Dr. Nchimbi na urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Nchimbi na urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanda2, Sep 27, 2009.

 1. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  [​IMG][​IMG]• Malecela, Dk. Salim, Prof. Mwandosya wajeruhiwa

  na Mwandishi Wetu


  [​IMG]
  NAFASI ya kuwania kiti cha urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivi sasa inaonekana kuzusha balaa yenye kuogopwa na wagombea mbalimbali, kutokana na kuzingirwa na mbinu chafu zenye kudhalilisha kwa kila mwenye kuiwania.

  Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili unaonyesha kwamba, baadhi ya hoja nzito za hivi sasa zinazohusisha baadhi ya wanasiasa na harakati za kugombea urais ndani ya CCM ama 2010 au 2015, zinatoa mwelekeo ule ule wa kuchaguana na kuchafuana kama ilivyokuwa mwaka 2005.

  Majeruhi wa kwanza wa siasa hizo safari hii ni aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ambaye jina lake limekuwa likihusishwa na harakati hizo kutaka urais.

  Lowassa mwenyewe katika mahojiano aliyofanya na gazeti dada la hili, alihusisha hoja hizo juu yake kuwa sehemu ya mkakati wa watu ambao hakuwataja, wa kumkosanisha na Rais Kikwete.

  Wachambuzi wengine wa mambo wanasema kwamba kusukwasukwa kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta nako kunahusishwa kwa namna moja au nyingine na harakati za urais ndani na nje ya chama hicho.

  Ingawa wana CCM wamekuwa wakikubaliana kuwa mwaka 2010, Rais Kikwete ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuendelea kugombea kwa tiketi ya chama chake, hali inaonekana kuwa tofauti na kinyang'anyiro cha mwaka 2015, ambapo majina kadhaa makubwa yamekuwa yakitajwa.

  Miongoni mwa wanaohusishwa na kusaka urais mwaka 2015 ni pamoja na Lowassa, Sitta, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha - Rose Migiro na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emmanuel Nchimbi.

  Hofu hiyo pia imewakumba baadhi ya vigogo waliowania kiti hicho mwaka 2005, ambao sasa wameonekana kuwa kimya zaidi huku wakisisitiza kutotaka kusikia au kukumbushwa yale yaliyowakuta katika mchakato huo uliowafanya wachafuke katika jamii kiasi cha kusababisha makovu yasiyofutika.

  "Bwana mdogo nisingependa uniulize kuhusu kuwania urais, kilichonipata mwaka 2005 siwezi kukisahau, urais ni tishio, sitaki kujihusisha nao tena," alisema mmoja wa aliyewahi kugombea nafasi hiyo alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima Jumapili.

  Baadhi ya wanachama wa CCM waliozungumza na gazeti hili wamebainisha matukio ya udhalilishaji na vitisho walivyofanyiwa wagombea waliowahi kujitokeza kuwania kiti hicho, ndiyo yanayowafanya waione nafasi hiyo mwiba.

  Hofu hiyo inachagizwa zaidi na mambo yaliyofanyika katika Uchaguzi Mkuu uliopita, ambapo Dk. Salim Ahmed Salim, aliyekuwa mmoja wa waliokuwa wakiwania nafasi hiyo alipozushiwa mambo kadhaa, ikiwamo kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa Rais wa Zanzibar, hayati Abeid Aman Karume.

  Dk. Salim pia aliambiwa si raia wa Tanzania (Mwarabu), pamoja na kuwa mwanachama wa Chama cha Hizbu ambacho kilikuwa kikiutambua utawala wa sultani visiwani Zanzibar, hivyo kuhusishwa moja kwa moja na Waarabu.

  Kashfa hizo kwa kiasi kikubwa zilichangia kuharibu sifa ya Dk. Salim ndani na nje ya CCM, hivyo kujikuta akikosa kutimiza ndoto yake ya kuwania kiti hicho ambacho kwa wakati huo kilikuwa na upinzani mkubwa ndani ya CCM.

  Baada ya kukumbwa na tuhuma hizo, Dk. Salim aliweka bayana wazi kuumia kwake na kutoridhishwa na mbinu chafu zilizokuwa zikitumiwa na washindani wake, hasa kundi la wanamtandao, kwa kumzushia mambo yenye kumhatarishia maisha yake, pamoja na kupandikiza chuki kwa Wazanzibari na familia ya Karume.

  Mgombea mwingine ambaye alionja adha ya kuwania urais ni aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, ambaye naye kupitia vyombo vya habari alianikwa kumiliki akaunti yenye zaidi ya sh trilioni tano nje ya nchi.

  Sumaye alionekana kushtushwa na habari hizo pasipo kujua ni mkakati kabambe wa kumchafulia jina lake ili asiweze kupitishwa na vikao vya juu vya chama hicho kuwa mgombea urais.

  Kiongozi huyo pia alishutumiwa kumiliki mashamba makubwa kwa njia zinazotiliwa shaka katika Kijiji cha Kibaigwa, wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma.

  Tuhuma hizo zilimfanya kiongozi huyo mstaafu kukwaa kisiki katika mchakato huo huku akiendelea kuugulia majereha aliyoachiwa na wanamtandao waliodhamiria kumuingiza Rais Jakya Kikwete, Ikulu pasipo kuangalia madhara ya mbinu zisizofaa walizokuwa wakizitumia.
  John Samwel Malecela, ni miongoni mwa majeruhi wa wanamtandao katika kinyang'anyiro cha urais, ambapo katika pilikapilika hizo alizushiwa maneno kadhaa, ikiwamo uhusiano wake na nchi za Kiarabu, ambazo zilikuwa zikimsaidia kifedha.

  Katika lengo hilo hilo la kumchafua Malecela, alihusishwa kutokuwa na uwezo wa kukikalia kiti hicho kutokana na umri wake kuwa mkubwa, tofauti na Kikwete ambaye alipambwa kwa nyimbo za kuwa ni kijana na mwenye kufanya kazi kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya.

  Wakati propaganda hizo na mambo mengine yakiendelea, Malecela alijitokeza na kudai kuwa mbinu zinazotumika si za kiungwana, huku akiwaponda wale wanamuona mzee huyo hafai kuongoza, kwa kuwaambia kuwa kiti cha urais si kwa watu wenye nguvu za kubeba zege, bali huhitaji busara, utulivu wa mhusika pamoja na kuzungukwa na watendaji imara.
  Wachambuzi wa masuala ya siasa waliziona mbinu za wanamtandao zilikuwa mbaya na zisizofaa katika medani ya siasa, kwa kuwa zililenga kuchafua majina ya watu na kupandikiza chuki ambazo mwisho wake ni kukigawa chama na wananchi.

  Wakati wanasiasa waliojitokeza kuwania urais wakishughulikiwa kwa stahili hizo mwaka 2005, Lowassa anatajwa kuwa na ushawishi mkubwa ndani na nje ya CCM iwapo atasimama kugombea nafasi hiyo mwaka 2015.

  Pamoja na ushawishi huo unaoelezwa kuwa anao Lawassa, bado atakabiliana na wakati mgumu dhidi ya Membe ambaye ameshaanza kupigiwa chapuo ya kuwania kiti hicho Dk. Asha -Rose Migiro naye anaweza kutoa changamoto kubwa katika kinyang'anyiro hicho hasa kutokana na uwezo wake wa kuongoza Umoja wa Mataifa.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa wanabashiri Migiro anaweza kupata wakati mzuri kwa kuwa baadhi ya watu hivi sasa wangependa kuona mageuzi kwa nchi kuongozwa na rais wa kike mwanamke kama ilivyo Liberia. Wachambuzi hao pia wanaonya kwamba kama vigogo wa CCM hawataacha matumizi ya kampeni chafu katika kuwania kiti hicho, makundi ndani ya chama hicho yatakimaliza na kuna hatari uhusiano baina ya wanachama ukazidi kudorora kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele.


  [​IMG]

  [​IMG]
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Dakta bandia hana sifa za kuiongoza Tanzania.
   
 3. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Tayari kakaa mkao wa kula wewe utasema daktari feki mwenzako anakata mbuga.kama ni Daktari feki kwanini aliposhinda ubunge wapinzani hawakwenda mahakamani kuweka pingamizi dhidi yake?
   
 4. l

  lageneral Member

  #4
  Sep 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli nchi inaelekea pabaya,hata nchimbi anafikiria kuwa raisi wa Tz.Naomba kitu hiki kisitikea wakati ni kiwa hai.Lazima watu waende mahakamani kuulizia uhalali wa elimu yake.
   
 5. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hata Nchimbi???? hahahahaha huko ni kufulia kisiasa nchini.
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kama nchimbi nae atakuwa rais basi nitashawishika kuihama nchi hii na kuungana na kina Julius ughaibuni!itakuwa haina maana,hasa nikumbuka panchi aliyopigwa pale mzumbe university(by then IDM) wakati anagombea urais wa serikali ya wanafunzi
   
 7. F

  FOE Member

  #7
  Sep 27, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi wanaIDM walimpa kweli? Labda kwa kipindi hicho it was too early for him to prove his incompetence.
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  mhhhh hii habari inanitisha mno.nitAHAMA NCHI.
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  wampe wapi bwana!alipigwa panchi ya kufa mtu dakika za majeruhi.kama unavyowajua wanafunzi wa vyuo,hata uwashawishi vip lakini wakishajua tu weakness zako umekwisha.
   
