Dr. Mwakyembe: Sikumhoji Lowassa kwa sababu ushahidi dhidi yake ulikuwa unajitosheleza!

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Dk Mwakyembe, Nassari wapimana






Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari
IN SUMMARY
  • Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.

Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape (Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna haki hapo,” alisema.

Kauli za Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”

Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.

“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.
 
Tunateua wasomi tena weledi ili wainyoshe nchi hii maana vilaza tokea mwanzo wapo sasa no wakati wa wasomi wa PhD kuonesha umahiri wao uwe zero au vyovyote ila umahiri kwanza
 
Richmond na suala la makonda wapi na wapi,nassari kachemka aibue na ya epa ila suala la makonda halina uzito na halituhusu watu wa mikoani akiwemo yeye nassari

Richmond janga la Taifa, makonda msala wa dar
Umeambiwa watumishi 9000 Bashite afu unasema Bashite sio issue ya kitaifa! Hao 9000 wanakula kodi zetu pasi na uhalali wa elimu!
 
Kodi zenu wapi,wee nae unatoaga kodi ipi sasa,mkurupuko tu kila kitu mnapinga. Hapo wanamuongelea makonda pekee,Rais wa dar na sio unavyotaka kupindisha maneno hapa.

Wa mikoani suala lake halituhusu
Umeambiwa watumishi 9000 Bashite afu unasema Bashite sio issue ya kitaifa! Hao 9000 wanakula kodi zetu pasi na uhalali wa elimu!
 
Richmond na suala la makonda wapi na wapi,nassari kachemka aibue na ya epa ila suala la makonda halina uzito na halituhusu watu wa mikoani akiwemo yeye nassari

Richmond janga la Taifa, makonda msala wa dar
Sheria haiwezi kuwa Dar peke yake! Double standard haikubariki,iwe Dar au kwingineko! Nassari kuhoji ni haki yake na Mwakyembe km waziri husika na ni yeye aliongoza kamati ya Richmond ni sawa akitumia rejea hiyo kuhalalisha ripoti ya Nape.
 
Hebu kwanza nijibu,ripoti ya richmond ilichukua muda gani kukamilika? Ya nape ilikamilika masaa matatu tu hayo mengine ya 24 geresha tupu. Ripoti ya nape imejaa majungu
Sheria haiwezi kuwa Dar peke yake! Double standard haikubariki,iwe Dar au kwingineko! Nassari kuhoji ni haki yake na Mwakyembe km waziri husika na ni yeye aliongoza kamati ya Richmond ni sawa akitumia rejea hiyo kuhalalisha ripoti ya Nape.
 
huyu inasemekana si mnyakyusa ni mtu mwenye asili ya malawi. si hata jimboni kwake hawakumtaka sema alipita kwa nguvu ya usd. ndo mambo hayo. wanyakyusa sijawah ona wana tabia za kipuuzi kama hizi. mi nimeoa mnyakyusa ndugu zake wana misimamo na hawana njaa.


Mbona Wanyakusya nasikia ni watu smart sana?
huyu anatokea wap?
mm km mwana ccm bado naendelea kumshangaa huyu mzee
 
Eti huyu ndio Dr.wa sheria!!!
Mkuu nakukubali kwa kuwa wakwanza kukomenti karibu ktk kila thread flani hapa jf....ni ama wewe au boban, mwanahabari huru, na mwingne jina sikumbuki.
Habari,
Ilikuwa ni mtifuano wa kurushiana maneno kati ya Mbubge Joshua Nassari na waziri wa habari dr Mwakyembe akimhoji kwanini swala la Richmond wakati akiwa mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi hakumhoji waziri mkuu kipindi hicho na akasimama kutoa hukumu bungeni lakini kwa swala la Bashite anadai hakuhojiwa na uchunguzi haujakamilika.

Ndipo kulizuka mtutano wa kutupiana maneno huku Mwakyembe akidai swala la Richmond hakukuwa na haja ya kumhoji kwa kuwa riport ilikuwa na ushahidi wa kujitosheleza ila kwa makonda ni ushabiki tu na hakuna ushahidi wa kujitosheleza
 
Back
Top Bottom