Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,175
- 43,936
Mimi nafikiri kutokana na mazingira ya ununuzi wa awali wa mitambo hiyo michakavu kutoka kwenye kampuni feki ya Richmond...Kusapoti ununuzi wa mitambo hiyo bila vigezo vitakavyojitosheleza mbele za wananchi kunaweza kupelekea mitizamo kwamba there is some sort of ufisadi....Honestly hata kama ni uamuzi wake wa kisiasa..Kuwapa hao watu mipesa yote hiyo na wakti kuna maswali yanaoyotakiwa kujibiwa ni swala linalohitaji maelezo ya kina.
Naona umezungumzia sana kuhusu "kutofautiana naye kimaelezo" Kumbuka ni tofauti za maamuzi na utekelezaji na si tu "maelezo" Malezo aliyoyatoa bado hayawezi kuhalalisha ununuzi wa mitambo hiyo na hivyo basi atueleze nia yake haswa ilikuwa ni nini na si tu kusema haogopi kuitwa fisadi ama kuonekana ana mtizamo wa tofauti.
Na pia unaposema mmetofautiana kisiasa una maana gani? Yani Zitto a lobby kumsadia Rostam na Lowassa na Karamagi halafu useme ni utofauti wa kisiasa tu, well kama wewe ni CHADEMA kama Zitto then utofauti wenu wa kisiasa unahitaji maelezo zaidi.
Ukishindwa kuwaelesha wana JF utaweza vipi kuwaelewesha wananchi kama si kuwadanganya na wizi mtupu?
Zitto ana uamuzi gani katika suala la ununuzi wa majenereta? akiamua yanunuliwe yatanunuliwa? na akiamua yasinunuliwe je?
Akitaka kujitetea kuwa hana uamzi,basi inabidi awaombe wanakamati wake radhi kwa kuongea kama vile anawawakilisha. Pia kama yeye ni mwenyekiti halafu anatowa maelezo yanayopingana na msimamo wa kamati yake then ndio maana watu wanahoji kwanini.
MKJJ umesema ana uamuzi gani na wakati huo huo ulisema huo ni uamuzi wake wa kisiasa...Sasa si ina maana alikuwa na nia ya kuwasaidia watu flani flani kisasa? Vipi kuhusu kifedha?
Naona unazidi kuleta siasa kwasababu toka huo msimamo uwe wake na si wa kamati basi tunataka kupuuzia na kuleta taswira ya kwamba kwasababu alichokizumgumzia hakina uzito kwenye maamuzi...Sasa vikao na kina Dk Rashid vilikuwa vya nini?
Kama ushauri wake usingehojiwa si ungefuatwa? Na kama ulikuwa ni uamuzi wake binafsi ambao ana uhakika kuwa hauta affect uamuzi wa ununuzi then kwanini aliutoa? Nani alimuuliza?
Tukiangalia vizuri, the guy has to offer some sort of akcnowledging that there is screwing up.
Zitto hawezi omba msamaha, hilo litamwaribia zaidi..Ni matamanio ya walio wengi kwa nia tofauti kuona Mh Zitto anaomba msamaha...
yanayotokea nchi hii yanasikitisha sana. Hivi kweli nchii tumeshidwa kuwa na mipango ya muda mrefu ya kupata umeme wa kutosha. Upungufu wa umeme unaotokana na kukosekana kwa mvua umekuwa ukitokea karibu kila baada ya miaka miwili. Tumeshidwa namna ya kuliondoa taifa katika tatizo hili?. Ebu tujifunze wenzetu wamewezaje pata umeme wa kudumu. Kama kukopa tufanye hivyo tuondokane na tatizo hilo. Inawezekana suala la kutafuta umeme wa dharula imekuwa miradi ya wanasiasa na chama tawala!!!. Naomba JF members tuendelea Kupiga kelele sana juu ya ufisadi uliokidhiri ndani ya serikali hii. Ama sivyo nchi hii hakuna future.
