Dr Mary Nagu: Bunge Sasa Lina Amani

Dr Mary Nagu: Bunge Sasa Lina Amani

Dr Mary Nagu amesema Bungeni jioni hii kuwa Bunge sasa lina amani sana baada ya wenzetu wale wanaoleta vurugu kuwa nje!
Pia amesema kuwa vurugu zinazotokea mara kwa mara Bungeni kwa sasa zimehamia mtaani maana waleta fujo wako huko.

Kwa mtu makini yeyote Bunge la tokea Jumatatu limepooza sana, likiwa limejaa makofi na Pongezi.


weweeeeeeee yahaya unaishi wapi?
longo longo nyingi saaana
 
EE MUNGU wa Israel tunakuomba ujidhihirishe tu walau kwa siku moja tu kufuatia hofu inayoendelea kutanda kufuatioa yanayotokea Arusha na kwingineko.

Mungu tunakuomba uonekane tu kwa siku moja sisi tulio wanyonge tunaangamizwa. Wamebinafsisha nchi nzuri uliyotuumbia pamoja na raslimali za asili ulizotugawia wanyonge, sasa wanawaita mataifa makubwa waje kutunyang'anya wakiwaita wawekezaji. MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo wameidhinisha tupigwe eti kwa sababu tunaulizia kinachoendelea, MUNGU sikiliza maombi yetu.

Tunakushukuru kwa kutuletea waassis kama Nyerere Karume na akina Sokoine waliotuachia alama za umoja na upendo sisi tulio wanyonge, sasa wapo mabingwa wa kunadi raslimali na kupiga mnada kila kitu ee MUNGU sikiliza kilio chetu AMEN

Kunachochote ulichofanya kuondoa hayo yasiyo mema?kama bado utakuwa unataja jina la mungu bure

japokuwa sifam biblia lakini nadhan kuna maneno yanayofanana na "Jisaidie na me nitakuwa nawe"
yaani fanya jambo fulani kisha uombe msaada wa mungu..
 
Wanadhani wananchi wa miaka ya 1992 bado ni walewale, ambao walikuwa wanaendeshwa kwa propaganda ya fikra za mwenyenyiti, nchi zote zilizoendelea zinakubali changamoto ktk serikali zao na kuzifanyia kazi, tatizo Tanzania viongozi wetu wako kichama zaidi kuliko kuwahudumia wananchi, this Tanzania is for Tanzanians and not for a certain political party, I support any political party which is fighting for well being of its citizen
 
Jioni ya leo ndio nimeamini Hawa viongozi wakiongozwa na Mwigulu Nchemba, Nagu, Hawa Ghasia na wengine nimekubali wana mambo ya hovyo, badala ya kuchangia bajeti wao wanazungumzia beyond doubt kwamba chadema ndio waleta vurugu na Ghasia kaenda mbali zaidi kwa kuwatuhumu ndesa na Mbowe kwamba wakanda wanasababisha vurugu kwa wenzao.

Je mahakama imethibitisha ni CDM?
je tufikirieje kwamba ni wenyewe ndio wauwaji ndio wanajisafisha?
Je tutajuaje kwamba ndio mbinu mpya baada ya kuona wameshindwa?
Kwa hakika nimeona hakuna weledi kabisa kwa watu hawa

Nafikiri viongozi wangu hawa wamebaki kuzungumzia watu, udini, ukanda, ukabila n.k kwasababu yale ya msingi chama chetu kimeshindwa kabisa.

