DPP aeleza sababu Nusrat Hanje kuachiwa huru

Mkurugenzi wa mashtaka nchini Tanzania (DPP), Biswalo Mganga leo Jumatano Desemba 2, 2020 ameeleza uamuzi wake wa kumfutia mashtaka kada wa CHADEMA, Nusrat Hanje ambaye Novemba 27, 2020 alivuliwa uanachama wa chama hicho pamoja na wenzake 18.

Nusrat ambaye alikuwa katibu wa baraza la vijana CHADEMA (BAVICHA) alikaa mahabusu siku 163 na siku moja baada ya kutoka mahabusu jina lake lilikuwa miongoni mwa majina 18 ya wanawake walioapishwa Novemba 24, 2020 mjini Dodoma kuwa wabunge wa viti maalum.

Mbali na CHADEMA kupinga kuapishwa kwa wanawake hao kwa madai kuwa majina yao hayakupitishwa na kamati kuu ya chama hicho na kwamba kilichofanyika ni usaliti, pia walihoji kitendo cha Nusrat kutoka mahabusu na moja kwa moja kuapishwa wakati alipaswa kujaza fomu Novemba 20, 2020 na alitoka mahabusu wakati muda wa kujaza fomu hiyo ukiwa umepita.

Akizungumza na wanahabari leo katika gereza kuu la Karanga mjini Moshi, Mganga amesema yeye ndio aliyemwachia kada huyo kutokana na mamlaka aliyonayo chini ya kifungu 91 cha CPA cha 2002.

DPP Mganga alitoa kauli hiyo wakati akitoa taarifa ya kuwafutia mashtaka watuhumiwa 72 ambao walikidhi sifa za kufutiwa mashtaka kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kubambikiwa makosa.

Mganga alimtaja mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuwa yeye na wenzake angeweza kuwashtaki kama Nusrat lakini aliamua kufuta mpango huo kutokana na uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.
Inawezekana DPP haja elewa hoja iliyopo.
Hoja kuu sio mamlaka yake kisheria, na wala si kwamba watu wamechukizwa na kitendo cha Nusrat kuachiwa huru.
Bali utaratibu ulio tumika kumtoa gerezani ndio hoja kuu, hasa ukizingatia kwamba taratibu za kimahakama na muda wa kazi.
Ninavyo jua ni kwamba DPP anamshtaki mtu mahakamani na mahakama inamsomea mashtaka yake kama yalivyo wasilishwa na DPP. Na ikitokea DPP amefuta mashtaka anawasilisha mahakamani na mahakama inamsomea msamaha huo kama ulivyo wasilishwa na kumuachia huru.
Ama DPP mamlaka yake yapo juu zaidi ya mahakama kwamba akikufutia mashtaka basi hakuna utaratibu mwingine wa kimahakama we unatimka zako tu?
Na hili la Mbowe na wenzake kutokuwashtaki kama alivyomshtaki Nusrat ina maana alimuonea? Au Nusrat uchaguzi mkuu haukumuhusu kama Mbowe na wenzake, ama makosa yao yalifutwa na uchaguzi mkuu?
 
Nusrat alitolewa mahabusu saa tatu na nusu usiku.Sheria za Tanzania haziruhusu kumtoa mahabusu mtuhumiwa katika muda huo.Huu ni muendelezo wa uvunjaji wa sheria katika serekali mfu ya Magufuli!
Sheria ipi? Hebu tutajie
 
hawa watu wako na akili timamu na wameelimika. Tatizo maelekezo yanawafanya waonekane wapuuzi.
 
Mkurugenzi wa mashtaka nchini Tanzania (DPP), Biswalo Mganga leo Jumatano Desemba 2, 2020 ameeleza uamuzi wake wa kumfutia mashtaka kada wa CHADEMA, Nusrat Hanje ambaye Novemba 27, 2020 alivuliwa uanachama wa chama hicho pamoja na wenzake 18.

Nusrat ambaye alikuwa katibu wa baraza la vijana CHADEMA (BAVICHA) alikaa mahabusu siku 163 na siku moja baada ya kutoka mahabusu jina lake lilikuwa miongoni mwa majina 18 ya wanawake walioapishwa Novemba 24, 2020 mjini Dodoma kuwa wabunge wa viti maalum.

Mbali na CHADEMA kupinga kuapishwa kwa wanawake hao kwa madai kuwa majina yao hayakupitishwa na kamati kuu ya chama hicho na kwamba kilichofanyika ni usaliti, pia walihoji kitendo cha Nusrat kutoka mahabusu na moja kwa moja kuapishwa wakati alipaswa kujaza fomu Novemba 20, 2020 na alitoka mahabusu wakati muda wa kujaza fomu hiyo ukiwa umepita.

Akizungumza na wanahabari leo katika gereza kuu la Karanga mjini Moshi, Mganga amesema yeye ndio aliyemwachia kada huyo kutokana na mamlaka aliyonayo chini ya kifungu 91 cha CPA cha 2002.

DPP Mganga alitoa kauli hiyo wakati akitoa taarifa ya kuwafutia mashtaka watuhumiwa 72 ambao walikidhi sifa za kufutiwa mashtaka kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kubambikiwa makosa.

Mganga alimtaja mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuwa yeye na wenzake angeweza kuwashtaki kama Nusrat lakini aliamua kufuta mpango huo kutokana na uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.
Ndiyo maana sisi wananchi tunawapenda sana EU na US na siyo hawa wakoloni weusi kina ngosha!
 
Freeman Mbowe kuachiwa huru, siyo tatizo, Nusrat Hanje ni tatizo! Hii ni ngumu kueleweka katika hali ya kawaida!
 
Yaani hii nchi imeoza kabisa, DPP anakiri kuna watu huwa wanabambikiwa kesi, sasa wanawachukulia hatua gani hao wanaowabambikia wengine kesi?
Tutakapo vuna mabua wote tunahusika iwe anayepiga vigelegele,anae cheka na hata yule aliyeamua kutojishughulisha.
 
Tungepata japo kamfano kamoja kamfungwa aliyewahi kutolewa usiku kwa mujibu wa sheria, ingekaa poa sana..
 
Ni jambo jema!

Kutoka mahabusu direct Bungeni hata Nelson Mandela alipumzika kidogo kabla hajatimba Ikulu.

Mungu mbariki Nusrat!
Bado wewe tu Kuteuliwa, sijui unagundu maanake propaganda zako umewashinda hadi wa China.
 
ALiyembambikia makosa mwenzie kafanywa nini? AU kumbambikia kosa mtu, SIYO KOSA?

Halafu sijaona sababu iliyotolewa na DPP inayomuhusu Nusrat..
 
Ni jambo jema!

Kutoka mahabusu direct Bungeni hata Nelson Mandela alipumzika kidogo kabla hajatimba Ikulu.

Mungu mbariki Nusrat!
Tatizo baadhi ya viongozi nchini "Chile" ni waongo wanadanganya watu wazima kama vile tuko enzi zile za miaka ya 70 wakati siku hizi watu wameshaelimika hata ukimdanganya anakukubalia kwa kukuheshimu ila rohoni anaujua ukweli[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nusrat alitolewa mahabusu saa tatu na nusu usiku.Sheria za Tanzania haziruhusu kumtoa mahabusu mtuhumiwa katika muda huo.Huu ni muendelezo wa uvunjaji wa sheria katika serekali mfu ya Magufuli!
Shida siyo DPP amewaachia wakina Nusrat, hilo jambo ni kweli lipo ndani ya uwezo wake.

Tatizo linakuja sheria inasema DPP akitoa hiyo ruhusa,lazima apeleke order yake mahakamani kwanza then mahakama/hakimu ndio anatoa order ya mhutumiwa kutolewa gerezani.

Sasa kwenye kesi ya Nusrat, DPP ametoa order na magereza wameifatisha moja kwa moja na kumtoa Nusrat kitu ambacho ni kinyume na sheria.

Kwa maana hiyo,kutoka kwa Nusrat gerezani bado kunaendelea kuwa na utata hata baada ya DPP kutolea ufafanuzi.
 
Huyu jamaa uwa ana kibri fulani ukimtazama. Any way Mungu ndiye muhukumu wa haki
Mbali na kibri, majivuno na roho mbaya ukimtazama vizuri machoni anapokuwa anaongea utagundua kwamba amejaa uovu. Anatumika vibaya sana.
 
Jamaa hana tofauti na yule wa dodoma ni mwendo wa kutii maagizo tu Ili minyoo isikose shibe
 
Back
Top Bottom