Tanzania ni nchi yenye umakini sana katika suala la kuwa na mipango ya muda mrefu.
omarilyas
Hana sababu kama haamini hajakosea. Kama atatambua alikosea na dhamira yake itamuonesha hivyo basi atajua cha kufanya lakini asiombe radhi kwa sababu ya kuturidhisha mimi na wewe au kuwa politically correct.
Omarilyas, hapa sikubaliani na wewe. Nitakupa mfano mmoja tu pamoja na kuwa kuna mifano mingi sana. Viongozi wetu hupiga kelele kila kukicha kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu, lakini vitendo vyao siku zote haviendani na kauli hiyo. Katika bajeti ya nchi ya kila mwaka Wizara ya kilimo hupata asilimia ndogo sana ambayo haiendani na kauli hiyo kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu. Na matokeo yake kilimo chetu kimekiwa ni kile kile cha kutumia jembe la mkono miaka nenda miaka rudi.
Kama Obama Rais wa Taifa kubwa anaweza kukubali makosa basi Zitto naye anaweza kukubali makosa..[/B]
Wapi nimesema msimamo wake ni sawa na wa kamati yake? Kuna yule mwanamama aliyekuwa nje ya nchi ambaye na yeye alisema ameshtushwa na uamuzi wa Zitto na akasema wazi kuwa si msiamo wa kamati,na Mwakyembe alishampigia Zitto kelele kuwa anaingilia kazi ambazo si zake..Kwa hiyo mlipoamua kuitoa kamati yake na kudai ni uamuzi wake binafsi then tubaki hapo..Kwenye mjadala kuhusu uamuzi wake "binafsi wa kisiasa" Ama "maelezo" kama unavyotaka tuelewe.Umeuona msimamo wa Kamati yake?
Unasoma mengi kuliko kilichosemwa.
Msimamo wa kamati siujui ila ni tofauti na msimamo wa Zitto.Unaujua msimamo wa kamati hasa ni nini?
Hana sababu kama haamini hajakosea. Kama atatambua alikosea na dhamira yake itamuonesha hivyo basi atajua cha kufanya lakini asiombe radhi kwa sababu ya kuturidhisha mimi na wewe au kuwa politically correct.
My point ni kuwa Zitto haitaji kutoa maelezo zaidi ya aliyoyatoa. Wote tunajua alichosema. Wapo ambao hawakubaliani naye na wapo wanaokubaliana naye.
Hana sababu kama haamini hajakosea. Kama atatambua alikosea na dhamira yake itamuonesha hivyo basi atajua cha kufanya lakini asiombe radhi kwa sababu ya kuturidhisha mimi na wewe au kuwa politically correct.
Kaka hiyo haina maana kuwa hatuna mipango ya muda mrefu. Ipo tena mingi tu. Hata katika sekta ya KILIMO kaka. Ukitoa mipango mingi ya miaka ya nyuma hivi sasa kuna Mpango wa ASDP (Agriculture Sector Development Programe) ambao ulipaswa kupatiwa shilingi trilioni moja kila mwaka kwa miaka saba.
Zitto anaweza kuamini hajakosea, lakini umma wa Watanzania haukubaliani na aliyoyasema kwa maana nyingine Watanzania wengi tunamuona kakosea. Wakati mwingine ni bora ukubali kwamba umeteleza na kauli uliyoitoa ilikuwa na kasoro. Kama Obama Rais wa Taifa kubwa anaweza kukubali makosa basi Zitto naye anaweza kukubali makosa.
Binadamu hatuko perfect na unapojikwaa ni bora kukubali badala ya kung'ang'ania kwamba sikujikwaa. Credibility na Reputation ya Zitto imeingia dosari kubwa sana kama ataendelea kung'ang'ania kwamba hakukosea basi atakuwa na wakati mgumu sana siyo tu kwenye nyanja za siasa bali nyanja zozote atakazotaka kushiriki baadaye.
