Dr. Dau aingilia mchakato wa ugawaji viwanja Mafia

Dr. Dau aingilia mchakato wa ugawaji viwanja Mafia

Wana jf naona mnamsakama sana huyu Dr.Dau hata kama ana mchango mkubwa katika shughuli za maendeleo hasa ya nchi yake.
Hivi ni watu wangapi hujenga na kuimarisha miji yao wanayotoka? Yaani kuwatetea watu wa Mafia ili waweze kupata ardhi ndogo ya kumiliki katika maeneo yao pia ni udini?
Hebu acheni kueneza sumu mbaya.Nani asiyejua kuwa ni viongozi wangapi wa serikali wamemaliza viwanja vyooote vya mji wa Dar es Salaam na wenyewe wamebakia weupeeeeeeeeeeeeeeeeeee wanakimbilia maporini tena wanawacheka kwa kufanya hivyoooooo.
Sasa wameingia Mafia pia wagawane wawaache wa Mafia pia weupeeeeeeeeeeeee.Mambo haya mpaka lini.
Alichofanya Dr.Dau ni kizuri sana tena saaaaaaaaaaaannnaaaaaaaaaaaa cha kuwaokoa wanyonge wa Mafia ili wapate ardhi ya kuishi.Nawaambia watanzania wenzangu wa Mafia waungane na Mzee Dau kufanikisha uwezekano wa kurudisha ardhi yao kwao.
 
Kama hii ndio hoja ya "uenyeji" na "wageni" ndio inasimamiwa basi waliosema kuna suala la Ubaguzi waweza kuwa na hoja zaidi. Binafsi ningependa kusikia hoja kuwa taratibu zimevunjwa au sheria fulani imevunjwa, rushwa n.k Lakini kwamba Mngoni hawezi kununua Kiwanja Mafia kwa sababu anatoka Songea SIYO hoja na ikikubaliwa Mafia itabidi ikubaliwe sehemu nyingine nchini. Itakuwaje Mzaramo ambaye anataka kununua kiwanja Bukoba? au Mnyaturu anayetaka kununua kiwanja Kisarawe?

Ningependa hoja itolewe ambayo haihusiani na kuwagawa Watanzania kwa misingi ya mahali wanakotoka kwani Mtanzania anayo haki ya kununua ardhi mahali popote katika TAifa lake. Itolewe hoja yenye nguvu kidogo kuliko yenye hisia za kibaguzi maana kama hoja ya mahali inaweza kutolewa na ikaangaliwa itakuwaje kama wale wanaopewa ni Wakristu na wakazi wengi wa Mafia ni Waislamu? Je, Wakristu hawawezi kununua ardhi maeneo ya Waislamu wengi?

Labda swali ni sheria au taratibu gani zilikiukwa katika kuwapatia hao watu wengine viwanja? Na ni kweli hakuna wazaliwa wa mafia ambao wamegawiwa viwanja hivyo au ni wale waliopewa ili kuwanyamazisha?
Napatwa na woga kwa hiki ulichochangia Mzee M/kijiji. Huu si mchango wa caliber yako hata kidogo. Na hii sasa inadhihirirsha kuwa ukombozi wa mlalahoi wa Tanzania hautafanikiwa kwa kuwa watanzania si wamoja abadan. Miongoni mwa tatizo linalopigiwa kelele na wanaharakati wengi hapa nchini ni mgawanyo usio sawa wa raslimali za nchi hususan kwa watu wa daraja la chini. Hawa hawana access ya makazi bora, lishe bora, mavazi bora, elimu bora nk. Hivyo tambua kuwa mtetezi yeyote wa equal sharing ya resources za nchi ni lazima afikirie namna atakavyoweza kuwawekea mazingira ya kupata huduma hizi kwa kada ya watu hao. Viwanja/Ardhi/Makazi ni miongoni mwa masuala hayo. Sasa kwa kesi ya mafia hoja ni kwamba, wale indigenous people; yaani wakazi walio wengi ni maskini ikiwa pamoja ni maskini wa makazi bora ambayo yanaanzia na viwanja. Hivyo mpango wa ugawaji viwanja ni dhahiri ulipaswa kutoa vipaumbele kwa wakaazi wa mafia(regardless dini yao au asli yao). Nasema mkaazi wa mafia na si mpita njia wa mafia kama watumishi/watu wa mahoteli ambao wengi wao wana possibility ya kuondoka katika muda fulani na huenda wameshajenga base katika maeneo mengine waliyochagua wenyewe katika safari yao ya kikazi na si kwa yeyote mwenye uwezo wa kununua/kumiliki kutokana na hadhi yake(kumbuka watumishi walio wengi katika ngazi za wilaya wanakuwa na jukwaa moja kwa kuwa wanakuwa na sifa/hadhi na elimu inayolingana hivyo kuwa rahisi kupata accessibility ya mambo flani) na kwa kiasi fulani kuwatenga wakaazi wa wilaya au eneo hilo. Sina maana kuwa asiye mkaazi hawezi kupata au hana ruhsa ya kupata, nazungumzia suala "priority" kwa wakaazi wa kudumu wa eneo hilo ima kwa wao wenyewe au kwa uzao wa asli ya familia yake kwa sababu kwa nature ya Tanganyika ilivyo wana competition capability ndogo ukilinganisha na watumishi ambao hawa watumishi mimi nawaona kama ni daraja la kati kwa mfumo wa maisha ya Tanganyika na wengi wao wanamiliki makaazi/wana uwezo wa kufanya hivyo pia katika maeneo mengine ya nchi yetu na kupelekea kile kinachoitwa "hoarding" ya viwanja. Matokeo yake tukiamua kutumia nguvu ya ushindani, tutajikuta huyu mkaazi wa mafia(kumbuka siyo mafia tu ni popote Tanzania mfumo ntakaouunga mkono ni huo) hatofaidika hata na raslimali nyepesi kabisa ambayo ni makazi, yes hana uwezo wa kupanda gari kwenda kigoma kununua kiwanja na kuanzisha maisha na hata uwezo akiwa nao nguvu za kiuchumi zinamzuia kutokana na namna alivyoandaliwa! Ni bahati mbaya tu haya yanatokea pwani kwa sababu harakati za maisha tuliyonayo zinawavutia zaidi watu pwani kuliko bara, lakini am sure ingelikuwa kinyume tatizo hilihili lingelijitokeza. Hivyo bac, equity isipoangaliwa tutafika pahali mtanzania X ana access ya makazi zaidi ya kumi katika maeneo tofauti na mtanzania y atakuwa hana access ya makazi hata alipozaliwa kitu ambacho kitaleta matabaka ya ajabu sana huko mbeleni. MM, najua ww ni Mtanzania, pamoja ya kwamba labda wewe na mimi hatujakulia vijijini, lakini huko vijijini(kuanzia ngazi za wilaya wakaazi wa kawaida wana hali mbaya hivyo lazima wasaidiwe njia bora za kupata mahitaji yaliyo katika maeneo yanayowazunguka hili haliepukiki. Kwa namna fulani, tofauti baina ya mtanzania na asiye mtanzania ni sawa na tofauti baina ya Mkigoma na Mkilimanjaro; wote ni wanadamu wenye mahitaji yaleyale wanaotofautishwa na mipaka ambyo ni man made lakini wanaharakati popote duniani wanataka priority kwa raslimali za nchi yake ianzie kwa wananchi wa Nchi hiyo simply kwa kuwa asiye raia wa nchi ile inaaminika kuwa jukumu la kufaidika na keki ya dunia linaweza pia kufanywa na nchi ambayo yeye raia! Please MM na wana JF wengine, tufikie pahali tuwe fair kama tunataka umoja haya mambo ya uislamu/ukristo/umachame/umakuwa hayataondoka asilani hivyo tukubali tu sote ni watanzania lakini tunaotoka sehemu tofauti ndani ya nchi so suala la kudai ubaguzi katika masuala ya ki-equity kama hili halitatusaidia. Kwa kumalizi mimi binafsi naunga mkono kipaumbele cha viwanja kianze kwa wakaazi wa kudumu wa eneo hilo (popote Tanzania) ili waweze atleast kupata hiyo haki yao ya makazi kwa kwani haki nyingine tayari zinachukuliwa na mafisadi ili kutotoa nafasi kwa wengine kuanza kupata haki ya ku-hoard na kufanya biashara wakati wengine wanatafuta haki ya kulala tu. {Usiwafanye sehemu ya watu fulani wawe na hali ya juu sana kwa kupitia mgongo wa kuwafanya watu wengine wawe na hali ya chini sana}
 
