Dr. Mwakyembe: Sikumhoji Lowassa kwa sababu ushahidi dhidi yake ulikuwa unajitosheleza!

Swali la Mbunge wa Arumeru Mashariki hakulijibu akarukia hoja zake mpya ambazo zathibitisha huyu Mheshimiwa ni kilaza.

Lowassa hakupewa nafasi ya kujitetea lakini Bashite alipewa hakuitumia.

Bashite ni haki kuhukumiwa lakini Lowassa haikuwa haki kumhukumu bila kumpa nafasi ya kujitetea.

Lowassa alilalamika Bungeni hakupewa haki hiyo ya kujitetea sasa huyu ni dakitari wa sheria zipi anayedai Lowassa hasafishiki?

Tujuacho sisi Lowassa hana tuhuma ya kujibu au aliyowahi kutuhumiwa na ndiyo maana bosi wako wa zamani wewe Mwakyembe mstaafu Rais JK aliliona hilo na kubaini kujiuzulu kwa Lowassa ulikuwa ni uwajibikaji wa kisiasa na wala siyo kijinai.

Mwakyembe angelikuwa ni mwadilifu angelijiuzulu uwaziri ndani ya baraza la mawaziri la JK walakini kwa sababu maamuzi yake Mwakyembe ni "tumbo street" tu na hana jipya kabisa ndiyo maana hujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe!

Kama kauli za JK aliziona ni batili mbona hakujiuzulu? Kama Lowassa alikosea kijinai mbona hajawahi kuliomba Bunge iwakilishe taarifa hiyo TAKUKURU na DCI ili ifanyiwe kazi?

Hata leo kinamzuia nini Mwakyembe kupeleka upuuzi wake TAKUKURU na kuishia kutishia wapinzani walianzishe tena suala la Richmond.

Richmond/ Dowans walishinda kesi ya mabilioni na Mwakyembe kaufyata sasa huu ukelele bungeni wa yeye kutumia madaraka vibaya ya kuzima khashfa ya Bashite kwa khoja za kutosikilizwa jambo siyo kweli na hata Bashite mwenyewe hana malalamiko.

Inakiwaje Waziri mzima awe mtetezi wa mtuhumiwa wa kujipatia madaraka ya umma kinyume na sheria kama siyo kilaza au hajiheshimu?
mkuu inawezekana tatizo ni kubwa zaidi ya hapo.
inaweza kuwa ni "psych." case. si bure hii.
 
Wakujipendekeza ndio hao
 
Kitu ambacho sikujui ni hiki Naomba Msaada. Ile mahakama ya mafisadi ilianzishwa ya kazi gani? Tunaye fisadi anayetajwa kwa miaka 9 sasa mh. Lowassa na Dr makweyembe ana ushahidi wa kutosha kwa nn hapelekwi??
 
Richmond na suala la Makonda wapi na wapi,Nassari kachemka aibue na ya EPA ila suala la Makonda halina uzito na halituhusu watu wa mikoani akiwemo yeye Nassari.

Richmond janga la Taifa, Makonda msala wa Dar.
Makonda hana hati miliki Dsm, anaweza kuhamishwa pia maana ni mtumishi wa Umma
Kwa hiyo si sahihi kudai kwamba eti suala la Makonda haliwahusu watu wa mikoani
Think twice!
 
Huyu mzee toka apate ule ugonjwa wa ngozi naona akili yake in kutu kabisa..Yaani daktari wa sheria anwezaje kuonea mautumbo kiasi hiki.? anakiri hakumhoji Lowassa ,eti ushahidi ulikuwa unajitosheleza ,,,huyu mwendawazimu nini?Halafu eti ndio alikuwa waziri wa sheria huyu ndio maana kafukuzwa kwenye ile wizara bora akakaa kwenye wizara wa wenzie akina hamorapa ndio wataelewana ..Sijawahi kuona mnyakyusa mwenye akili zina kutu kama huyu baba
 
Dk Mwakyembe, Nassari wapimana

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari
IN SUMMARY
  • Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.

Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape (Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna haki hapo,” alisema.

Kauli za Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”

Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.

“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.

1. Nichangie ninavyoona mimi.
2. Dr Harrison Mwakyembe ni mwalimu wa sheria na inabidi anapoongelea masuala ya sheria awe anatuelimisha sheria zinasema nini na zinahitaji nini.
3. Ibara ya 13(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) inaelekeza kwamba: "Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba - (a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika."
4. Moja ya kanuni za 'natural justice' (ambayo Ibara ya Katiba hiyo hapo juu imezingatia) inasema 'no person should be judged unheard'.
5. Pia kuna kesi R v Sussex Justices, Ex parte McCarthy ([1924] 1 KB 256, [1923] All ER Rep 233), ambayo ilishaamriwa huko Uingereza ambayo ni precedence, iliweka kanuni kwamba 'si tu haki itendeke, lazima ionekane ikitendeka'. Msingi wa kanuni hii ni kuondoa manung'uniko katika utoaji haki na kufanya kila upande kusema upande wake ili hakimu aweze kutoa hukumu sahihi kwa kusikiliza pande zote mbili.
6. Kwa hiyo, Dr Mwakyembe anaposema 'waliona wana ushahidi wa kutosha na hawakuwa na haja ya kusikiliza upande wa pili' (kwa maoni yangu) si sahihi maana kama mambo yakifanyika kwa mtindo huu (upande mmoja tu kuona una ushahidi wa kutosha bila ya kusikiliza upande wa pili), then kesi nyingi zitaamriwa kwa namna ambayo haizingatii kanuni hii ya natural justice na zitaleta manung'uniko mengi.
 
