Dr. Slaa akwea pipa na kuondoka nchini [PROPAGANDA]

Dr. Slaa akwea pipa na kuondoka nchini [PROPAGANDA]

Status
Not open for further replies.
MAASKOFU,,,, WAMSHUKIA Dr. Slaa

======
Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam

BAADHI ya viongozi wa dini na wananchi wamesema shutuma za aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa kuwa baadhi yao walihongwa na Mgombea Urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa, ni upuuzi mtupu.


Wamemtaka atoe ushahidi wa madai hayo kwa kutaja majina ya viongozi na kiasi walichohongwa, wakisisitiza kuwa hizo ni siasa za majitaka na kwamba anaifanyia kazi CCM ili apate njia ya kurudi katika chama hicho.
______
Rais wa TEC azungumza:

Akizungumzia shutuma hizo, Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, amemtaka Dk. Slaa kutoa ushahidi wa madai yake kuwa maaskofu wa kanisa hilo wamehongwa na Edward Lowassa.


Akizungumza na MTANZANIA kwa simu yake ya mkononi, Askofu Niwemugizi alieleza kushangazwa na tuhuma hizo zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi ya maaskofu bila uthibitisho.

“Hizo taarifa ndiyo nazisikia kwako, lakini kama kweli amesema hivyo kwa nini hakuweka ushahidi kuanzia majina ya maaskofu hao waliopewa fedha, kiasi na zilikopokelewa. Lakini kwa upande wangu binafsi sijapokea kiasi chochote kutoka kwa mtu yeyote.


Askofu Niwemugizi alimtaka Dk. Slaa kutoa uthibitisho wa maaskofu wa kanisa hilo kupokea fedha kutoka kwa Lowassa waweze kutoa uamuzi.

“Lowassa nimewahi kukutana naye nilimwalika kwenye shule yangu ya seminari kule Biharamulo… shule yenyewe inaitwa Katoke na nilimuweka wazi sababu za kumwalika na sikupokea kiasi chochote cha fedha kutoka kwake,”

alisema askofu huyona kuongeza:

“Athibitishe hilo aonyeshe kiasi cha fedha na majina ya maaskofu, mimi sijapata kiasi chochote labda kama nimetupiwa kwenye akaunti yangu bila mimi kujua lakini nasisitiza atoe ushahidi.”


Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekosti, William Mwamalanga alisema kauli za Dk. Slaa zina dalili ya kuleta kisasi fulani.

“Angekuja mapema kabla ya taratibu hizi kuanza tungemwelewa lakini kwa sasa yupo nyuma ya wakati. Kwanza ameonekana amesukumwa afanye aliyofanya na hilo haliwezi kuwabadilisha Watanzania walioamua kutaka mabadiliko,”alisema na kuongeza: “Hotuba yake haina mashiko na taifa halihitaji watu wabinafsi,”alisema Mchungaji Mwamalanga.

Askofu Gwajima azungumza

Naye Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekana kuwa mshenga wa Edward Lowassa kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema) .

Pia amekana kuhusika kuwarubuni kwa fedha maaskofu 30 wa Kanisa Katoliki ambao wanadaiwa kumuunga mkono Lowassa katika mbio zake za urais baada ya kuhongwa fedha.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Askofu Gwajima alisema Dk. Slaa ndiyo risasi ya mwisho iliyokuwa imebakia ndani kati ya bunduki ya CCM ili kuwaokoa.

Alisema yote yaliyosemwa na Dk. Slaa ni tuhuma za uongo hivyo wananchi wazipuuze kwa kuwa mwanasiasa huyo anatafuta uungwaji mkono kwa wananchi aelekee CCM.

“Yaani ni uongo kabisa tena uongo mweupe, imedhihirisha wazi kuwa huyu mtu asingefaa kuwa rais. Ni dhahiri ameona akiwasema wanasiasa wenzake watamjibu kwenye majukwaa yao ya siasa, lakini sasa amewasema maaskofu kwa kuwa wao hawana majukwaa.

“Kwa hiyo namshauri hayo mambo ya kuwahusisha maaskofu na uchaguzi aache uongo wa namna hiyo. Nafikiri awaseme wanasiasa wenzake kuzungumzia mambo ya siasa ila kuwahusisha maaskofu si mambo ya busara,” alisema.

Akizungumzia suala la kuwa mshenga wa Lowassa na Chadema, Askofu huyo alisema anafikiri Dk. Slaa ametumwa na waliomtuma, hivyo anawafanyia kazi watu.

“Kwa kawaida inashangaza kwamba kama watu wawili wanagombana, inatakiwa awepo mtu wa kuwaunganisha, ila anaposema maaskofu 34 haileti maana, haiingii akilini… ameingiza Gwajima, Rostam (Aziz) na maaskofu, haeleweki anachozungumza. Lakini ninachosema kuna waliomtuma ni watu ambao anawafanyia kazi.

“Kikubwa ni kwamba baada ya Lowasaa kuchaguliwa kugombea urais kwa Chadema alichukia, alifikiri Lowassa hataendelea kuwa na umaarufu, sasa anaona Lowassa anakwenda, hiyo imemtia hasira anataka kumchafulia Lowassa, ndiyo maana anaongelea Lowassa Lowassa tu.

“Kwa mfano alisema Lowasa angekuja na wabunge wenyeviti wa CCM, ina maana angemkubali Lowassa aje nao, sasa angekuja nao asingekuwa fisadi? Ni swali zuri ila amekwepa kulijibu.


“Nafikiri Dk. Slaa ndiyo risasi ya mwisho iliyobakia ndani ya bunduki ya CCM. Natoa wito kwa waumini wangu wafahamu kuwa hizi tuhuma ni za uongo na namsihi huyo daktari asihusishe maaskofu na uongo wake abaki nao mwenyewe,” alisema Askofu Gwajima.

