Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

Da wakuu nimekalia kutibu watu kumbe kunauhondo unanipita huku JF da habari njema sana yaani raha.
 
kafumu kashafumuliwa na kashinde kashinda kesi....aahaahaaaa magamba mwaka huu watajuta kuifaham cdm!
 
sheria ni msumeno, mlifurahia mlipopata ahueni lile suala la mgomo kwa waalim - mkapata ahueni tena suala la madaktari -- sasa leo hii mnataka kuigeuka mahakama kuwa haijatenda haki?

Pole sana dr. kafumu ni vizuri sasa ukajikita kwenye sekta ya madini uliyosomea maana tunahitaji wataalam sana.

Leo ndio umejuwa kuwa mahakama inatenda haki?
 
CCM na CHADEMA jifunzeni jambo moja muhimu: Msiwaachie baadhi ya watu wenu kumiliki MAJIMBO. Wakiondoka, wakiondolewa, wakifa,..., mnapata tabu sana kubaki na majimbo haya. KInachotokea hapa Igunga ni athari za moja kwa moja za kumwachia Rostam Aziz akawa mmiliki wa Jimbo hili. Msisubiri KATIBA ya NCHI iwawekee ukomo wa wagombea wenu kwenye majimbo haya. Katiba za vyama vyenu zinaweza kulimudu hili.
 
Sasa hata mahakama zimewachoka hawa magamba.Wanabebwa na sasa hawabebeki tena.

Kila chenye mwanzo kina mwisho.

Hata mahakama zinaona uovu wao na zinaundwa na watanzania wale wale ambao hata ndugu zao nao wanateseka kutokana na utawala huu mbovu.
nadhani baada ya Mh. Tundu Lissu 'kupiga msitari' na kuainisha kati ya Black&white ya hawa majaji wetu watakuwa wameanza kushktuka. Maana kuwa subjected kwenye 'vodafasta' ni aibu na kila mmoja anajitahidi asiwe upande huo hivyo kutumia muda wao kulinda fani hii.
Wasiwasi ni kuwa bado wamo na tunasubiri 'watulize' tena pale A-town!

 
Kama na ushindi wa Urais ungekuwa una pingwa mahakamani, sasa hivi nchi ingekuwa mikononi mwa wananchi wenyewe! Big up CDM!
 
ccm itabaki kwenye histori kama ilivyo historia ya mtu wa kale.
 
Ukweli ni kwamba, kama CHADEMA au vyama vya upinzani tungeamua kupinga ushindi wa majimbo yote yanayoshikiliwa na CCM, wangevuliwa ubunge wote. Na hata raisi kama ingekuwa kuna sheria inayoruhusu hili, angevuliwa uraisi muda mrefu sana. Viva CHADEMA, tulianza na MUNGU, tunaendelea na MUNGU, tutamaliza na MUNGU.
 
Samahani kamanda wangu mimi niko mbali na mji sasa heading imenishtua nikafurahia then ndani sipati ukweli very sorry!

Hamna shida Mkuu ila itv, tbc, star tv na radio one wamerusha hewani CDM wameshinda kesi jimbo liko wazi Mkuu....
 
Uchaguzi ukirudiwa CCM hawataweka mgombea. Hii ni aibu mbaya sana, wapiga kura hawakumpenda Kafumu serikali yote ikiongozwa na wastaafu wanahamia Igunga kuwalazimisha wapiga kura wampihie Kafumu kura kiko wapi.
Pesa za umma zilizoteketea kwa kuwalipa viongozi hao, wake za watu waliomwiguliwa wakati huo na wale waliokufa kwa kutekwa nyara wakati huns pia ahadi hewa zilitolewa wakati wa kampeni. Nimesahau na binfuki za mifukoni zilizotishia watu wakati huo. Bure kabisa hakuna haja ya kulazimisha jambo lisilokwenda.
 
hoja ya imamu wa igunga kuwataka waislam kutoipigia cdm kwa madai kwamba ilimdhalilisha mwanamke wa kislam;jaji alifanya maamuzi kwa manufaa ya mlalamikaji kutokana na ushaidi kudhibitisha mahakamani kwamba ni kweli imamu alitoa kauli hiyo bila kuwa na ushahidi kwamba vijana wa cdm ndo walitenda hayo.hoja nyingine taarifa aliyoitoa mukama kwmba cdm waliingiza nchini makomandoo33 kutoka nje ya nchi,hakimu baada ya kuridhika na ushahidi alikubali kwamba nia ilikua kuwatisha wananchi....
 
hatukuckia uamuz wa mahakama mpaka hukumu ilipotolewa dats y 2nasema mahakama imetenda haki, but kwa lema hukumu ilivuja 1 day b4 wat can u say abt that??@Ritz
 
Back
Top Bottom