Mfano CCM watazungumzia nini kuhusu Elimu?
- CCM watazungumza nini kuhusu Ajira kwa vijana?
- CCM watazungumza nini kuhusu ulinzi na usalama wakati huu?
-CCM watazungumza nini kuhusu faida za uwekezaji?
-CCM watazungumza nini kuhusu kodi?
-CCM watazungumza nini kuhusu Reli?
-CCM watazungumza nini kuhusu bandari?
-CCM watazungumza nini kuhusu Maji?
-CCM watazungumza nini kuhusu Shirika la ndege la Taifa?
naweza kuendelea kuorodhesha mpaka kesho, kwa hali ilivyo mtazamo wangu ni kwamba viongozi hawa wamefilisika kisera chama chetu kimeshindwa kila kona, kazi iliyobaki ni kuzungumzia watu na kupandikiza chuki za kikabila, kidini, kikanda, TUWAOMBEE VIONGOZI WETU KWA MUNGU KWASABABU HAWAJUI WAFANYALO....
 
Dr Mary Nagu amesema Bungeni jioni hii kuwa Bunge sasa lina amani sana baada ya wenzetu wale wanaoleta vurugu kuwa nje!
Pia amesema kuwa vurugu zinazotokea mara kwa mara Bungeni kwa sasa zimehamia mtaani maana waleta fujo wako huko.

Kwa mtu makini yeyote Bunge la tokea Jumatatu limepooza sana, likiwa limejaa makofi na Pongezi.

Bunge halijapooza sema tatizo lenu mmezoea kusikia matusi na malumbano.

Hivi ndivyo inavyotakiwa iwe watu wajibizane kwa hoja sio ku shout.
 
Wacha wapongezane si mafisadi hao watu wa kuwakemea hawapo.
Hii ni dhairi hata kibaka akiiba na akasepa bila kukimbizwa siku hiyo anajipongeza na kusema kuna amani.
Wabunge wete ndio hivyo tena wanashangilia na kuona wana amani na wametulia hili watuibie vizuri
 
Wanaomfuata hawa

Hawa-Ghasia1.jpg
1560.jpg

majanga ya kitaifa
 
Dr Mary Nagu amesema Bungeni jioni hii kuwa Bunge sasa lina amani sana baada ya wenzetu wale wanaoleta vurugu kuwa nje!
Pia amesema kuwa vurugu zinazotokea mara kwa mara Bungeni kwa sasa zimehamia mtaani maana waleta fujo wako huko.

Kwa mtu makini yeyote Bunge la tokea Jumatatu limepooza sana, likiwa limejaa makofi na Pongezi.

Hivi huyu bado yuko na waziri mkuu mstaafu au kesha-mpiga "Kibuti?" Ama kweli mazoea ya ushangingi yana tabu
 
Hiyo ndio amani wanayotaka CCM......KUTUKOSOLEWA NA KUZUIWA KUIBA......nyuma ya SHOPPERS PLAZA huyu mama kajenga ghorofa yake kubwa sana.....sijui kapata wapi pesa hiyo
 
Niliwaona wajinga wakimpigia makofi Pinda aliposema polisi wawapige watu wanaokaidi amri. CCM wabunge wengi ni magalasha tu sasa ukimjulisha na waziri mkuu mwenye kauli za hatari ambazo ni kinyume na katiba na haki za binadamu basi ujue hakuna kitu pale.
 
Kwao amani ni yale makelele ya ndioooo......baada ya kuibuka kutoka usingizini.
 
Unatafuta cheo kwa magamba ndio maana umeweka identity yako. Hupewi bila kuhonga.

Thanks for your opinion, but unapaswa kuelewa jambo kabla hujacomment. Nb. Usidhani kila mtu ni mwoga kama wewe, si lazima kila mtu atumie fake ID kama wewe foolish guy.
 
Thanks for your opinion, but unapaswa kuelewa jambo kabla hujacomment. Nb. Usidhani kila mtu ni mwoga kama wewe, si lazima kila mtu atumie fake ID kama wewe foolish guy.
Nimekwambia tu fact mkuu mara umeshanitukana. Magamba wanang'oa watu kucha macho na sasa wanapiga mabomu na kuua watu kwa kusema kweli. Sasa wewe kama unasema uwongo sawa unaweza kuwa na real identity ili wakifurahishwa wakupe cheo.
 
Back
Top Bottom