Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

siye maamuma wa mambo ya sheria tumeambiwa (na tumeamini) kuwa rais amevunja katiba kwa jinsi anavyoi-treat opposition camp, nk.

sasa hii ya Mwakyembe kusimama bungeni na kutamka bayana kuwa rais hajavunja katiba siyo suala la kulifanyia mzaha. kwa nafasi ya bunge katika katiba yetu tamko la Mwakyembe kupitia chombo hiki is a very serious "declaration" (it's tempting to term it an "allegation" but maybe it is not until legally (un)proven).

so response ya opposition isiishie kujibizana na Mwakyembe kupitia majukwaa bali kwa kupitia process iliyoainishwa kikatiba ili ku-prove kuwa kweli rais ameisigina/hajaisigina katiba. what is the problem with this approach? kuna wanasheria wabobevu kwenye eneo la katiba wengi tu - watumike hawa!

"So response ya opposition" ni kuhamsisha uvunjifu wa Katiba kuingiza wananchi kwenye mgogoro na Serikali yao, kwa sababu hakuna kifungu cha Katiba ambacho Rais amevunja, ambacho wangetumia wanasheria wa kambi ya upinzani kwenda mahakamani kwa Kifungu 30(3) cha Katiba, nanukuu:
"30(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu."
 
Kama umeweza kunyofoa kipengele cha Ukomo wa Uongozi ndani ya Chama Utashindwaje kunyofoa hicho kipengele kwny Katiba ya Nchi kama ungetokoea Muujiza ukapewa dola?
unazungumzia nini ndugu? kuchukua dola? hoja hapa ni kuwa katiba haijafuatwa na rais na waziri anamtetea kwa hoja ya kuwa chadema wenyewe hawafuati katiba,
 
Hapo ndo kajidhalilisha ameonyesha ni jinsi gani anavyomjali Magufuli kuliko watanzania eti hajavunja katiba...mi nasema hawa wanaojiita ma Dk. na ma Prof. wanadhalilisha elimu ya TZ
kuna tofauti gani yeye akisema katiba inavunjwa na anvyosema Mbowe kuwa Rais anavunja katiba? umepewa njia bora ya kufuata kama unalosema unauhakika nalo nenda mahakamani, huko ndiko sheria na katiba hutafsiriwa, sasa kukaa hapa na kulalamika haiku saidii
 
"So response ya opposition" ni kuhamsisha uvunjifu wa Katiba kuingiza wananchi kwenye mgogoro na Serikali yao, kwa sababu hakuna kifungu cha Katiba ambacho Rais amevunja, ambacho wangetumia wanasheria wa kambi ya upinzani kwenda mahakamani kwa Kifungu 30(3) cha Katiba, nanukuu:
"30(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu."

swali: hicho kwenye red kimefanyika tayari???
 
Kwanza atueleze kwa kina ununuzi wa mabehewa fake deni ndyo tutamuelewa. Haya yote ata kama ni kweli hatuwezi muelewa sababu ni mwizi anatetea tumbo lake 2.
 
unazungumzia nini ndugu? kuchukua dola? hoja hapa ni kuwa katiba haijafuatwa na rais na waziri anamtetea kwa hoja ya kuwa chadema wenyewe hawafuati katiba,

Hapo alikuwa anazungumzia Moral Authority ya alieleta hiyo hoja, Kama Shule ulikuwa unaenda kula Ubuyu huwezi kumuelewa Dr.
 
Mimi shutuma zangu kwa Dr harrison ni hizi, huku jimboni kwako miaka yote uliyokuwa madarakani, umetufanyia nini wewe mbunge wetu, hata prof mwandosya na HEKIMA zake ana kila sababu za kusema amefanya kitu jimboni kwake...


2020 KUPATA KURA ZETU EHEEEE....
Inabidi tuwaulize nyie ambao mlimpigia kura. Kama hakufanya chochote inakuaje mlimrudisha mahkman?
 
CHUNGUZA FALSAFA KATIKA BUSARA NA HEKIMA ZAKO.
Hakuna kipimo cha ufahamu, ukidhani unafahamu sana huwa ni dalili za uwendawazimu unapoongea sana ukiwa huna jawabu la kelele zako.
Busara ni upole na hekima, katika utulivu huu miujiza na uumbaji huonekana katika maono ya vijana na ndoto za wazee wetu.
Binadamu salama ni yule asiyetia risks yoyote katika mifumo ya maisha kwa kauli na matendo yao, wao huona makosa na kuyadhibit bila hata mkewe kujua, huona fursa za heri na kuzitumia pasipo jirani kusononeka, matendo na hekima zao hazichunguziki.

