Kwanza ni ruhkusa kwa watu kujadili juu ya kesho yao ili waanze kutafakari juu ya makosa ambayo yamefanyika katika vipindi vingi vya kiutawala wa nchi hii toka uongozi wa mwl Nyerere ututoke uliotoa dira ya dhana nzima ya kiuongozi kuwa ni kuonyesha njia.Kuna watu wanajaribu kumbeza mleta hoja juu ya values za Dr kitila kuwa ama mgombea urais ama kuwa kiongozi mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania.
Kiufipi Dr KItila ana value zote za kuwa kiongozi wa watu katika ngazi yoyote ya kiutumshi wa ummah,nenda miaka ya nyuma alipoongoza Taasis ya Daruso utapata rekodi yake,njoo katika nafasi yake ya umoja wa wahadhiri kama makam M/kiti UDASA utapata rekodi yake,lakini pia utapata rekodi yake katika nafasi yake ya ukuu wa Idara ya Psychology pale mlimani,waulize wahadhiri na wanafunzi he is derivering.
Kuna watu wanadhani unaweza kuwa na sifa za kiuongozi katika kuongoza watu halafu uwezo huo ukufunge katika mipaka ya ubunge tuu,huku hawajui kwamba hata Rais anaongoza Taifa ambalo ni watu,mbunge naye anaongoza Taifa ambao ni watu.Hebu niambieni juu ya uzoefu wa Mwl Nyerere kuwa Rais nini kilimuwezesha ni ubunge,ubalozi,ualimu ama uwezo na uzalendo????hebu nielezeeni juu ya Mzee Mandela ni ubunge,uwaziri,ubalozi au ni uwezo na uzalendo???toka Nyerere ang'atuke hatujawahi kupata Rais Mwadilifu kama yeye japo hakuwahi kuwa waziri au mbunge wa Butiama!!Miaka mingi tumepatia kuchambua wale wote waliokuwa waandishi wake wa habari,mawaziri wake na wengine washauri wake wa kisiasa tukidhani kwamba labda watakuwa wameambukizwa uwezo,uzalendo na uadilifu!!! kumbe aah wapi all of them are " African crew of Bandity" japo wanauzeefu wa kutosha wa kuishi na mwl Nyerere,uzoefu wa kiutendaji lakini siyo uzoefu wa uzalendo,uadilifu na uthubutu wa kiuwezo.Mwl Nyerere hakuwahi kuwa mzoefu wa uongozi wa juu,ubunge au uwaziri zaidi ya uwezo,uadilifu,uzalendo na uthubutu bado aliweza kufanya maamuzi mazito yaliyo ifanya Tanzania ing'are katika jamii ya kimataifa.,misingi yote ya Taifa hili tunaililia juu ya ukabila,udini,mapengo ya kitabaka,mshikamano wa kitaifa ulijengwa na mtu ambaye kabla ya hapo alikuwa haijui ikulu wala uzoefu wa kibunge,bali yote haya aliyajenga kwa silaha ya uzalendo,uadilifu na uwezo vitu ambavyo kwa anaye mfahamu dr Kitila hawezi kuvibishia.
Watanzania miaka KARIBU 35 YA CHAGUZI ZETU Tumeendelea kudiriki kuendelea kulewa na baadhi ya bandit leaders eti kwasababu wamewahi shika nafasi kubwa zilizo nyingi huku tukisahau kwamba mwl Nyerere aliyejenga misingi ya mishikamano ya Taifa hili alikuwa na silaha ya uadilifu,uzalendo na uwezo na siyo umaarufu wa vyeo vingi vya kisiasa.,tunaompinga mtu eti kwa sababu hajawahi kuwa mbunge tujitathimini kwa swali la kwamba Ndg Mwinyi alikuwa Rais wa Zanzibar kabla ya uRAIS muungano vipi aliweza kukidhi matarajio ya uadilifu wake,uzalendo wake na uwezo wake???bado tulirudia circle ile ile mwaka 1995 tukamchagua Mr Clean Benjamin Mkapa kwa dhana ya aliwahi kuwa Mwandish wa Habari wa Mwl,Ubalozi,uwaziri katika nafasi mbalimbali[uzoefu kibao wa kimataifa] tumeona uzalendo wake,uadilifu wake na uwezo wake kwa miaka aliyoongoza na kutawala Taifa hili.,bado tukazidi kujenga imani ya nguvu kwamba huyu ndg Kikwete ana uzoefu wa miaka mingi kichama na kiserikali kwa kushika nafasi mbalimbali za kitaifa na kimataifa tukijua uzoefu wa kilevi ndicho kinacholisibu Taifa hili,tukasahau juu ya uzalendo wa mtu,uadilifu wake na uwezo wake!!!hatimaye tunakuja kuja kuwa mashuhuda wa Bandit Cabinate na Bandit Government
Bado tunaelekea 2015 tunauliza juu ya Kuwahi kuwa waziri Dr kitila baadala ya Kuwahi kuwa Mzalendo na Kuwahi kuwa mwenye uwezo!!!!!!
kama kweli tutakuwa tunaendelee kuwatafuta marais kwenye baraza la mawaziri,Bungeni na ngazi zingine za watu kuwa AU au UN kuwa ndiyo pekee walio na suluhu ya kansa ya uongozi basi nitaamini kwamba kweli kila jamii hustaili uongozi wa stairi yake.kwamba Vichaa huo na kiongozi kichaa,kwamba majambazi huwa na kiongozi jamazi,kwamba waelewa huwa na viongozi waelewa.
Mjadilini Dr Kitila kwa uwezo wake,uadilifu wake na uzalendo wake na siyo ubunge wake au uwaziri wake na pengine ujumbe wake wa UNO.asante.