Dr. Dau, Prof. Kapuya wawajibishwe; NSSF ishitakiwe!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Jinsi ambavyo walitaka kinyume cha sheria kuondoa Taasisi ya Moyo kutoka mahali pake kwa kutumia amri za kibabe:

a. Dr. Dau/NSSF kwa kutuma magari ya wagonjwa na kujaribu kutaka kuondoa wagonjwa hospitali ilhali akijua hakukuwa na amri ya mahakama iliyotolewa kuamuru hilo.
b. Na hata walipokuja na amri, amri hiyo haikuwa halali kama ilivyooneshwa na Mahakama ya Rufaa.
c. Kwa kusababisha usumbufu wa kihisia, mahangaiko na hali ya wasiwasi kwa wagonjwa wa moyo na hivyo kutishia maisha yao.
d. Dr. Kapuya kwa maneno yake ya kibabe ambayo yalisababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa ilhali akijua hakukuwa na amri yoyote halali ya mahakama kufanya walichotaka kufanya. Maneno yake ya kusema THI itaondolewa hata ikibidi wagonjwa kuondoka na dripu ilikuwa ni ya kiimla na ya kizandiki.

e. Kwa kusababisha upotefu wa mapato kwa siku zote hizi ambapo jina la THI lilikuwa linachafuliwa kwa makusudi na hivyo kufukuza biashara.
 
Mkjj, hoja zako dhaifu....na inaonesha hata uwezo wa kufikiri nao unapungua kwani haupo huru kufikiri...
Hivi unafikiri usipolipa ukashitakiwa umefanya kosa? Hakukuwa na Amri ya Mahakama? au THI walio appeal against hukumu ya Awali ya Mahakama?...

Unakumbuka Mabenki DSM walipokuja juu kuhusu madeni yao na Scandinavia?

Dawa ya DENI kulipa,....Dawa ya Jino Kung'oa
 
kesi dhidi ya NSSF haihusiani na suala la deni; inahusiana na jaribio lao la kutaka kuwahamisha wagonjwa kwa nguvu na kinyume cha sheria. Kitendo chao cha kutangaza kuwa watawahamisha wagonjwa kwa nguvu hata wakiwa na dripu mkononi kimewaletea udhaifu na usumbufu mkubwa wagonjwa na taasisi yenyewe. Kwa vile walijaribu kutekeleza kitu ambacho hawakuwa na uwezo nacho kutekeleza wakati wakijua kesi ya deni bado iko mahakamani nahitimisha jambo moja tu nalo lilikuwa ni kuitishia taasisi ya moyo kulipa deni kwa mbinde na kwa pinde.

Kwa vile mahakama ya rufaa imeona kuwa eviction notice haikuwa sahihi (kama nilivyoonesha hapa zaidi ya wiki tatu zilizopita) ni wazi kuwa NSSF walifanya makosa makubwa ambayo lazima wayalipie.

Hili liwe funzo kwa taasisi nyingine kuwa huwezi kuamua tu kwa vile una uwezo na serikali iko nyuma yako kujitengenezea sheria yako mwenyewe. Na suala la kodi nalo naamini mahakama itaoona uonevu mkubwa na hujuma iliyofanywa na NSSF wakishabikiwa na serikali. Watch me.
 
Mkjj, hoja zako dhaifu....na inaonesha hata uwezo wa kufikiri nao unapungua kwani haupo huru kufikiri...
Hivi unafikiri usipolipa ukashitakiwa umefanya kosa? Hakukuwa na Amri ya Mahakama? au THI walio appeal against hukumu ya Awali ya Mahakama?...

Unakumbuka Mabenki DSM walipokuja juu kuhusu madeni yao na Scandinavia?

Dawa ya DENI kulipa,....Dawa ya Jino Kung'oa
Chuma, sina hakika kama siku hizi dawa ya jino ni... daima kung'oa!!! Tunahitaji kutafakari zaidi!
 
Chuma, sina hakika kama siku hizi dawa ya jino ni... daima kung'oa!!! Tunahitaji kutafakari zaidi!

Sawasawa mheshimiwa! In fact dentist watakwambia kwamba the general wisdom ni kwamba kwanza lazima wafanye kila kitu kuitibu na kuzuia ising'olewe jino, kwa dawa na kuziba tundu.
Chuma, this analogy is not the best katika argument yako.
 
Kwani anayedaiwa ni Dr. Masau as a person au kampuni ya THI?
 
Mkjj, hoja zako dhaifu....na inaonesha hata uwezo wa kufikiri nao unapungua kwani haupo huru kufikiri...
Hivi unafikiri usipolipa ukashitakiwa umefanya kosa? Hakukuwa na Amri ya Mahakama? au THI walio appeal against hukumu ya Awali ya Mahakama?...

Unakumbuka Mabenki DSM walipokuja juu kuhusu madeni yao na Scandinavia?

Dawa ya DENI kulipa,....Dawa ya Jino Kung'oa

Mkuu Heshima mbele wote tunafahamu kwamba NSSF ni shamba la bibi sas kuna haja gani ya kulipa
Yeye akae tuu kuanzia sasa hivi kila siku majaji watakuwa wanaumwa kesi ikitajwa
Bora yeye anafanya kazi ya wito na sio wengine
Hivi mbowe wa chadema alilipa lile deni lake kwa shamba la bibi yaan NSSF ?
 
Mkora.. kaangalie ripoti ya Mkaguzi Mkuu ya mwaka 2006/2007 inapatikana hapa http://www.nao.go.tz halafu utuambie kama Mbowe kalipa au la. Lakini hii mada inahusu utendaji mbovu wa NSSF ambao umesababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa na madhara ya kisaikolojia kwa kitendo chake cha kinyume cha sheria.
 
China to build heart institute in Tanzania

APA-Dar es Salaam (Tanzania) China will build a training and surgical heart institute with a capacity to accommodate 100 patients at once at the Muhimbili National Hospital in Tanzania’s commercial city of Dar es Salaam, the Parliamentary Committee on Foreign Affairs, Defence and Security Chairman, Wilson Masilingi, told APA here on Friday.

Masilingi said the move came was a gesture of friendship and strong ties that exist between Tanzania and China over many decades.

“The centre will be a five-storey building with two surgical theatres as well as space to accommodate 100 heart patients,” id Masilingi said.

China has pledged to assist the country with a number of projects, one being the building of an international conference centre at Salender Bridge in Dar es Salaam, he said.

“The project is at the designing stage. The Chinese government will build an agricultural research centre, whose construction is due to start anytime from now,” he added.

According to Masilingi, Tanzania will benefit from Chinese agricultural experts as well.

Masilingi, who together with other members of parliament, had just returned from an official visit of China, was briefing journalists about the tour.

Tanzania sends hundreds of heart patients to India every year at a considerable expense.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom