Mwanakili90
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,568
- 246
100% nakubaliana nawe
Labda nijaribu kueleza za wanao mtetea EL
- Nadhani wana mkubali zaidi EL kuwa ni kiongozi ambaye yupo tayari kufanya maazi magumu kwa manufaa ya walio wengi Maana hii nchi inahitaji kiongozi jasiri
- Hawaamini kuwa EL pekee yake anasitahiri kubebeshwa lawama za Ufisadi ikiwa ile ilikuwa ni system ilikuwa na watu wengi kama alivyo sema huko NEC kuwa kila hatua Mkuu alijua kinachoendelea
- Wanasema ndani CCM mtu anayeweza kuingoza hii nchi awe mchapa kazi hivyo EL ni mchapa kazi sijui kigezo wanachutumia (Haya ni badhi tu ya maoni ya watu humuhumu )
Huku kulia lia kwa wafuasi wa Lowassa kunaonyesha kabisa kwamba huyu bwana yuko desperate kujisafisha wakati alishapa nafasi ya kuyasema hayo na mbele ya bunge lakini kwa woga wake na kwa sababu ya kujua kwamba yeye ni mhalifu katika hilo, akakimbilia kuhusisha ripoti ile na uwaziri mkuu wake.
Leo kwa ulevi tu, watu wanaanza kuingiza concept za natural justice ambao hata hawana weledi nazo na kudhani kwamba uchafu uliomtapakaa bwana huyu utasafishwa kwa porojo za humu JF. Awadaganye hao hao wajumbe wa NEC na wafuasi na wapambe wake mbumbumbu, siyo watanzania wenye ufahamu.
Ilikuwaje akashindwa kufanya maamuzi magumu ya kukataa kujiuzulu na kujitetea bungeni kama alivyofanya kwenye vikao vya NEC ya ccm, ili hao wote wachafu waliojazana ndani ya ccm na serikali yake wawajibike?? Kwa kufanya hivyo angekuwa amefanya maamuzi magumu kwa manufaa ya watu wengi, kuliko alivyoamua kujiuzulu kwa manufaa ya mshikaji wake.
Lakini kuna school of thought inayodai kuwa Ripoti ya Mwakyembe ilikuwa profesionally conducted (M/Kijiji), ilifuata hadidu za rejea zilizotolewa na Bunge, na EL hakuwamo katika hadidu za rejea lakini, hata hivyo bado alipewa fursa ya ku-excercise natural justice ndani ya bunge, na badala yake:
(1) EL hakuitumia hiyo fursa, aliamuwa mwenyewe kwa hiari yake kujiuzuru
(2) Alikuwa na kila fursa aliyohitaji ndani ya Bunge kupinga, kuzuwia, kujitetea, lakini yeye alichagua kulalamika tu na kisha akaamuwa kujipima na kujiuzuru huku akiacha fursa zilizopo zikimshangaa kwa nini hataki kuzitumia...!!!!
Wataalamu wa Sheria:
- Je natural justice ina mipaka- kwamba lazima mtuhumiwa aipate katika mazingira fulani au ndani ya muda fulani?.
Je kama Mwakyembe alikanyaga haki hiyo ya EL, je kisheria anaendelea kuikanyaga hadi leo?
Anaweza, lakini kwenye sheria kuna msemo "justice delayed is justice denied" Hata kitendo cha kumnyima Lowassa haki ya kujitetea kabla ya tume kuandika ripoti kilikuwa ni kuchelewesha haki ya Lowassa na hivyo kumnyima haki.Je Lowasa ana nafasi ya kuyasema leo yale ambayo angeyasema kama Mwakyembe angempa hiyo ''NJ''
Hili ni swali ambalo EL tu anaweza kulijibu. Logically thinking, ukichukua matamshi yake alipojiuzulu, ameepuka damage kwa chama na serikali yake. Kwangu mimi hili linaweza kabisa kuwa kumlinda Kikwete na serikali yake.Je kwanini EL hataki kusema hata alipopata forum tofauti i.e NEC-
Hatuwezi kujua kabla hayajasemwa, lakini kuna mambo fulani ambayo yamefanyika ambayo hayawezi kutofanyika tena.Mathalani tumemuona George Bush kampongeza Kikwete kwa kusema, in effect "You fired that thief, god job". Lowasa kashakuwa tainted, kashajiuzulu etcKama EL atayasema leo je yataleta mgeuko ''twist'' mpya kwenye sakata hili?
Kwa sababu si muwazi na kuna vitu/watu analindaJe kwanini pia Mwakyembe hataki kusema yale ''mengine'' waliyoyaacha?
Hatujui mpaka yasemwe, lakini kuna mambo hayawezi kufutika kama nilivyosema hapo juu.Je kama Mwakyembe atayasema leo je bado yanaweza kuclear wingu liliopo kuwa EL alionewa? au yatamtia hatiani zaidi EL ?
FairPlayer, naomba tuwe fair katika jambo hili...Naomba nikujibu kifupi tu. Sifahamu uwezo wako wa kufikiri au ufahamu ila jibu ni FUPI. NEC ya CCM ni CLOSED meeting, taarifa zake hazirushwi na vyombo vya habari. Bunge ni OPEN meeting. KIongozi hawezi kuanika mambo ya ndani hadharani kama unavyofikiri.
Mwakyembe (na usomi wake wote) mpumbavu -sio mjinga-. As in idiot, and not ignorant. Kashasoma sana kupewa benefit of doubt ya ignorance, kawa muhadhiri wa kutumainiwa ati.
Hili linanifanya nijiulize sana kuhusu quality ya elimun yetu. Kama hata mhadhiri maarufu wa sheria anaweza kuchemsha hivi, tutegemee nini kutoka kwa sio tu wahadhiri wetu wapya, bali hata wahitimu wetu wapya.
Yoyote ambayo hujayasema katika ripoti, halafu ukasema "kuna mengine sijayasema katika ripoti" unakuwa ushayasema kwa namna moja ama nyingine. Unakuwa kama yule mkimbizi wa vita aliyelala chini ya nyasi, akasikia adui kauliza "kuna aliyebaki hai tumpe maji?". Akaamini na kujibu "Mimi nipo hai". Akamalizwa hapo hapo.
Kama kuna mambo hayaelezeki katika ripoti, huyazungumzii kabisa. Husemi hata kwamba hayaelezeki, kwa sababu ukisema tu hayaelezeki ushaanza kuyaelezea. Mwanasheria aliyebobea anatakiwa kuelewa hili a la "You have the right to remain silent, anything you say can and will be used against you".
Na kutoka hapo ( statement ya "kuna mengine sijayasema katika hii ripoti") unapata the worst of both words.
Wale waliotaka usiseme watakuona mbaya kwa sababu umesema kuna mengine hujayasema, ume spill beans kwamba kuna zaidi ya uliyoyasema.
Wale waliotaka useme watakuona mbaya kwa sababu umesema kuna mengine hujayasema ambayo wangetaka uyaseme.
Hatujali sababu iliyomfanya Lowassa asihojiwe.
Tunajali kwamba Lowassa hakuhojiwa, na kwa sababu hakuhojiwa anasema hakutendewa haki na ripoti nzima imejaa ukungu wa maswali.
Naomba nikujibu kifupi tu. Sifahamu uwezo wako wa kufikiri au ufahamu ila jibu ni FUPI.
NEC ya CCM ni CLOSED meeting, taarifa zake hazirushwi na vyombo vya habari.
Bunge ni OPEN meeting.
KIongozi hawezi kuanika mambo ya ndani hadharani kama unavyofikiri.
FP,
Huna sababu ya kuhoji uwezo wangu wa kufikiri, unatakiwa kujibu hoja. Kama kila mtu ataanza kuhoji uwezo wa mwenzake, tutaishia kufanya mipasho badala ya mjadala.
Kama kamati ya mwakyembe ilisoma ripoti yake kwenye open forum, Lowasa akapewa nafasi ya kuzungumza kwenye open forum kwa mujibu wa taratibu za bunge, lakini akaishia kulalamika badala ya kutoa utetezi wake, halafu wewe unataka kutushawishi kwamba bungeni hapakuwa mahali sahihi pa lowasa kuusema ukweli, basi nami nalazimika kuhoji uwezo wako wa kufikiri na ufahamu wa mambo.
Sakata la richmond lilitokea bungeni na ndipo lowasa alitakiwa kujieleza lakini hakufanya hivyo. Kwenda kulizungumzia sakata hilo kwenye kikao cha nec, miaka mitatu baada ya kubwaga manyanga ni dalili8 tosha kwamba anafanya hivyo kutafuta huruma ya chama chake ili kimsafishe na aweze kufikia ndoto yake ya kuwania na hatimaye kuwa raisi wa nchi hii. Kama angekuwa kiongozi makini, na kama angekuwa hakuhusika na richmond, angejitetea pale pale bungeni. Lakini kwakuwa alihusika, hakuwa na njia nyengine zaidi ya kubwaga manyanga, na huo ndio ukweli mnaojaribu kuupotosha, wakati kila mtu anayetumia vizuri bongo yake anafahamu.
Kwa mtu anayelitazama sakata hili la lowasa kushindwa kuzungumza madudu ya richmond bungeni na kukimbilia kwenye chama, halafu wanaibuka watu kutaka kumsafisha kwamba hahusiki, hashindwi kuona ni kwa namna gani watu mnavyochezeshwa muziki msioufahamu.
Mkuu,
Pamoja na ukweli wote uliouleza hao jamaa hawawezi kukuelewa kwa sababu wana kazi moja tu, kumsafisha mfadhili. Kwanza huo usiri wa NEC uko wapi wakati siku hiyo akiongea aliacha simu zake wazi akiwa ameziunganisha na mhariri mpambe wake!!!
Pili huko NEC wanakojengea hoja kwamba alipasua jipu, ni jipu gani hilo mbona hasemi alivyotuingiza kwenye mkataba amekazana na kuvunja mkataba. Watu wanasimamia utetezi wa kumpigia simu JK kuhusu kuvunja mkataba, tangu lini serikali ikaendeshwa kwa simu!
Inasikitisha kuona watu wamekazana kulazimisha uongo uwe ukweli utadhani Tanzania bila EL haiwezekani.
Lowasa alipima, akijiona ni mhalifu akajiuzulu, hakuna aliyemlazimisha, na hicho ndio kitanzi chake atakachokufa nacho, na kila anapohangaika kukitanzua ndivyo anavyokikaza zaidi!!!