Dr. Mwakyembe: Sikumhoji Lowassa kwa sababu ushahidi dhidi yake ulikuwa unajitosheleza!

Tumbo ni kitu kibaya sana...tumbo linaweza kukufanya msomi mzima ukatembea uchi kutoka Gongolamboto hadi Posta saa 6 mchana. MaCCM ni majitu manafiki na vigeugeu sana.

CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi ni mwaka 2020 kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kifisadi kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka kubebeshwa ‘magunia ya misumari’ ya bei ya juu ya umeme, mfumuko wa bei wa kutisha, elimu duni, maisha duni, ufisadi wa kutisha, EPA na matatizo lukuki yanayosababishwa na panya (CCM) hawa wasiokuwa na haya! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.

It’s a matter of time before CCM dynasty comes to an end, and that’s when magambas will apprehend the significance and power of the people. Desolately, CCM have been ignoring and looking down their noses at common Tanzanians for many years. Time has now come when citizens can no longer endure CCM’s tyranny and corrupt rule. Everybody is tired of living like a slave on a land endowed with an assortment of natural wealth which only benefits the minority fisadis and a few elites in power while majority Tanzanians lead very miserable lives.

What comes around goes around. Let CCM go to hell for good because they have absolutely failed to uplift the living standards of millions of Tanzanians at the expense of a few fisadis whose gargantuan stomachs never fill up! And no one should be blamed for the hatred and grudge that many Tanzanians hold against CCM and their crooked government except fisadis themselves who, horrendously, decided to gnaw the cassava-made boat by which they were sailing!
 
Dk Mwakyembe, Nassari wapimana

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari
IN SUMMARY
  • Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.

Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape (Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna haki hapo,” alisema.

Kauli za Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”

Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.

“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.

HAHAHAA ULIMSHINDWA KUMNYOA UUKAWEWESEKA SEMBUSE LEO

WAKATI ANAMALIZIA ALISEMA KUNA MAMBO AWEZI WEKA HAPA.. ASEME HAYO MAMBO N YAPOO NA KAMA ALIWEZA KUTAJA MTU ALISHINDWA NINI MPAKA AKAWA NA KIGUGUMIZI
 
Kodi zenu wapi,wee nae unatoaga kodi ipi sasa,mkurupuko tu kila kitu mnapinga. Hapo wanamuongelea makonda pekee,Rais wa dar na sio unavyotaka kupindisha maneno hapa.

Wa mikoani suala lake halituhusu
Hulipi kodi eeh!
 
Mwakye ni mnafiki ana jali nafsi. Amewaondoa ktk ajira wengi kwa fitna zake. Mfano ni Paul Chizi aliyekuwa CEO wa ATCL na kumuweka shemeji yake Capt. Lazaro. Si kumng`oa huyo tu amepiga dili pale terminal two ujenzi wa VIP lounge. Asijifanye msafi hana usafi wo wote hata ubunge aliupata kwa mbinu.
 
polisi , jeshi , mgambo, mahakama ya kawaida, mahakama ya mafisadi vyote vyenu lakini mnalia chonde chonde na kina Kubenea na magazeti yao, jamani !!! ...kama Lowasa mchafu kwa nini hakamatwi apelekwe mahakamani? Eti kesi ya Richmond imeisha, imeisha lini wakati mitambo ya Richmond ipo pale Ubungo inaitwa Symbion? mlisemaLowasa mchafu, hasafishiki, tutamkamata tutampeka kwenye mahakama ya mafisadi, leo mmeongeza tutamnyoa nywele kwa chupa..... halafu badala ya kuamuru wakamataji wakamkamate mnalia na kubenea na magazeti....kubenea ni jeshi au polisi?
 
Bahati nzuri mijizi iliyokuwa CCM imeamia Chadema. Kule imekutana na majambazi na mikwepa kodi. Ndio maana Watanzania hawawapi nafasi ya kuongoza Nchi.
 
Hakika kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu aliyesoma na anayejisomea !

Embe alisoma, ila Nasari anajisomea.

