protection act- Chadema wanasheria waanze kusoma hizi sheria.
Katika kipengele hichi cha sheria ya data protection, CCM, Tume na NIDA wanatakiwa mara moja kufanyiwa Auditing ya Cyber security compliance ya mifumo yao yote ya Tehama kabla hatua yoyote ya uchaguzi kuendelea
3. Integration ya mifumo ya NIDA.
Katika Sheria za uanzishwaji wa NIDA(ziko online), inasema hivi "NIDA ITAKUWA TAASISI PEKEE NCHNI YENYE RUHUSA YA KUKUSANYA NA KUTUNZA TAARIFA ZA UTAMBULISHO WA MTU"
kama umefanya Siphoned ya mifumo ya Taarifa ya NIDA (kuhamisha data kutoka database ya NIDA na kutunza kwenye database yako) NIDA wanatakiwa wakushitaki na kulingana na uzito wa kesi yako unakuwa umevunja Sheria za Usalama wa Taifa, ni Ukweli usiopingika Kuwa CCM inatumia APIs au direct connection na mifumo ya NIDA hili unaweza thibitisha hata sasa kwenye mfumo wa mtandao wa usajili wa CCM, ingiza taarifa zote zisizo sahihi, NIDA ndio itakwambia taarifa sio sahihi.
Hapa Chadema, vyama vyote, Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama, Taasisi za Kiraia na NGOs zinatakiwa zidai mkataba uliotumika kati ya CCM na NIDA, pamoja na kufanyia auditing mfumo wote wa CCM kujua ni taarifa zipi CCM huzipata, wanazitumiaje, wanazitunzaje (Sheria za NIDA haziruhusu mtu yoyote zaidi yako kukutunzia namba yako ya NIDA ikiwa plain text bila kibali maalumu), na usalama wake.
4. Cyber Data Espionage
Cyber espionage, or cyber spying, is a type of cyber attack in which an unauthorized user attempts to access sensitive or classified data or intellectual property (IP) for economic gain, competitive advantage or political reasons.
Sheria za usalama wa Taifa (Nation Security ACT) inasema hivi huruhusiwi kumiliki/kushare any sensitive, classified document, information, code, password or hash inayoweza kutumika dhidi ya maslahi ya taifa. Bila ruhusa sahihi . Taarifa zote za NIDA ni sensitive na classified information, kwa ajili ya matumizi ya Serikali ya Tanzania pekee. Hapa lazima Chadema wadai taarifa binafsi za mainjinia wote walihusika kuunda mifumo ya CCM, Security clearance, setup ya development, access level waliyopewa, Chadema wana wanasheria wengi na wazuri waziangalie hizi documents.
National security act.
Data protection act
Cybercrime act
Katiba (hapa wao ni wataalamu sana)
Sheria za msingi za kuanzishwa tume za uchaguzi na NIDA.
Mwisho Chadema wamsafirishe Dr Slaa na viongozi wao wa mahusiano ya kimataifa nje ya Tanzania haraka iwezekanavyo kama wataka kuescalate hili swala kimataifa, they have a very strong case.