Dr. Slaa adaiwa kumwandikia meseji ya vitisho IGP

Katika hali ya kushangaza ambayo haikutarajiwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Emmanuel Nchimbi amemuumbua mkuu wa jeshi la polisi nchini-IGP Said Mwema.
Waziri Nchimbi amesema usiku wa kuamkia Jumapili IGP Mwema alimpigia simu kumtaarifu kwamba Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa ameapa ni lazima chama chake kifanye mikutano ya hadhara na maandamano na kamwe hawatambui zuio la polisi.Kama vile haitoshi IGP Said Mwema akafoward SMS aliyotumiwa na Dr Slaa kwa waziri Nchimbi kuthibitisha maneno yake.Lengo la IGP ni kuomba msaada wa waziri Emmanuel Nchimbi.
Kauli hiyo imethibitisha lawama za muda mrefu za CDM kwamba jeshi la polisi halifuati sheria katika kazi zake badala yake linafuata maelekezo ya wanasiasa.Ikumbukwe Waziri Nchimbi ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

Source:Chanel 10

Kusoma alama za nyakati kwa watawala ni somo gumu sana. Daima wengi hawawezi kulifaulu.
 
Anafanya kazi kwa kutegemea kuambiwa kweli nchi ina viongozi mazezeta, mtu unaajiriwa kufanya kazi yako na sio kufata mtu fulani atasemaje, ina maana alikuwa hajui nini anachokifanya, huyu ndio tunamuita IGP,......
 
Waziri wa mambo ya ndani amesoma ujumbe wa simu ambao DR. Wilbroad Slaa Amemtumia IGP Mwema ujumbe unaomtaarifu kuwa aandae Askari, bunduki, na risasi za kutosha kwa ajili ya mauaji ya halaiki ya watu na wajiandae kwenda mahakama ya wahalifu ya kimataifa THE HAGUE! source news TBC1
 
AHADI YA 'UWAZIRI MKUU' KWA MWANACHADEMA ITAUA WENGI HADI KUNAKOFIKA 2015:
KIFO CHA DAUDI MWANGOSI KULE KIJIJI CHA NYOLOLO MKOANI IRINGA NI KWAMBA KIJANA KANASA KWENYE MTEGO SI WAKE


Mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, afia msalaba si wake kwa kuchinjwa kinyama kwa kuwa tu moyo wake ulimtuma kutetea kile chenye maslahi kwa taifa dhidi ya maslahi ya CCM wilayani Mufindi.

Mauaji haya wenye ukatili mkubwa na kudhalilisha utu wa Mtanzania kule katika kijiji cha Nyololo wala hayakutokea tu kama ajali bali ukweli wa mambo ni kwamba dhamira hii ilifahamika masaa 48 kabla ya zoezi la CHADEMA kwenda kufungua mashina ya kichama wilayani hapo. Swala kwamba polisi wanafanya maandalizi kwenda kuua Mufindi ni jambo lililoenea kwingi kwa zaidi ya asilimia 70 ya watu wa Mkoa wa Iringa isipokua undani wa akina nani wanaenda kuuaua na kwa mtindo gani pekee ndicho kilichobakia siri kuu kwa jeshi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa nyeti tulizonazo toka nyuma ya pazia, mhanga Daudi Mwangozi, kilichomuua ni kule kugundulika kuingiwa moyo wa upendo na kuamua kutahadharisha mapema na taarifa nyeti kuokoa MASLAHI YA UMMA mauaji ya kutisha yaliopangwa na nguvu zilizodhamiria kutetea CCM kwa gharama yoyote ile dhidi ya uongozi wa juu CHADEMA walioko mkoani hapo kwa ziara ya kikazi.

Ndugu yetu Mwangosi ambaye alifika mapema katika eneo la kazi pale kijiji cha Nyololo na kuonekana kubadilishana utani na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA, wala hakua hataa na chembe cha taarifa kwamba umati wote uliokusanyika mahali pale majuzi ulikua ni wa kumhudhurisha yeye katika harusi ( harusi nyinginezo katika maisha ni kule kuzaliwa na pili kuoa au kuolewa) yake ya mwisho katika maisha.

