ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,950
- 6,981
mwaka 20o9 nilikuwa na shughuli zangu katika bank ya nbc tawi la chuo kikuu cha dar-es salaam.
Baada muda akaingia magufuli,wakati huo akihangaikia na phd yake pale udsm, na kuanza kupiga soga na mtu mmoja.baadaye kidogo akaingia dkt wa kike mhadhiri udsm ambaye hajaolewa mpaka sasa.(naomba nisimtaje jina). Sasa magufuli alipomwona huyo mwanataaluma baada ya kusalimiana akamwuliza ,tena kwa sauti ya juu ,kiasi cha kila mtu aliyekuwepo ndani kusikia :''vipi umeshapata mchumba?''
nilimtazama huyo mwanataaluma na uso wake ulionyesha wazi kufaidhaika sana...kwa mtazamo wa baadhi ya wadau waliokuwepo pale, magufuli alikuwa amefanya utani usiopendeza na unaodunisha heshima ya mtu hasa jinsia ya kike.nami nilifadhaika sana.
Binafsi sikufurahishwa na kauli ya namna hiyo tena kutolewa na mtu wa hadhi ya waziri wa serikali.
Ni kweli kabisa magufuli ni mropokaji tena asiyechukua muda kupima kauli zake.hana busara wala hekima ingawa amepita shule.
ni vema tukumbuke kumpongeza prof.abdalah safari kwa kuwa ndiye aliyekuwa akiiwakilisha chadema katika hiyo kesi.
bolded red sina cha kusema, lakini napendekeza tumfanyie harambe ya kumshukuru kwa uwakilishi uliotukuka. Mungu amjalie maisha marefu zaidi