Dr. Slaa adaiwa kumwandikia meseji ya vitisho IGP

Amepatwa na ugonjwa wa kuweweseka maana anajua kuwa yeye ndiye anatakiwa kuachia ngazi.
He is diverting the truth for a short while.
It will backfire for sure

Hao ndio tunaambiwa viongozi vijana! worse than their parents if you ask me!
 
Ni kweli maneno hayo yote waziri kasema au mtoa mada kadondoshea chumvi kidogo?

Kama ni kweli, tatizo zito hapo.

Mkuu hakuna chumvi wala magadi. Fuatilia vyombo vya habari jioni hii utajionea kwa macho na kusikia kwa masikio yako mwenyewe.
 
anajidai kushangaa nini na wakati anajua kila kitu.

Anashangaa alafu anatufanya na sisi tunamshangaa. Hivi sm ya Dr Slaa ndio iliyomfanya yule askari akamuua mwandishi? Labda Nchimbi atusaidie tu tujue nani alimpa order yule askari ya kuua, na kwanini? Na kabla hajarukia kwenye majibu ya sm ya Dr Slaa labda atueleze hiyo SM ilitumwa baada ya matokeo/mazungumzo gani? Je nini hasa kilichomfanya Dr Slaa a-react kwa hiyo message. Na je wakati Mwema anapata hiyo message alimforwardia Nchimbi au Nchimbi alikuwa next to him au walikuwa wanapanga kitu fulani or what? Something is missing here......

 
Nchimbi anaugua ugonjwa gani? Hapo kwenye red it is obvious tayari ana conclusion sasa tume ya nini? Kwa nini anatumia kodi ya wananchi kufanya kazi ambayo tayari ana majibu?

kesho ukiamka utasikia mengine,,,,,na hukumu ikitoka ni kama ya zombe
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hao ndio tunaambiwa viongozi vijana! worse than their parents if you ask me!
This is really discouraging.
Vijana kushika dola bado sana,nafasi ya wazee bado ipo sana...
hatujaudhihirishia umma pasipo na shaka kama tupo trustworthy and reliable...
 
  • Thanks
Reactions: FJM
huwezi kuongea kuhusu mkuu wa polisi namna hiyo... lowassa siku zote anasema hii nchi haina uongozi hilo ndio tatizo kubwa la hapa kwetu...mheshimiwa ongea na beste wako aachie madaraka uchukue hii nchi haya matatizo yaishe...tunakoenda huko ni pabaya na wote tunajua hilo
 
Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameelezea kushangazwa kwake na ukimya wa mkuu wa jeshi la polisi nchini juu ya sakata la kuuwawa kwa mwandishi wa habari mkoani Iringa.

Waziri Nchimbi amedai kuwa siku moja kabla ya Chadema kufanya mikutano na ufunguzi wa ofisi za chama wilayani Mufindi Dr. Slaa alimtumia 'sms' mkuu huyo wa jeshi la polisi nchini akimtaka ampigie simu haraka pia vinginevyo aandae risasi za kutosha kwa ajili ya kuwaua kwani hawangekuwa tayari kuvumilia uonevu na ukandamizaji unaofanywa na jeshi lake.

Waziri Nchimbi anadai kitendo cha IGP kuendelea kukaa kimya bila kutoa tamko lolote kufuatia kifo cha Mwangosi siku moja baada ya kupokea 'sms' toka kwa Dr. Slaa, na kitendo cha jeshi la polisi kushindwa kumkamata Dr. Slaa kinamuonyesha kwamba yeye (IGP) ni dhaifu sana, ama hajui wajibu wake, na iwapo huko mbeleni Dr. Slaa atakuwa raisi wa nchi atampuuza na kumdharau sana.