Siku zote wakati ukuta, wahenga husema, muda wa Malika Israeli kuchukua roho ya Mwangosi ulipowadia, mwenzetu alimaziza hatua zote za kutendewa haki kikatiba kwa maana ya kwamba ndani ya kitu kipindi cha wastani wa dakika kama 35 hivi kijana mwenzetu alishakutana na (1) polisi waliomnasa kwa kosa ambalo jamii ya Tanzania bado inasubiri kufahamishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na jeshi lake, (2) akaswekwa rumande ndani ya dakika 5 tangu akamatwe, (3) dakika ya 21 tayari Mkurugenzi wa Mashitaka nchini alikwishaandaa faili yake kule Dar es Salaam na kuirudisha Iringa kwa (4) hakimu Kamuhanda (mdogo wake Seth Kamuhanda wa Ikulu) tayari kwa kutoa hukumu juu ya hatima ya kijana Daudi sawasawa na mapenzi ya makao makuu nchini.

WaTanzania wenzangu, hukumu ya kifo kilopotolewa na Kamanda Kamuhanda kupitia kwenye radio call pale kwenye gari la umma lililokua limeegeshwa pembeni kidogo tu kutoka machinjioni Nyololo, kijana mmoja kati ya vijana watatu wa 'vikosi maalum' nchini waliopelekwa Iringa siku tatu tu kwa shughuli maalum ndiye aliyetekeleza agizo la Kamuhanda tena kwa ufundi wa hali ya juu iliowaduaza hata vijana chipukizi kwenye jeshi la FFU pale Iringa.

Ndio, ukweli wa mambo ni kwamba huyu kijana mwenzetu Daudi Mwangosi kamwe hakunyimwa haki ya kusikilizwa na jeshi makini chini ya mzalendo namba 6 kitaifa kwa viwango vya CCM Chamwino, Saed Mwema, kama katiba inavyoelekeza kwa mtuhumiwa wa kosa lolote lile, bwana huyu hakunyimwa muda wa kuita mwanasheria wake kuja kumtetea dhidi ya hii nguvu kubwa yenye maelekezo moja tu; maslahi ya CCM kwanza, maslahii ya taifa itategemea na hali itakavyoruhusu.

Naam, nasema kwamba si siri kwamba Mwangozi hakunyimwa haki ya kuwaaga marafiki zake hata Ken Simbaya analitambua hilo, hakunyimwaa haki ya kuwaaga wazazi na familia zima kwa maana kwamba mzazi wake wa Magogoni alionekana kumpenda zaidi kitaifa.

Ukweli wa mambo ni kwamba mwenzetu Daudi Mwangosi kimsingi aliruhusiwa na hakimu Kamuhanda kutekeleza mambo mengi sana tu ndani ya kipindi hicho cha dakika 35 isipokua tu ni kwamba ilimezwa na zile za jopo lililokua likimsafirisha toka hapa duniani kwenda ulimwengu mwingine huko ahera.

Hakika baadhi ya chipukizi hawa walionekana wazi kutokuamini macho yao jinsi gani kijana mwenzao Daudi Mwangosi waliomuona chini ya dakika 15 zilizopita akiwa amependeza ajabu na kitendea kazi yake begani (kamera) jinsi gani alivyogeuka rundo tu la nyama mahali pale.

Kwa taarifa tulizo nazo hadi hivi sasa, baadhi ya hawa vijana wanahali mbaya mno kisaikolojia tangu siku waaliporejea mjini Iringa wakitokea kwenye hiyo kazi nyeti Mafinga, mji mdogo nje kidogo ya Iringa lakini yote juu ya yote WaTanzania wengi bado wanaendelea kutanabahi juu ya nini hasa kilichomfikisha huyu mwenzetu mahali hapo.

Sote tunajua kwamba tangu CHADEMA kiamue kwamba utani wa kuwa chama cha uchaguzi au cha msimu ndio basi tena, ni ukweli kwamba viongozi wa CCM hawajakaa wapate kufahamu kitu amani moyoni wala kule kujistarehesha kitu kwa kiburi cha kobe kugoma kutembea pindi aguswapo isipokua mambo ni mchakamchaka ulimi nje afadhali ya siku jana kwao kisiasa nchini.

Katika hali ya kuonyesha hayo mafanikio makubwa na kuendelea kukubalika kwa chama cha upinzani nchini hakika linaonekana kuleta tabasamu na nuru ya maisha iliopotea miaka mingi tangu Mwalimu Nyerere, kiongozi pekee aliyewadekeza sana wananchi wa taifa hili, atutoke.

Licha ya msururu huo mrefu wa mafanikio kwa CHADEMA, mtazamo kwa upande wa pili ni huzuni kuu kuona CDM kuonyesha kukubalika kupindukia kila kukicha tayari kumesababisha songombingo si tu katika kundi la wanasiasa wa kambi ya chama tawala bali pia kwa theluthi ndogo ya wanasiasa chipukizi ndani ya CHADEMA yenyewe ambayo nayo inajitafsiri kuumizwa sana kisiasa na mafanikio haya ya tangu kuzaliwa mtoto 'Movement for Change (M4C)' ambayo kila siku wanaonekana kulipiga chenga kutokushiriki shughuli zake lakini bila mtu yeyote kuhisi utupu wowote wa uhiari wao huu kutokujipanga wazi wazi na jeshi la kisiasa la chama chao ambacho hivi sasa ni lulu kwa zaidi ya 70 % ya wapiga kura nchini.

Naam, ni siri ilio nje kabisa kwa Wana-CHADEMA walio wengi kwamba ni hili hili kundi dogo la baadhi ya wanasiasa chipukizi na wenye kuegemea udini wanaojihisi kwamba wao hawana chao katika mafanikio haya makubwa CHADEMA, hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba kiota chao cha kutingishia kiberiti cha udini tayari kilishasambaratishwa na CDM mara baada kuingiza chamani jopo kubwa la wanachama mali zaidi, waaminifu zaidi na mahiri zaidi kwenye michepuo yao ya kitaaluma na kuheshimika sana kijamii, ambao ndio hivi sasa wameamua kuunda umoja na kundi mojawapo kati ya vikundi kibao ndani ya CCM kujaribu kutupa karata yao ya mwisho kabla ya kuinua rasmi mikono yao juu mbele ya nguvu ya umma wa Tanzania.

Kama mtu atakua anadhani kwamba usemi kwamba 'hofu kuu na kiwewe humgeuza hata simba kuwa paka' ulikosewa basi kwa taarifa yako utakua umekosea sana tena ajabu. Mbali na CDM kuonekana kuwa ni tishio la uhakika kuendelea kwa utawala wa CCM kwa zaidi ya miongo 4 hivi sasa, mafanikio yake makubwa ya kufungua utitiri wa matawi kila kona ya dunia, kukubalika zaidi huko na hata kupewa michango mikubwa mikubwa ki-hali na mali ndio kabisaaaa kimeingiza hofu kuu ndani ya CCM vikundi vyake vyote nchini na hata kuamuliwa kufanyika kwa msururu wa vikao ndni na nje ya nchi kutafakari kwa pamoja NINI KIFANYIKE KWA KIWANGO MITHILI YA BIG BANG / AU GAME CHANGER ili kuzuia CHADEMA kukamata dola kiulaini kiasi hiki.

Naam, ni hiyo hiyo hofu kuu na kiwewe cha ajabu kisiasa nchini kufuatia mabadiliko kisiasa kwa kasi mwangwi wa sauti inayofanywa na CHADEMA na washirika wake nchini na kiwewe chake ndio cha kile kilichowasukuma baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu CCM kufanya vikao vya siri kibao na kisha kuamua BORA LAWAMA KULIKO FEDHEHA inayokisubiri chama hiki kwenye sanduku la kura miaka michache ijayo.

