Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

Magamba this is special ded kwa Nchemba. Mipasho si fani yangu lakini just this once.
Mnalooo, mtajibebaje? Heyaheya.....
Jinsi nilivyoumia siku mnatangaza Kafumu kihuni natumaini maumivu yenu ni maradufu hasa pale jimbo litakapotwaliwa rasmi.
Damu ya Kamanda Mbwana will haunt you na pia za wale wote waliopoteza maisha na kuumizwa kwenye harakati hizi za ukombozi wa pili wa Mtanzania.
 
sidhani hii hukumu kama ipo sahihi
Nenda court of apeal. hoja za Chadema zilikuwa 13, Jaji amezikubali 8 nyingine amezikataa hazikuwa na ushahidi wa kutosha. Habari ndio hiyo upendi saga chupa ubwie.
Hongera sana Tundu Lisu sasa ni dhahiri Majaji wote wenye viwango vya ujaji watakuwa wanataka kulinda hadhi zao na hakuna tena hukumu za kufikirika.
 
Pro-Chadema bana kwa unafiki mara waseme hawana imani na mahakama za Tanzania, mahakama ikifanya kazi yake na mgombea wa Chadema akashinda wanashangilia, mahakama ikifanya kazi yake mgombea wa CCM akashinda wanasema Ikulu imeingilia maamuzi mahakama...mie naamini maamuzi ya mahakama na haki imetumika...pongezi kwa JK kwa kujenga mahakama zenye haki maamuzi ya mahakama yaheshimiwe pole sana Dr Kafumu, ndio siasa zina raha yake na machungu yake.
Mimi ninachojua bado mahakama hazipo huru, kuna uwezekano kabisa hapa kafumu hajatendewa haki ila ikulu wameagiza apigwe chini ili kupunguza kelele za wapinzani
 
There are currently 2450 users browsing this thread. (541 members and 1909 guests)

Big Up JF long Life JF
 
images
 
poleni wanaigunga mtaanza tena kuona vituko vya wana ccm huko,my take mle ccm,mlale cdm as usual
 
hela zetu jamani............. hapo si inamaana uchaguzi mwingine? uuwwwwwwwwwwwwwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Hivi mie mnijuze ukamishina wa wa madini na ubunge wapi na wapi
 
Asubuhi

Kumekucha hapa Tabora.Nimeamka nikiwa na shauku kubwa ya kujua kitakachotokea.Nimekuja hapa Igunga kushuhudia haki ikitendeka. Sikulala vyema jana...mara Kafumu,mara Kashindye ndotoni.Tuache hayo.Mnamo saa 12:30 nikajisogeza viwanja vya Mahakama Kuu hapa Tabora.Nilitumai kuwa nitakuwa wa kwanza kufika.Haikuwa hivyo.Watu walikuwa wamesheheni vya kutosha katika viunga vya Mahakama Kuu.Sijui walilala hapahapa?!

CCM waingia

Wakichagizwa na nyimbo za John Komba,wanachama wa CCM waliwasili hapa Mahakamani.Ingawa hawakuwa wengi kiiivyo,lakini walionekana waliojiandaa.Wakawa wanaimba huku wakizungukazunguka huku na huko viunga vya Mahakama Kuu Tabora. Ni raha ilioje!

CHADEMA nao...

Wanachama na wafuasi wa CHADEMA nao waliwasili kwa mamia.Viwanja vikajaa.Nyimbo za ukombozi za kama Sinema za Sarafina na nyinginezo zilihanikiza anga la Mahakama Kuu.Mwito wa People's power ukatawala. Mwe! Raha kweli...

Wenye kesi...

Mnamo saa mbili hivi,Mwalimu Kashindye aliwasili.Alionekana mchangamfu na mwenye matumaini.Aliongozana na Wakili wake aliyekuwa na Wasaidizi wake wawili.Si mwingine;ni Prof.Abdallah Safari. Wanaongea na kuchekacheka.Sijui nisiendelee?

Dr.Kafumu naye anawasili akiwa na Mawakili wake wawili.Kwakweli siwajui.Labda macho yangu ya kizee yalinizuia kuwaona vyama.Pia,walizongwa mno na washabiki wao.Macho yangu ya kizee yakaninyima uhondo.Ingawa walizongwa kwa shangwe,hawakuwa na furaha.Walinyongea pamoja na kuwa wenye furaha za kulazimisha. Dr.,kwa muda mwingi alikuwa busy kuongea na simu akijitenga mbali na wafuasi wake kufanya hivyo.Huo ndio ukweli.

Dola yaonekana

Magari yaliyosheheni polisi wa kutuliza ghasia yapatayo kama manne yaliwasili.Yakafuatiwa na gari la maji ya kuwasha. Askari wengi hawakushuka magarini.Yamekuwa haya tena? Ila,wananchi wakaendelea na yao.

Mlango wafunguliwa

Mlango wa Mahakama Kuu Tabora,kuruhusu watu waingie chumba cha Hukumu,ulifunguliwa saa 3 kamili.Ilikuwa mshikemshike.Kila mtu alitaka kuingia ndani.Mminyano kwelikweli.Nikapata bahati ya kusukumiwa ndani na kundi la vijana.Nikashukuru pamoja na kupata maumivu ya hapa na pale. Wenye kesi na Mawakili wao;wananchi wa kawaida kila mtu alikaa sehemu yake tayari kwa hukumu.Maongezi ya hapa na pale;huyu na yule yakateka chumba cha Mahakama.

Mara: Coooooooooourrrrrrrrrrrrrrrrt!

Wote tukasimama.Itaendelea kesho kwakuwa nimepata wageni hapa nyumbani kwangu...
 
Wale walio karibu na Kichaa Lusinde, msaani wa rap za matusi, amkumbushe kunywa sumu aliyoahidi ikiwa CDM ingeshinda Igunga
Unadhani CHADEMA imeshinda Igunga? Ni kodi zetu zitatafunwa upya kule Igunga. SIASA inazidi kuwa MRADI mkubwa sana unaolipa NCHI hii kwa visingizio vya DEMOCRASIA, UTAWALA WA SHERIA, huku wanaIgunga wenyewe wakiendelea kutaabika tu.
 
Bila shaka sasa ndio atajua siasa za TZ zilivyo! Ni kama kaota ndoto kuwa amekuwa mbunge kaamka asubuhi akagundua kuwa zilikuwa ni ndoto tu
 
Hivi nani alikuwa campagn manager wa Kafumuliwa? ha ha ha ha ha Burn karudi na Arumeru....?
 
Huyu atakuwa mzalendo wa kweli sio wale makanjanja!

kwa kweli ripoti ya TL imewafungua macho majaji wetu. nchi zote duniani majaji waadilifu huwa wanaheshimiwa sana. tusubiri hukumu ya rufaa ya kamanda lema. naskia jaji kihiyo mbarouk s mbarouk naye yumo kwenye jopo. maajabu haya yapo tz tu, jaji wa supreme court ana bachelor of arts! magamba ondokeni fasta tuirekebishe nchii. uwiiiiii.
 
Back
Top Bottom