tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,198
- 27,821
Dr Kigwangala ameitahadharisha CCM kuwa makini na nguvu za UKAWA kufuatia kuinyanganya CCM 20% ya viti kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ulioisha hivi punde. Dr Kigwa aliyasema hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha UZALENDO kinachorushwa na ITV.
Kigwangala alisema wananchi wa leo sio wale wa miaka 5 au 10 iliyopita. Ametumia nafasi hii kumuonya Rais Kikwete atekeleze maazimio yote ya bunge dhidi ya mafisadi wa ESCROW bila kusita kwani asipofanya hivyo anazidi kukididimiza chama wakati yeye muda wake unakaribia kuisha. "Rais asipotekeleza maazimio ya bunge anazidi kukiweka chama chetu katika wakati mgumu", alisema.
Aidha, mwanasiasa huyo mkongwe amewaomba watu wa CCM kuacha kufanya siasa kwa mazoea na kwa kutumia hila na ujanjanja. Ameenda mbali zaidi kwa kuwataka CCM waache kuwakumbatia mafisadi kwani kufanya hivyo wanaweka rehani uhai wa chama.
Source: ITV
MAONI YANGU
Nampongeza Kigwa kwa kusema ukweli, tofauti na wanaCCM wengine wanaoubeza Muungano wa UKAWA.
:israel: