Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,303
Nadhani wamechemsha ni mtoto wa Mzee Nelson Mandela, ambaye mandela alimtangaza rasmi kuwa kafa na UKIMWI
Aliyechemsha nani? Bwana Kitila Mkumbo?
Nadhani wamechemsha ni mtoto wa Mzee Nelson Mandela, ambaye mandela alimtangaza rasmi kuwa kafa na UKIMWI
Alipokuwa Rais hakusema habari ya umaskini na ukimwi, yeye alisema straight up kwamba HIV haiambukizi AIDS, period!Hakuuliza mtoto wa mbeki kufa kwa ukimwi..aliuliza impact ya ile kauli yake(ukimwi ni impact ya umasikini) aliyoitoa akiwa rais
Hamsumbui vichwa vyenu kufikiria swali la Kitila Mkumbo(Kama kweli aliuliza maana namuona kwenye uzi lakini hajitokezi kutoa ufafanuzi). Kama Mbeki alisema UKIMWI ni ugonjwa unaotokana na umaskini inakuaje mtoto wake (ambaye si maskini) afe kwa UKIMWI? Hili ni swali lenye mantiki maana kauli hiyo ya Mbeki ilizua mjadala sasa ukipata fursa ya kumuuliza lazima ujue kama ana msimamo kama huo tena au ameshaubadili.Sioni sababu ya Mbeki kujaa povu angekuwa muungwana tu na kujibu maswali.
Naona huyo muuliza swali aliuliza tu kujionesha kwamba anafuatilia sana mambo ya Mbeki hakuwa na nia yeyote ya kupata clarification kwa faida ya wote.
Tatizo ni swali la Nkumbo kuonekana limeegemea zaidi kukomoa badala ya kuhitaji maelezo yaani kiudaku udaku. siyo swali informative ambalo lingeleta jibu la kuelimisha ila ni swali la kishari lisilohitaji kujibiwa. ie ukiwa na information ambazo nkumbo anasema alizitoa mbele ya mbeki then unaulizia msimamo wa mtu huku ukisisitiza kua hata mtoto wako (ambaye supposedly hakua maskini ila alikufa na ukimwi) hii ni kumpose a will kwa mtu na siyo kutaka kujua msimamo.
Mbeki ni msomi wa zamani na aliona huu ni ujinga ndiyo maana hakujibu. swali lilitakiwa kuwekwa kwanza kwenye kuondoa dhana ya kua maskini pekee yao ndiyo wanakufa na AIDS halafu jamaa akijibu kama ni maskini ndiyo wanakufa zaidi au akikataa then unaweza kutoa mfano wa mtoto wake kama a follow up question au kuweka msisitizo wa swali na siyo mwanzo tu unaanza na udaku. hii kama vile ulikua umempania na hiyo hukutaka maelezo au information yeyote toka kwake.
hata hawa jamaa wa BBC wa vipindi vya maswali magumu kama richard Frost, Hardtalk n.k wanauliza maswali personal pale inapobidi (siyo swali la mwanzo) na mara nyingi kama mtu anapiga chenga hili linakua follow up. Huwezi kuinsult intelligence ya mtu mbele za watu hata mimi ningekua defensive na nisiendelea na maswali.
Hapana. Kitila alionyesha jinsi gani ana ufinyu wa kufikiri, kuuliza swali ambalo linahusu familia binafsi, juu ya jambo ambalo halikuwa topic ya mazungumzo. Angesubiri siku Mbeki yuko kwenye vikao kuhusu Ukimwi ndio aulize swali kama hilo. Na unapouliza swali usiingize mambo binafsi ya familia. Alitaka nini hapa, kumkumbusha Mbeki uchungu wa kufiwa mwanae? Nani anaependa kifo cha mwanae kiwe mjadala wa hadhara? Nimefanya kazi na Kitila, nilimheshimu hadi niliposikia kafanya upuuzi huu wa kujitafutia umaarufu binafsi.
