Dr. Slaa adaiwa kumwandikia meseji ya vitisho IGP

Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameelezea kushangazwa kwake na ukimya wa mkuu wa jeshi la polisi nchini juu ya sakata la kuuwawa kwa mwandishi wa habari mkoani Iringa.

Waziri Nchimbi amedai kuwa siku moja kabla ya Chadema kufanya mikutano na ufunguzi wa ofisi za chama wilayani Mufindi Dr. Slaa alimtumia 'sms' mkuu huyo wa jeshi la polisi nchini akimtaka ampigie simu haraka pia vinginevyo aandae risasi za kutosha kwa ajili ya kuwaua kwani hawangekuwa tayari kuvumilia uonevu na ukandamizaji unaofanywa na jeshi lake.

Waziri Nchimbi anadai kitendo cha IGP kuendelea kukaa kimya bila kutoa tamko lolote kufuatia kifo cha Mwangosi siku moja baada ya kupokea 'sms' toka kwa Dr. Slaa, na kitendo cha jeshi la polisi kushindwa kumkamata Dr. Slaa kinamuonyesha kwamba yeye (IGP) ni dhaifu sana, ama hajui wajibu wake, na iwapo huko mbeleni Dr. Slaa atakuwa raisi wa nchi atampuuza na kumdharau sana.


MY TAKE:
Kauli ya Waziri Nchimbi dhidi ya IGP Mwema hadharani inaonyesha kuna kutokuelewana baina yao!?
inaonyesha jeshi hilo alifuati sheria na utashi wake bali kwa maelekezo kutoka juu wameumbuka! wameanika adharani tulilokuwa tukieleza kuwa vituko vya polisi ni vya ccm
 
Mkuu unamfahamu E Nchimbi yupi?
Leo waziri nchimbi kauthibitishia umma wa watanzania kwamba jeshi la polisi linafanya kazi kwa maelekezo ya wanasiasa.
It seems hapa maelekezo yao(wanasiasa wa ccm) hayakutekelezwa kikamilifu. Kwahiyo ameamua kutafuta political gain kupitia mauaji haya.


Ndiyo maana nashangaa mkuu....

Kwa mtu wa calibre ya E. Nchimbi, hii haikutakiwa kutoka kwake.........

Something is really wrong...!
 
mzee pole kwa msima, huo ni msiba wa kwetu sote...nasema hivi kwasababu sijaelewa ulichoandika nahisi unaomboleza kama sisi wengine tu.

kwa upande mwingine, kitu walichokifanya polisi hakitakiwi kuvumiliwa kabisa na umma wa watz, nitashangaa kama hatutaandaa maandamano ya amani kulaani kitendo hicho ili hata kama sisi hatutatoa hukumu (kwasababu mtoa hukumu ni Mungu pekee ndo anayejua kutoa kisasi barabara), umma wa watz, dunia nzima na selikali ijue kuwa watz tumesikitishwa sana na mauaji haya ya wazi bila hata sababu ya maana, na waache mara moja kufanya hivyo. wale waliofanya kitendo hicho tunataka ionekane wazi kabisa na watz wote kuwa wamekamatwa na kufikishwa mbele ya haki, viongozi waliotoa amri waadibishwa kwa kufukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani na watz tuone wazi...yaani haki isisemwe tu kwamba imetendeka, tuone kwa macho yetu haki ikitendeka juu ya wauaji hawa.mkutano ule ulikuwa wa watu wachache sana tena kijijini nyololo kule, very few people ambao walikuwa wanafungua tawi tu la chama.....sikuona kama kuna umuhimu wowote wa polisi kwenda pale kwasababu lisingetokea lolote lile...hivi polisi wasingeenda pale kingetokea chochote jamani wakati watu walikuwa wanafungua tawi? au polisi waliogopa kufungua tawi pale wanachama wa ccm watahama labda kwasababu kitu kipya yaani tawi la chadema limefunguliwa?....mambo gani haya jaman? tangu nizaliwa sijawahi kuona kifo kibaya kama alichokufa yule jamaa hapa tz...si ajali ya gari, ni mtutu wa polisi?...mtu yuko mikononi mwa polisi badala ya kumpeleka lock up kama ana kosa, mnampiga marurngu na mateke akiomba msaada mnamuweka chini halafu mnapiga bunduki ya bom, mkijua kabisa bom hilo huwa likilipuka linaua kama mtu yuko karibu au likilipukia mwilini mwa mtu...
 
Tatizo ni kuwa wapo watu wanafikiria kila kinachoamriwa na POlisi ni halali na hivyo mtu anapaswa kutii. Dhamira ya mwanadamu haimtumi kutii agizo au amri ambayo anajua si halali au ni ya kikandamizaji. Chagonja akija nyumbani kwako na kukuambia ruka ruka kichura utaruka kwa sababu amesimama na uniform yake na nyota zake mabegani? Well.. wapo watakaosema "ruka tu si polisi kaamuru"!!!

