Wanabodi,
Nimetafakari kidogo bila majibu kwa nini Serikali, baadhi ya Usalama wa Taifa na baadhi ya Wakuu ndani ya CCM wanakuwa wanafiki kiasi hiki juu ya wagombea watarajiwa ambao tayari wamepanga timu zao za maandalizi.
Kwa walio karibu na "corridor of power" hakuna asiyejua state inavyomuandaa John Emmanuel Nchimbi kama mteule mpya wa Mkuu wa Kaya kumrithi pale Magogoni. Mipango yake na harakati zote zinaratibiwa na State. Lowassa anajua, Pinda anajua, Membe anajua na wengine tumepata kujua. Sasa kwa nini kila kukicha wapambe wameng'ang'ana na Lowassa tu kama vile wengine hawafanyi?
Binafsi simaini kama kuna mtu anatarajia kufanikisha jambo lolote maishani bila maandalizi, mikakati na jitihada. Hawa wanaowaandaliawengine ufalme kwa nini hawataki kuona wala kusikia wengine wenye Uwezo wa kujiandalia wakifanya hivyo? Miujiza huonekana kama vitu vitokeavyo bila kutarajiwa lakini nayo ili mtu imtokee lazima afanye maandalizi i.e kutubu, kujitakasa, na kusali kwa imani. Kwa nini hawa "wenye mteule wao mfukoni" hawataki kusikia wenye uwezo wakijiandaa?
Kuanzia sasa nami natangaza kujiunga na timu Lowassa ili nikajue kwa nini anahofiwa kuliko wengine wote.