Kaka hiyo haina maana kuwa hatuna mipango ya muda mrefu. Ipo tena mingi tu. Hata katika sekta ya KILIMO kaka. Ukitoa mipango mingi ya miaka ya nyuma hivi sasa kuna Mpango wa ASDP (Agriculture Sector Development Programe) ambao ulipaswa kupatiwa shilingi trilioni moja kila mwaka kwa miaka saba. Kaka ukipitia kwa umakini mpango huu wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo huo utashangaa sana inakuwaje tunaanza kuja na mipango ya bandikabandua kama ule wa mbolea na fedha za EPA na kuacha kuuwezesha mpango huu ili ufanikiwe.
Tatizo kubwa katika mpango huu ni kuwa haukushirikisha wadau wengi katika kuuandaa, umekosa uhalali kwa upande wa walengwa halisi, unategemea msaada wa nje kuweza kuugharamia na zaidi wanasiasa wengi hawaujui kwa undani na hivyo kuuona hauna maslahi yao kisiasa haswa katika kutimiza malengo yao ya muda mfupi.
Fuatailia mpango huo pamoja na mabadiliko ya kisera yanayoendelea uone ni jinsi gani watanzania tunavyopenda kuja na mipango ya muda mrefu lakini hatuko tayari kukomaa nayo kutokana na mapungufu yetu kimfumo na kibinfsi.
omarilyas
Mzee Mwanakijiji,
Sawa mkuu nimekusoma lakini katika kujifunza kwako ongeza hayo majibu yangu...utaepuka mengi sana kwa sababu hata siku moja Adui yako hakutakii mema na kamwe hawezi kukusaidia isipokuwa kwa faida yake..
Nikirudi ktk issue ya Mh. Zitto nadhani anahitaji kutoa samahani hasa hapa JF kwani wapo tuliomsamehe lakini wapo ambao bado wanatia shaka sana maelezo yake humu ndani.
Mkuu mimi sina shaka kabisa na Zitto huko nje isipokuwa anapokuja hapa kijiweni na taarifa kama ile ndugu yangu ilikuwa shock!..Na hasa aliposisitiza ndio msimamo wake na kuponda watu tunaoishi nje kwamba hatulijui joto la jiwe!..
Kifupi tumalize kama alivyosema Ogah, walioelewa wameisha elewa na kama Zitto ni mtu wa kujirudi atafahamu alichemsha nje ya hapo hatuwezi kumpinda tena..
Hii issue inanikumbusha sana madai ya CCM kuhusiana na sakata la EPA.. Fedha za EPA hazikuibiwa ila zilitoka kisheria kwa mashirka feki kama Kagoda yaliyoundwa kwa minajiri ya fedha hizo. Fedha hizo zikapewa uhalali kwa sababu ya dharura, na nia ya chama CCM kushinda uchaguzi 2005....Hivyo vibali vikatolewa.... Wakachota na kuzitumia...sasa wananchi wanapolalamikia mpango mzima, chama kinatuambia kuna baadhi ya watu (kina Rostam/Lowassa ndio wabaya lakini sio chama kizima, wakati ubaya wa hawa watu unatokana na fedha zilizochukuliwa Benki kuu nje ya sheria kwa ajili ya kampeni za uchaguzi, watu wakavuta zaidi ya kiwango kilichokusudiwa...
Kisheria kila aliyezipokea fedha zile ni mshirika wa wizi huo ikiwa ni pamoja na Wabunge waliotumia fedha hizo kwa Takrima ya uchaguzi wa mwaka 2005 lakini wajanja wakahalalisha takrima (pindisha sheria)..
Well, one can argue umuhimu wa kushinda CCM uchaguzi na vigumu sana kwa mwanaCCM kuona uharamu wake ikwa takrima sio haramu kikatiba.. kwa madai kwamba wakosefu ni kina Rostam walioiba zaidi na tujifunze kutenganisha Rostam, Kagoda, EPA na Uchaguzi..