 10. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #10
  Sep 27, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  5

  nadhani wa kuhama ..bora mjiandae kuhama ..maana hakuna anayeijuwa kesho..na siasa hazitabiriki!!..kwani hapa mmewataja vijana wengi....kwa nini nchimbi peke yake ndie awe hoja...hii ina maana ana weight...!!...na amekomaa kisiasa...

  nadhani ni mapema mno kuanza kampeni za 2015.....lolote hapa kati linaweza tokea na kubadili upepo wa kisiasa....ila pamoja na hayo mimi projection zangu ni kuwa rais wa tanzania mwaka 2015 atakuwa kijana yeyote mwenye miaka 38 hadi 45...leo,.........wote ambao wametajwa wanaozidi miaka niliyoweka hapo wasahau nafasi ya urais.....,na vijana wenye miaka 38 hadi 45 ..ambao wanautaka urais basi wapange vema karata zao,wapate uzoefu,wajenge network....na walinde afya zao kama mboni ya jicho lao....!!!
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Pamoja na matatizo yetu, Tanzania hatujawa that "LOW" ya kuleta huyu kijana kuwa rais!!! hana calliber, mvuto, upeo wala chochote cha kiongozi wa nchi, hata visiwa vya comoro tu let alone Tanzania

  Kama anasoma hii message basi aelewe hivyo, na dossiers zake zipo kwa baadhi ya walio karibu yake, awe huru tu kutafuta ubunge halafu asubiri teuzi

  Kama wengi mlivyosema, akiwa Rais, nahama nchi!!! Period
   
 12. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kipindi kile Sumaye anawania kugombea urais kwa tiketi ya ccm,nilisema siko tayari kuongozwa na sumaye.Hivi juzi mkawa mnasema oooh Karume ndo rais ajae,Iam not ready for that too.Sasa naona mmekuja na kali nyingine,Nchimbi! No,mi naamini mtakuwa mnamsingizia tuu.Nina uhakika kabisa hayo mawazo hayajawahi kumpitikia kabisa katika akili yake.Kwani yeye mwenyewe anajua hawezi,THATS IT.
   
 13. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  endelea kuomba mungu asigombee!maanake akipitishwa tu ni rais
   
 14. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nchimbi hakuna kitu hapo. Doctorate yake fake sasa sijui waTanzania atawaeleza nini
   
 15. M

  Msharika JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Dk. Salim pia aliambiwa si raia wa Tanzania (Mwarabu), pamoja na kuwa mwanachama wa Chama cha Hizbu ambacho kilikuwa kikiutambua utawala wa sultani visiwani Zanzibar, hivyo kuhusishwa moja kwa moja na Waarabu.

  Kashfa hizo kwa kiasi kikubwa zilichangia kuharibu sifa ya Dk. Salim ndani na nje ya CCM, hivyo kujikuta akikosa kutimiza ndoto yake ya kuwania kiti hicho ambacho kwa wakati huo kilikuwa na upinzani mkubwa ndani ya CCM.


  Baada ya kukumbwa na tuhuma hizo, Dk. Salim aliweka bayana wazi kuumia kwake na kutoridhishwa na mbinu chafu zilizokuwa zikitumiwa na washindani wake, hasa kundi la wanamtandao, kwa kumzushia mambo yenye kumhatarishia maisha yake, pamoja na kupandikiza chuki kwa Wazanzibari na familia ya Karume.

  >>>>Kama Dr Salim ambaye ameshashika highest international posts akiwakilisha Tanzania, Mbona Rostam Aziz aulizwi wala kuchambuliwa urai wao na wanamtandao? Hili litagarimu taifa, kama mwananchi mwenye uchungu na nia ya kuikomboa Tanzania, inanipa hali ya kujisikia kuanzisha mchakato wa kuuliza uraia wa rostam, NI mtanzania au mpakistani au mkanada?
   
 16. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hi inaonyesha jinsi gani ulivyo shabiki wa Nchimbi, Iliwahi kusema kuwa wewe ni Kada maarufu na ulikataa kabisa, Kwanini umesema Nchimbi tu pekee yake?? Hana nini Kipya
   
 17. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2009
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inaonekana kuwa "Rais" Tanzania ni "Rahisi". Hata mwendawazimu anaweza kuwaza kiongozi wa nchi.
   
 18. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wakati wanasiasa waliojitokeza kuwania urais wakishughulikiwa kwa stahili hizo mwaka 2005, Lowassa anatajwa kuwa na ushawishi mkubwa ndani na nje ya CCM iwapo atasimama kugombea nafasi hiyo mwaka 2015.

  Ushawishi wa Lowassa ni wa kifisadi. Watanzania hatutakubali tena kumchagua Rais anayebebwa na mafisadi. Huyu na mafisadi wenzake wasipoteze muda kwa kuwazia urais, badala yake wafikirie jinsi ya kuanza maisha mapya jela pale nchi itakapopata 'uhuru' halisi na kuongozwa na watu wenye uchungu na nchi yao!
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mbona mlikubali kuchagua rais aliyefanya kampeni kwa pesa za kifisadi.au unajifanya hujui kulwa hela za KAGODA zilimuweka madarakani huyo anayeongoza sasa.hakuna wa kufungwa hapo na kwa mtazamo wangu kuna siku tutabaki mdomo wazi pale miongoni mwa hao mafisadi atakapokuwa rais..
   
 20. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nonono!!!! hiyo post aliyonayo sasa sijui kwanini watu hawamwambii jamaa amtoe tu hapo mara moja.upuuzi mtupu!
   
Loading...