DOWANS waisamehe TANESCO deni lote!

DOWANS waisamehe TANESCO deni lote!

Huyo munai ni wa wapi hapa Tanganyika??? Natamani tuanze kuwapiga mawe hawa wahusika wote, sababu mambo yao ya gizagiza tu. Anaishi wapi huyo?
 
Dowans sasa yalainika, wafuta deni kwa Tanesco

Na Richard Makore

25th February 2011

headline_bullet.jpg
Sasa wataka walipwe tu Sh. bilioni 36



Januari(4).jpg

January Makamba

Kampuni ya Dowans Tanzania Limited ya kufua umeme wa dharura ambayo ilishinda kesi dhidi ya Tanesco katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na kupewa tuzo ya Sh. bilioni 94, sasa imelainika na imetangaza kusamehe deni hilo.
Uamuzi huu ambao unatangazwa baada ya kuwapo kwa malumbano makali nchini juu ya hukumu ya ICC na kiasi cha fedha kilichotolewa, sasa Dowans wanataka Tanesco ilipe tu Dola za Marekani milioni 24 (Sh. bilioni 36 tu). Fedha hizo ni gharama halisi ya umeme uliouzwa kwa Tanesco.

....................................Hata hivyo Dowans imesema licha ya kutoa msamaha huo, Tanesco bado imeshindwa kujibu kama imeukubali msamaha huo au la ili mazungumzo yaanze.

Munai alidai fedha wanazolidai shirika hilo kwa sasa zinakaribia Sh. bilioni 99 badala ya Sh. bilioni 94 za mwaka jana.
Alisema ongezeko hilo limetokana na kampuni ya Dowans kuitoza Tanesco kila siku Dola za Marekani 11, 800 (Sh. milioni 15.3) kama gharama za kuweka mtambo hata kama hauzalishi umeme na kwamba nyongeza ya gharama hizo ilianza kutozwa kila siku tangu Juni 15, mwaka 2010 hadi sasa.

Alisema deni la Sh. bilioni 94 liliishia Juni 14, mwaka 2010 na baada ya hapo limekuwa likiongezeka siku hadi siku. Munai aliwaambia waandishi wa habari walioambatana na kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuwa kampuni yake haina tatizo kuhusu kusamehe deni hilo, lakini Tanesco muda wote imekuwa haitaki kukubali msamaha huo.
Aliongeza kuwa ikiwa Tanesco na Serikali watakataa kupokea msamaha huo nje ya mahakama na wao wataacha sheria iendelee kuchukua mkondo wake.

Munai alisema mkataba kati ya Dowans na Tanesco unasema kuwa ikiwa pande hizo mbili zitatofautiana na zikaenda kwa msuluhishi maamuzi yatakayotolewa yatatakiwa kuheshimiwa na pande zote na hakuna upande utakaoruhusiwa kukata rufaa.
“Kwa mujibu wa mkataba huu, Tanesco haiwezi kukata rufaa kwa kuwa kipengele hicho kinawazuia na wao wanajua, lakini hajui ni kwanini hawataki kuwaambia wananchi ukweli,” alisema.
CHANZO: NIPASHE
Tanesco wakikubali huo msamaha watakuwa wamekubali kushindwa katika kesi na pingamizi walilolitoa litakuwa halina maana. Anayekubali msamaha ni yule aliyekili kosa. Hawa mafisadi ni wajanja sana wakati kesi iko mahakama kuu wanajifanya eti kutoa msamaha! kwa nini wasisubiri kesi iishe?

Halafu mnaona mafisadi yanavyojua kujilinda, hapo kwenye bold blue, eti kwenye mkataba waliweka kipengere cha kutokukata rufaa!! Halafu mwakilishi wa serikali anasaini tu kijingajinga, PUMBAVU KABISA. RA alijua kuwa kukitokea kupelekana mahakamani atawafix kwa kuwanunua hao ICC baada ya hapo hakuna kukata rufaa.
 
Thank you mr. Mis-cote. Siyo lote. Na siyo Dowani ila JK maji shingoni. People's power.
 
Basi mwanangu ngoja nikusimulie hadith ili ulale eee,

Hapo zamani za kale ilikuwa hiviii;