Richmond na suala la Makonda wapi na wapi,Nassari kachemka aibue na ya EPA ila suala la Makonda halina uzito na halituhusu watu wa mikoani akiwemo yeye Nassari.

Richmond janga la Taifa, Makonda msala wa Dar.
Kuwa na tumia akili zako kabla ya kutoa mawazo yako. Wizara iliyokuwa inajadiliwa ni Tamisemi, na wakuu wa mikoa wako kwenye Wizara hiyo. Kwa hiyo Mh. Nasari zidhani alifanya kosa kuingiza mjadala wa Makonda. Na ndiyo maana kama unafuatilia kuna Mbunge mmoja wa CCM Bukombe Mh. Doto Bilago alimwaga radhi kuhusu vyeti vya Makonda akitaka wanaohusika na Wakuu wa mikoa kuondoa kadhia hiyo
 
Mbona Wanyakusya nasikia ni watu smart sana?
huyu anatokea wap?
mm km mwana ccm bado naendelea kumshangaa huyu mzee
huyo mwakiembe amechanganya damu ndo mana analidhalilisha kabila la watu wa huko yaani hata mm namshangaa sana ujue naona kachanganya sio pyua mnyaku
 
Nani alipima kwamba umejitosheleza? Ni kwa Sheria ipi inayotoa malmlaka kwamba ushahidi ikiwa tosha anayetuhumiwa asihojiwe! Huo mwingine si na picha unayo nini kimebaki!
 
2020 Iwe isiwe anang'oka kyela. Tuna ukichainwa na Mvuto wake umeshuka sana, anakurupuka tu.
 
1. Nichangie ninavyoona mimi.
2. Dr Harrison Mwakyembe ni mwalimu wa sheria na inabidi anapoongelea masuala ya sheria awe anatuelimisha sheria zinasema nini na zinahitaji nini.
3. Ibara ya 13(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) inaelekeza kwamba: "Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba - (a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika."
4. Moja ya kanuni za 'natural justice' (ambayo Ibara ya Katiba hiyo hapo juu imezingatia) inasema 'no person should be judged unheard'.
5. Pia kuna kesi R v Sussex Justices, Ex parte McCarthy ([1924] 1 KB 256, [1923] All ER Rep 233), ambayo ilishaamriwa huko Uingereza ambayo ni precedence, iliweka kanuni kwamba 'si tu haki itendeke, lazima ionekane ikitendeka'. Msingi wa kanuni hii ni kuondoa manung'uniko katika utoaji haki na kufanya kila upande kusema upande wake ili hakimu aweze kutoa hukumu sahihi kwa kusikiliza pande zote mbili.
6. Kwa hiyo, Dr Mwakyembe anaposema 'waliona wana ushahidi wa kutosha na hawakuwa na haja ya kusikiliza upande wa pili' (kwa maoni yangu) si sahihi maana kama mambo yakifanyika kwa mtindo huu (upande mmoja tu kuona una ushahidi wa kutosha bila ya kusikiliza upande wa pili), then kesi nyingi zitaamriwa kwa namna ambayo haizingatii kanuni hii ya natural justice na zitaleta manung'uniko mengi.
Na sijui wakati mwingine hawa wabunge wetu wanasheria wanakuwa wapi wasitoe ufafanuzi wa hoja zake kwamba haziendani na misingi ya kisheria. Inawezekanaje mwalimu wa sheria anaweza kutamka maneno kama hayo bila kujali kwamba anapotosha watu kwa makusudi. Hata kama anaweza kusema alikuwa na vielelezo vya ushaidi lakini mtuumiwa lazima apewe mwanya wa kufanya utetezi wake kutokana na vielelezo vilivyopo. Basi kwa maana yake nyepesi ni kwamba mtuhumiwa ukishapata ushaidi na vielelezo ahukumiwe mara moja bila kuwepo utetezi
 
Sasa mbona issue ya Bashite clouds ripoti haijatoka hadi leo au safari hii utafanya mahojiano pande zote mbili?!
 
Siasa ikitumika vibaya inakuwa kero kuifuatilia.Sasa mwakyembe anataka richmond irudi bungeni ili aje na ushahidi wa kummaliza Lowasa wakati ameshiriki kuanzisha mahakama ya mafisadi.Sasa kwanini asimshitaki Lowasa huko?Hii phD ya mwakyembe anaitumiaje?Au ndio anaitumia kukana hata maandishi yaliyompa hiyo phD
 
Back
Top Bottom