Lengo la kumsambaratisha mwili mwandishi huyu ilikua ni KUTIA HOFU UMMA WA TANZANIA kwa kuwa hiyo SILAHA YA HOFU NA KUTOKUJIAMINI ni silaha iliokilea vema CCM kukalia madaraka kwa zaidi ya miongo 4 hivi sasa bila mtu yeyote kupaza sauti juu ya kitu haki lakini kwa programu ya elimu ya uraia inayoendeshwa kote nchini na asasi zisizo za kiserikali na pia CHADEMA tena kwa mafanikio makubwa hadi vijijini, wana-Chimwaga kwa tathmini yao hivi majuzi wakuja kubaini kwamba wananchi, kwa viwango vya juu sana kiminyanyaso wamefikia mahala hawana hofu tena na serikali ya CCM pamoja vyombo vya dola vinavyotumika kiitikadi zaidi.

Lengo la pili lililofanya NEC-CCM alioongoza rais Kikwete kwa notisi ya dharura Majuzi mjini Dodoma kuamua kufanya msururu wa mauaji kila CDM wanakofanyia mkutano wa kisiasa ni kule kutafuta kukishawishi chama hiki cha upinzani kukubali kuingia kwenye laini ya kufanya vurugu ili CCM kiweze kupata urahisi na kisingizio cha kuwadhibiti barabara na zaidi kuwaua baadhi ya viongozi tumainio na wenye msimamo usioyumba kwenye chama hicho.

Itakumbukwa kwamba CDM wamejitahidi sana kukinyima nafasi hiyo CCM hivyo chama tawala kushindwa pakuweza kufaidi kutumia nguvu za dola kwa faida yao kukidhibiti wahasimu wao. Ni kweli kwamba wengi wetu wahatambui jinsi gani silaha hii ya CDM kujichagulia KUTOKUKUMBATIA VURUGU, hata kichokozwe na kuchokonolewa vipi, ilivyochangia sana tena sana kukiimarisha chama hiki na kukidhoofisha maradufu CCM angali anazo na silaha za kivita zilizoagizwa toka Iran na bila kusajiliwa popote. Katika hili la silaha ni faraja kubwa kwamba tayari Jumuia ya Kimataifa inakaribia sana kufanya jambo humo.

Kwa kuahirisha tu taarifa hii juu ya kifo cha Mwangosi kwa msalaba wa wengine, ni muhimu kudokezea tu japo ki
dogo kwamba maandalizi kutekeleza mauaji ya kisiasa kule Mufindi wala ilifanyika kwa hisani ya Mwana-CDM aliyeinya uia kuona viongozi wake wa juu wakiuaua ili ndoto ya ahadi ya Uwaziri Mkuu uweze kutimia kwa uhakika zaidi mnamo 2015.

Kwa taarifa tulizo nazo hata hivi sasa kuna baadhi ya taarifa za chama na nyingine nyingi zikiwa ni za kupika zinaendelea kujadiliwa na kuwekewa mikakati hivi sasa nje. Haya yote ni sehemu ya maandalizi kambambe vikao vya siri vilichofanyikia mjini Dar es Salaam wiki moja Kamanda Lema alipokua Ulaya, baadaye kukafanyika nyingine Dodoma kabla ya kikao cha dharura cha NEC-CCM, na sasa sehemu nyingine ikiendelea kule Adis Abbaba Ethiopia.

Mungu aziweke roho za Ally (Morogoro) na Daudi (Iringa) mahala pema peponi huku tukiendelea kufunga kwa sala kwa ajili ya na wale wengine wengi ambao CCM tayari kinainuia kuwapunja haki ya kuishi na uhuru wa maoni kwa kutetea maslahi binafsi na mabilioni yaliofichwa Uswisi.

Wapenda mabadiliko wote, mapambano mbeeeeele kama tai mpaka CCM na mafisadi wake wote hata wale waliojificha ndani ya vyama vya upinzani wote kung'olewa madarakani kwa nguvu ya kura zetu kwa pamoja.