Wanaotuhumiwa kufanya uhuni na ufisadi kwenye ugawaji wa viwanja kisiwani mafia ni Mbunge wa Mafia, pamoja na DC na baadhi ya maofisa mwaka jana waliorganise tamasha la MASHOGA kinyume na matakwa ya wananchi wa kisiwa hicho. Naona wameamua kuumaliza mwaka kwa kugawa ardhi ndogo ilipo ya wananchi kwa maswahiba wao bila kuzingatia udogo na wanamafia wenyewe. This wont end well kama ileee ya tamasha la mashoga kwani nalo lilipitishwa na hawa hawa wanaogawa ardhi kifisadi....hebu tujikumbushe yalojiri juu ya Tamasha la mashoga:

zaidi soma hapa:


YAH: KUPINGA TAMASHA LA MASHOGA KISIWANI MAFIA:​

Sisi kama wenyeji wa kisiwa hichi na wenye nia uchungu na kisiwa hiki tumesikitishwa na hatua ya baadhi ya wenye mahoteli ya kitalii kwenye kisiwa hichi pamoja na uongozi mzima wa wilaya (DC) na halmashauri kutoa kibali kwa kundi la burudani toka Ugiriki kuja kufanya vitendo vya ushoga kwa kutumia mgongo wa Tamasha la muziki. Pia tumesikitishwa na DC wetu bwana Mangochie Manzie kukubali kutoa kibali kwa hawa vijana 3,000(revelers) bila kupata ridhaa ya wenyeji wa Kisiwa hichi (Public consultation). Tungependa ifahamike kuwa sisi kama wenyeji wa Kisiwa hichi tunakaribisha wageni lakini ni LAZIMA wazingatie na waheshimu mila na taratibu zetu na moja kati ya hizo mila zetu USHOGA haumo!

Kitendo cha kutaka kuleta vijana hawa mashoga hapa kisiwani kufanya vitendo vyao kwa siku 14 mfululizo hakikubaliki kimaadili na tunawaunga mkono wana Mafia na hasa wazazi ambao hawako tayari kuona watoto wao wakishuhudia vitendo vya kishoga, utumiaji wa madawa ya kulevya ambavyo ni si mila na desturi yetu kama waTanzania.

Kama mjuavyo Mafia ni kisiwa cha amani na ndio maana kimekuwa kinaongoza kwa utalii wa scuba diving duniani na tunaendelea kuwakaribisha watalii ambao wanakuja na kutuheshimu na wanaoelewa umuhimu wa kutunza mazingira ya kisiwa hichi.

Hivi kwa mfano mazingira yashachafuliwa ni sisi watu wa Kisiwa hiki ndio tutasafisha au halmashauri? je wanazo pesa za kusafisha na kuokota toilet papers zitakazo achwa na hawa Mashoga kwenye mashamba yetu?

Kwa kawaida ya Mashoga hawatokaa sehemu moja hapa kisiwani na watataka kwenda kufanya uchafu wao kwenye fukwe zetu hapa kisiwani, hivi Uongozi wa Kisiwa hichi utatoa polisi wangapi kwa kila kundi la hawa mashoga kufanya mambo yao? kwani sidhani kama wananchi watakaa na kushangilia vitendo hivi vikifanyika hadharani.

Tungependa kuufahamisha umma kuwa hawa waandaji tamasha hili lilipofanyika kwenye kisiwa cha Skyros, watu walililalamika sana pamoja na kuwa Wagiriki wana mitizamo ya ku liberali kwenye mambo haya lakini hali ilikuwa mbya kiasi cha Polisi kuvamia na kusitisha lile Tamasha kwani lilikuwa linaelekea kuvujinka kwa amani.

Katika kipindi hichi ambacho tunaelekea kwenye Uchaguzi je ni kweli Serikali inataka kuona uvunjikaji wa amani katika kipindi hichi tunachoelekea kwenye Uchaguzi kwa kukubali hili tamasha la Mashoga?

Je jeshi la polisi linazo resources za kulinda mashoga 3,000 usiku na mchana kwa siku saba mfulululizo?

Kwa nini Bwana Mike Athanassakis ambaye ndiye mratibu wa hili Tamasha hili la Mashoga hataki kukutana na viongozi wa Kisiwa hichi na kuwaeleza kwa kinaga ubaga nia yake?

Maandaji wa Tamasha hili wamesema wamepata ushirikiano wa karibu na kampuni ya uwindani na utalii inayojiita KARIBUSANA ambayo iko chini ya
Costa Coucoulis,Angela Damas,Chyrista Batou na Mark Evans ambao wanajiita wahifadhi wa mazingira kwenye tovuti yao lakini wakati huo huo wako tayari kuhakikisha kuwa mazingira ya kisiwa chetu yanachafuliwa na hawa wageni.

Je Mbunge na DC wa Kisiwa hichi watakuwa wanatekeleza ilani ya chama gani kulikubali hili Tamasha la Mashoga?

Je wilaya iliyo masikini kuliko zote Tanzania inahitaji Tamasha la muziki au tunahitaji miradi ya Maendeleo?

Je BASATA na Wizara ya Utalii wameamua ku promote USHOGA Tanzania?

Hospitali zetu hapa zinatia aibu na mbaya zaidi huduma za afya kwa mama zetu na dada zetu wanapojifungua zipo katika hali duni, hivi kweli mheshimiwa DC na timu yake wameona kwa sasa tunachohitaji ni hili Tamasha?


MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo: Friends Of Mafia: TAMKO KUHUSU TAMASHA LA MASHOGA

MICHUZI: Mafia kunani tena???


Dont tell me kuwa Shah anahusika na mambo ya matamasha ya mashoga huko kwenu Mafia

kama ni kweli sishangai kuona mnaogopa wageni
 





Imagine mtu kama mbunge wa Songea DEVOTH LIKOLOLA anapewa kiwanja lakini mzaliwa pale Mafia na aliyeoomba kihalali alikosa.




Nadhani katika hili umejaribu kumnasua Dr. Dau kutoka kwenye dhambi ubaguzi wa kidini lakini dhambi hii ya ubaguzi inaendelea kukutafuna.

Kwamba Devotha Likokola kwakuwa ni mbunge wa songea hastahili kuuziwa kiwanja huko mafia, sio!?

Kama hiyo ni mojawapo ya sababu za Dr. Dau na wenzake kupinga baadhi ya watu kugawiwa viwanja huko mafia, basi wote mnaogelea katika bahari moja, ya ubaguzi! wa kidini na kikabila kwakuwa huyo mliyemtolea mfano anawakilisha wale mnaowapinga wasipate viwanja huko mafia.

Sasa maajabu ni kwamba hao mnaopinga wakuja wasipate viwanja kwenu mafia ndio hao hao mliojilimbikizia viwanja katika maeneo mengine ya nchi!!
 
Kama mkazi wa Mafia anaomba kiwanja na anakosa na mkazi wa nje anapata kisa ni MBUNGE, clearly kuna mambo mawili kisheria.

La kwanza, sheria imevunjwa na haki ya mtu nyang'anywa na la pili sheria itakua na loophole kuachia ufisadi ufanyike. Sasa wale ambao ni "wataaalumu" wa sheria tunaomba watuangaze.

Kusema kuwa bwana Dau ni mdini si hoja ya msingi katika mada hii. Swala la msingi ni kwamba inakuaje mkazi wa Mafia anakosa kiwanja na anaenda kupewa mtu ambaye si mkazi. Kumbuka, wakazi wa Mafia wengi hali zao ni dhoofu. Na yule ambaye anauwezo wa kutoka alikotoka na kuja Mafia kuchukua ardhi inadhihirsha kuwa anauwezo wa kifedha kuliko a normal Mafian. Sasa je priority apewe mtu mwenye hela au mkazi wa Mafia?