MYTAKE:
Kauli ya Waziri Nchimbi dhidi ya IGP Mwema hadharani inaonyesha kuna kutokuelewana baina yao!?
Nadhani Mh Dr Nchimbi:
  1. hana taarifa kamili
  2. anakisasi na CDM juu ya kutokukubalika kwake songea
  3. anafanya makusudi (kama mpango wa serikali) ili ionekane CDM ni wakorofi
  4. hajui kuwa wananchi sasa hawatishiwi nyau!
  5. ni muhimu akaangalia picha kwanza za polisi walivyomshambulia marehemu ndiyo aseme kama kulikuwa na confrotation ya kumuingiza Dr Slaa.
  6. Mwema na Dr Slaa nadhani ni wahanga wa wanasiasa (mwema anapokea malekezo ya kisiasa ili amthibiti Dr Slaa)
Nadhani ili tego bovu la tear gas canister likuwa lielekezwe kwa Dr Slaa ila sema basi huyo dogo aliyelipua ilikuwa bahati mbaya.
Walio karibu na Dr Nchimbi wamshauri kuwa watanzania watamchukia zaidi kama ataendelea kuwa na moyo mgumu wa kushindwa kuelewa ushahidi wa macho.
 
Katika hali ya kushangaza ambayo haikutarajiwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Emmanuel Nchimbi amemuumbua mkuu wa jeshi la polisi nchini-IGP Said Mwema.

Waziri Nchimbi amesema usiku wa kuamkia Jumapili IGP Mwema alimpigia simu kumtaarifu kwamba Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa ameapa ni lazima chama chake kifanye mikutano ya hadhara na maandamano na kamwe hawatambui zuio la polisi.

Kama vile haitoshi IGP Said Mwema akafoward SMS aliyotumiwa na Dr Slaa kwa waziri Nchimbi kuthibitisha maneno yake. Lengo la IGP ni kuomba msaada wa waziri Emmanuel Nchimbi. Waziri Nchimbi ameonyesha Message hiyo kwa waandishi wa habari.

Kauli hiyo imethibitisha lawama za muda mrefu za CDM kwamba jeshi la polisi halifuati sheria katika kazi zake badala yake linafuata maelekezo ya wanasiasa.Ikumbukwe Waziri Nchimbi ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

Source: Chanel 10
 
Hizi sarakasi hizi. Serikali na polisi wasitafute mchawi! Kwa hiyo anavodai Dr slaa alisema aandae mabomu na risasi za kutosha naye alifanya kweli?
Mwema na Nchimbi mjue muda muda wa kudanganya umma haupo tena, na muone mnavoruka sarakasi huku mmevaa taulo mbele ya watoto.
 
Hizo zote ni porojo vitu muhimu ambavyo vinavyotakiwa kutolewa maelezo ni hivi vifuatavyo:-
1. Amemchukulia hatua gani RPC kwa kuto zuia kifo hicho wakati alikuwepo kwenye tukio na alipewa taarifa na mwandishi mmoja wa habari lakini aridharau?
2. Aliyeua na kujerui polisi mwenzie ni polisi na anajulikana je IGP amechukua hatua gani kwa huyo polisi hadi sasa?
3. Pia tulisikia kauli kwamba IGP alitakiwa awe amekwisha mkamata Dr.Slaa kwani kutokufanya hivyo ni udhaifu na iwapo Dr. Slaa atakuwa Rais hapo baadae atamdharau sana Said Mwema, kwa kauli hii inaonekana waziri moja kwa moja amekubaliana na kushindwa kwa CCM 2015
 
Hizo zote ni porojo vitu muhimu ambavyo vinavyotakiwa kutolewa maelezo ni hivi vifuatavyo:-
1. Amemchukulia hatua gani RPC kwa kuto zuia kifo hicho wakati alikuwepo kwenye tukio na alipewa taarifa na mwandishi mmoja wa habari lakini aridharau?
2. Aliyeua na kujerui polisi mwenzie ni polisi na anajulikana je IGP amechukua hatua gani kwa huyo polisi hadi sasa?
3. Pia tulisikia kauli kwamba IGP alitakiwa awe amekwisha mkamata Dr.Slaa kwani kutokufanya hivyo ni udhaifu na iwapo Dr. Slaa atakuwa Rais hapo baadae atamdharau sana Said Mwema, kwa kauli hii inaonekana waziri moja kwa moja amekubaliana na kushindwa kwa CCM 2015

Na kweli porojo nyingine ni vituko.
 
kauli ya nchimbi haikubaliki kabisa..yeye ndiye alitakiwa kujiuzuru kwanza kama alivyofanya Mzee Mwinyi wakati ule..
 
Enough is enough!!!na wakamkamate ili waone upepo wa watanganyika kama ni ule ule au umekuwa kimbunga sasa....tuna hasira sana na manyanyaso ya policcmagamba na shemeji zao wote.
 
Back
Top Bottom