Dr Kigwangala aikemea CCM na kuikubali UKAWA

Dr Kigwangala aikemea CCM na kuikubali UKAWA

Nape anafanya siasa kama mchekeshaji wa mfalme. Anasema tu ili mradi kikwete afurahie
 
Leo kwa mara ya kwanza nimemuona Kigwa ana akili au tuseme amebadilika. Nadhani huwezi kumuweka tena kwenye kundi la watu kama Nape au Baadhi ya Wabunge wa CCM. Ameongea ukweli na kukiri kuwa CCM inafanya mambo kwa mazoea na kwamba kujisafisha baada ya kutenda madudu ni kazi ngumu.
Majadiliano yake na Salum Mwalimu wa Chadema kweli yalikuwa ya kizalendo hasa na hayakuwa ya kishabiki.
Mkuu ameona unafiki haulipi.
 
Nape anafanya siasa kama mchekeshaji wa mfalme. Anasema tu ili mradi kikwete afurahie
Nape anaweza kuwa kiongozi chini ya JK tu na si mtu mwingine,subiri baada ya 2015 hutalisikia tena jina la nape kwenye siasa za nchi hii.
 
CHRISS LUKOSI myalukolo wetu wa kule UK hasikiki nimemmisi jukwaani kukitetea chama chetu. Kule nyumbani pia hawa Chadema wanazidi kupaa. Tokea uokoe jahazi ndugu yangu
 
serikali ya ccm imejaa wanafiki na wambea ccm walitarajia watawala milele lazima watambua watanzania tunataka mabadiliko ambayo tumeyakosa ndani ya ccm
 
ameongea vizuri, hasa aliposema watz wanaangalia mtu sio chama, ukiweka mtu safi hutapata kazi kumnadi wakati wa kampeni. ni kazi kuanza kumsafisha mtu kisha uanze kunadi sera za chama.
 
Ila ajilinde tu maana haya Maintarahamwe yeyote ndani ya chama chao ambaye anaamua kusema kweli bila kificho humuona ni adui yao mkubwa sana na hivyo kupanga mipango ya kwenda kumng'oa kucha bila ngazi, kumpofua macho na hata kumuua ili asiendelee kuwasumbua wenye nyumba yao kuendelea kutesa kwa zamu. Sasa zamu ya kutesa ya fisadi Kikwete inakaribia ukingoni wameanza maandalizi ya nguvu ya kuendelea kutesa kwa kupitia fisadi mpya watayempitisha aendeleze ufisadi wao nchini.
 
kwa tetesi zilizopo mkuu wa kaya amewatupa kweny uwaziri Kigwa na deo, anakwenda kuwaharibu tu haya majembe, kama mimi sikubali , uwaziri wa miezi kumi tu?
 
Kama sio mizengwe na makundi ya wenye noti huyu ndiye mtu pekee wa ccm anayeweza kunitoa nyumbani kwenda kupiga kura wengine woote ni kama kuurudisha utawala wa sasa. Mda wa mtandao umeisha ,tukiuendeleza nchi yetu haitakalika.

Kigwangala anaweweseka na joto la Bashe
 
wapi LB7 akina Faizafoxy,lizaboni,simiyu yetu et all...!!!
Dr.Kigwa you have nailed...Wanahitajika watu realistic kama huyu ndani ya ccm

Sasa unawaita hao waje wafanye nini? we boya kweli.
 
tpaul kigwa wako lazima aseme hivyo sasa kwani ameshasoma alama za nyakati na kugundua kuwa safari hii hakuna atakayembeba kwenye kura za maoni na kuna vijana zaidi ya watatu akiwemo husein bashe ambao watakuwa wapinzani wake. kwa hiyo ungempa ushauri wa bure tu badala ya kumpongeza kwamba ahamie chama chochote kilichomo ukawa huenda akaambulia ubunge wa kuteuliwa. Wewe hushangai mtu unayemwita mwanasiasa mkongwe anataka kumshinikiza rais afanye maamuzi jinsi anavyotaka yeye.? Kwa kifupi tu Kigwa sio CCM kusema kwamba akiondoka itakufa. ameikuta ccm na ataondoka ataiacha ccm kama ilivyo na ndoto yake ya kuwa itadidimia akaiote nzega kwa muda uliobakia wa ubunge wake.
Dr Kigwangala ameitahadharisha CCM kuwa makini na nguvu za UKAWA kufuatia kuinyanganya CCM 20% ya viti kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ulioisha hivi punde. Dr Kigwa aliyasema hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha UZALENDO kinachorushwa na ITV.

Kigwangala alisema wananchi wa leo sio wale wa miaka 5 au 10 iliyopita. Ametumia nafasi hii kumuonya Rais Kikwete atekeleze maazimio yote ya bunge dhidi ya mafisadi wa ESCROW bila kusita kwani asipofanya hivyo anazidi kukididimiza chama wakati yeye muda wake unakaribia kuisha. "Rais asipotekeleza maazimio ya bunge anazidi kukiweka chama chetu katika wakati mgumu", alisema.

Aidha, mwanasiasa huyo mkongwe amewaomba watu wa CCM kuacha kufanya siasa kwa mazoea na kwa kutumia hila na ujanjanja. Ameenda mbali zaidi kwa kuwataka CCM waache kuwakumbatia mafisadi kwani kufanya hivyo wanaweka rehani uhai wa chama.

Source: ITV

MAONI YANGU
Nampongeza Kigwa kwa kusema ukweli, tofauti na wanaCCM wengine wanaoubeza Muungano wa UKAWA.

:israel:
 
Huyu Kigwangalla ni dokta wa nn eti? Mbona kashindwa kumtibia baba yake mzazi, mgonjwa hoi hajiwezi. Inasemekana haendi hata kumjulia hali. Tangu aukwae ubunge 2010, hajakanyaga nyumbani kwa Mzee Kipwangalla, hamjali, kamtelekeza kabisa. Hamhudumii kwa chakula wala matunzo yoyote. Baba wa mbunge, Dr. Hamisi Kigwangalla, alias Saidi Bagaile juzi alitoa post akisema anampeleka Mzee wake India kwa matibabu. Taarifa za uhakika ni kwamba huo ni uongo, hajaenda India. Yupo jijini, busy na mambo yake. Kikwete upo? Huyu kijana wako hafai, ana laana ya wazazi wake. Anaendesha shangingi, huku wazazi wake wanataabika kwa maradhi na njaa.! Bashe, Allan na Bonge. Mmeona mambo yenu ya kitapeli?
 
ccm ingekua na vijana kama kina kingwangala au filikunjombe ingefika mbali tatizo haiwataki vijana kama hao ina wataka wenye elimu ya kufikilishwa na kuaminishwa pasipo kuruhusu akili zao kufanya kazi kama @nape MSALANI LAKI sipesa Simiyu Yetu na wenzao wengine
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom