Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,380
- 39,333
Jinsi ambavyo walitaka kinyume cha sheria kuondoa Taasisi ya Moyo kutoka mahali pake kwa kutumia amri za kibabe:
a. Dr. Dau/NSSF kwa kutuma magari ya wagonjwa na kujaribu kutaka kuondoa wagonjwa hospitali ilhali akijua hakukuwa na amri ya mahakama iliyotolewa kuamuru hilo.
b. Na hata walipokuja na amri, amri hiyo haikuwa halali kama ilivyooneshwa na Mahakama ya Rufaa.
c. Kwa kusababisha usumbufu wa kihisia, mahangaiko na hali ya wasiwasi kwa wagonjwa wa moyo na hivyo kutishia maisha yao.
d. Dr. Kapuya kwa maneno yake ya kibabe ambayo yalisababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa ilhali akijua hakukuwa na amri yoyote halali ya mahakama kufanya walichotaka kufanya. Maneno yake ya kusema THI itaondolewa hata ikibidi wagonjwa kuondoka na dripu ilikuwa ni ya kiimla na ya kizandiki.
e. Kwa kusababisha upotefu wa mapato kwa siku zote hizi ambapo jina la THI lilikuwa linachafuliwa kwa makusudi na hivyo kufukuza biashara.