Matokeo ya hatua zao hizo za kiungwana tunayafurahia maisha tukiamin ni miujiza kutoka mbinguni! Huku ni kukosa ufahamu tunaodai kuwa nao. Huku tukizidi kushindana kwa vijembe vya ufahamu.

Jaman anaejua habezi wasiojua Bali hufadhaika moyon kwa ajili yao maana athari za mjinga hudhuru na asiyezichuma. Ukitaka kujua upuuzi wa mashindano ya ufahamu wao, angalia ni nani kati yao anauwezo wa kushinda nafsi yake dhidi ya kisasi kwa mwenzake?. Haya ni mabishano ya ulevi wa sifa, hongo n.k.

Nikikuita mjinga, ukanilipa kwa kuniita fara hicho ni kisasi kibaya kuliko kuua kwa panga. Visasi vya namna hizo huwatoka wenye ufahamu usio na uhai ndani yake.

Ufahamu wenye uhai ndani yake upo kwa binadamu mwenye uwezo huu...

1. Kujua utu wake, uhodari na udhaifu wake na kuuthibitisha.

2. Kutafsiri uhusiano uliopo kati ya udhaifu wake ama uhodar wake na aina ya matokeo yawe hasi ama chanya kwa kuangalia aina na mfumo wa maisha anayoishi sasa kwa misingi ya falsafa zake.

3. Uwezo wa kukiri makosa yanayotokana na udhaifu ama uhodar wake pasi kukwepa kuwajibishwa au kujiwajibisha mwenyew.

4. Kuwa na hekima itakayoepusha kuangamiza maisha ya wanaomzunguka kutokana na athar za nguvu ya nafsi yake na uvutano wa nafsi zetu.

Wengne ni dhaifu mifumo huwavuta na kuwasomba bila hata wao kutaka au kufundishwa. Hapa ndo huasisiwa vitendawili vya, Ningelijua...nisingeli..., Majuto ni...., Namlaumu/namlaani....nk.

5. Asiye na simile na shetani. Maana misingi mingi ya harakat za haki za binadamu is all about the devil consciousness forms.
Zaidi nitawadadavulia nikijisikia. Maana huwa ctaki sifa. KUTAKA SIFA, HONGO, POMBE, MAJIVUNO, UBISHI, HASIRA, WIVU, TAMAA NA UJUAJI vyote hupunguza uwezo wa kufikiri. Hivyo ukisikiliza hoja ya mtu kabla ya kumuunga mkono tafakar kwanza, je msingi wa hoja zake zimejengwa juu ya dhamira gan kati ya hizo hapo juu? Ukishindwa kuoanisha misingi hiyo hapo juu ukaishia kuunga mkono tu jua wew ni mgonjwa wa kundi hilo hivyo ni sehem ya hasara ya taifa sio hazima. WAJINGA HUUNGWA MKONO NA WAJINGA WENZAO DAIMA WATAVUTANA NA KUFURAHIANA.

By Mwl Mimi.
 
Mbn unalalamika sana na hata siku moja hajasema kuvunja Katiba kifungu kipi, acha kukalili kijana
Unauhakika vifungu vilivyovunjwa havikuwai kuelezewa? Acha kudandia ndege kwa mbeke wewe. Kitu kama hukijui kaa kimya sio lazima ucomment
 
Unauhakika vifungu vilivyovunjwa havikuwai kuelezewa? Acha kudandia ndege kwa mbeke wewe. Kitu kama hukijui kaa kimya sio lazima ucomment
Mie na wewe nani kadandia ndege kwa mbele? Kaa kimya kijana achana na siasa za mihemko
 
Huyo ndio Mwakyembe katika ubora wake,Mwanasheria kiwango cha PhD jamani nchi hii ina shida sio masihara unawapambanuaje msomi wa kiwango hicho na hawa wenye elimu za kawaida??Kama anasema raisi hajavunja sheria,wakati vifungu viko wazi kabisa kwenye sheria ya vyama vingi ya 1992 huyu kaamua kujitoa akili na kutetea ujinga ili bora mkono uende kinywani.Nenda jimboni kwake sura yake halisi utaiona eneo la kuzunguka soko na maeneo ya maduka kashindwa kuweka lami nusu km tu achilia mbali watu kushea maji na vyura loo!! puu!!.
 
