DOWANS waisamehe TANESCO deni lote!

kuna habari zimeenea huku mitaani kwetu kwamba nchi hii inajiongoza yenyewe , Rais hana uwezo wa kutawala na hukuna tofauti yoyote ya rais akiwepo au akiwa hayupo. kweli watanzania tunastahili pongezi tunaweza kujiongoza wenyewe

Huo ndio ukweli kwa sasa hakuna Raisi
 
Capacity charges to be paid by tanesco dowans wakifanya biashara ni chamtoto kwa hiyo 94bn!!!

Sio wajinga dowans hao!!!

Nakubaliana nawe kuwa hao Dowans sio wajinga na kuachia (94b) hivi hivi. Watakachofanya ni kuwa kama service charge halali ni 152m kwa siku basi watafanya 250m (152 halali +100m kufidia lile deni ealiloonyesha mbele ya umma kuwa wamesamehe). dawa ni kutaifisha mitambo kwa kuliingiza taifa kwenye hasara za kuingia mkataba na kampuni feki - Richmond. (Mitambo hii ilikuwa ya Richmond kampuni feki.
 
Nakumbuka wakati Mkapa anamaliza muda wake wananchi walimuomba abadili katiba agombee tena, kwa hekima zake alikataa.
JK usipokuwa makini na kukemea uchafu huu wa kifisadi ipo siku utasikia wananchi wako wamechoka uongozi wako na kukutaka uachie madaraka kama hulindi kodi ya Watanzania.
Hawa jamaa wanajiamulia tu kama vile nchi haina Rais.
Hivi JK huyaoni haya au ndo kusema uko busy na safari za nje!!????
JK timiza wajibu wako kama vile wananchi walivyokupa imani yao kuwaongoza,
Tetea Rasilimali na Kodi ya Watanzania, sio kuchukuliwa kiholela kama hivi tunavyoshuhudia,

JK Ogopa kuliliwa na Watanzania kwa kutolinda rasilimali yao.
 
Hapo kimefanya kizungu mkuti...hawajasamehe deni bali wamebadilika rangi kama kinyonga sasa watakachofanya ni kuongeza gharama katika huduma....tusije kuanza kushangilia tutalia ......vizuri ni kutaifisha mitambo na kukamata mafisadi wote.
 
Na kwanini Radio Tumaini iwe ndio source ya hiyo habari kubwa hivi, wakati tunajua hiyo redio inaishia Magomeni, na sisi wa huku SWEKA hatuijui!

JK anangoja ROSTAM amwelekeze cha kusema...Otherwise asingekaa kimya wakati nchi ipo kwenye hali ya hatari hivi!

pliz pliz pliz
 
Ilipaswa sasa hivi tuwe tunazungumzia tanessco kuisamehe dowans kwa kuizalilisha na si dowans kuisamehe tanesco...
 
Na warudishe mihela yetu waliyokuwa wanaichota TANESCO kila siku kitapeli kupitia mikataba yao hewa, wasijitoe ufahamu

Wakati walikuwa wanawasha umeme na ww unawasha ac na kulala na mkeo mbona hukuwa unasema ? wa tz acheni kupenda bure vitawafikisha pabaya sana
 
"Munai alisema ikiwa serikali itahitaji kuuziwa mitambo hiyo kampuni hiyo haitakuwa na pingamizi iwapo itakataa itauza mitambo hiyo kwa watu wengine wanaohitaji. Alisema hadi sasa fedha inayohitajika kulipwa kwa kampuni hiyo si bilioni 94 kama wengine wanavyofikiri bali kiwango hicho kilianza kupanda tangu Juni 15 mwaka jana..." source...kutoka katika mjadala wa kamati ya bunge...

Hapo palipokuwa "bolded" ndio penye "catch"! - kwa haraka haraka unaweza furahia kusamehewa, lakini kuna makubwa zaidi ya hiyo bil94! ama kweli kazi tunayo Watanzania!
 
tatizo la nchi hii unaweza kukuta jamaa kashakunja mshiko wake sisi huku na uduwanzi wetu tupo tupo tu tunanadanganywa kasemehe deni,

najua kuna watu wa hazina humu tujulisheni habari za ukweli jamani
 
Eti umesema kusamehe ....??? My foot!! Hebu Dr Mwakyemba sasa kafungueni kesi uzuri dhidi ya hawa matapeli na kutaifishwe kabisa huo mtumba wao hapo Ubungo.

Cha zaidi WE NEED A CLEAN BREAK na mienendo yote ya kitapeli kama hii hivyo rekebisheni sheria na taratibu ziwe ngumu zaidi ili tusije tukawakuta tena mawaziri kama Karamagi wakizunguka ovyo tu na mihuri yetu mifukoni mwake jinsi tu apendavyo na hata kusafiri nayo kwenda kusaini mikataba kisiri majumbani kwa watu Ulaya.

Waziri wetu wa Nishati na Madini, Mhe John Mnyika, hakikisha kwamba mikataba yote ya wizara hiyo inatangazwa upya na watoa huduma wapya wapatikane kwa njia ya ushindani, shirikishi na yenye uwazi zaidi. Hatutaki tena biashara na Dowans wala mjomba wake - wawe on your BLACK LIST kabisa.

Hebu tuwekeeni barua hiyo yenye ushahidi wa Lowassa na Rostam Aziz kujiamulia walivyoamua. Hatutaki surprises zaidi tena katika eneo hili wala kuhujumu mitambo ili wahindi wakauze mijenereta Kariakoo na vyama fulani kupitia vitenesi vyao huko jioni.
 
Na kwanini Radio Tumaini iwe ndio source ya hiyo habari kubwa hivi, wakati tunajua hiyo redio inaishia Magomeni, na sisi wa huku SWEKA hatuijui!

JK anangoja ROSTAM amwelekeze cha kusema...Otherwise asingekaa kimya wakati nchi ipo kwenye hali ya hatari hivi!
Nadhani walikuwa wanasoma yaliyoandikwa kwenye magazeti ya leo. Liko gazeti limeandika hivyo; nilikuwa nasikiliza kipindi cha watanzania tuongee magazeti cha RFA lakini kwa bahati mbaya sikupata jina la gazeti
 
Back
Top Bottom