_______
Maoni ya wananchi:
-------
Alphonce Boniface ambaye alipiga simu MTANZANIA na kujitambulisha kuwa ni mpiga kura, alisema Dk. Slaa ambaye jana alijitambulisha kuwa ni mtu masikini na anashindia mihogo, awaeleze Watanzania fedha alizotumia kuita waandishi wa habari katika hoteli kubwa ya Serena pamoja na kulipia vipindi vilivyorushwa moja kwa moja vimegharamiwa na nani.


Alisema alichokisema Dk. Slaa ni kukipigia debe Chama Cha Mapinduzi (CCM) na anachokitaka ni kuingia katika kampeni za chama hicho.

“Orodha ya mafisadi aliowataja … ni vema angeenda kushtaki Serikalini/mahakamani ili Lowassa achukuliwe hatua na si kuwaeleza wananchi kwani kufanya hivyo hakuna faida yoyote.


“Tunamtaka Dk. Slaa aache siasa za majitaka aende mahakamani aeleze yale anayoyajua na kutoa ushahidi ili Lowassa apelekwe mahakamani au achukuliwe hatua.

Alisema zipo nchi mbalimbali kama vile Sudan, Kenya na Afrika Kusini ambazo wagombea wao walikuwa na tuhuma za mauaji, ubakaji, kuhodhi ardhi lakini wananchi waliwapenda na kuwapa uongozi na wanafanya vizuri.

“Wananchi tunatakiwa tuamke na tuwe makini kuchagua viongozi ambao wataweza kutatua changamoto zinazotukabili na si kusikiliza siasa za wagombea ambao wanashindwa kutekeleza ahadi zao.


Chanzo: Mtanzania gazeti
 
picha hiyo ya mwaka jana usituzuge na kutuharibia siku kwa umbea na uongo wako.

Tupe picha ya leo inayomuonyesha alipo tofauti na hivyo hiyo picha bado itasimamia ukweli wake maana unapopinga kitu lazima uwe na jibu la hicho unachokipinga
 
Jamani naomba niulize tofauti na siasa huyu Dr. ni kazi ipi huwa anafanya?
 
hana akiba ya maneno huyo mzee ................ viongozi wa dini aliwahusisha ili iweje? alimis target ya adui yake!

Swali la kujiuliza nani alitaka kujua habari za kuoa kwake?alafu anasema serikali imemzuia kuoa?Slaa pale ndipo alipojichanganya sana.Imani ya KIKRITO ndiyo inambana ktk hili yeye anasingizia serikali.Kwa maandiko matakatifu Slaa ni MZINZI na Hakuna mbingu ya WAZINZI.
 
Swali la kujiuliza nani alitaka kujua habari za kuoa kwake?alafu anasema serikali imemzuia kuoa?Slaa pale ndipo alipojichanganya sana.Imani ya KIKRITO ndiyo inambana ktk hili yeye anasingizia serikali.Kwa maandiko matakatifu Slaa ni MZINZI na Hakuna mbingu ya WAZINZI.

Kumbe MZINIFU, usafi wake upo wapi???
 
Ukishabikia ukawa unashabia tunda ambalo waloupanda mti hawapo nao ni Dr.slaaa na prof.lipumba. sasa wenyewe wasile wewe ule huoni kama ni sumu? IKULU SIO HODI YA WAGONJWA WALA IKULU SIO SEHEMU YA MATINGATINGA. KAENI CHONJO WAKAWA KWANI NI Wakawaida sana kwa CCM tuachieni sisi hao ACT Wazalendo
 
Last edited by a moderator:
Watashindanaaaaaaa..lakinini hawatatushinda ukawa.

Hivi huko alikokimbilia kutumbua Pesa za hata aliyotumwa kuyafanya atajisikiaje akisikia mwehu mmoja wa kisiasa aliyechoshwa na ulaghai kaenda kule Karatu na kumcharaza bakora hamda wa ishirini mzee Slaa eti kwa kuzaa mtoto mwongo na mlaghai?
Unapofanya mambo ya kuigusa jamii lazima utumie akili sana kufikiria wengine na sio tumbo lako tuu
 
Style ile ile ya Prof. Lipumba... Na walinzi wake ni wale wale ... CCM kwishnei ... Vijana walioandamana eti kuuunga mkono hotuba ya slaa wapewa kibano wanasema wamelipwa buku 5000 na Tshirt za CHADEMA ...
Kama ailivyokuwa kwa mwenzake Pof. Lipumba mara baada ya kufanya press conference alikwea pipa. Vivyo hivyo Dr. Slaa naye kakwea pia leo. Habari za uhakika ni kuwa anaelekea USA.

11951889_10203657338754355_8273820177259980967_n.jpg

11951248_10203657337074313_6252291186441749736_n.jpg

11988613_10203657337994336_3016629590105493389_n.jpg
 
unaongea pumba tu.dr slaa au pr lipumba ni nani kwangu.yesu kristo hayupo haimaanishi niukane ukristo wangu.kwa hiyo km slaa au lipumba hyupo ndo watu waachane na ukawa?keep in mind kila mtu an uhuru wa kuamini anachoona ni sahihi.usinichagulie mwanasiasa wa kumuamini.
 
Kama ailivyokuwa kwa mwenzake Pof. Lipumba mara baada ya kufanya press conference alikwea pipa. Vivyo hivyo Dr. Slaa naye kakwea pia leo. Habari za uhakika ni kuwa anaelekea USA.

11951889_10203657338754355_8273820177259980967_n.jpg

11951248_10203657337074313_6252291186441749736_n.jpg

11988613_10203657337994336_3016629590105493389_n.jpg

Kamanda nikupe salute🎓
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom