Mbeki alitoa tathimini yake kuhusu ukimwi na kugusa familia nyingi hapa barani Africa(Je tathimini ya mbeki ilikusudia kukomoa familia ziliziothirika kwa UKIMWI?)
Dr.Kitila mkumbo kamuuliza swali kutokana na tahthimini yake mwenyewe tena kwa kumtajia familia yake na kuunganisha familia yake ili ku-prove hypothesis ya kauli ya Mbeki.
Mtazamo wako una prejudice kuwa Dr.Mkumbo alikusudia eti kumkomoa.
Hivi swala la ukimwi kwenu ni swala la kificho kiasi hichi????
Mbeki ni public figure na anapaswa kuulizwa jambo lolote linalomuhusu liwe linamfurahisha au liwe linamkera.
Watanzania wengi ni waoga sana kiasi cha kusababisha kuacha baadhi ya mambo yakienda ovyo kwa kuogopa kuuliza viongozi wao just because ni viongozi tu.
Hapana, hiyo itakuwa ni hitimisho kutokana na anachoripoti "Daudi Mchambuzi," ambacho hatuna uhakika nacho kwa sababu kuna wengine wanashuhudi swali tofauti na hilo.
Tunataka kuona swali la Kitila mstari kwa mstari!
nani kakuambia kuwa sijui kama Dr. Kitila kama kauliza swali hili au la?
bado hujaeleza kwa nini swali kama liliulizwa katika mazingira ya kuelimishana ya chuo kikuu kinachoheshimika Africa kama UDSM? Nkumbo angekua na kipindi chake kama vile Hardtalk na Kitila Nkumbo au Dr Nkumbo hapo sawa mazingira na jukwaa hilo lingefaa kuuliza swali kama lile au Nkumbo angekua ni mchangiaji wa kawaida ie mwanfunzi au mgeni kama mimi toka nje ya chuo sawa ila siyo mtu mwenye mamlaka UDSM.
Tunataka kuona swali la Kitila mstari kwa mstari, ndio. Lakini asipokanusha hapa kinachoripotiwa na Daudi Mchambuzi itabidi tukikubali kwa kanuni ya watu wa pwani inayosema "kunyamaza kimya maana yake ni sawa na kujibu NDIO"
Huwezi kutumia dhana ya uongo kujenga swali lako ikisha ukatarajia mtu mzima na shughuli zake akusahihishe, hasa ikiwa dhana hiyo inachembe chembe za kukusuta unaeulizwa. Hilo ni moja.
Swali linalobeba dhana ya uongo linamvunjia heshima muulizwa na taasisi anayoihudumia huyo muuliza. Unajua kaabisha Chuo Kikuu na Chadema kwa kiasi gani kwa swali lake hilo?
Wewe kama hujui kama Kitila aliuliza swali hilo au la, kwa nini unamtetea kuwa alifanya jambo jema kuuliza swali hilo? Au ndio unafata mkumbo wa Mkumbo?
Hebu angalieni ukilaza wa Kitila; Doctor wa UD anashindwa hata kupata facts kwanza kabla ya kuuliza swali. Ndio maana tunasema elimu yetu UD imeshuka kwa kuwa na lecturers kama yeye, ambao wanakurupuka bila kuwa na facts zote. Kitila anapaswa kumuomba msamaha Mbeki;
Fresh inquiry ordered into death of Mbeki's son
THABO MBEKI HAD A SON BUT HIS SON, KWANDA MBEKI, WAS KILLED IN THE 80's but he and his wife didn't have any other children except this son.
Kwanda Mbeki disappeared in South Africa in 1981 while attempting to join his father and other anti-apartheid activists in exile. He is assumed to have been killed by agents of the white government, but his body, like those of hundreds of others who disappeared while resisting minority rule, was never found.
Mr Mbeki has rarely spoken of his own family's losses, and referred to them only in general terms when he gave evidence to the TRC. Last week, however, the President wrote in his weekly ANC newsletter: "I too, and especially my mother, regret that the TRC process did not succeed to unearth the truth about what happened to our own loved ones who disappeared without trace - my brother Jama Mbeki, my son Kwanda Mbeki and my cousin, Phindile Mfeti."
Mr Mbeki did not ask the TRC to investigate the disappearances, but the case of Kwanda Mbeki was referred to the TRC by his mother, Olive Mpahla. She said he disappeared when on his way to visit his uncle, Mr Mfeti, although accounts exist of him having been seen in exile. But the TRC did not have the time or resources to investigate a large proportion of cases, including those of the President's family.
kwako wewe mtoto ni mpaka umzae, huwezi kum-adopt?