Dr. Slaa kasema kitu kilichowazi tu; agizo la polisi la kuzuia mikutano halikuwa halali. Sasa kama halikuwa halali kwanini kulitii?
 
Kuna mambo mawili ambayo nayadhania baada ya kauli iliyomtoka waziri Nchimbi kuhusiana na huo ujumbe aliousoma.
1. Binafsi ninahisi waziri kakurupu kutamka huo aliouita ujumbe wa Slaa(nikiwa na maana ni ujumbe pandikizi). Kwa ninavyofahamu maadili ya uongozi,sio rahisi kunyoosheana vidole mbele ya kadamnasi kwa minajili ya kujisafisha au kujipatia haki.

2. Ujumbe huo una mantiki ndani yake. Jaribu kujiuliza kwa nini ujumbe mzito kama huo umsababishe Inspekta Mwema kukaa kimya pasi kuchukua hatua zozote. Hapa nahisi ni kweli polisi walikuwa wamejiandaa kutekeleza hayo yaliyotukia na pengine kuna waliomtonya Slaa kabla.
 
Mie ni kati ya watu ambao nilikuwa na "Un decided vote" nikiwa sina mlengo!Lakini kwa ubabe huu nadhani nishajua kura yangu nitampa nani!
 
SLAA AMTISHA IGP MWEMA


  • Atuma ujumbe, asisitiza kuvunja sheria
  • Mrema aja juu, CHADEMA inabebwa
  • UVCCM wamshukia John Tendwa.


Vurugu za CHADEMA mikoani zimechukua sura mpya, baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa, kumtumia ujumbe wa vitisho Mkuu wa Jeshi la polisi(IGP), Said Mwema.

Ujumbe huo uliotumwa kwa njia ya simu ya mkononi unamtaka IGP Mwema kuhakikisha askari wanakuwa na mabomu ya machozi, bunduki na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kupambana na wafuasi wa CHADEMA watakaokuwa wakifanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini.

Dr Slaa pia amesema iandaliwe karamu ya mauaji, kwa kuwa wafuasi wa CHADEMA wamejipanga kukabiliana na polisi wataksokuwa wakiwadhibiti.

Pia amemueleza IGP Mwema na askari wake wajiandae kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai (ICC), iliyoko The Hague, nchini Uholanzi.

Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, alisema hayo jana alipozungumza na gazeti hili kuhusu vurugu zilizotokea juzi, mkoani Iringa na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha chanel ten, Daudi Mwangosi.

Chagonja alinukuu ujumbe uliotumwa kwa IGP mwema uliosema “Wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha maana mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya The Hague”



Akizungumzia ujumbe huo, Chagonja alisema unaonyesha kiburi,ukaidi na kutotii sheria, hivyo jeshi la polisi litachunguza na kutoa taarifa kuhusu hatua zitakazochukuliwa.

Kama Miraji Kikwete na Mwigullu Nchemba wamekuwa Dr. Slaa sawa kabisa!
Lakini kama ni Dr. Slaa huyu anayeijua sheria hapo imekula kwenu pamoja na huyo mpumbavu wenu wa wizara gani sijui ya ulinzi au ya ujambazi!
Ni tahira tu anaweza kutuma ujumbe wa kihuni namna hiyo!

endeleeni kuirahisishia chadema kuchukua madaraka ya nchi yetu
 
Sem 2708
Nimecheka sana hahaha, anakazi ya kuunganisha....hahaha
 
Tatizo ni kuwa wapo watu wanafikiria kila kinachoamriwa na POlisi ni halali na hivyo mtu anapaswa kutii. Dhamira ya mwanadamu haimtumi kutii agizo au amri ambayo anajua si halali au ni ya kikandamizaji. Chagonja akija nyumbani kwako na kukuambia ruka ruka kichura utaruka kwa sababu amesimama na uniform yake na nyota zake mabegani? Well.. wapo watakaosema "ruka tu si polisi kaamuru"!!!

Dr. Slaa kasema kitu kilichowazi tu; agizo la polisi la kuzuia mikutano halikuwa halali. Sasa kama halikuwa halali kwanini kulitii?

kweli mkuu.alafu mbona hii haikuwa siri! Dr Slaa aliwaeleza wanahabari kuwa IGP aliamua kupokea simu yake baada ya kumuandikia sms kali. Polisi wanachanganywa na wanasiasa tena hata madiwani tu wa ccm!
 
hao wapumbavu tuu sijaona mantiki ya ujumbe huo ni njia tu ya kujisafisha ili waonekane wema kwa watu ila Mungu ameshaamua kuwaumbua so its too late hakuna tena mtu atakaewaamini
 
Back
Top Bottom