Dr Hussein Mwinyi awe rais wa Tanzania 2015

Status
Not open for further replies.
Huyu kijana safi hana ufisadi hata kidogo, kama umemsikia kwenye kashifa yoyote ile useme.

2015 - Hussein Mwinyi
2025 - Ridhiwani Kikwete
2035 - Kama kuna mjukuu wa Karume atapewa nafasi hapa

Umenimaliza mkuu kumbe ni porojo tu
 
naona unataka tusiendelee na mada ya Kucheza Ki-Chenge Ki-Chenge

Endelea nayo mkuu ila unajua mada ya Chenge italeta wasomaji wengi kwa hiyo inabidi unaweka pia habari kama hii ili isomwe - mambo ya ratings na audience if you know what I am saying.
 
Hao kina Masha na Membe wataendelea kuwa mawaziri au watapewa vitengo maalumu vya ulaji kidogo watulie. Kwa sasa mambo yote ni kwa Hussein Mwinyi maana hata hivyo ni zamu ya Zanzibar kutawala.

Baada ya Mwinyi tunamuaanda kijana safi na mtanashati - Ridhiwani Kikwete

Asante sana wewe ndio umenimaliza kabisa.
 
Pole sana Mwikimbi na Matiko Matare. Tunaongelea yajayo na sio yaliyopita kwa sasa. Kwa sasa ngoma ni Husseini Mwinyi 2015 na Ridhiwani Kikwete 2025

Hawa jamaa unaowataja, wazazi wao wenyewe hawana uwezo. Between JK na AHM wanashindana who is the worst president ever in TZ history. Sasa hawa watoto wao uwezo wao upo wapi? Hebu tueleze mwenzetu labda una data tusizozijua. Kama baba yake alimsaidia kukwepa JKT hiyo tayari ni corruption sasa huo usafi wake sijui uko wapi.

Halafu mtu kutuambia kuwa jamaa ni msomi kwa vile ana medical degree ni kuwatukana waTZ wakati tunajua tunawasomi kiasi gani!
 
Utaziona porojo mkuu lakini ngoma iko serious hapa.

Ok Mkuu Ngoma iko sawa nimekupata.

Umenikumbusha mwaka 2005 wakati naelekea kwenye uchaguzi nilienda na mtanzania mmoja yeye aliniambia tunaelekea kumtafuta double ruksa. Simkumbuki vizuri yule jamaa labda kama ni mwanachama hapa atakumbuka.

Nafikiri alikuwa ameisha fanya analysis za kutosha aliyoyasema nayaona sasa hivi. Kuwa tayari JK ni double ruksa. Kwa maana nyingine ni afadhali RUKSA kuliko JK. kwa hiyo vijana wao wanaweza kuwa triple RUKSA nk.

naona uko siriasi mkuu
 
kwa nini usiseme masaka for 2015 president?

Mbona huwaulizi wale waliosema kuwa Dr Slaa awe president 2010 wajipendekeze wenyewe? kuna makosa gani kusema kuwa Mwinyi na baadaye Kikwete watoto wawe mapresidents?
 
Ok Mkuu Ngoma iko sawa nimekupata.

Umenikumbusha mwaka 2005 wakati naelekea kwenye uchaguzi nilienda na mtanzania mmoja yeye aliniambia tunaelekea kumtafuta double ruksa. Simkumbuki vizuri yule jamaa labda kama ni mwanachama hapa atakumbuka.

Nafikiri alikuwa ameisha fanya analysis za kutosha aliyoyasema nayaona sasa hivi. Kuwa tayari JK ni double ruksa. Kwa maana nyingine ni afadhali RUKSA kuliko JK. kwa hiyo vijana wao wanaweza kuwa triple RUKSA nk.

naona uko siriasi mkuu

Exactly,

Yaani baada ya Kikwete, unarudisha ngoma zanzibar na unamweka Dakitari wetu Mwinyi akiongoza sambamba na Ndugu yake Karume kule Zanzibar, baada ya hapo, ngoma inarudi bara kwa kijana safi na mtanashati Ridhiwani wa Kikwete. watu weweeeeeeeeee!

Mambo ya triple play hayo if you know what I mean
 
Wewe jiunge na timu ya ushindi, hao kina Masha na Membe hawana nafasi ya kushinda mchakato wa ccm kule idodomya.

Nimeshajiunga kwenye kamati nilipokutana nao Sullivan Summit Arusha.
 
Exactly,

Yaani baada ya Kikwete, unarudisha ngoma zanzibar na unamweka Dakitari wetu Mwinyi akiongoza sambamba na Ndugu yake Karume kule Zanzibar, baada ya hapo, ngoma inarudi bara kwa kijana safi na mtanashati Ridhiwani wa Kikwete. watu weweeeeeeeeee!

Mambo ya triple play hayo if you know what I mean

fungeni hii thread ni ujinga mtupu, hii siyo nchi ya kifalme
 
Huyu jamaa hajui maisha ya Watanzania kama alivyo George Bush wa Marekani. Tunataka mtu wa kawaida ambaye tumeona mafanikio yake na si lazima awe mwanasiasa kwa sasa. Vilevile muda bado anaweza kutokea mtu mwenye talent zaidi. Hao watoto ni walewale!!!
 
hata marekani kwenyewe wameshindwa na kina kenedy, bush, clinton na wenzao wanarithishana madaraka. Au hujasikia kuwa Chelsea Clinton anataka useneta pia baadaye agombee uraisi?

Mkapa angekusikia angekuita mvivu wa kufikiri. Sio kila kitu wanachofanya wamarekani ni kizuri. Kama Marekani imeruhusu wanaume kuoana haina maana Tanzania itafanya busara ikiruhusu hilo. Tutakuwa tunaendelea kuonekana kuwa ni idiots.
By the way, kwanini mnazungumzia 2015 wakati 2010 ipo. JK has a fight to fight kuwafanya watu watawale vipindi viwili ni kama free ride. Ni lazima apiganie ashinde. Kama Mwinyi akitaka kujaribu ajaribu kwa credential zake na sio za baba.
 
Kwa vile Zitto ameonekana kuwa ana nia ya kugombea uraisi mwaka 2015 baada ya muda wa maendeleo ya uhakika yanayoletwa na Kikwete kuisha. Ni vyema sasa ikaangaliwa kwa upande wa ccm ni kina nani wenye uwezo wa kugalagaza wapinzani kwenye uchaguzi. Ni ukweli kuwa ccm itashinda tena kwa kishindo 2010 na kwa kishindo zaidi 2015, 2020, 2025, 2030, 2035 nk, mimi naanza na huu uchaguzi wa 2015 na kumpendekeza Dr Mwinyi kwa hii nafasi muhimu kabisa.

Ni msomi na mchapakazi mzuri. Ni mchamungu na msafi. Mwenzetu huyu ni mpole na mkarimu kama baba yake. Ruhusa na maendeleo ya watanzania wote kama aliyoleta baba yake. Ataendeleza sera za maendeleo za ccm na kuwanyima wahafidhina nafasi ya kuvuruga nchi.

Dr Hussein Mwinyi for president of Tanzania - 2015


Wandugu naomba tumuache huyu punguani.Huu ni uchafu wa hali ya juu,unatushushia hadhi mkuu.Haufai hata kuwekwa kwenye udaku!
 
Wandugu naomba tumuache huyu punguani.Huu ni uchafu wa hali ya juu,unatushushia hadhi mkuu.Haufai hata kuwekwa kwenye udaku!

Ni vema kuheshimu mawazo yake...Hii ya kukimbilia kuhukumu ina madhara yake..
 
i dont care nani atagombea kwa upande wa ccm kwa kipindi kinachokuja.
swala si kutaka ccm pekee iendelee kutawala.mi nadhani wapinzania wajizatiti kuingia bungeni hapo ndipo tutaona kwa dhati uwezo wa serikali kufanya kazi.imagine kina lipumba,mrema,mtikila na wengine wao wangekua bungeni tungekuwa na bunge la aina gani...inasikitisha kila mtu anakimbilia kugombea uraisi hata kama anaona kuwa hana uwezo hata wa kupata kura japo asilima zaidi ya tano.hizo nguvu wangezielekeza katika kupata wabunge wengi zaidi...
 
Tuache hizi siasa na campaign za majina. Kabisa hazitufai.

Ziongelewe sifa na sera zinazotakiwa kuikomboa Tanzania. Baada ya hapo ndio kuangaliwe ni kundi gani (chama) au mtu gani (independent) anaweza kuwa Kiranja kwa dira hiyo.

Nchi yetu inahitaji no nonsense leadership yenye kutovumilia ubadhirifu wowote ule.
With hindsight, inegfaa hata kuchambua aliosema JK and kutathmini nini kimefanyika na muda uliobaki na kutumia hiyo kama ujuzi wa kujua kiongozi gani huko mbele achaguliwe na uzoefu wao wa kukeep promises and what they have delivered throughout their public office careers
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom