Dkt. Mathayo na Ana Kilango: Same "Wachina" wa Tanzania mpaka "VILAZA" wa Kilimanjaro

Pdidy,
Baba wa Taifa aliwaita wananchi wa Same "wachina wa Tanzania" baada ya kushuhudia juhudi za wananchi kujitolea kuchimba barabara kwa utaratibu unaitwa "msaragambo." hatuna haja ya kumuita Baba wa Taifa atuletee maendeleo, kwani uwezo huo tunao, kinachokosekana ni uongozi toka kwa wabunge wetu tuliowapigia kura.
 
bangusule
bangusule has no status.
Member

MKUU BANGUSULE..MAENDEELEO YA SEHEMU YANALETWA NA WENYE SEHEMU HUSIKA...KIDOGO UMENICHANGANYA KUHUSU ELIMU..SASA KAMA SHULE IMETOA DIV 0,N DIV 4...HAWA WABUNGE WAPELEKE WATOTO WAO HAPO AU???
SWALA LA MSAADA KWAKONI HIVI KAMA UPO DAR ....NENDA WIZARA YA ELIMU JITAMBULISHE WE NI MWANA SAME...KUNA TATIZO HILI HILI NA LILE KWENYE WILAYA YETU...UNAJUA NINI WATAITAJI USHAHIDI NENDA KAWALETEE...THEN WATAKUULIZA UNA UHAKIKI TATIZO NI WALIMU???USIJE KUTA WANA WALIMU WA KUTOSHA TATIZO MOJA VIJANA WWENGISASA AWATAKI KUSOMA HATA KAMA UWAPELEEKEE WALIMU 100 KAMA UTAKI KUSOMA UTOFAULU THAT GIVEN.....SO WAKIKUSUMBUA MBUNGE WAKO NI WAMBALI SANA ...WAZIRI WA ELIMU NI WAZIRI WAKO...NENDA WIZARA YA ELIMU ULIZA NANI WAZIRI OMBA APPOINTMENT...NA KAMA UMETOKEA SAME STRAIGHT KUWA MPOLE WAH WANAONANA KWA APP..WAKIKWAMBIA KESHO NJOO KESHO ..NATUMAINI UTASAIDIWA ..SASA BASI HUYU WAZIRI AKIKULETEA UHUNI MKIMBILIE KILANGO/AMA MALECELA////NA KUKUSAIDIA UKIMAPATA MALECELEA ATAKUSAIDIA ZAIDI MAANA ANATAKA MKEWE ARUDI MWAKANI SO ATA MAKE SURE AKUNA LINALOARIBIK A KABISA

happy valentino
 
Pdidy,
ningefurahi kama tungekuwa na shule zenye hadhi ya kusoma mtoto wa mbunge. hicho ndicho ninachopigania hapa. nawaomba na wengine wapiganie sehemu nyingine ziwe na shule zenye hadhi hiyo.

mawazo ya kwenda wizara ya elimu ni mazuri. muda ukifika tutakwenda huko wizarani. sasa hivi tunajaribu kuangalia wabunge wetu watachukua hatua gani. kuna ambayo yako ndani ya uwezo wetu, ni kiasi cha mbunge kuhamasisha tu. baada ya hapo ndiyo tutakuwa na uhalali wa kuwashika mashati viongozi wa kitaifa.

kama mwaka 47 wazee wetu waliandamana na kuweka mgomo wa mwezi mmoja dhidi ya DC Muingereza, basi matatizo hayo yasipotatuliwa wananchi wa Same tutakodi mabasi ya Zafanana tupige kambi wizara ya elimu.
 
Wapare na wa aminia, toka enzi za ukoloni historia inaonyesha ni wafuatiliaji wazuri wa haki, hata ikibidi kuuza mbuzi kwa kesi ya kuku ili mradi haki ipatikane...........!!!!!!!!!!!

ila Mkuu umejaribu kuwauliza wabunge kama walisha wahi kufuatilia juu ya matatizo hayo???? kama bado ni halali kuwatupia lawama ukizingatia wamekaribia kumaliza muhula wao, lakini ni kama nimesha wahi kumsikia kilango akiongelea miradi ya umwagiliaji same na kuna kipindia alikuja kuhamasiha vikundi vya akina mama wakulima huko same..........
 
Hoja ya ndugu yetu Bangusule ina maana kiasi kidogo sana. Ina maana kwasababu matatizo yapo na yanahitaji kutatuliwa. Haina maana sana kwa sababu anaitoa bila kuwa na vielelezo vya kutosha kuhusiana na sababu za kuwepo matatizo hayo, na hatua ambazo wananchi wa Same wameshachukua kutatua matatizo hayo. Ama sababu zilizotolewa hazitoshi asilani.

Wakuu, mimi nimesoma thread yote na kusikitishwa sana na maendeleo yanayodorora ya Wilaya ya Same kama ambavyo Bangusule ameyataja. Kama kweli hali ndio hiyo, basi jitihada za haraka zinatakiwa kuchukuliwa na wote wenye mapenzi mema na maendeleo ya Same.