Mhadhiri Mwandamizi wa UDSM, Dr. Kitila Mkumbo jana alimpa wakati mgumu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.
Hiyo ilikuwa ni katika wakati wa maswali kwa Mbeki baada ya hotuba yake katika ukumbi wa Nkrumah wa UDSM.
Swali la Dr. Kitila lilijikita katika kauli ya Mbeki, wakati akiwa madarakani, kuwa UKIMWI hauenezwi na ngono ila shida na umaskini wa wananchi. Dr. Kitila alimkumbusha Mbeki juu ya kifo cha mtoto wake (wa Mbeki) kilichosababishwa na UKIMWI. 'Unaendelea kusimamia kauli yako?' aliuliza Dr.Kitila
Mbeki aliacha kujibu hilo swali. 'I will not respond to that pinching question' alisema Mbeki. Na hapo ndipo ukawa mwisho wa maswali kwa Mbeki ingawa swali la Dr.Kitila lilikuwa la pili tu.Prof. Mukandala alimaliza muda wa maswali ghafla
joyce hata wewe akili yako finyu na elimu yako nadhani ni kuliko unavyomtathimini dr. kitila ebu tizama sarufi yako inadhihirisha ulofa wakokitila hapo kweli alikosa busara na alihuliza swali kama sifa flani hivi aonekane nae kahuliza swali ,pia hakukuwa na haja ya yeye kumtaja mtoto wa mbeki kwani ni masuala ya kifamilia...hekiama hana akili finyu huo udokta kapewa kwa njia za panya yaelekea....mgeni akija kwake anaweza kumuhuliza vitu kama hivyo?
Inaonesha kuwa mtu anaejiita "doctor" Kitila Mkumbo, hajui alifanyalo na zaidi alitaka kujionesha mbele za watu.
Kwanza kabisa, kama yeye si mwanafunzi hapo alikuwa hapaswi kuulizia maswali, hiyo ilikuwa ni fursa ya wanafunzi kuuliza ili wapate kujifunza, yeye huyo angechukuwa fursa hiyo kuwatazama wanafunzi wanachouliza, wanavyojibiwa na baadae kwenda kuvijengea hoja akiwa na wanafunzi wake.
Ikiwa hao ndio wakufunzi wa Tanzania, si hasha tunatoa wanafunzi wa vyuo ambao hata spelling hawajui.
Mhadhiri Mwandamizi wa UDSM, Dr. Kitila Mkumbo jana alimpa wakati mgumu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.
Hiyo ilikuwa ni katika wakati wa maswali kwa Mbeki baada ya hotuba yake katika ukumbi wa Nkrumah wa UDSM.
Swali la Dr. Kitila lilijikita katika kauli ya Mbeki, wakati akiwa madarakani, kuwa UKIMWI hauenezwi na ngono ila shida na umaskini wa wananchi. Dr. Kitila alimkumbusha Mbeki juu ya kifo cha mtoto wake (wa Mbeki) kilichosababishwa na UKIMWI. 'Unaendelea kusimamia kauli yako?' aliuliza Dr.Kitila
Mbeki aliacha kujibu hilo swali. 'I will not respond to that pinching question' alisema Mbeki. Na hapo ndipo ukawa mwisho wa maswali kwa Mbeki ingawa swali la Dr.Kitila lilikuwa la pili tu.Prof. Mukandala alimaliza muda wa maswali ghafla
bado hujaeleza kwa nini swali kama liliulizwa katika mazingira ya kuelimishana ya chuo kikuu kinachoheshimika Africa kama UDSM? Nkumbo angekua na kipindi chake kama vile Hardtalk na Kitila Nkumbo au Dr Nkumbo hapo sawa mazingira na jukwaa hilo lingefaa kuuliza swali kama lile au Nkumbo angekua ni mchangiaji wa kawaida ie mwanfunzi au mgeni kama mimi toka nje ya chuo sawa ila siyo mtu mwenye mamlaka UDSM.
Mtoto gani wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI?
*Kama Mkumbo ameuliza kweli suala kwa namna hiyo, ninaelewa kwa nini Mbeki amekataa kulijibu, kwa sababu limekaa kusuta zaidi ya kutaka ufafanuzi........Ila sidhani kuwa Mkumbo ameuliza suala hilo, hivyo lilivyo