Dowans inadai Tanesco fidia ya bilioni kadhaa kwa mujibu wa hukumu ya ICC......Hatuna namna ni lazima tulipe hilo deni....wanaharakati wapinga malipo ya Dowans..... CC ya ccm waagiza serikali isilipe Dowans kwanza isubiri uamuzi wa mahakama.....UVCCM wadai wamtukana PhD wa ukweli kuhusu umiliki wa Dowans.....Ngeleja: Kikwete siyo mmiliki wa Dowans.....Kikwete: Siwafahamu wamiliki wa Dowans (Lakini serikali yake inasema ni lazima walipwe)......Kafulilia apeleka hoja binafsi bungeni....Dowans wasajili tuzo yao mahakama kuu.....Wanaharakati wasajili pingamizi mahakama kuu kuhusu tuzo ya Dowans.....January amwandikia Ngeleja barua.....January achakachuliwa kuwa M/kiti wa Kamati ya nishati.......Ngeleja atoa kauli ya serikali Bungeni.....January asema mitambo ya Dowans iwashwe....Ali Hadaiwi aongea na wahariri wa habari bila kamera (na simu zao pia zilikuwa hazina kamera).....Ali Hadaiwi akagua mitambo......Ali hadaiwi atinga Ikulu.....Dowans yaisamehe Tanesco deni (lakini wanadai nyingi kuliko walizosamehe).....

oooo mtoto mzuri unasinzia ee, basi tutaendelea na hadithi kesho eee, lala salama ee.
 
I MUST BE DREAMING!!

Eti wakuu..
Huyu Munai ni kama nani pale Dowans? na alikuwa wapi siku zote hizo...
 
waliopo hawawezi hata kutaifisha hii mitambo yaani ni wapuuzi wa kufa mtu
 
I MUST BE DREAMING!!

Eti wakuu..
Huyu Munai ni kama nani pale Dowans? na alikuwa wapi siku zote hizo...


Stanley Munai ni Mkurugenzi wa fedha pale dowans
ila ngereja anamjua kama mmiliki wa dowans........
 
Basi mwanangu ngoja nikusimulie hadith ili ulale eee,

Hapo zamani za kale ilikuwa hiviii;

Dowans inadai Tanesco fidia ya bilioni kadhaa kwa mujibu wa hukumu ya ICC......Hatuna namna ni lazima tulipe hilo deni....wanaharakati wapinga malipo ya Dowans..... CC ya ccm waagiza serikali isilipe Dowans kwanza isubiri uamuzi wa mahakama.....UVCCM wadai wamtukana PhD wa ukweli kuhusu umiliki wa Dowans.....Ngeleja: Kikwete siyo mmiliki wa Dowans.....Kikwete: Siwafahamu wamiliki wa Dowans (Lakini serikali yake inasema ni lazima walipwe)......Kafulilia apeleka hoja binafsi bungeni....Dowans wasajili tuzo yao mahakama kuu.....Wanaharakati wasajili pingamizi mahakama kuu kuhusu tuzo ya Dowans.....January amwandikia Ngeleja barua.....January achakachuliwa kuwa M/kiti wa Kamati ya nishati.......Ngeleja atoa kauli ya serikali Bungeni.....January asema mitambo ya Dowans iwashwe....Ali Hadaiwi aongea na wahariri wa habari bila kamera (na simu zao pia zilikuwa hazina kamera).....Ali Hadaiwi akagua mitambo......Ali hadaiwi atinga Ikulu.....Dowans yaisamehe Tanesco deni (lakini wanadai nyingi kuliko walizosamehe).....

oooo mtoto mzuri unasinzia ee, basi tutaendelea na hadithi kesho eee, lala salama ee.

Jamani yanahitajika mabadiliko ya mapema mno kuliko tunavyodhani, unless otherwise tutaendelea kusikiliza hizo hadithi kila kukicha..
 
Ukiachilia ushabiki wa kisiasa, kila mtu anasahau kuwa kuna tembo sebuleni (elephant in the room) a.k.a. mgao na tatizo kubwa la umeme in general nchi nzima wakati huohuo kuna mitambo ingesaidia kupunguza hili tatizo.

Seriously it is about time, serikali iharakishe namna zote za uzalishaji umeme hapa nchini ikiwa ni pamoja na mitambo hii ambayo tayari iko hapa. tanesco na dowans wawe fare na wazi kwenye mikataba yao na wawe wawazi kwa umma tuache porojo na siasa mashine ziwashwe na walete nyingine ikiwezekana. Maana hii mitambo inatumia gesi ya hapahapa.

Kuna watu wanatoa mada ya kutaifishwa hii mitambo, naipinga hoja hii sababu ikitaifishwa na kupewa tanesco mbali ya gharama ya kutaifisha na athari zake kwa sera nzima ya uwekezaji nchini, tanesco ni shirika lililochoka na kujaa urasimu na siasa halina uwezo wowote wa kuendesha hizo mashine.

Wakati umefika mitambo iwashwe tupate umeme ili viwanda vyetu vipata angalau mwanya wa kukua na kuongeza ajira na kupunguza makali ya maisha kwa watanzania.

Mwisho wa siasa muda wa vitendo ni sasa!
 
Mi sasa hivi sitaki kusikia ishu ya hela, ninachotaka ni umeme. Walipe, wasilipe, najua hakuna kitakachobadilika chini ya serikali ya mafisadi...
 