Picha hizi mbili zote ni matukio yaliyojiri tar 2.9.12. Wakati yanatokea Serikali ilikuwa imetoa wito wa kusitisha mikutano ya siasa kwa ajili ya shughuli ya sensa, sasa walikuwa wanamaanisha CCM hawahusiki nalo? Mbona hao polisi hawakusambaratisha mkutano huo? CDM walikuwa wanafungua matawi wakati CCM walikuwa wanafanya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi.

12.jpg
 
Si ndio mabwana zake? Lazima awalambe miguu.
Hili mh. Tundu Lisu alisha waambia huwezi kuwa mjumbe wa kamati za siasa then ukawa mtumishi wa serekali ni kinyume na katiba ya jamhuri ya muungano wakawa wanabisha sasa hii imedhihirisha kuwa ni kweli jeshi letu linatumika kisiasa hapa nchimbi nae akamatwe, Pia nchimbi nae aseme baada ya kutumiwa hiyo sms na IGP aliamuru nini? hii pia inamuweka hatiani kua aliamrisha mauaji ama la alikaa kimya bila kutumia njia mbadala kuweza kutatua tataizo hili na hii ni kwa maslahi ya chama chake na si kuwatumikia watanzania bila kujali itkadi zao nae pia akamtwe
 
Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameelezea kushangazwa kwake na ukimya wa mkuu wa jeshi la polisi nchini juu ya sakata la kuuwawa kwa mwandishi wa habari mkoani Iringa.

Waziri Nchimbi amedai kuwa siku moja kabla ya Chadema kufanya mikutano na ufunguzi wa ofisi za chama wilayani Mufindi Dr. Slaa alimtumia 'sms' mkuu huyo wa jeshi la polisi nchini akimtaka ampigie simu haraka pia vinginevyo aandae risasi za kutosha kwa ajili ya kuwaua kwani hawangekuwa tayari kuvumilia uonevu na ukandamizaji unaofanywa na jeshi lake.

Waziri Nchimbi anadai kitendo cha IGP kuendelea kukaa kimya bila kutoa tamko lolote kufuatia kifo cha Mwangosi siku moja baada ya kupokea 'sms' toka kwa Dr. Slaa, na kitendo cha jeshi la polisi kushindwa kumkamata Dr. Slaa kinamuonyesha kwamba yeye (IGP) ni dhaifu sana, ama hajui wajibu wake, na iwapo huko mbeleni Dr. Slaa atakuwa raisi wa nchi atampuuza na kumdharau sana.


MY TAKE:
Kauli ya Waziri Nchimbi dhidi ya IGP Mwema hadharani inaonyesha kuna kutokuelewana baina yao!?
Mwita, Mwenyezi hana mchezo.Walizoea kufanya udanganyifu mochuari na kutupa taarifa za kupika.
Leo Mungu kaweka wazi kila kitu, hawana pa kushika, hawana utetezi.
Kinachotokea ni kuweweseka, kila mtu alijaribu kukamata ubua maji yasimsombe.

Tunasema Nchimbi na Mwema waondoke kwanza kabla ya uchunguzi wowote.
Kuwepo kwao tu ofisini kunaingilia uchunguzi. Na uchunguzi ufanyike genge la mauaji likiwa magereza.
Genge linajulikana kwa majina na sura,wameonekana wakipiga na kushangaa kilichotokea.

Nchimbi and Mwema out!
 
Itafika mahali usalama wa familia za polisi utakuwa mashakani. Uvumilivu utakapoisha na watu watakaposema sasa kufa basi, jino kwa jino ndipo watakapoelewa kwamba kila mtu ana mikono ya kuweza kutoa roho ya mwingine na si wao pekee ndio wenye uwezo huo. NIMEMALIZA.
 
Slaa tunakomba wewe Josephine na Junior kwenye kuzigawana hizo risasi za IGP.
 
Nani awaaamini wauaji wa raia wasio na hatia! ccm bado wanapropaganda za kizamani
 
Mtambo wa mwigulu alonunua yerusalemu umeanza kazi zake. Dr. Slaa ni mtu makini hawezi kucheza kipuuzi hivi kama ishu ya kumtesa ulimboka.
 
slaa tunakomba wewe josephine na junior kwenye kuzigawana hizo risasi za igp.

acha hizo brother! Ningekutusi tusi kubwa kuliko yote ila nishachoka na ban za hapa! Kwahiyo wewe unafurahia mtu kuuwawa kikatili sio? Na-guess tommorow atauwawa mtu wako wa karibu ndio utajua nini ni nini! Atauwawa baba yako au mama yako au mwanao au mkeo na polisi tuone kama utashabikia kama hivi!
 
Mwita, Mwenyezi hana mchezo.Walizoea kufanya udanganyifu mochuari na kutupa taarifa za kupika.
Leo Mungu kaweka wazi kila kitu, hawana pa kushika, hawana uetetezi.
Kinachotokea ni kuweweseka, kila mtu alijaribu kukamata ubua maji yasimsombe.

Tunasema Nchimbi na Mwema waondoke kwanza kabla ya uchunguzi wowote.
Kuwepo kwao tu ofisini kunaingilia uchunguzi. Na uchunguzi ufanyike genge la mauaji likiwa magereza.
Genge linajulikana kwa majina na sura,wameonekana wakipiga na kushangaa kilichotokea.

Nchimbi and Mwema out!

Mkuu ninachojiuliza hapa itakuwaje kama IGP Mwema ataamua kujibu mapigo? Je kuna athari gani kwa upande wake akikaa kimya?
 
wote wawili wameparaganyika tu kuvichwa.


Hapa sijaelewa kitu,

Naona bora IGP Mwema ambaye amekaa kimya. Kukaa kimya kwa watu wazima, wenye busara zao wanaelewa tu kuliko kuongea na kuchafua hali hewa!

Anyway, huyu siyo E Nchimbi ninayemfahamu!!
 
naona kila mtu anatetea kibarua chake! lakini polisi kuua kwa makusudi bado kupo palepale so wote wawajibike kwa kuua kwa makusudi. No more blah blah
 
Hapa sijaelewa kitu,

Naona bora IGP Mwema ambaye amekaa kimya. Kukaa kimya kwa watu wazima, wenye busara zao wanaelewa tu kuliko kuongea na kuchafua hali hewa!

Anyway, huyu siyo E Nchimbi ninayemfahamu!!

Mkuu unamfahamu E Nchimbi yupi?
Leo waziri nchimbi kauthibitishia umma wa watanzania kwamba jeshi la polisi linafanya kazi kwa maelekezo ya wanasiasa.
It seems hapa maelekezo yao(wanasiasa wa ccm) hayakutekelezwa kikamilifu. Kwahiyo ameamua kutafuta political gain kupitia mauaji haya.
 
Kama kawaida wamerudia mchezo wao wa kutumia sms spoofing kudanganya uma eti DR.SLAA kamtumia nchibi na IGP sms ya vitisho na mwisho imeandikwa mimi DR.SLAA. uwezo wa kufikiri kwa hii govt umefika kikomo wanakaribia kukata roho. mtandao wa simu uliopitisha hiyo sms ubainishe kama ni kweli. hovyooo... vijana tunajua IT mpaka kumoyo ndo mdanganye uma. na kwa taarifa yenu nimeanza kuwafundisha hata wasiojua kusoma jinsi hizo sms zinavyoandaliwa mtakoma kutemper na vijana. go to hell wahusika wote
 
Kama kawaida wamerudia mchezo wao wa kutumia sms spoofing kudanganya uma eti DR.SLAA kamtumia nchibi na IGP sms ya vitisho na mwisho imeandikwa mimi DR.SLAA. uwezo wa kufikiri kwa hii govt umefika kikomo wanakaribia kukata roho. mtandao wa simu uliopitisha hiyo sms ubainishe kama ni kweli. hovyooo... vijana tunajua IT mpaka kumoyo ndo mdanganye uma. na kwa taarifa yenu nimeanza kuwafundisha hata wasiojua kusoma jinsi hizo sms zinavyoandaliwa mtakoma kutemper na vijana. go to hell wahusika wote

Hujasomeka mkuu...
 
Back
Top Bottom