Ndugu Zangu,
Leo wakati nikitafakari deni letu kwa Dowans nimemkumbuka Mwalimu. Angekuwepo Mwalimu Nyerere hakika asingetafuna maneno katika hili la Dowans. Angesema neno moja tu; HATULIPI! kama vile kwenye tamthiliya ya M-Italia Dario Fo, mshindi wa tuzo ya Nobeli mwaka 1997 kwenye fasihi.
Hili la Dowans ni itikadi. Waafrika Wajamaa tusikubali mabepari hawa wafikie hatua ya kutunyanyasa hivi. Najiuliza; hivi ni kwa nini Serikali yetu inashindwa kesi nyingi za madai? Hivi hatuna wanasheria wa kupambana kuilinda nchi yetu na ufisadi huu?
Ndugu zangu,
Shilingi bilioni 94 ni nyingi. Hivi tunazitoa hivi hivi huku tunakenua meno. Tuseme tu HATULIPI. Kwani watatufanya nini? Si ina maana ya kesi kuendelea. Tujenge hoja mpya. Walau tuonyeshe tunapambana. Na tukishindwa raundi ya pili, basi, tuhakikishe "Tunakula sahani moja' na waliotuingiza kwenye deni hili. Maana tumefahamishwa majina ya wamiliki wa Dowans lakini bado hatuwajui wamiliki. Maana, kufahamishwa mtu ni kitu kimoja, lakini kumjua mtu ni kitu kingine.
Tusidanganyane, mtu hawezi kutoka Singapore akatua Dar akaenda mpaka CRDB bila ya kuonyeshwa njia na mwenyeji. Tuonyeshwe sasa hao Watanzania wenzetu waliowaonyesha wamiliki wa Dowans njia ya kwenda CRDB!
Ndugu Zangu,
Hata kama tunalazimishwa kulipa, basi, hata kupiga kelele tunashindwa. Tupige kelele; Hatulipi! Non Si Paga!
Na hilo ni Neno La Leo
Maggid
'Kwenye mgao wa umeme'
Iringa.
mjengwa