Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

Unajua hauwezi kusema mdahalo, halafu unawaalika Dr Slaa, Lipumba na Makaidi kwa ujumla hao wako mrengo mmoja. Halafu uku unamuweka Zitto sasa sielewi muendesha mdahalo ana maana gani? Nawatuzungumzia nini? Au ana mpango Fulani nyuma yake? Jamani tusikulupuke kuandaa midahalo isiyo na tija kwa Taifa. Lai yangu hata prof angeweze asiende, na Dr Makaidi vilevile. Au kama Zitto anawakilisha chama tawala labda, na agenda nini? Hauwezi ukasema uchaguzi wakati NEC haijaalikwa, hauwezi ukasema umoja katika vyama wakati ofisi ya msajili haijaalikwa. Nimeshangaa sana, nampingeza Dr. Slaa na chama chao kugundua hila hizo. Mungu yuko na wenyehaki.
 
Kwani umoja wa vyama vya upinzani Nigeria walitokea wangapi? Acha ushabiki usio na tija, demokrasia haipimwi kwa kuwa na wagombea wengi la hasha, Bali hupimwa kwa umoja, mshikamano, kuaminiana na kutegemeana kaka.
 
Zitto ni Mgombea Urais?Katiba inamruhusu?Huyo Mafuruki angeuita Mdahalo wa Wenyeviti wa vyama vya siasa labda ila sio Wagombea Urais,kama ni wagombea Urais Zitto hana sifa hizo kinachofanyika anataka kuleta fujo tu ndiyo maana wengi wanaamini Zitto anatumika,Hongera Dr Slaa kwa kukwepa Mshale.

Well spoken.
 
Slaa hajui uchumi ni nini lazima atoke nduki teh teh teh teh teh
 
Wadau tuseme tunayoyaishi Hakuna wa kumfananisha na ZZK katika siasa za hoja hapa Tanzania.Zitto anajua huwez kumfananisha na Mbulula Slaa.
 
Mwenye akili tinamu,huu aio mdahalo bali mazungumzo,hivyo Dr.slaa hawezi.Ccm wawaweke wagombea wao na Dr slaa wafanye mdahalo huo tuone lakini aio huu ambao unaleta watu
 
Kama amekimbia ujue huo ni woga wa kisiasa,halafu taarifa ya mdaharo hakuanao tangu zamani, maoni yangu ni kwamba kakimbia wachumi!
 
Huo sio mdahalo, yaani siku hizi kila mtu anaweza kuandaa midahalo? si walishafanya wa wagombea CCM na wote wakakataa mbona hamkusema? waliona sio standard, hawa wakina mfuruki wafanye mambo wanayoyaweza tangu lini wanafanya midahalo si wanafanyaga round table? kweli Tanzania nchi ya ajabu kwa hiyo leo hii kila mtu anaweza kufanya kila kitu wanachofanya wengine, Kwani yule mama anayefanyaga midahalo siku zote yuko wapi? au wamemuona hafai wao ndio wataweza? hivi nani anayeangalia hivyo vituko? acheni kuvamia fani aibu tena nimeona leo wamepewa headline na mwananchi kwa kuwa anakaa kwenye board, hivi hawa mwananchi wanasabu gani ya ku risk heshina ya gazeti lao kwa kuripoti kitu wanachojua kabisa hakitatokea kwa kuwa watu wao hawana uwezo wala historia ya kufanya hilo. yule mama nae ananiboa inamaana hafanyi midahalo tena? Sasa ndio nini hivi? 2010 mbona alifanyakazi kubwa? hii ndio shida ya watanzania hakuna consistence sasa wametokea makanjanja subiri uone
 
Hakuna mwenye uwezo wa kuanda midahalo kama yule mama Rosemary Mwakitwange na Tanzania Tunayoitaka, Watanzania tuache wivu usiokua na maendeleo na kuharibu ubunifu na juhudi za watu. hata wakina ITV walipoingilia kutaka kuiba kipindi kama walivyozoea waliumbuka, mpaka mzee wa watu Warioba akaaibishwa na Makonda, leo hii hakuna hata media inayofanyakazi kama ile tuliyoiona 2010, kwa nini tusiheshimu vipaji na kazi za watu na kuwatia moyo? sasa are you people in competition? Tazana sasa aibut tupu huhitaji kuwa mtaalamu kujua kuwa Mfuruki na vibaraka wake wamechemsha. watu wasivamie fani waache yule mama afanyemambo yake. tulifaidika 2010 kwa mara ya kwanza tuliwaona opposition wakiongea na tukawapigia kura, Mfuruki ulikua wapi? hawa watu wasifanye mchezo na michakato hii na wapigwe marufuku kabisa hata kuita hivi vitu mdahalo, hii siyo fani yako unafuata nini huku? hivi inakuwaje mambo hayana vigezo? au kwa kuwa fani ya uandishi wa habari imedharaulika kila mtu anaweza kuifanya. leo hii wakina Zembwela, mamiss sasa mdahalo sio kipindi cha michezo na sports, ni mambo ya sera za nchi na matarajio ya wananchi, tunaomba yafanywe na wanayoyaweza tu kwanza tayari tunauzoefu hatuhitaji makanjanja humu kama hamuamini mtaona kesho watakavyopata aibu tena na tena
 
Na huyo mfuruki naye hamnazo mdahalo wa wagombea wakati michakato ndani ya chama haijaisha wanakwenda akina nani?
 
Back
Top Bottom