Dr. Slaa adaiwa kumwandikia meseji ya vitisho IGP

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
SLAA AMTISHA IGP MWEMA


  • Atuma ujumbe, asisitiza kuvunja sheria
  • Mrema aja juu, CHADEMA inabebwa
  • UVCCM wamshukia John Tendwa.


Vurugu za CHADEMA mikoani zimechukua sura mpya, baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa, kumtumia ujumbe wa vitisho Mkuu wa Jeshi la polisi(IGP), Said Mwema.

Ujumbe huo uliotumwa kwa njia ya simu ya mkononi unamtaka IGP Mwema kuhakikisha askari wanakuwa na mabomu ya machozi, bunduki na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kupambana na wafuasi wa CHADEMA watakaokuwa wakifanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini.

Dr Slaa pia amesema iandaliwe karamu ya mauaji, kwa kuwa wafuasi wa CHADEMA wamejipanga kukabiliana na polisi wataksokuwa wakiwadhibiti.

Pia amemueleza IGP Mwema na askari wake wajiandae kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai (ICC), iliyoko The Hague, nchini Uholanzi.

Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, alisema hayo jana alipozungumza na gazeti hili kuhusu vurugu zilizotokea juzi, mkoani Iringa na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha chanel ten, Daudi Mwangosi.

Chagonja alinukuu ujumbe uliotumwa kwa IGP mwema uliosema "Wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha maana mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya The Hague"



Akizungumzia ujumbe huo, Chagonja alisema unaonyesha kiburi,ukaidi na kutotii sheria, hivyo jeshi la polisi litachunguza na kutoa taarifa kuhusu hatua zitakazochukuliwa.
 
...Ujumbe huo ni fake haukutoka kwa Dr Slaa. Bali umetoka mwa mhuni Mwigulu na wahuni wenzie wa magamba.


hahaha! Mkuu una hasiraaa! Anything is possible nae si mwanadamu tu? anaweza cheza hio faulo.
 
Hivi ule mtambo wa kutengeneza msg kwa kutumia simu za watu uliosemwa na Marando na unaomilikiwa na MTOTO WA KIGOGO umeshakamatwa?

By the way! Sioni vitisho katika msg hiyo.
 
...Ujumbe huo ni fake haukutoka kwa Dr Slaa. Bali umetoka mwa mhuni Mwigulu na wahuni wenzie wa magamba.

Mkuu BAK,
Uko sahihi. Huu ujumbe umetoka kwa majuha tu. Wanatapatapa ila mwisho wao umefika. Ila sasa ngoja upelekwe kunakistahili. Uchafu kama huu hauwezi kusumbua vichwa vyetu, GT.
 
Hivi ule mtambo wa kutengeneza msg kwa kutumia simu za watu uliosemwa na Marando na unaomilikiwa na MTOTO WA KIGOGO umeshakamatwa?

By the way! Sioni vitisho katika msg hiyo.
Ni kweli kabisa hakuna uhusiano na vitisho na kama hii kwao ni vitisho basi kweli wajiandae na mimi nipo tayari hata sasa hivi kuuawa kutetea nchi yangu dhidi ya ccm na polisi
 
Slaa ni mtu mdogo sana nchi hii, na hawezi kuitisha dola, mbona sasa kila siku anafyata mkia na kukubali kuahirisha maandamano na mikutano yake ? hapo yaonyesha huyu jamaa ni mwoga na ni maneno zaidi. Nakumbuka vurugu za arusha huyu slaa si ndie alikuwa amejificha kwenye maspika , sio huyu ?

kweli wajinga wali wao , dola haiwezi kutishwa na maneno hayo na watasimamia sheria. Yeye ajibu mauaji anayoyafanya kwa watu wasio na hatia, r.i.p mwagosi siasa za kina slaa zimekuponza
 
Ni kweli kabisa hakuna uhusiano na vitisho na kama hii kwao ni vitisho basi kweli wajiandae na mimi nipo tayari hata sasa hivi kuuawa kutetea nchi yangu dhidi ya ccm na polisi


Nenda kauwawe mkuu, mkeo na watoto usijali ntawalea mie uwezo ninao mkuu
 
Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameelezea kushangazwa kwake na ukimya wa mkuu wa jeshi la polisi nchini juu ya sakata la kuuwawa kwa mwandishi wa habari mkoani Iringa.

Waziri Nchimbi amedai kuwa siku moja kabla ya Chadema kufanya mikutano na ufunguzi wa ofisi za chama wilayani Mufindi Dr. Slaa alimtumia 'sms' mkuu huyo wa jeshi la polisi nchini akimtaka ampigie simu haraka pia vinginevyo aandae risasi za kutosha kwa ajili ya kuwaua kwani hawangekuwa tayari kuvumilia uonevu na ukandamizaji unaofanywa na jeshi lake.

Waziri Nchimbi anadai kitendo cha IGP kuendelea kukaa kimya bila kutoa tamko lolote kufuatia kifo cha Mwangosi siku moja baada ya kupokea 'sms' toka kwa Dr. Slaa, na kitendo cha jeshi la polisi kushindwa kumkamata Dr. Slaa kinamuonyesha kwamba yeye (IGP) ni dhaifu sana, ama hajui wajibu wake, na iwapo huko mbeleni Dr. Slaa atakuwa raisi wa nchi atampuuza na kumdharau sana.
Katika hali ya kushangaza ambayo haikutarajiwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Emmanuel Nchimbi amemuumbua mkuu wa jeshi la polisi nchini-IGP Said Mwema.

Waziri Nchimbi amesema usiku wa kuamkia Jumapili IGP Mwema alimpigia simu kumtaarifu kwamba Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa ameapa ni lazima chama chake kifanye mikutano ya hadhara na maandamano na kamwe hawatambui zuio la polisi.

Kama vile haitoshi IGP Said Mwema akafoward SMS aliyotumiwa na Dr Slaa kwa waziri Nchimbi kuthibitisha maneno yake. Lengo la IGP ni kuomba msaada wa waziri Emmanuel Nchimbi. Waziri Nchimbi ameonyesha Message hiyo kwa waandishi wa habari.

Kauli hiyo imethibitisha lawama za muda mrefu za CDM kwamba jeshi la polisi halifuati sheria katika kazi zake badala yake linafuata maelekezo ya wanasiasa.Ikumbukwe Waziri Nchimbi ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

Source: Chanel 10

MY TAKE:
Kauli ya Waziri Nchimbi dhidi ya IGP Mwema hadharani inaonyesha kuna kutokuelewana baina yao!?
 
IGP Mwema anateuliwa na Rais ambaye ni shemeji, na Dr. Nchimbi anateuliwa na Rais ambaye ni best friend na mkampeni wake mkuu 2005. Sasa ni nani zaidi kati ya hawa wawili? For a fair game, wote waondoke!!
 
Ngoja waanze kuparanganyika. Ajiuzulu basi ili IGP afuate njia maana ndivyo JK alivyosema wakati anatangaza Baraza lake hilo jipya.
 
mimi nahisi anajiosha kutokana na kauli yake aliyoitoa A/kusini kutofautiana na ya jeshi la polisi hivyo kujiondoa kuwajibishwa.MY TAKE : WAZIRI MCHIMBI KAMA ANABUSARA AJIUZURU.
 
Huyu hamtakii mema IGP , anataka awe wa kwanza kutangulia The Hague? Aanze yeye
 
Back
Top Bottom