Kwanza sijawahi kusikia popote kuwa kuna mtoto wa Mbeki alikufa kwa ukimwi. Najua mtoto wa Mandela alikufa kwa ukimwi. Sasa Kitla alitaka kujionyesha yeye ni CIA sana au nini?
Dr.Kitila mkumbo kamuuliza swali kutokana na tahthimini yake mwenyewe tena kwa kumtajia familia yake na kuunganisha familia yake ili ku-prove hypothesis ya kauli ya Mbeki.
Hapana, usimsafishe Mbeki, Mbeki hakusema hivyo, Mbeki alipingana na nadharia za sayansi kwa kudai kwamba HIV haisababishi UKIMWI.Kwani kauli ya mbeki kusema umaskini ndo chanzo cha ukimwi
Hapana, hiyo itakuwa ni hitimisho kutokana na anachoripoti "Daudi Mchambuzi," ambacho hatuna uhakika nacho kwa sababu kuna wengine wanashuhudi swali tofauti na hilo.Kwa maana hiyo, Kitila ni muongo mwizi, maana hakuna mtoto wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI
Dr.Kitila sio mwizi hjaiba chochote, Mbeki alipaswa kumjibu kuwa mtoto wake hajafa kwa ukimwi.Kwa maana hiyo, Kitila ni muongo mwizi, maana hakuna mtoto wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI
Kwani kauli ya mbeki kusema umaskini ndo chanzo cha ukimwi unadhani ilizigusa familia ngapi za kiafrika?
unadhani iliwakumbusha watu wangapi juu ya ndugu zao waliofariki kwa ugonjwa huo??
Je Mbeki alivyotoa kauli hiyo alikusudia kuwakumbusha wanandugu wa marehemu juu ya wapendwa wao waliokufa kwa ukimwi??
Msipende kuwa-pet viongozi kwa maswali ya kuwafurahisha tu.
Mtoto gani wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI?
*Kama Mkumbo ameuliza kweli suala kwa namna hiyo, ninaelewa kwa nini Mbeki amekataa kulijibu, kwa sababu limekaa kusuta zaidi ya kutaka ufafanuzi........Ila sidhani kuwa Mkumbo ameuliza suala hilo, hivyo lilivyo[/QUOTE Sidhani kama Dkt. aliuliza katika context hiyo, lakini kama kweli alifanya hivyo then, that was the stupid question
Dr.Kitila sio mwizi hjaiba chochote, Mbeki alipaswa kumjibu kuwa mtoto wake hajafa kwa ukimwi.
Kwa nini waliokuwepo kwenye mkutano huo wanaleta habari nusu nusu??
kitila hapo kweli alikosa busara na alihuliza swali kama sifa flani hivi aonekane nae kahuliza swali ,pia hakukuwa na haja ya yeye kumtaja mtoto wa mbeki kwani ni masuala ya kifamilia...hekiama hana akili finyu huo udokta kapewa kwa njia za panya yaelekea....mgeni akija kwake anaweza kumuhuliza vitu kama hivyo?
Huwezi kutumia dhana ya uongo kujenga swali lako ikisha ukatarajia mtu mzima na shughuli zake akusahihishe, hasa ikiwa dhana hiyo inachembe chembe za kukusuta unaeulizwa. Hilo ni moja.
Swali linalobeba dhana ya uongo linamvunjia heshima muulizwa na taasisi anayoihudumia huyo muuliza. Unajua kaabisha Chuo Kikuu na Chadema kwa kiasi gani kwa swali lake hilo?
Wewe kama hujui kama Kitila aliuliza swali hilo au la, kwa nini unamtetea kuwa alifanya jambo jema kuuliza swali hilo? Au ndio unafata mkumbo wa Mkumbo?
Botswana ni nchi maskini? mbona ukimwi umeshamiri? Wacha kumshabikia Mbeki.