Kutokana na maelezo yaliyotangulia, inaelekea tatizo ni la kiWilaya zaidi ya kiJimbo. Inaelekea uongozi wa wilaya una matatizo. Wana Same wanatakiwa waangalie matatizo hayo kutokea wilayani kuanzia Halmashauri nzima ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya, Watendaji wote wa Wilaya, Makatibu Tarafa, Maafisa Elimu na Maafisa Kilimo, Diwani na pia Mbunge wao. Kurukia moja kwa moja kuwa tatizo ni wabunge, sidhani kuwa ni sahihi. Si sahihi kwasababu hata wakibadilishwa wabunge hao, bila kuangalia utendaji wa wengine wote waliopo, si ajabu tatizo likawa kubwa zaidi. Kama kuna nia ya kupata utatuzi, basi wana Same waache siasa za lawama kwa waBunge, waanze kutafuta solution ya matatizo yao.

Siamini hata kidogo kuwa matatizo hayo yametokea baada ya waBunge hao kuingia madarakani miaka mitatu iliyopita. Matatizo yaliyopo yamesababishwa na wananchi na baadhi ya viongozi waliopo Same. Ni wananchi wa Same ndio wenye uwezo wa kuyatatua matatizo yaliyopo. Fanyeni yaliyo-mema kwa Same yenu ili mpate maendeleo mnayoyahitaji. Msisubiri mpaka uchaguzi ufike halafu muanze kulaumu, hamtapata maendeleo yoyote kwa namna hiyo, zaidi ya kuacha donda kuwa gumu kutibika na kuzama kwenye ufukara. Mbunge hana uwezo mkubwa wa kutatua matatizo yote, hasa kama wananchi hawataki kuyatatua.

Mkitaka, badilisheni Mbunge, halafu muone kama mtapata suluhu kutoka kwa Mbunge huyo mpya. Tatizo liko mikononi mwenu Ngugu yangu Babgusule, acheni kulitafuta kwenye mikono ya wengine.
 
Mwaka jana mwishoni nilipata nafasi ya kupita jimboni Same, nikaa kwenye bar moja maarufu sana pale stendi iitwayo PADECO, wakati tunapiga mbili tatu kama kawaida story za politics zikaanza.....

In general wadau wa Same mjini wanasema Dr. Mathayo hajawafanyia chochote kipya toka aukwae ubunge wa jimbo hilo na 'watoto wa mjini' niliokuwa nao wanadai hatapata kitu 2010. Wanadai kila akija jimboni anaishia 'kuwagongea' dada zao, kuzungusha round kwenye mabaa na kushinda na jamaa mmoja kinyozi ambaye ndiye anamtegemea kumpa taarifa za yote yanayojiri jimboni hapo. Kuna wasiwasi pia kwamba majukumu ya uwaziri aliyopewa yamemtia woga wa kupigania maslahi ya watu wake na kumnyima muda wa kushughulikia kero za wapiga kura wake.

Tatizo la barabara lipo lakini sidhani kama ni kubwa sana kwa kuwa zinapitika hata mvua ikinyesha, although something needs to be done kuhusu barabara ya Same-Kisiwani-Gonja-Ndungu- Kihurio kwa kuwa ni muhimu kwa biashara na inaserve idadi kubwa ya watu. Matatizo makubwa ya Same kwa uzoefu wangu ni maji, njaa na ajira:

1.Maji- mabomba mengi yaliyopo kwenye majumba ni kama mapambo tu kwa miaka mingi,
kila mbunge anayekuja anaahidi kulipatia ufumbuzi hili tatizo lakini wote wamechemsha
so far.
2.Njaa- naamini hili linaletwa na ukame ambao umeigubika wilaya hiyo kwa miaka mingi,
na kwa kuwa kuna ukosefu wa maji ya bomba, kilimo kitaendelea kuwa mazingaombwe.
3.Ajira- Enzi za Mgonja kulikuwa na kiwanda cha mafuta ya pamba cha PADECO na kile
cha vyombo vy udongo cha KIDC na kweli wakazi wengi walikuwa na ajira zao huko,
lakini the sad story ni kuwa vimekufa, yamebaki majengo na mitambo tu!

Naamini kabisa haya ni matatizo ambayo yako ndani ya uwezo wa mbunge, kama angepatika mbunge mkali akaikoromea serekali, akawa lobbyist mzuri, akawa anaorganise fund rising kwa ajili ya jimbo lake,etc naamini inawezeka kabisa.
 
Hoja ya ndugu yetu Bangusule ina maana kiasi kidogo sana. Ina maana kwasababu matatizo yapo na yanahitaji kutatuliwa. Haina maana sana kwa sababu anaitoa bila kuwa na vielelezo vya kutosha kuhusiana na sababu za kuwepo matatizo hayo, na hatua ambazo wananchi wa Same wameshachukua kutatua matatizo hayo. Ama sababu zilizotolewa hazitoshi asilani.

Wakuu, mimi nimesoma thread yote na kusikitishwa sana na maendeleo yanayodorora ya Wilaya ya Same kama ambavyo Bangusule ameyataja. Kama kweli hali ndio hiyo, basi jitihada za haraka zinatakiwa kuchukuliwa na wote wenye mapenzi mema na maendeleo ya Same.

Kutokana na maelezo yaliyotangulia, inaelekea tatizo ni la kiWilaya zaidi ya kiJimbo. Inaelekea uongozi wa wilaya una matatizo. Wana Same wanatakiwa waangalie matatizo hayo kutokea wilayani kuanzia Halmashauri nzima ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya, Watendaji wote wa Wilaya, Makatibu Tarafa, Maafisa Elimu na Maafisa Kilimo, Diwani na pia Mbunge wao. Kurukia moja kwa moja kuwa tatizo ni wabunge, sidhani kuwa ni sahihi. Si sahihi kwasababu hata wakibadilishwa wabunge hao, bila kuangalia utendaji wa wengine wote waliopo, si ajabu tatizo likawa kubwa zaidi. Kama kuna nia ya kupata utatuzi, basi wana Same waache siasa za lawama kwa waBunge, waanze kutafuta solution ya matatizo yao.

Siamini hata kidogo kuwa matatizo hayo yametokea baada ya waBunge hao kuingia madarakani miaka mitatu iliyopita. Matatizo yaliyopo yamesababishwa na wananchi na baadhi ya viongozi waliopo Same. Ni wananchi wa Same ndio wenye uwezo wa kuyatatua matatizo yaliyopo. Fanyeni yaliyo-mema kwa Same yenu ili mpate maendeleo mnayoyahitaji. Msisubiri mpaka uchaguzi ufike halafu muanze kulaumu, hamtapata maendeleo yoyote kwa namna hiyo, zaidi ya kuacha donda kuwa gumu kutibika na kuzama kwenye ufukara. Mbunge hana uwezo mkubwa wa kutatua matatizo yote, hasa kama wananchi hawataki kuyatatua.

Mkitaka, badilisheni Mbunge, halafu muone kama mtapata suluhu kutoka kwa Mbunge huyo mpya. Tatizo liko mikononi mwenu Ngugu yangu Babgusule, acheni kulitafuta kwenye mikono ya wengine.

Recta,

Sikubaliani na wewe kabisa kwenye hili. Labda ili kusaidia inabidi ku define maana ya kiongozi au uongozi. Kwa kifupi uongozi tunaweza kusema ni uwezo wa kuonyesha njia pamoja na ku mobilize watu pamoja na resources zingine kwa ajili ya kutimiza lengo fulani.

Sasa kwenye wilaya, mwakilishi wa wananchi kwa sehemu kubwa ni mbunge na madiwani. Hawa ndio wamechaguliwa na wananchi ili wawe vinara wao na wawasaidie kufanya hizo kazi mbili za uongozi; kuonyesha njia (vision or strategy) na mobilization of resources.

Maendeleo ya wilaya yanapoanguka, kwa wananchi, watu wa kuwabana ni wabunge, madiwani na serikali kuu. Kwa rais na serikali yake anawabana wakuu wa wilaya na watendaji wengine.

Kama ni kweli maendeleo yanaporomoka wilaya ya Same, ni dalili tosha viongozi waliopo wameshindwa kazi. Kwa mkazi ni obvious lawama zake atapeleka kwa wabunge na madiwani.
 
hali ya maendeleo katika wilaya ya Same imedorora tangu Dr.Mathayo na Anna Kilango wachaguliwe kuwa wabunge wa same magharibi na same mashariki.

- Mkuu huu wako ni uongo either wa makusudi au wa kutokujua kinachoendelea huko Same Mashariki, ambako binafsi nimeshikri sana katika kumsaidia mbunge wa hilo jimbo kuepeleka vitu muhimu sana vilivyokuwa vinakosekana katika jimbo hilo toka Tanzania tupate uhuru. Nimeshiriki kutafuta hela za visima 30 vya kisasa ambavyo vinajengwa sasa hivi huko na taifa zima linafahamu, na pia nimeshiriki kupeleka baiskeli za walemavu 20, walemavu ambao katika maisha yao yote toka tuwe huru wamekuwa hawawezi kushiriki kwenye shughuli za maendeleao ya jimbo lao kwa sababu ya kukosa baiskeli za kutokea nje ya nyumba zao ni hivi karibuni tu baada ya kukabidhiwa baiskeli hizo na mbunge huyu ndio wamtoka rasmi nje na kuanza kushirki katika shughuli za jimbo lao,

- Ni kweli kuwa kuna wachache walioko humu Jf ambao wako nje ya nchi ndio unaonekana kuwapata na huu wako ambao ni uongo wa mchana, ndio maana niliwahi kumwambia mbunge wa huko anapokwenda kufanya shughuli zake aende na waandishi wa habari ili wapime kila wakati amefikia wapi na maendeleo, na siku zote mbunge wa huko anaenda na waandishi na hata ninapoandika sasa hivi yupo huko Same East, nimeongea naye jana tu na siku zote habari za huko ziko kwenye taifa kutokana na profile ya bunge machachari wa huko, kwa hiyo mkuu wangu kama ni kilaza basi hapa ukweli unajiweka wazi kwamba exactly nani ni kilaza.
 
hali ya ELIMU ni mbaya sana. wilaya ya same imeshika mkia katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba na ule wa kidato cha nne.

- Hili ni tatizo la taifa zima infact kuna wanafunzi waliopasi kwenda form one na hakuna shule za kwenda hii kwa national level sasa unasema ni mbunge wa Same East ndio anahusika na kushuka kwa elimu au kukosekana kwa shule za sekondari kwa ajili ya wanafunzi wapya katika taifa?,

- Tanzania sasa hivi kama taifa tumetoka hata kwenye ripoti za elimu za dunia na Africa, ambako zamani katika Africa tulikuwa namba moja na sasa hata kwenye kumi za mwisho hatumo, unasema na hili nalo ni tatizo la mbunge wa Same East?

Hizi hukumu ulizitoa toka mwanzoni mbunge mpya alipochaguliwa, na mpaka leo naona umeamua kuzi-upgrade, mkuu naomba ukae pembeni waachie wananchi wa Same East wanufaike na maendeleo wanayoletewa na mbunge wao mpya, tena naomba nikufahamishe wkamba mafisadi sasa hivi wamepleka watu kuwasumbua wabunge wote wapiganaji, lakini hakuna fisadi anayeweza kufikiria hata for one second kupeleka mtu Same East kumsubua Mama Super K, never maana mafisadi wote wanajua cha moto huo, na hakuna mwananchi wa Same East anayeweza hata kuwasikiliza, kuanzia wewe na hao mafisadi kina Mama Kaboyoka, ambao wamekuwa wakipokea hela kutoka kwa a known fisadi Yona hata wakati wa uchaguzi uliopita wananchi walikataa na kumchagua Mama Super K, sasa mkuu cha muhimu ni kwamba kama mna ubavu basi jitoseni tena kwenye uchaguzi muone kama kilichowapta uchaguzi uliopita!

- Agaion si unaona sasa kilaza ni nani kati ya wewe mpiga debe wa Mama Kaboyoka na mbunge aliyechaguliwa na wananchi wa Same East?
 
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuisifu wilaya yetu na kutuita "Wachina" wa Tanzania. nina hakika akifufuka leo na kushuhudia uongozi mbovu wa Dr.Mathayo na Anna Kilango, akaona na matokeo ya mitihani ya watoto wetu atageuza kauli yake na kutuita "VILAZA" WA KILIMANJARO.

Hivi wewe kweli unauweza huo ubunge?, maana hata kazi za wabunge huzijui unakurupuka na kutupa lawama kwa Ng'ombe wakati mboga imeliwa na Paka. Ukitaka kujua ni nani mwenye majukumu hayo rejea wilaya ya Bukoba, aliyewacharaza viboko walimu ni mkuu wa wilaya si mbunge.

Unaposema kuhamasisha maendeleo ni hamasa gani hiyo wakati mbunge hata resource hana, unaposema kuwa wa mwisho unataka mbunge akafundishe. Wewe hoja yako ni butu labla toa maelezo zaidi ni jinsi gani wilaya ya Same wabunge wake wapo tofauti na wa sehemu nyingine kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano hapo unaweza pata sababu na sauti ya kuleta kitchen sink politics hapa. Wewe kama unataka kugombea ubunge ulitakiwa ufanye kampeni hizi miaka mitano iliyopita, zunguka jimboni toa misaada lipa walimu vizuri, wajengee nyumba bora ili watoto wapate huduma bora ya elimu. Ila wabunge wa sasa ninapojua hawapewi fedha za kujenga madaraja, shule na vitu vingine majimboni mwao zaidi ya kuwasikiliza wapiga kura wake na kupeleka mawazo yao bungeni. Sasa walaumu kwa kutowakilisha mawazo ya watu wa Same kama wewe kuwa hamtaki mafisadi waguswe n.k
 
- Mkuu huu wako ni uongo either wa makusudi au wa kutokujua kinachoendelea huko Same Mashariki, ambako binafsi nimeshikri sana katika kumsaidia mbunge wa hilo jimbo kuepeleka vitu muhimu sana vilivyokuwa vinakosekana katika jimbo hilo toka Tanzania tupate uhuru. Nimeshiriki kutafuta hela za visima 30 vya kisasa ambavyo vinajengwa sasa hivi huko na taifa zima linafahamu, na pia nimeshiriki kupeleka baiskeli za walemavu 20, walemavu ambao katika maisha yao yote toka tuwe huru wamekuwa hawawezi kushiriki kwenye shughuli za maendeleao ya jimbo lao kwa sababu ya kukosa baiskeli za kutokea nje ya nyumba zao ni hivi karibuni tu baada ya kukabidhiwa baiskeli hizo na mbunge huyu ndio wamtoka rasmi nje na kuanza kushirki katika shughuli za jimbo lao,

- Ni kweli kuwa kuna wachache walioko humu Jf ambao wako nje ya nchi ndio unaonekana kuwapata na huu wako ambao ni uongo wa mchana, ndio maana niliwahi kumwambia mbunge wa huko anapokwenda kufanya shughuli zake aende na waandishi wa habari ili wapime kila wakati amefikia wapi na maendeleo, na siku zote mbunge wa huko anaenda na waandishi na hata ninapoandika sasa hivi yupo huko Same East, nimeongea naye jana tu na siku zote habari za huko ziko kwenye taifa kutokana na profile ya bunge machachari wa huko, kwa hiyo mkuu wangu kama ni kilaza basi hapa ukweli unajiweka wazi kwamba exactly nani ni kilaza.

Mkuu FMES,

Kwi kwi kwi!!! nimecheka sana huu mchango wako.

Binafsi silijui jimbo la Same ila kwa experience yangu na majimbo mengine ya Tanzania kinachotakiwa na ambacho kinakosekana zaidi ni leadership and not sponsorship.

Misaada ni muhimu tu kuongezea pale ambapo kuna juhudi za wazi za ku mobilize resources zilizopo ili zisaidie kuwaletea wananchi maendeleo.

Nimeona miradi ya maana inayojengwa na wageni na inakufa siku tu wanapoondoka.

Kinachoendelea sasa kwenye majimbo mengi ya Tanzania ni wabunge kufanya ziara kwenye majimbo yao na kugawa misaada michache waliyotafuta huko Dar au nje na kuamini wanaleta maendeleo.

Nina wasiwasi sana kama strategy kama hiyo inafanya kazi.
 
Kitu kimoja ambacho nimejifunza hapa JF ni kwamba kuna makundi mawili makuu ya waandishi. Kuna wachangiaji wa mada (positively) na washabiki wa mada. Kundi la kwanza, yaani wachangiaji wa mada wanaelewa umuhimu wa kuelimishana na wanaamini kabisa maoni na mchango wao unaleta impact fulani katika jamii. Kundi la pili, yaani kundi la washabiki, wanaamini kabisa kwamba hiki ni kijiwe cha wahuni tu waliokosa kazi na wanakuja kupoteza muda wao. Kundi hili linaweza kuamua kumshabulia mtoa mada negatively tu, hata kama wao wenyewe hawana ushahidi wa kutosha.

Nimesema haya baada ya kupitia posts zote zilizochangia hii thread. Kuna waliomponda Bangusule bila wao kutoa ushahidi wowote. Kuna waliomponda na kutoa ushahidi wao (kama alivyofanya FMES). Na kuna wale pia walioshabikia tu positively bila kuwa na vigezo. Labda ningependa kusema tu kwamba, kama huna ushahidi na yale unayotaka kuchangia, ni bora tu ukatoa maoni ambayo hayataathiri mtiririko wa mada. Bangusule katoa ushahidi wa matokeo ya kidato cha nne kama kielelezo kwamba wilaya ya Same inafanya vibaya katika masomo. Hili bado mnalipinga? Website ya matokeo ipo na mnaweza kwenda kuangalia. FMES katoa hoja kuhusu uchimbwaji wa visima. Hili hatuna ushahidi nalo, lakini FMES anaweza kuweka ushahidi wake.

All in all, kazi ya wabunge ni kuwakilisha kero na maoni ya wananchi waliowachagua. Bangusule kama mkazi wa Same ana kila haki ya kuhoji wabunge wake pale anapoona hali ya maendeleo sio kama anavyotarajia.
 
- Hili ni tatizo la taifa zima infact kuna wanafunzi waliopasi kwenda form one na hakuna shule za kwenda hii kwa national level sasa unasema ni mbunge wa Same East ndio anahusika na kushuka kwa elimu au kukosekana kwa shule za sekondari kwa ajili ya wanafunzi wapya katika taifa?,

- Tanzania sasa hivi kama taifa tumetoka hata kwenye ripoti za elimu za dunia na Africa, ambako zamani katika Africa tulikuwa namba moja na sasa hata kwenye kumi za mwisho hatumo, unasema na hili nalo ni tatizo la mbunge wa Same East?

Mkuu FMES,

Hapa nakubaliana na wewe kwa asilimia 100. Tatizo la shule mbovu na zisizo na resources za kutosha ni tatizo la nchi nzima.

Ni matokeo ya sera mbovu za Lowassa kufikiri anaweza kujenga shule za secondary kila kata kwa muda wa miaka miwili.

Tatizo liko kwenye strategy ambayo ndio sisi Watanzania kama nchi tumeamua kufuata, hii ya kwamba quantity ni bora kuliko quality.

Ndio tunahitaji watoto wetu wengi zaidi wasome lakini sio kwa mwendo huo. Kama Lowassa alikuwa na jibu la kuongeza uwezo wa taifa kwenye elimu kwa asilimia zaidi ya 5000% kwa mwaka, tungempendekeza apate nobel prize ya Economics.

Bahati mbaya mkuu Pinda naye juzi katoa amri kama hizo hizo. Hawaongelei kabisa quality, wamekazania quantity.

Hii ni sera mbaya ya CCM na inaleta balaa kubwa kwenye elimu.

Ila tu kwa kiongozi makini inatakiwa asaidie kwenye wilaya yake au mkoa wake kupunguza hili tatizo la quality mbaya kwenye shule za seconday za kata.
 
Last edited:
katika suala la KILIMO ule mradi maarufu wa kilimo cha umwagiliaji Ndungu una hali mbaya sana. kuna maradhi ya mpunga yameingia na wakulima hawana msaada wowote toka kwa mbunge wao Anna Kilango.

- Visima 30 vipya vya maji, viemfunguliwa na rais wa jamhuri huku huizi habari zikiandikwa na media zote za bongo, na mpaka siku hiyo wananchi wa Same East kwa furaha kubwa wakampa zawadi ya kondooo wawili rais wa jamhuri ambao mpaka leo ukipita pale Ikulu kule nyuma kulikouwa na mbuni zamani utawakuta, wewe unasema uongo huu wa mchana bila hata aibu mkuu vipi?

- Sasa unafikiri Mama Super K, alitafuta hivi visima kwa ajili ya nini kama sio wakulima wake na hasa mashamba yao ya mpunga? Mkuu wangu Iowa State kuna kijana mmoja anayetoka jimbo hilo la Same East, ambaye amepigana sana kuepeleka madawa na misaada mbali mbali akishirkiana na mbunge wake kwa ajili ya mashamaba ya mpunga infact in the next three weeks mbunge huyu anatakliwa kwenda Iowa, kuwakilisha makadiro yote ya misaaada inayotakiwa huko, ili wafadhili waliotafutwa na huyu kijana waweze kutoa msaada huo, na ni ishu ambayo hata bunge zima la Tanzania limefahamishwa na hata Spika ambaye kwa kuguswa na hilo la huyu kijana wa Iowa na mbunge, wamewaalika wafadhili rasmi kutembelea bunge, watakapokuja bongo next month, sasa wewe wenzako wa kutoka hilo jimbo wanashughulika badala ya kusubiri mbunge, wewe uko hapa kupiga domo na kukshifu kiongozi si unaona sasa maana hasa ya kilaza hapa kwamba wewe ndiye hasa kilaza tena wa mchana, maana mimi nafahamu vilaza wengi huwa wanakuwa wa usiku watu wakiwa wamelala, au?

Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuisifu wilaya yetu na kutuita "Wachina" wa Tanzania. nina hakika akifufuka leo na kushuhudia uongozi mbovu wa Dr.Mathayo na Anna Kilango, akaona na matokeo ya mitihani ya watoto wetu atageuza kauli yake na kutuita "VILAZA" WA KILIMANJARO.

- Aliwaita "Wachina" wa Tanzania kwa sababu ya huu uchina wako unaouonyesha hapa, wa kutokujua kinachofanyika kwenye jimbo na kukimbilia huku JF kutukana viongozi ambao hujawahi kuwa na heshima nao hata toka walipochaguliwa kwa sababu mgombea uliyemtaka alikataliwa na wananchi sasa since then umakuwa na kilio sana na mbunge wa Same East ambacho huwa tunaita kilio cha wachina kama Mwalimu alivyowaita.

- Mimi sijawahi kusikia kwamba Same East iliwahi kuwa na maendeleo kuliko majimbo yote ya bongo wakati wa Mwalimu, mpaka kuifkia kuitwa wachina na Mwalimu that is nonesense ambayo sielewi mkuu umeitoa wapi, Mwalimu akifufuka leo atakuona wewe ndiye kilaza tena wa ajabu sana kwa sababu wakati mbunge anawatafutia maji wananchi wake tena kwa hela za misaaada na wafadhili toka ndani na nje badala ya kukaa akiomba msaada wa serikali, wewe unalilia kumtukana haya matusi ya nguoni ndio hasa ukilaza wa mchana mkuu, sisi tumezoea kuona vilaza wa usiku sio wa mchana kama wewe, next time kabla hujarukia jimbo la wananchi jaribu kutafuta facts kwanza, otherwise unakwua kilaza wa mchana mkuu.

Sasa hivi mkuu wangu niko jela DC ninasubiri kuona jamaa zetu walioko rumande, lakini nitakurudia tena baadaye maana ni muhimu kuweka record staright.

Thanxs!
 
Sunday, 16 March 2008, Habari Leo

Mbunge huyu awe mfano

Dk. Shukuru Kawambwa akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Same Mashariki wakati akizindua miradi ya maji ya kisima iliyojengwa kwa juhudi za mbunge wa jimbo hilo Bi. Anne Kilango Malecela. Mwishoni mwa mwaka 2007 aliyekuwa Waziri wa Maji Dk. Shukuru Kawambwa alifanya ziara katika mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza, Mara na Shinyanga, ziara iliyokuwa na lengo la kukagua ujenzi wa miradi ya maji pamoja na kuzindua visima vya maji.

Kati ya mikoa hiyo aliyotembelea mhe. Waziri wa Maji mkoa wa Kilimanjaro ziara yake ilielemea zaidi kwenye uzinduzi wa visima tofauti na mikoa mingine.

Wilayani Same katika jimbo la Same Mashariki Dk. Kawambwa alizindua jumla ya visima ishirini vyenye thamani ya shilingi milioni 40 kwenye tarafa ya Gonja katika zile kata za Mtii, Bombo, Vuje pamoja na ile tarafa ya Ndugu kata ya Kihurio. Visima vyote alivyozindua Dk. Kawambwa vimefungwa kwa pampu za mkono na kufuata vyanzo vya asili lengo likiwa kurahisisha upatikanaji maji hasa ikizingatiwa upatiakanaji maji chini ya ardhi ya milima ni migumu.

Miradi hiyo ya visima iliyozinduliwa Wilayani Same imeinua asilimia ya upatikanaji wa maji ya bomba kutoka makisio ya asilimia 5 katika kata ya Mtii hadi 30, asilimia 20 kata ya Vuje hadi 35, asilimia 43 kata ya Kihurio hadi 62 na ile asilimia 12 kata ya Bombo hadi 25. Kwa sasa asilimia 70 ya wananchi wa jimbo la Same Mashariki wanaishi milimani ambako kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa maji na kusababaisha asilimia 30 ya wakazi wa eneo hilo kupata magojwa yanayotokana na maji yasiyo salama.

Wakati wa ziara yake katika jimbo hilo la Same Mashariki Dk. Kawambwa alipongeza jitihada binafsi za mbunge wa jimbo la Same Mashariki Bi. Anne Kilango Malecela za kuasaidia upatikanaji huduma za majisafi na salama katika jimbo lake kutoka asilimia 46.5% hadi 49% Pongezi hizo za Waziri wa Maji kwa mhe. Anne Kilango Malecela zinastahili kabisa kwa kuwa mbunge huyo alipagana kufa na kupona kuhakikisha anawapatia wapiga kura wake huduma ya majisafi pasipo kuitegemea zaidi serikali.

