DPP aeleza sababu Nusrat Hanje kuachiwa huru

Sasa kama kumbe DPP anaweza Kuamua tu Kuwafutia Mashtaka walioko Gerezani mbona wapo Watanzania wengi waliosingiziwa na hawasamehi?
 
Kwahiyo ni uamuzi tu,usio na tija,ni uamuzi unaotumika kisiasa,

Yaani unaamua tu,unaamka asubuh,umetoka kulala na mkeo,unacheki Sheria inakuruhusu kufanya kitu flani,unafanya,tu,hakuna mchakato,hakuna maandalizi,na kwanini unamuachia mtu,usiku,siku nzima,ulikuwa wapi,kwanini siku hiyo usiku,huyu jamaa,akili hana. Kabisa,

Hata Rais anammlaka ya kusamehe wafungwa,lakini hakurupuki tu,katoka,kukata gogo,anapiga simu magereza,na kuwaambia muachieni fulani.

Pls do not insult our intelligence,this is a fuckup,
Kama ndivyo si afadhali angenyamaza kuliko kutoa sababu za kijinga kama hivyo
 
Mkurugenzi wa mashtaka nchini Tanzania (DPP), Biswalo Mganga leo Jumatano Desemba 2, 2020 ameeleza uamuzi wake wa kumfutia mashtaka kada wa CHADEMA, Nusrat Hanje ambaye Novemba 27, 2020 alivuliwa uanachama wa chama hicho pamoja na wenzake 18.

Nusrat ambaye alikuwa katibu wa baraza la vijana CHADEMA (BAVICHA) alikaa mahabusu siku 163 na siku moja baada ya kutoka mahabusu jina lake lilikuwa miongoni mwa majina 18 ya wanawake walioapishwa Novemba 24, 2020 mjini Dodoma kuwa wabunge wa viti maalum.

Mbali na CHADEMA kupinga kuapishwa kwa wanawake hao kwa madai kuwa majina yao hayakupitishwa na kamati kuu ya chama hicho na kwamba kilichofanyika ni usaliti, pia walihoji kitendo cha Nusrat kutoka mahabusu na moja kwa moja kuapishwa wakati alipaswa kujaza fomu Novemba 20, 2020 na alitoka mahabusu wakati muda wa kujaza fomu hiyo ukiwa umepita.

Akizungumza na wanahabari leo katika gereza kuu la Karanga mjini Moshi, Mganga amesema yeye ndio aliyemwachia kada huyo kutokana na mamlaka aliyonayo chini ya kifungu 91 cha CPA cha 2002.

DPP Mganga alitoa kauli hiyo wakati akitoa taarifa ya kuwafutia mashtaka watuhumiwa 72 ambao walikidhi sifa za kufutiwa mashtaka kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kubambikiwa makosa.

Mganga alimtaja mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuwa yeye na wenzake angeweza kuwashtaki kama Nusrat lakini aliamua kufuta mpango huo kutokana na uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.

Kwanza nataka kuuliza, hicho ndicho alichozungumza pekee au kuna habari haikufikishwa hapa?

Sasa basi kwa maelezo kama haya halafu watanzania wenzangu tunaona watu hapa kuwa wameridhika na maelezo haya. hebu jamani kwa muda mfupi kuweni kama sisi tusiokuwa na vyama halafu mjiulize masuali kwa upeo bila ya kupendelea upande wowote ule. Itakuwaje mkurugenzi wa mashitaka anaamua kulijulisha taifa kuwa anawaachia au amewaachia watuhumiwa kadhaa kwa sababu tafauti lakini anazishindwa kubainisha sababu zaidi ya moja.

Halafu watu mnaridhika na hilo. Pia kwa kauli yake mwenyewe mkurugenzi wa mashitaka anasema kuwa kuna waliobambikiziwa makosa, na tena watanzania tunaridhika na hilo bila kuuliza masuali kwa mfano wamebambikiziwa makosa na nani? watafanywa nini hao waliowabambikizia wenzao makosa, jee serikali itawalipa fidia hao walioweka ndani bila ya makosa yeyote yale? jee Nusrat alibamkiziwa makosa au ameachiwa "kutokana na sababu mbali mbali"?

Na suali kuu zaidi ambalo watanzania ingelibidi kuuliza ni tutajuaje kama wabambikizaje wa makosa hii sio mara yao ya kwanza? Jee mkurugenzi wa mashitaka atazifanyia uchunguzi kesi zote za nyuma ambazo wabambikizaji walihusika nazo? Takriban kisheria katika mataifa yote duniani pale inapogundulika afisa fulani wa polisi amekuwa corrupt na amembambatikia mtu makosa, kesi zake zote alizozifanyia kazi huangaliwa upya, jina lake hutajwa na husimamishwa kazi hadi pale uchunguzi unapokamilika, jee hilo litafanyika Tanzania?

To be honest kwa tulivyo watanzania, hakuna atakaethubutu kuuliza lolote, hata waandishi wa habari ambao moja ya majukumu yao ni kuuliza na kuupata ukweli kwa manufaa ya umma wote watakaa kimya! but hey Tanzania oyeeeeee!!!!
 
Mkurugenzi wa mashtaka nchini Tanzania (DPP), Biswalo Mganga leo Jumatano Desemba 2, 2020 ameeleza uamuzi wake wa kumfutia mashtaka kada wa CHADEMA, Nusrat Hanje ambaye Novemba 27, 2020 alivuliwa uanachama wa chama hicho pamoja na wenzake 18.

Nusrat ambaye alikuwa katibu wa baraza la vijana CHADEMA (BAVICHA) alikaa mahabusu siku 163 na siku moja baada ya kutoka mahabusu jina lake lilikuwa miongoni mwa majina 18 ya wanawake walioapishwa Novemba 24, 2020 mjini Dodoma kuwa wabunge wa viti maalum.

Mbali na CHADEMA kupinga kuapishwa kwa wanawake hao kwa madai kuwa majina yao hayakupitishwa na kamati kuu ya chama hicho na kwamba kilichofanyika ni usaliti, pia walihoji kitendo cha Nusrat kutoka mahabusu na moja kwa moja kuapishwa wakati alipaswa kujaza fomu Novemba 20, 2020 na alitoka mahabusu wakati muda wa kujaza fomu hiyo ukiwa umepita.

Akizungumza na wanahabari leo katika gereza kuu la Karanga mjini Moshi, Mganga amesema yeye ndio aliyemwachia kada huyo kutokana na mamlaka aliyonayo chini ya kifungu 91 cha CPA cha 2002.

DPP Mganga alitoa kauli hiyo wakati akitoa taarifa ya kuwafutia mashtaka watuhumiwa 72 ambao walikidhi sifa za kufutiwa mashtaka kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kubambikiwa makosa.

Mganga alimtaja mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuwa yeye na wenzake angeweza kuwashtaki kama Nusrat lakini aliamua kufuta mpango huo kutokana na uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.
The man is very hopeless like a small donkey. Amefafanua nini sasa hapo .
 
Sasa kama kumbe DPP anaweza Kuamua tu Kuwafutia Mashtaka walioko Gerezani mbona wapo Watanzania wengi waliosingiziwa na hawasamehi?
Mkuu Genta navutiwa sana na michango yako. Huwa huna unafiki kabisa, upande wowote ukikosea unakemea na ukifanya vizuri unasifia
 
ikiwa DPP anaweza kuwabanbika watuhumiwa makosa na kuwafungulia kesi za bandia, nchi hii sasa imefikia mahali pabaya sana. Ni Mungu tu anayejua tunakotoka na tunakoelekea.
 
Kimaadili, jambo linalofanya kitu kiwe sahihi nje ya mchakato sahihi wa kufikia jambo husika, ni nia njema ya jambo husika. Sina kipimo cha kujua nia njema iliyojificha katika uharaka wa kumuachia Mh. Hanje.

Endapo ilibidi atolewe usiku usiku ili kumpa fursa ya kuapa asubuhi, je ni nani aliyekuwa nyuma ya jambo ilo mwenye nguvu kiasi cha kumfahamisha DPP ahamue kutumia busara ya kumuachia kiongozi usiku usiku ili kumuwezesha kuwahi kiapo asubuhi ya siku iliyofuatia?
 
Mkuu Genta navutiwa sana na michango yako. Huwa huna unafiki kabisa, upande wowote ukikosea unakemea na ukifanya vizuri unasifia
Asante kwa Kuvutiwa nami hapa JF Mkuu. Na tabia yangu hii hii ya kuwa Muwazi na Mkweli imenifanya niwe Mchukiwaji na Mpigwa Majungu sana.
 
Back
Top Bottom