Mtaelewa hapo kuwa ukisoma halafu usipoendelea kusijisomea basi kwisha habari yako.
 
Dk Mwakyembe, Nassari wapimana

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari
IN SUMMARY
  • Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.

Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape (Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna haki hapo,” alisema.

Kauli za Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”

Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.

“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.

Huyu mwanasheria vipi? Hivi sheria inasema kama una ushahidi wa kutosha humpi haki mtuhumiwa kujitetea???? Kama ushahidi umepikwa vizuri je? Ina maana utafungwa tu???? Hii sheria ya wapi????
 
Wabunge wali base kwny Report ya Mwakyembe kwa kuwa Mtuhumiwa ( Lowassa) alipewa Fursa ya kujitetea ili Wabunge wasikie upande wa Pili akaamua kujiuzulu sasa Kama Mtuhumiwa kakataa kujitetea ulitaka Wabunge wa base kwny nini zaid ya Mapendekezo?

Hata Wewe ukifikishwa Mahakamani ukapewa Fursa ya kujitetea ukashindwa basi hukumu huegemea kwny Mashtaka na ushahidi ulioletwa na si vinginevyo!
Fursa ya kujitetea unatolewa wakati gani? Wakati wa kusikuliza kesi au wakati wa kusoma hukumu?

Je kwa Bashite fursa ya kusikulizwa ilitolewa au haikutolewa? Msijitoe ufahamu ktk suala la bashite. Mazingira ya kesi ya Bashite na Lowassa yamefanana sana. Tena kwa Bashite ndio yamekaa vzr zaidi mana aliitwa ili asikilizwe akakataa.

So km ni hukumu km unavyosema ilipaswa imshukie Bashite mana alifwatwa kuhojiwa in the right time (kabla ya report haijaandikwa) na hakutaka kujitetea. Lowassa anasema kama angepewa hiyo opportunity angejitetea.

Asiyeona tatizo na wehu alioufanya mwakyembe kwenye issue ya Bashite ni lazma naye ana tatizo.
 
Kama akina Nassari walijua Lowassa hakuhojiwa kwny Richmond ilikuaje wakaweka jina lake kwny orodha ya Mafisadi Papa na kuiweka kwny Tovuti rasmi ya Chama?

Hawa cdm ndiyo mafisadi wakuu, halafu hawana haya,
Rejeeni miaka ya list of shame ya Mwembeyanga ya mwaka 2008 mpaka mwaka juzi 2015 ambapo ghafula walibadilika. Ndiyo walibadilika na kuanza kusema kuwa huyu si fisadi. Duu waTanzania walishangaa... lkn kuna wengine walifuata mkumbo wakaanza kuimba wimbo wasioujua.

Cdm ni wachumia tumbo tu hawana lolote. Miaka yote walikuwa wanapiga kelele bungeni na kuonekana kwenye runinga lkn huku twiga wakiibwa, makontena yakiibwa, wafanyakazi hewa kila kona, wanafunzi hewa kila chuo, rushwa kubwa kubwa kila kona. Sasa najiuliza sijui kelele zao zilikuwa zinasaidia nini.

JPM ni kila kitu Jembe hoyeee.
 
Pimbi ni pimbi,ingekuwa nihivyo hâta mahakamani watu wangefungwa bila kuhojiwa!?!
bora katolewa katiba na sheria ilikuwa niaibu!! Mtu anafanya vitu hâta rais anamshangaa. Kishamba sana hiki kijamaa
 
Ushahidi wa majungu na ule wa cctv camera upi ni dhahiri na wenye kujitosheleza?
 
Mwambie Mbowe ailete taarifa ya Richmond.. Bungeni tumalize kazi

Taarifa kamili anayo Dr. Harisson Mwakyembe, aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati teule ya kuchunguza sakata la kampuni ya Richmond. Kamati hii iliteuliwa na marehemu S. Sitta. Sintoshangaa kusikia mtu muhimu ameisha kufa. You're a blid. deaf and uncouth stup.i..d
 
Back
Top Bottom