Dr Kigwangala aikemea CCM na kuikubali UKAWA

Leo kwa mara ya kwanza nimemuona Kigwa ana akili au tuseme amebadilika. Nadhani huwezi kumuweka tena kwenye kundi la watu kama Nape au Baadhi ya Wabunge wa CCM. Ameongea ukweli na kukiri kuwa CCM inafanya mambo kwa mazoea na kwamba kujisafisha baada ya kutenda madudu ni kazi ngumu.
Majadiliano yake na Salum Mwalimu wa Chadema kweli yalikuwa ya kizalendo hasa na hayakuwa ya kishabiki.
 
hayo ndio mawazo wanaotakiwa kupewa ccm,lakini kwa kuwa ni sikio la kufa hawaelewi
 
Kigwangala anatafuta umaarufu wa kijinga, Dhambi ya kumtelekeza baba yake inamtafuna
 
hata huyo jamaa nae ni kada kweli kweli sema tu kwa sasa anaona maji yamefika shingoni kwa sasa hawana ujanja kilichobakia kwao ni kuingalia ukawa kwa macho zaidi ya mawili
 
Mi binafsi nishawahi kuweka uzi humu uliyosema; Kufanya vibaya kwa CCM kumechangiwa na ukimya wa raisi wetu " mods wakaitoa sasa nawaomba na hii muitoe.
 
Dr Kigwangala ameitahadharisha CCM kuwa makini na nguvu za UKAWA kufuatia kuinyanganya CCM 20% ya viti kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ulioisha hivi punde. Dr Kigwa aliyasema hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha UZALENDO kinachorushwa na ITV.

Kigwangala alisema wananchi wa leo sio wale wa miaka 5 au 10 iliyopita. Ametumia nafasi hii kumuonya Rais Kikwete atekeleze maazimio yote ya bunge dhidi ya mafisadi wa ESCROW bila kusita kwani asipofanya hivyo anazidi kukididimiza chama wakati yeye muda wake unakaribia kuisha. "Rais asipotekeleza maazimio ya bunge anazidi kukiweka chama chetu katika wakati mgumu", alisema.

Aidha, mwanasiasa huyo mkongwe amewaomba watu wa CCM kuacha kufanya siasa kwa mazoea na kwa kutumia hila na ujanjanja. Ameenda mbali zaidi kwa kuwataka CCM waache kuwakumbatia mafisadi kwani kufanya hivyo wanaweka rehani uhai wa chama.

Source: ITV

MAONI YANGU
Nampongeza Kigwa kwa kusema ukweli, tofauti na wanaCCM wengine wanaoubeza Muungano wa UKAWA.

:israel:

Yes, uko sahihi kumpongeza lakini Kigwa sio mwanasiasa mkongwe. Utakosa jina la kuwapa wenye sifa ya ukongwe. Hata ungemwita anayechipukia au mwanasiasa kijana
 
mimi nikiona mtu anasifia ukawa naanza kutilia mashaka akili yake siyo bure.[/QUOTE.
Ulishawahi kuitilia shaka akili yako? Kama hujawahi anza sasa, kama utakuwa genuine utagundua umechelewa sana na hiki ndicho chanzo kikuu cha wewe kutowaelewa wengine kwa sababu hujawahi tilia shaka akili yako hata siku 1. Unajua hata vichaa huwa wanatiliashaka akili za watu wazima kwanini hawaokoti makopo kama wanavyofanya wao. Je hawa sio wenzio unaofanana nao?
 
Modes hawakupenda ukipige mawe live chama chao
 
mimi nikiona mtu anasifia ukawa naanza kutilia mashaka akili yake siyo bure.[/QUOTE.
Ulishawahi kuitilia shaka akili yako? Kama hujawahi anza sasa, kama utakuwa genuine utagundua umechelewa sana na hiki ndicho chanzo kikuu cha wewe kutowaelewa wengine kwa sababu hujawahi tilia shaka akili yako hata siku 1. Unajua hata vichaa huwa wanatiliashaka akili za watu wazima kwanini hawaokoti makopo kama wanavyofanya wao. Je hawa sio wenzio unaofanana nao?

Jibu zuri sana Hili!
 
Yes, uko sahihi kumpongeza lakini Kigwa sio mwanasiasa mkongwe. Utakosa jina la kuwapa wenye sifa ya ukongwe. Hata ungemwita anayechipukia au mwanasiasa kijana

samahani ukongwe ni miaka mingapi
 
Kigwa kakubali mwenyewe mziki,Nzega Mjini vijiji 20,UKAWA 13,CCM 7,mpaka leo pale CCM wilaya ni kama pamefiwa
 
Dr Kigwangala ameitahadharisha CCM kuwa makini na nguvu za UKAWA kufuatia kuinyanganya CCM 20% ya viti kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ulioisha hivi punde. Dr Kigwa aliyasema hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha UZALENDO kinachorushwa na ITV.

Kigwangala alisema wananchi wa leo sio wale wa miaka 5 au 10 iliyopita. Ametumia nafasi hii kumuonya Rais Kikwete atekeleze maazimio yote ya bunge dhidi ya mafisadi wa ESCROW bila kusita kwani asipofanya hivyo anazidi kukididimiza chama wakati yeye muda wake unakaribia kuisha. "Rais asipotekeleza maazimio ya bunge anazidi kukiweka chama chetu katika wakati mgumu", alisema.

Aidha, mwanasiasa huyo mkongwe amewaomba watu wa CCM kuacha kufanya siasa kwa mazoea na kwa kutumia hila na ujanjanja. Ameenda mbali zaidi kwa kuwataka CCM waache kuwakumbatia mafisadi kwani kufanya hivyo wanaweka rehani uhai wa chama.

Source: ITV

MAONI YANGU
Nampongeza Kigwa kwa kusema ukweli, tofauti na wanaCCM wengine wanaoubeza Muungano wa UKAWA.

:israel:
Hivi Kigwangala amekuwa mwanasiasa kwa muda gani kustahili kuitwa mwanasiasa mkongwe? Je Ngombale Mwiru na Malecela tutawaweka kundi gani?
 
Kama anajua siasa za ccm ni za kijanja janja mbona akuweka wazi kuwa mwenyekiti wake aliiba kura na alipatikana kwa rusha,wote ni walele
 
Back
Top Bottom