It seems wanaJF are so blinded by hatred on bwana Dau on the basis of his religious belief. Mambo ya NSSF na ugawaji wa ardhi Mafia, mambo ya dini na ugawaji wa ardhi Mafia yanaingiaje. The guy anatetea haki ya an average Mafian watu hamtaki. Sasa ni kitu gani hasa mnataka?
 
Tunaenda na jf style

invisible unaweza kuiweka top kama kiambatanishi.....
attachment.php

attachment.php


attachment.php

View attachment 41088

View attachment 41086

View attachment 41083
 
..waache ubaguzi.

..hiyo ardhi angepewa Mhindi,Muarabu,au Mzungu, usingesikia malalamiko yote hayo.

..mbona Dr.Dau ni mkaazi wa Dar kwa miaka mingi leo amekuwa "mkereketwa" wa ardhi ya Mafia.
 
Hii kama ni mziki bas ndio kwanza ni bashraf maana mziki kamili unafuata

JF Style
 
​hakuna uzawa katika kugawa ardhi watanzania wote ni sawa
 
..waache ubaguzi.

..hiyo ardhi angepewa Mhindi,Muarabu,au Mzungu, usingesikia malalamiko yote hayo.

..mbona Dr.Dau ni mkaazi wa Dar kwa miaka mingi leo amekuwa "mkereketwa" wa ardhi ya Mafia.

Una uhakika na unachokisema ?
 
Kama hii ndio hoja ya "uenyeji" na "wageni" ndio inasimamiwa basi waliosema kuna suala la Ubaguzi waweza kuwa na hoja zaidi. Binafsi ningependa kusikia hoja kuwa taratibu zimevunjwa au sheria fulani imevunjwa, rushwa n.k Lakini kwamba Mngoni hawezi kununua Kiwanja Mafia kwa sababu anatoka Songea SIYO hoja na ikikubaliwa Mafia itabidi ikubaliwe sehemu nyingine nchini. Itakuwaje Mzaramo ambaye anataka kununua kiwanja Bukoba? au Mnyaturu anayetaka kununua kiwanja Kisarawe?

Ningependa hoja itolewe ambayo haihusiani na kuwagawa Watanzania kwa misingi ya mahali wanakotoka kwani Mtanzania anayo haki ya kununua ardhi mahali popote katika TAifa lake. Itolewe hoja yenye nguvu kidogo kuliko yenye hisia za kibaguzi maana kama hoja ya mahali inaweza kutolewa na ikaangaliwa itakuwaje kama wale wanaopewa ni Wakristu na wakazi wengi wa Mafia ni Waislamu? Je, Wakristu hawawezi kununua ardhi maeneo ya Waislamu wengi?

Labda swali ni sheria au taratibu gani zilikiukwa katika kuwapatia hao watu wengine viwanja? Na ni kweli hakuna wazaliwa wa mafia ambao wamegawiwa viwanja hivyo au ni wale waliopewa ili kuwanyamazisha?

​hakuna uzawa katika kugawa ardhi watanzania wote ni sawa

Jamani bora kuuliza na mkaeleweshwa basis ya malalamiko ni nini.

Ninafahamu fika kuwa idadi ya waombaji ilikuwa ni kubwa sana ukilinganisha na viwanja vilivyopo. Hivyo basi, isingekuwa rahisi kwa kila aliyeomba akapata mahitaji yake. Kwa mantiki hiyo, sisi wakazi wa Mafia INCLUDING huyo Dr Dau hawana tatizo la kukosa kiwanja na tunaamini kabisa hata wenzetu hao waliokosa viwanja kama kama wengine , hawana tatizo na hilo.


Kitu ambacho kinachotatiza hapa kama ileee ya TAMASHA LA MASHOGA MAFIA mwaka jana, (na ndiyo msingi wa malalamiko ya Dr Dau na wenzake ) ni kuwa ofisi ya Mkurugenzi haikuweka wazi vigezo vilivyotumika kugawa viwanja hivyo. Hali hii inatia mashaka hasa ukizingatia kuwa wengi waliopewa viwanja hivyo si wakazi wa Mafia ambayo ki jiografia ni kisiwa kidogo ambacho hakina raslimali yoyote ile zaidi ya ardhi ndogo iliopo na na baya zaidi wengi wa hao waliopewa ni watumishi wa Halmashauri na hasa watumishi wa Idara ya Ardhi, jambo ambalo ni kinyume kabisa na misingi ya Utawala Bora [principles of good governance].

Cha kijiuliza DC wa Mafia bwana Mangochie Manzie, Mbunge wa Mafia bwana Abdulkarim Shah (Bulji) pamoja na madiwani wanatekeleza ilani ya Chama gani? Kwa sababu ni wazi kuwa hawa hawa mwaka jana walipigania TAMASHA LA MASHOGA liende kisiwani Mafia, mwaka huu wameamua kujipatia viwanja wao na wake zao KIFISADI bila kuweka maslahi ya wana Mafia kwanza kama wakazi wa pale
 
SlidingRoof,

..mnaanza ubaguzi kwenye ardhi, then what is next?

..sasa ktk list uliyoileta tueleze ni yupi wa Mafia na yupi ni "mtu wa kupita."

..pia ktk hao wa Mafia tueleze ni wapi wakaazi wa kudumu wa huko, manaake tunaelewa kwamba Dr.Dau kalelewa kariakoo, na muda mwingi yupo dsm kutokana na majukumu yake.

NB:

..hivi wakazi wa Dar nao waanze kunyanyasa wenzao wa mikoani kwamba wasipate viwanja hapa mjini?
 
SlidingRoof,

..mnaanza ubaguzi kwenye ardhi, then what is next?

..sasa ktk list uliyoileta tueleze ni yupi wa Mafia na yupi ni "mtu wa kupita."

..pia ktk hao wa Mafia tueleze ni wapi wakaazi wa kudumu wa huko, manaake tunaelewa kwamba Dr.Dau kalelewa kariakoo, na muda mwingi yupo dsm kutokana na majukumu yake.

NB:

..hivi wakazi wa Dar nao waanze kunyanyasa wenzao wa mikoani kwamba wasipate viwanja hapa mjini?

kuna hoja mbili kuu za msingi ambazo nashangaa hutaki kuzi address:

1. Hawa hawa waliopitisha hii kitu ndiio hao hao walioleta TAMASHA LA MASHOGA kisiwani Mafia mwaka jana. Je hawa watu wana maslahi na wakazi wa Mafia?

Je hawa watu kwa mtazamo wako wanayo moral authority ya kuamua nani apewe nini Mafia ? Je wewe unaunga mkono ushoga?

2. Wengi wa waliopewa hivyo viwanja ni staff wa Halmashauri pale na je huoni kama kuna conflicts of interests?

3. Hujauliza kwa nini idara ya ardhi Mafia ilificha na haikutoa vigezo vya kutoa hivi wiwanja sasa wewe huoni hapo kuna matatizo ya transparency?
 
SlidingRoof said:
kuna hoja mbili kuu za msingi ambazo nashangaa hutaki kuzi address:

1. Hawa hawa waliopitisha hii kitu ndiio hao hao walioleta TAMASHA LA MASHOGA kisiwani Mafia mwaka jana. Je hawa watu wana maslahi na wakazi wa Mafia?

Je hawa watu kwa mtazamo wako wanayo moral authority ya kuamua nani apewe nini Mafia ? Je wewe unaunga mkono ushoga?

2. Wengi wa waliopewa hivyo viwanja ni staff wa Halmashauri pale na je huoni kama kuna conflicts of interests?

3. Hujauliza kwa nini idara ya ardhi Mafia ilificha na haikutoa vigezo vya kutoa hivi wiwanja sasa wewe huoni hapo kuna matatizo ya transparency?

SlidingRoof,

..siungi mkono ushoga.

..suala la ugawaji viwanja linatakiwa liangaliwe kwa mtizamo wa KISHERIA na siyo kuleta hadithi za mashoga.

..kama idara ya ardhi haikutoa vigezo au haikuweka utaratibu uliowazi wa kugawa viwanja hivyo then kuna tatizo hapo.

..lakini pia nimeona tatizo kubwa zaidi ktk hoja zako za awali ambapo ulikuja na shutuma za KIBAGUZI dhidi ya wa-Tanzania ambao hawana asili ya Mafia. Uzawa au asili ya eneo husika si kigezo cha kisheria cha kupata ardhi au makazi ktk nchi yetu.
 
It is a shame to start to put citizen into tribal areas. What I thought is a norm for people to settle anywhere in the country seem to be violated by the "natives of mafia". this in my opinion is utterly rediculos.

Of course anyone can settle anywhere in the country lakini that doesnt mean locals should not be consulted before these decisions are made. The future is an ecologically protected Island such as Mafia ought to contain smaller, less crowded, more socially cohesive, sustainable and greener communities and thats what the locals are fighting for
 
SlidingRoof,

..siungi mkono ushoga.

..suala la ugawaji viwanja linatakiwa liangaliwe kwa mtizamo wa KISHERIA na siyo kuleta hadithi za mashoga.

..kama idara ya ardhi haikutoa vigezo au haikuweka utaratibu uliowazi wa kugawa viwanja hivyo then kuna tatizo hapo.

..lakini pia nimeona tatizo kubwa zaidi ktk hoja zako za awali ambapo ulikuja na shutuma za KIBAGUZI dhidi ya wa-Tanzania ambao hawana asili ya Mafia. Uzawa au asili ya eneo husika si kigezo cha kisheria cha kupata ardhi au makazi ktk nchi yetu.

Tatizo ni kuwa hao wanaogawa ardhi na ni hao hao walioleta tamasha la mashoga Mafia. Lakini tatizo kubwa zaidi ni kuwa ugawaji wa viwanja hivyo ulikuwa:

1. hauna misingi ya utawala bora,

2 ulijaa upendeleo

3. ulijaa vishawishi vya rushwa.

4. Haukuwa transparent

5. Haukufanyika public consultation

6. Haukuzingatia mazingira

Hata ingekuwa ni kijiji chenu haiwezekani ukakubali tuu watu waje wapewe bila wenyeji kuulizwa ukizingatia SPECIAL case ya kuwa sehem yenyewe ni kisiwa tena kidogo mno
 
Ndugu hapo juu umeeleza ukweli wa mambo. Mbona viwanja wakipewa wasomali, waarabu, wazungu hamlalamiki Dr Dau akitetea wananchi wenzie wa Mafia maegeuka fisadi. Tusisahau bongo waiosoma wote ni mafisadi. Mdini nadhani hii hoja ya muislamu akifanikiwa basi kapendelewa ni hoja dhaifu. anyway mi sina dini.

Naifahamu vizuri mafia coz' nimekaa pale almost 4 years! Sincerly, kama ni kutetea maslahi ya watu wa mafia; sio siri Dr. Dau ana wajibu huo hasa ukizingatia kwamba Mafia ni kisiwa kidogo sana with less than 30km from north to south (hiyo ndio longest distance). Na kwa jinsi ilivyo, wakati vinagawiwa viwanja vya Dongo, nilikuwa Mafia, na majority waliopata ni wageni. Hapa issue sio kwamba wageni hawana haki ya kupata viwanja mafia, bali maslahi ya wa-mafia wenyewe ni lazima yazingatiwe kwa hoja ile ile kwamba hiki kisiwa ni kidogo sana huku kukiwa na uhamiaji mkubwa wa watu kutoka bara(sio wakristo kama mtoa mada anavyotaka kupotosha). By the way, sijapata kuona watu wenye torelance ya hali ya juu (ya kisiasa na kidini)kama watu wa mafia, therefore am afraid mtoa mada anataka kupandikiza udini katika kisiwa hicho! Wakati nipo mafia nilikuwa na urafiki na wazee wengi sana wa mafia (ambao wote ni kama baba na babu zangu) lakini sikupata hata siku moja jamaa wakizungumzia masuala ya ukristo. Ni kweli, pale ulipotokea uhalifu, hususani wizi, walikuwa wana-blame wahamiaji kutoka bara na wala sio wakristo! Najuwa mto mada anaweza kuji-defend kwa kudai hakusema wamafia ni wadini; ninachotaka kusema ni kwamba asitake kupanda chuki za udini mafia; i like this island;
 
Back
Top Bottom