Nilipozungumza naye, mbunge huyo wa jimbo la Same Mashariki alisema anajisikia faraja sana anapoona wapiga kura wake wanapata huduma ya majisafi na salama jambo alilosema lilikuwa likimuumiza kichwa kwa muda mrefu. Aliongeza kwa kusema, upatikanaji huduma hiyo ni jitihada yake binafsi ya kusaka wafadhili wa kumsaidia kuwapatia huduma hiyo ya maji wananchi wake ambayo imekuwa adimu jimboni mwake na wilaya nzima ya Same.

Aliyataja baadhi ya makampuni yaliyomsaidia kufadhili ujenzi wa miradi hiyo ya visima kuwa ni kampuni za simu za Tigo na Vidacom, mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) pamoja na kampuni ya kifaransa ya Express, Wafadhili wa Iowa Satte Lited. ‘’Makampuni ya ndani nayo yanafadhili sana ili mradi mtu ujue namna ya kuandika proposal yako’’ Alisema Bi. Kilango

Alieleza kuwa, mkakati wake wa kuawapatia wananchi wa jimbo la Same Mashariki huduma ya majisafi umelenga kwenda kata hadi kata na kuongeza kuwa yeye akiwa mbunge atajisikia faraja sana pale atakapoona wapiga kura wake wanapata huduma ya majisafi na salama katika kiwango cha asilimia mia moja. Kwa upande wake Dk. Kawambwa alisema katika kuhakikisha tatizo la maji linatokomezwa mkoani Kilimanjaro serikali iko mbioni kuanzisha mradi mkubwa wa kitaifa unaojulikana kama mradi wa Tambararre ya Pare, mradi unaokadiriwa kugharimu shilingi bilioni 38.

Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa, mradi huo utakapokamilika utanufaisha vijiji 36 kutoka wilaya za Same na Mwanga zilizoko mkoani Kilimanjaro na ile sehemu ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Vijiji vitakavyonufaika na mradi huo mkubwa ni vile vya Hedaru, Mabilioni,GevaMakanya,Mgurasi,Bangalala,Chajo,Mwembe,Njoro,Ruvumferejini,Ruvu jiungeni,Majengo,Bendera,Mkonga Ijinyu na Mgandu vyote kutoka wilaya ya Same.

Vingine ni Kifaru,Kiruru Ibwejewa,Kisangara, Lembeni , Kiverenge,Kiti cha Mungu,Mbambua, Kileo,Kivulini,Kituri,Mgagao,Handeni,Langata Bora,Langata Kangongo, Nyabinda na kijiji cha Kirya vyote kutoka Wilaya ya Mwanga.

Kwa upande wa Wilaya ya Korogwe maeneo yatakayofaidika ni vijiji vya Bwiko,Mkomazi, Nanyogie,Manga, Mtindilio na Mikocheni

Waziri huyo wa Maji alibainisha kuwa, katika kuhakikisha mradi huo unaanza haraka tayari serikali imeomba ufadhili wa mradi huo kutoka Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Afrika (BADEA) ili isaidia ujenzi wa mradi.

Mbali na jitihada zinazooneshwa na serikali kuwapatia wananchi wa Wilaya ya Same huduma ya majisafi na salama lakini bado juhudi binafsi zilizooneshwa na mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Bi. Anne Kilango Malecela ambaye hivi karibuni alijipatia umaarufu katika sakata la Richmond zinapaswa kuigwa na wabunge wengine wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mara kwa mara tunashuhudia malalamiko ya baadhi ya wabunge kuilaumu serikali kushindwa kupeleka huduma kwa wananchi ikiwemo huduma ya majisafi na salama, kwa kiasi fulani lawama hizo zinaweza kustahili lakini isiwe kigezo cha mbunge kuacha kufanya juhudi za kuwapelekea maendeleo wapiga kura wake kwa kisingizio cha serikali kufanya kazi hiyo.

Iwapo wabunge wataiga mfano wa Bi. Anne Kilango Malecela basi uwezekano mkubwa wa Tanzania kupiga hatua katika nyanja tofauti ni mkubwa sana kwani kila mtu atakuwa anajua wajibu wake kama mbunge na kamwe hawezi kuwa tegemezi wa serikali. Mbunge huyo machachari alisema mtazamo wake mkubwa kwa sasa kama mbunge ni kutaka kuwaona wapiga kura wake wakiishi maisha mazuri na kuondokana na umasikini na magonjwa ambavyo vyote kwa pamoja vinaweza kuwafanya warudi nyuma kimaisha.
 
Unaposema kuhamasisha maendeleo ni hamasa gani hiyo wakati mbunge hata resource hana, unaposema kuwa wa mwisho unataka mbunge akafundishe. Wewe hoja yako ni butu labla toa maelezo zaidi ni jinsi gani wilaya ya Same wabunge wake wapo tofauti na wa sehemu nyingine kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano hapo unaweza pata sababu na sauti ya kuleta kitchen sink politics hapa. Wewe kama unataka kugombea ubunge ulitakiwa ufanye kampeni hizi miaka mitano iliyopita, zunguka jimboni toa misaada lipa walimu vizuri, wajengee nyumba bora ili watoto wapate huduma bora ya elimu. Ila wabunge wa sasa ninapojua hawapewi fedha za kujenga madaraja, shule na vitu vingine majimboni mwao zaidi ya kuwasikiliza wapiga kura wake na kupeleka mawazo yao bungeni. Sasa walaumu kwa kutowakilisha mawazo ya watu wa Same kama wewe kuwa hamtaki mafisadi waguswe n.k

Mkuu Hofstede,

Kama kazi na wajibu wa mbunge ni kama ulivyoandika hapo juu, tunapoteza bure kuwa na majimbo ya uchaguzi. Hizo pesa tungezitumia kwa kazi zingine.

Binafsi ningetaka kuwa na mbunge ambaye ana uwezo wa kumobilize resources zilizopo wilayani ili kusaidia kusukuma maendeleo ya wilaya. Ningetaka hii ndio iwe kazi kubwa ya mbunge, ukiachia ya kutunga sheria na kuikosoa serikali.

Kwa taarifa yako pesa nyingi zinapotea wilayani kwenye halmashauri, shauri ya kukosa uwezo na pia ufisadi. Laiti tungelikuwa na viongozi ambao wanaweza kusaidia kuhakikisha kile kidogo tulicho nacho kinatumiwa vizuri na kwa miradi inayoongeza tija, naamini tungekuwa tunasogea mbele. Mbunge mara nyingi ni katika watendaji wasomi walioko wilayani, inatakiwa awe chanzo na cheche ya maendeleo jimboni kwake.
 
Last edited:
FMES,

kwenye sifa tutatoa sifa na kwenye lawama tutatoa lawama. nampongeza mbunge kwa kujenga visima 30 na kutoa baiskeli 20 kwa ndugu zetu walemavu.

pamoja na kutoa pongezi hizo naomba kumkumbusha kwamba tuna matatizo makubwa sana ya elimu ktk wilaya yetu. matatizo hayo ameyakuta na hatuoni juhudi zozote katika kuyashughulikia. kama kuna lolote ambalo mbunge amefanya, basi tulipaswa kuona mabadiliko katika matokeo ya darasa la 7 na kidato cha 4.

SAME YASHIKA MKIA MATOKEO DARASA LA 7

na Dixon Busagaga

"SHULE ya Msingi ya Scolastica iliyopo Wilaya ya Moshi Vijijini imeongoza shule za msingi za mchepuo wa Kiingereza katika matokeo ya mtihani wa mwisho wa darasa la saba, mkoani Kilimanjaro.

Katika matokeo hayo shule za mchepuo wa Kiingereza zimefanya vizuri ukilinganisha na shule za msingi za kawaida ambapo kati ya shule 854 za msingi mkoani hapa, shule hizo zimeshika nafasi saba juu.

Afisa elimu wa mkoa wa Kilimanjaro,Theodory Massawe, alisema Wilaya ya Same imeonekana kufanya vibaya kwani kati ya shule kumi zilizofanya vibaya mkoani hapa, shule tisa zimetoka katika wilaya hiyo."

Alizitaja shule zilizofanya vizuri na wilaya zake katika mabano kuwa ni Katola(Mwanga), St Anne(Moshi vijijini) ,St Joseph(Rombo), Mudio Islamic(Hai), Royal(Moshi Vijijini), Kea(Moshi mjini), na Moshi Airport(Manispaa Moshi), Matala (Moshi Vijijini) na Eden Garden(Moshi Mjini).

Massawe alizitaja shule kumi zilizofanya vibaya na wilaya zake kwenye mabano ni Lekrimuni (Siha), Marindi, Makokane, Meserani, Maganda, mtundu, Kidundai Kadando, Ngama, na Emuguri zote kutoka Wilaya ya Same."
 
FMES katoa hoja kuhusu uchimbwaji wa visima. Hili hatuna ushahidi nalo, lakini FMES anaweza kuweka ushahidi wake.

- Mkulu wangu Zero, najua kua una akili sana bwa! ha! ha! ha!, haya kula ushahidi hapo juu bro!
 
FMES,

kwenye sifa tutatoa sifa na kwenye lawama tutatoa lawama. nampongeza mbunge kwa kujenga visima 30 na kutoa baiskeli 20 kwa ndugu zetu walemavu.

- Mkuu unasema unampongeza mbunge kilaza sasa baada ya kupewa ukweli ambao huujui, badala ya kuomba radhi kwa kukurupuka unatoa pongezi sasa baada ya kujaribu kuwadnagnya wananchi hapa JF kwamba huyu mbunge hafai? Tena ukamuita kilaza wakati wewe ndiye kilaza hasa kwa kurukia usiyoyajua badala ya kuuliza kwanza usaidiwe wewe umekurupuka na hukumu huku huna dataz wala facts, sasa kwa nini usikubali tu kuwa wewe ndiye kilaza hapa tena wa mchana!

pamoja na kutoa pongezi hizo naomba kumkumbusha kwamba tuna matatizo makubwa sana ya elimu ktk wilaya yetu. matatizo hayo ameyakuta na hatuoni juhudi zozote katika kuyashughulikia. kama kuna lolote ambalo mbunge amefanya, basi tulipaswa kuona mabadiliko katika matokeo ya darasa la 7 na kidato cha 4.

- Mkuu unazidi kunishangaza wewe ni mwananchi wa jimbo la Mama Anne Super K, ya baiskeli za walemavu hukuyaona, ya visima kama ushahidi ulivyo hapo juu hukuyaona, sasa eti unataka hapa JF tuamini kwamba umeyaona ya elimu ya huko "jimboni kwako?" Same East wewe mwenyewe huoni kwamba huna credibility tena mpaka hapo peke yake!
 
Back
Top Bottom