Anasema jamaa kama walikwazwa na Raisi wangeenda Mahakamani kudai haki,namuuliza Mwakyembe kwa Mahakama zipi? Mwakyembe anaendelea namnukuu kama walimwengua Dr Slaa na kumweka Lowasa bila kufata Katiba kwa hiyo Chadema hawana Moral Authority ya kumnyooshea kidole yeye Mwakyembe na Mwanasheria Mkuu,'' kwa hiyo ata kama Chadema walivunja katiba yao kwa hiyo wakae kimya wasihoji kuhusu uvunjaji wa katiba na sheria unaoendela hapa nchini''?

Kama upinzani unaheshimu Katiba ya JMT, kiasi cha kutoa tamko la UKUTA, basi ni vyema kuiheshimu Mahakama iliyopo kwa mjibu wa hiyo hiyo Katiba.

Kutokuhesimu Katiba ni kuvunja Katiba yenyewe. Hiki ndicho kinachowakwaza wanasiasa wa upinzani kiasi cha kuitwa "vigeugeu". Wao hasa ndio "wanasiasa uchwara".
 
Sasa nyie CCM nawashangaa sana, nyie mnataka msihojiwe kuvunja katiba ya nchi kisa Chadema wamevunja katiba yao? kwa hiyo tuseme hata chadema wakifanya jambo lolote baya nyie mtalifanya pia kwa kuwa chadema wamelifanya?
si bora walifanye kwenye chama sasa mkuu? wao wanalifanya kwenye katiba ya nchi yaani mwakyembe anafananisha katiba ya nchi na ya chadema. Hilo moja mbili sijaamini kwa cheo chake ndio anaweza jilamba kwa mzee kiasi hicho[emoji35] [emoji24] [emoji24][emoji36] [emoji36]
 
! kuna tofauti gani yeye akisema katiba inavunjwa na anvyosema Mbowe kuwa Rais anavunja katiba? umepewa njia bora ya kufuata kama unalosema unauhakika nalo nenda mahakamani, huko ndiko sheria na katiba hutafsiriwa, sasa kukaa hapa na kulalamika kama mke mjane alifiwa na mumewe kisha akaporwa mali na mume wa ndugu haiku saidii
Usije tumbo wazi bila kuonyesha jibu linalotakiwa.. Je Rais havunji katiba kama anavyosema Mwakyembe au anavunja kama tusemavyo watanzania tuliowengi nikiwemo mimi?
 
si bora walifanye kwenye chama sasa mkuu? wao wanalifanya kwenye katiba ya nchi yaani mwakyembe anafananisha katiba ya nchi na ya chadema. Hilo moja mbili sijaamini kwa cheo chake ndio anaweza jilamba kwa mzee kiasi hicho[emoji35] [emoji24] [emoji24][emoji36] [emoji36]
upuuzi kweli yani, na watu wanamtetea, hawa viongozi wetu wanatuona makondoo kiasi hiki
 
Hapo alikuwa anazungumzia Moral Authority ya alieleta hiyo hoja, Kama Shule ulikuwa unaenda kula Ubuyu huwezi kumuelewa Dr.
hajahoji katiba ya CCM amehoji katiba ya nchi, mwananchi yoyote ana haki ya kuhoji kama katiba ya nchi imekanyagwa, awe jambazi au mtu wa aina gani, ana haki ya kuhoji akiona mambo yanayomuhusu, katiba ya nchi inamuhusu kila mtu
 
Wao waendelee.kumdanganya mfalme kuwa kavaa nguo wakati yuko uchi. Siku ipo na inakuja, mwendawazimu mmoja atamwambia ukweli mfalme kuwa yuko uchi, na hapo ndipo hao akina Mwakyembe watalipa kwa unafiki wao.

Siasa ni kama msumeno hukata pande zote. Aliye madarakani leo kesho atakuwa mtawaliwa, na vivyo hivyo. Siku ipo na inakuja, wanadai Katiba ya nchi inavunjwa, watakuwa madarakani tukashuhudia wakivunja Katiba waziwazi.

Kuna ushahidi dhahiri kwa sasa, viongozi wa upinzani wanavunja Katiba ya Chama chao (rejea mada kuu) na Katiba ya nchi badala ya kwenda mahakamani (kifungu cha 30(3)) wanahamasisha mikutano ya hadhara na maandamano yasiyo na mwisho.
 
upuuzi kweli yani, na watu wanamtetea, hawa viongozi wetu wanatuona makondoo kiasi hiki
kwa kweli huku tunapoenda ni kubaya mpaka sasa raiya wanatamani bora asingekuwa mtanzania Maana ni aibu sasa.
 
Back
Top Bottom