Si uliiona nyomi ya jana Mwanza?
Unafikiri hawana hakiri kabisa?
Sasa wametambua kuwa upepo unawaendea vibaya wanajaribu kujiosha.
Msimamo uleule kwa CHADEMA mpaka kieleweke.
auto-pilotNi mambo mengi JK kateleza ila hili nchi inajiendesha yenyewe...hatuna Rais
Hii yote, ni gia ya kuipigia upatu Dowans, ipate kazi nyingine ya kuzalisha umeme! Baadae mtasikia, mitambo yao inanunuliwa au imekodishwa na Tanesco ili kumaliza mgao! Ukweli ni kuwa, Dowans hawana pa kupeleka hiyo mitambo, wala hawana sehemu nyingine wanapofanya kazi au wanapoweza kupata kazi ya kufua na kulangua umeme, zaidi ya Tanzania. Huyu Makamba ni dalali tu!
Mjukuu wangu acha kukata tamaa mapema hata jioni haijafika weeMi sasa hivi sitaki kusikia ishu ya hela, ninachotaka ni umeme. Walipe, wasilipe, najua hakuna kitakachobadilika chini ya serikali ya mafisadi...
TRA wako wapi kwani?
Ahsante sana Gurudumu kwa kutuhadithia Hadithi nzuri na ya kupendezaBasi mwanangu ngoja nikusimulie hadith ili ulale eee,
Hapo zamani za kale ilikuwa hiviii;
Dowans inadai Tanesco fidia ya bilioni kadhaa kwa mujibu wa hukumu ya ICC......Hatuna namna ni lazima tulipe hilo deni....wanaharakati wapinga malipo ya Dowans..... CC ya ccm waagiza serikali isilipe Dowans kwanza isubiri uamuzi wa mahakama.....UVCCM wadai wamtukana PhD wa ukweli kuhusu umiliki wa Dowans.....Ngeleja: Kikwete siyo mmiliki wa Dowans.....Kikwete: Siwafahamu wamiliki wa Dowans (Lakini serikali yake inasema ni lazima walipwe)......Kafulilia apeleka hoja binafsi bungeni....Dowans wasajili tuzo yao mahakama kuu.....Wanaharakati wasajili pingamizi mahakama kuu kuhusu tuzo ya Dowans.....January amwandikia Ngeleja barua.....January achakachuliwa kuwa M/kiti wa Kamati ya nishati.......Ngeleja atoa kauli ya serikali Bungeni.....January asema mitambo ya Dowans iwashwe....Ali Hadaiwi aongea na wahariri wa habari bila kamera (na simu zao pia zilikuwa hazina kamera).....Ali Hadaiwi akagua mitambo......Ali hadaiwi atinga Ikulu.....Dowans yaisamehe Tanesco deni (lakini wanadai nyingi kuliko walizosamehe).....
oooo mtoto mzuri unasinzia ee, basi tutaendelea na hadithi kesho eee, lala salama ee.
usiwe na hofu mjukuu tutakupa taarifa ASAP baada ya intelijensia yetu kupata majibu kamiliHuyo munai ni wa wapi hapa Tanganyika??? Natamani tuanze kuwapiga mawe hawa wahusika wote, sababu mambo yao ya gizagiza tu. Anaishi wapi huyo?
By Kambarage:
Sikilizeni WADANGANYIKA wenzangu. January Makamba ni wakala wa mafisadi. Amepewa ubunge na Rostam Aziz na Edward Lowassa ili wamtoe William Shellukindo aliyetoa uamuzi kamati ya ubunge ichunguze Richmond. Pia wamemuweka kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge ya Nishati na Madini ili kufanikisha ufisadi wa Richmond/Dowans na uporaji mwingine mkubwa kwenye umeme na madini.
Ndiyo maana siku zote January anazungumzia Dowans eti kama mitambo hiyo ndiyo suluhisho pekee la tatizo la umeme Tanzania. Gridi ya taifa ina upungufu wa 230MW. Dowans inaweza kuzalisha maximum 100MW. Hivyo hata Dowans ikiwashwa, mgao wa umeme bado utaendelea.
Mpango uliopo ni kuwa eti Dowans wajidai wamesamehe kulipwa tozo ya 100bn/- ya ICC halafu wawashe umeme na kuwauzia Tanesco. Lengo ni kusaini mkataba wa miezi 3 na Tanesco wa kununua umeme.
Baada ya kuisha kwa mkataba huu wa miezi 3, kamati hiyo hiyo ya January itaiagiza Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini inunue mitambo ya Dowans ili kukidhi tatizo la nishati.
Hivyo basi, ule mpango wa kifisadi wa siku nyingi wa kununua mitambo ya DOWANS utarudi kwa mlango wa nyuma na kuungwa mkono na wenyeviti kadhaa wa kamati za Bunge wakiongozwa na January Makamba, Zitto Kabwe, John Cheyo, Augustine Mrema, nk.
Kweli sisi Wadanganyika tutaendelea kuliwa mpaka kiama chini ya utawala wa CCM na mawakala wao kwenye kambi ya upinzani.
Kwani tuliwaomba watusamehe; tumewaambia hatuwalipi na majenereta yao hatununui wakitaka wakayauze Oman huko. Kwani wanogopa nini wakati kuna kesi zimefunguliwa mahakamani kupinga hiyo tuzo? Wanaogopa kushindwa kwenye mahakama zetu?
Kwa taarifa ya Radio Tumaini, leo asubuhi saa 3, Dowans wamekubali kusamehe shirika la TANESCO deni la Bil 94. Hii naona ni habari njema. Kitu ninachojiuliza ni sababu ipi iliyopelekea hatua hiyo kutoka kampuni ya DOWANS kufikia uamuzi huo kwa sasa.