Kwa taharifa ambazo mimi ninazo ni kwamba Dowans wapo tayari kuisamehe Tanesco lakini kwa masharti maalumu.
Bado hawajawasamehee ila wapo tayari endapo watakaa na kuzungumza na Tanesco wanatakiwa wayakubali hayo masharti ya kifisadi.

What the Hell? Who is Dowans? Ninapata Kichefu chefu hakika kwa jinsi ambavyo kila siku tunampa ujiko huyu mdudu Dowans. tumemfanya Dowans kujiona kuwa yeye ni big deal, kila kukicha DOWANS DOWANS nani weewee? Natamani Marehemu Sokoine afufuke sasa hivi, hakika neno Dowans ingekuwa ndo Mwisho na kulala giza kungeisha na angemaliza kazi mara moja.
Ee Mungu nakuomba weka ile roho ya Marehemu Sokoine Ndg Yetu Pinda awe na ujasiri na asilie tena hovyo, awe na uamuzi imara na atoe amri ya kukamatwa mara moja kwa mitambo ya DOWANS NA IWASHWE MARA MOJA ili huu wimbo wa DOWNS UISHE UANZE MWINGINE, Katika Jina Yesu, wote tuseme Amina!
 
Hii yote, ni gia ya kuipigia upatu Dowans, ipate kazi nyingine ya kuzalisha umeme! Baadae mtasikia, mitambo yao inanunuliwa au imekodishwa na Tanesco ili kumaliza mgao! Ukweli ni kuwa, Dowans hawana pa kupeleka hiyo mitambo, wala hawana sehemu nyingine wanapofanya kazi au wanapoweza kupata kazi ya kufua na kulangua umeme, zaidi ya Tanzania. Huyu Makamba ni dalali tu!
 
Si uliiona nyomi ya jana Mwanza?
Unafikiri hawana hakiri kabisa?
Sasa wametambua kuwa upepo unawaendea vibaya wanajaribu kujiosha.
Msimamo uleule kwa CHADEMA mpaka kieleweke.
 
VITUKO VYA MACK NA ZEMBWELA HIVI,HOW IS IT POSSIBLE AND WHY?
I there something behind that is not honest?
 
kweli nakubaliana na wewe maana haya mengi yametokea rais akiwa yuko safarini
tangu kikwete alipotoka tu jamaa wa Dowans akaingia..mmh au walikuwa wameshaweka dili ili ajifanye JK hakujua chochote?
kweli tuko kwenye autopilot . hana uwezo wa kutawala na hukuna tofauti yoyote ya rais akiwepo au akiwa hayupo. kweli watanzania tunastahili pongezi tunaweza kujiongoza wenyewe[/QUOTE]
 
sasa warudishe madeni ayo benki kisha wachukue mitambo yao wasepe, yaani wachape lapa kabla nguvu ya uma haijawageukia.

hatuitaki hiyo mitambo ya utata waondoke nayo maana neno DOWANS NI KICHEFUCHEFU TU LINATAKA KUFANANA NA DAWASCO!
 
By Kambarage:

Sikilizeni WADANGANYIKA wenzangu. January Makamba ni wakala wa mafisadi. Amepewa ubunge na Rostam Aziz na Edward Lowassa ili wamtoe William Shellukindo aliyetoa uamuzi kamati ya ubunge ichunguze Richmond. Pia wamemuweka kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge ya Nishati na Madini ili kufanikisha ufisadi wa Richmond/Dowans na uporaji mwingine mkubwa kwenye umeme na madini.

Ndiyo maana siku zote January anazungumzia Dowans eti kama mitambo hiyo ndiyo suluhisho pekee la tatizo la umeme Tanzania. Gridi ya taifa ina upungufu wa 230MW. Dowans inaweza kuzalisha maximum 100MW. Hivyo hata Dowans ikiwashwa, mgao wa umeme bado utaendelea.

Mpango uliopo ni kuwa eti Dowans wajidai wamesamehe kulipwa tozo ya 100bn/- ya ICC halafu wawashe umeme na kuwauzia Tanesco. Lengo ni kusaini mkataba wa miezi 3 na Tanesco wa kununua umeme.

Baada ya kuisha kwa mkataba huu wa miezi 3, kamati hiyo hiyo ya January itaiagiza Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini inunue mitambo ya Dowans ili kukidhi tatizo la nishati.

Hivyo basi, ule mpango wa kifisadi wa siku nyingi wa kununua mitambo ya DOWANS utarudi kwa mlango wa nyuma na kuungwa mkono na wenyeviti kadhaa wa kamati za Bunge wakiongozwa na January Makamba, Zitto Kabwe, John Cheyo, Augustine Mrema, nk.

Kweli sisi Wadanganyika tutaendelea kuliwa mpaka kiama chini ya utawala wa CCM na mawakala wao kwenye kambi ya upinzani.
 
Back
Top Bottom