Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa ameweka bayana kwamba chama hicho kikuu cha upinzani nchini hakitashiriki mdahalo wa wagombea Urais wa upinzani hapo kesho.

Kiongozi huyo aliyekuwa anasubiriwa na mamilioni ya Watanzania kwenye mdahalo huo ametoa sababu kubwa mbili kwa chama chake kutoshiriki...

Sababu ya kwanza ni kwamba CHADEMA bado haijampata mgombea Urais na mchakato wa ndani unaendelea.

Na sababu ya pili ni kwamba Ilani ya chama bado haijapitishwa na vikao vya juu vya chama hicho na itakuwa ni kichekesho kwenda kwenye midahalo bila kuwa na Ilani ya chama.

Dr Slaa amesema chama hicho kitakuwa tayari kushiriki midahalo ya aina hiyo mara taratibu za kumpata mgombea Urais zitakapokamilika ndani ya chama!

Amefanya uamuzi wa maana kwa sababu hii ingekipasua chama. Ingempa nafasi ya pekee kujipigia kampeni na wakuanyima wengine kwenye chama kujitangaza. Heko Dr. Slaa kwa kuliona hili.
 
CCM wameshafika zaidi ya 30, tuone kama CHADEMA baada ya Slaa atajitokeza mtu mwingine, akijitokeza unikate kidole.

kwa wanaoijua heshima ya nafasi ya urais wanatambua siyo kitu chepesichepesi kama CCM wanavyoona, ambako hata vibaka wanajitokeza!
 
Mkuu Ruttashobolwa nilikuambia lazima Dr.Slaa atoke nduki kwenye huu mdahalo.
 
Last edited by a moderator:
Safi Dr. Safi ukawa! Ninaimani na nyinyi, na nipo pamoja na watanzania wote walio tayari kwa mabadiliko, Mungu wa haki atutangulie.
 
Nilishauri CEORT wazingatie ratiba ndani ya vyama kabla ya kupanga ratiba yao

CCM wao wameruhusu wagombea wao waende sasa Lowassa na wenzake hawakua na sababu ya kuingia mtini
 
hao jamaa kabla ya kuandaa mdahalo wafanye utafiti kwanza midahalo inaandaliwaje hawa naona wanakurupuka ndio maana mdahalo wao wa kwanza haukufanyika nadhani Dr.Slaa ameona mtego huo kwani hata vigezo vya kuwaita hao watu hawakuweka kama ulikuwa ni wa viongozi wa vyama walipaswa waitwe vyama vyote au wagombea urais kupitia vyama vya upinzani navyojua Zitto hagombei urais kwanini wasimuite Mbatia
 
Mdahalo huo unalengo la kuwadhalilisha UKAWA

1. Zitto hana credibility za kupambanishwa na wakubwa tena walezi wake Kama Dr Slaa na Lipumba. Rejea usaliti wake na vurugu ndan ya cdm.Nin kipo nyuma ya pazia?

2. Kumkweza Zitto nakumlinganisha na akina Lipumba ni utovu wa nidham kwa waandalizi wa mdahalo huo.

3. Kwanini Zitto asishindanishwe na

-Lowasa
-Membe
-Magufuli
-Sumaye
-S. Sitta

kinachoendelea kwenye vichwa vya wandalizi wa mdahalo huo nikuchafua cv au kuzi-disvalue ionekane UKAWA ni ya watu wa low grade na hawafiti kwenye nafasi ya urais ambao niupumbavu Mkubwa.
 
we ni chizi na mngese ....hebu nambie huo mdahalo unahusu nini ? muandaaji mdahalo anatakiwa kujipanga upya ...mdahalo unahusu wagombea urais ...act nyie mshatangaza mogombea wenu ? kama angealika vyama ni sawa yeye anataja watu kushiriki kwenye mdahalo kabla hata ya kuuliza taratibu za vyama vyao vikoje asubiri vyama vitangaze wagombea then awaite aone kama kuna udhuru utatolewa....halafu huwezi kumuita zito umpambanishe na slaa hao hawako level moja ...zito saizi zake ni kina mnyika sio slaa wote wagombea ubunge...
 
Zitto ni msomi, lipumba msomi ila mzee wetu kichwa mchunga kazila kukusanywa na nguli hao.

Kama msomi mbona ccm hamchukua awe mgombea uraisi wenu wote waliotangaza nia ni mafisadi ndo maana hata walikimbia mdahalo ambao ulikuwa wa wagombea uraisi wa ccm pekee yao?
 
Last edited by a moderator:
Vyama vya Siasa vinakimbia midahalo.
 
Sasa wew unataka kusema nin , kwani makaidi, zitto wapi amesema anagomea uraisi

WEWE NI NDOROBO SANA, SLAA BADO SI MGOMBEA URAISI WALA HAJATIA NIA, BASI NAWEWE NENDA KASHIRIKI KAMA NI KUJIENDEA TU BILA TARATIBU, Ndorobo wewe
 
CCM waliconfirm kushiriki wakaingia mitini dakika za majeruhi tena bila taarifa.Hata hivyo Dr Slaa ataendaje kwenye mdahalo wa wagombea,kwani ameshatangaza nia kuwa ni mgombea? Hapo mwenye sifa ya kushiriki mdahalo ni Prof.Lipumba tu,ZZK hana sifa ya kushiriki kwa vile si mgombea.
Naunga mkono mkuu,-naye muandaji aache mapenzi binafsi Mpaka saa hii zzk Na Dr slaa hawana sifa za mdahalo huo, bw.mufuruki atulie wenye sifa watakuja tu
 
Back
Top Bottom