Nimebahatika kuzungumza na wajumbe wengi wa kamati ya Zitto, nimebahatika pia kuzungumza na wajumbe wengi wa kamati ya kina Mwakyembe, nimebahatika pia kuzungumza na watu wa ofisi ya Bunge, nimebahatika pia kusoma nyaraka za kamati ya Zitto na ile ya Mwakyembe, nimebahatika pia kusoma nyaraka za Waziri Ngeleja na mawasiliano yake na....... (nitaweka wazi siku mwafaka)... Nimebahatika pia kupata nyaraka zote muhimu na ambazo nadhani zitaanikwa JF soon.
Kwa maelezo hayo hapo juu, hakuna ambaye haiungi mkono Tanesco (si Dk. Rashidi) kupata mitambo mipya, hiyo iko katika mipango yao ya muda mrefu na mfupi. Hata wewe utapenda Tanesco wapate mitambo. Zitto anakosea kutosema asichosema na hivyo kutoa nafasi ya kuwachanganya watu, na kuna mahali alisema anafanya makusudi. Sijui anateka kutuambia nini. Pengine huu mjadala umesaidia sana kuwabana Tanesco mpaka wamekwama. Zitto amefanikiwa lakini amekuwa KAFARA wetu. Kama si Zitto suala hili lisingekuwa HOT kama ilivyo sasa na ndio maana limekuwa na wasemaji wengi na limesaidia mjadala kupaaa na kuwatisha kina Dk Rashidi am baya akageuka kuwatisha Watanzania.
Soma maandiko yake. Sikiliza matamshi yake ya SAUTI si ya kunukuliwa, utaona hakusema anaunga mkono kwamba lazima kunuliwa kwa DOwans. Kuna mahala amesema (narudia) kwamba kaama kuna ulazima wa kununua Dowans basi sheria zizingatiwe. na Kuwepo mjadala ili uamuzi ufanyike kwa HOJA si kwa JAZBA. Hapo sioni kosa la kimantiki ila kuna kosa la KISIASA kwam ba Dowans/Richmond ni alama ya mafanikio ya vita ya UFISADI kwa hiyo hatuwezi kukubali kwa gharama yoyote mtu yeyote (hata Zitto) kuuvunja huu MNARA wa vita ya UFISADI
Halisi,
Zitto nimemsoma kw amakini sana kauli zake hapa JF
1. Zitto alizungumza kwa niaba ya Kamati
2. Ni kweli Zitto alisema kama kuna ulazima wa kununua Mitambo ya Dowans basi sheria zifuatwe..............wat wakamuwekea sheria.........yeye akasema sheria mama haisemi hivyo....watu wakamwambia unaposoma sheria mama unatakiwa usome na regulations zake.....sikumsikia akijibu......Zitto anasahau kuwa sheria mama haiwezi kuainisha kila kitu
...
Halisi,
1. Msimamo wa TANESCO ulikuwa nikununua mitambo ya Dowans....eti wakidai ni "Opportunity" iliyojitokeza
2.Zitto akaja boldly kuweka msimamo wake hapa JF kuwa he stands with TANESCO......nafikrir hili kosa la KIMANTIKI na wala si kisiasa au
.
3.Kosa lake kisiasa ni kukubali kuburuzwa na msimamo wa kamati yake.......kama alivyotuonyesha awali kuwa anasimama na kamati yake
4.Nia yake ya kukutana na Kamati ya Shelukindo...naweza kuelewa ilikuwa ni opportunity nzuri kwake kupata support kama yeye KWELI alikuwa anapinga ununuzi wa Mitambo ambayo TANESCO wanaitaka i.e. DOWANS....unfortunately hiyo nafasi haikutokea......na akaja akaharibu zaidi kuja kuweka msimamo wake hapa JF........
....
Halisi: nimerudia mara mbili kuisoma thread yako ya awali na ninakiri kusema kwamba nashindwa kuelewa unasimama wapi katika sakata hili la Zitto na Dowans! Kuna mmoja umemjibu kuwa tatizo si Zitto, ni Dowans. Nadhani ungekuwa sahihi zaidi iwapo ungesema "chanzo ni Dowans, na si Zitto". Zitto kawahuzunisha mamilioni ya mashabiki wake kwa kuchukuwa msimamo ambao waliona asingeuchukuwa -- ni msimamo wa upande wa pili.
.
Mkuu Halisi, nakusoma na ninasoma kama ilivyo hapo juu, sio kama ulivyoandika.
Zitto kachemsha, aombe radhi.
Zitto hana sababu ya kuomba radhi kwa kuchukua msimamo alioamini kufuatana na taarifa zote alizokuwa nazo na dhamira yake kuwa alikuwa sahihi.
Kuna watu hapa naamini wanataka kutumia nafasi hii ya tofauti na Zitto kumsambaratisha na kumdunisha kijana huyu na ikiwezekana kumkatisha tamaa. Zitto kama mwanasiasa yeyote au Mtanzania yeyote mwingine ana haki ya kuwa na msimamo wake tofauti na wa watu wengine.
Mambo ya siasa za "fuata upepo" yamepitwa na wakati. Ati kwa vile watu wengi JF wamepinga ununuzi wa majenereta ya Dowans basi Zitto alitakiwa naye awe upande huo kwa sababu moja tu nayo ni kufanana (uniformity). Kwamba ili kweli tujue yuko upande wetu basi ni lazima awe na msimamo kama wa kwetu.
Matokeo yake ni kuanza kuwa na wanasiasa wa kuturidhisha kujisikia vizuri. Wanasiasa wasio na mawazo yao bali yale ya mkumbo.
Imesemwa vizuri tangu mwanzo kuwa Zitto alichukua msimamo ambao kisiasa ulikuwa na makosa makubwa. Hili wala halina ubishi. Tatizo ni kuwa makosa hayo tunayaona sisi na yeye hajayaona au hajashawishika kuyaona. Kilichonisikitisha sana katika mjadala huu ni kuwa mara nyingi watu wanaposhindwa kujenga hoja wao huleta vioja.
Badala ya kumuita Zitto kila aina ya majina kwa sababu hana msimamo kama wa mtu mwingine lilikuwa ni jukumu la watu kumshawishi kwa hoja. Sehemu moja ambapo nilipenda mjadala huu ni pale lilipokuja suala la Kisheria na Kanuni za Manunuzi ya serikali. Pale palikuwa na hoja na ushahidi wa hoja. Lakini wengine hawawezi hayo na wao kwao kwa vile "wameumizwa" basi wanachukulia tu kawasaliti.
I'll tell you what, Nitawachukua watu wenye ujasiri wa kina Zitto anyday kuliko viongozi ambao wanafuata upepo wa wafadhili wao au mabwana zao.
Lakini kubwa zaidi ni kuwa ni kutofanya maamuzi ya kisiasa kweli kwa mtu kuweka imani, hisia na vionjo juu ya mtu mmoja kuwa huyo mtu hatakiwi kukuudhi, kuchukua msimamo kinyume na wewe au hata kupingana na wewe! Kwamba akienda nje ya mstari uliojichorea basi mtu huyo ni msaliti, fisadi na katugeuka, ati hatumwelewi. Huwezi kuweka imani yako juu ya mtu mmoja namna hiyoo hiyo.
Katika maisha haya nimejifunza kuwa marafiki watakusaliti, ndugu watakukana, adui atakuwa mwokozi na wale uliowadharau watasimama kama mashujaa! Yote ni sehemu ya hili drama tunaloliita maisha. Hivyo, kweli Zitto kachukua msimamo tofauti ambao kisiasa haukuwa na hekima (kama alivyosema Halisi na wengine) lakini kufikia mahali pa kumshusha na kumfanya duni na kujaribu kumuangamiza na ati kumtaka ajiuzulu na kuomba radhi ni jazba isiyo na sababu!
Ninafahamu bado kuna watu ambao wana kisasi na kijana huyu na umaarufu wake na mvuto wake na sasa wanataka kutumia nafasi hii kumuangamiza hasa kuelekea 2010. Nakumbuka jinsi walivyojaribu baada ya mambo ya Buzwagi na kifo cha Mhe. Wangwe, nguvu zile zile zipo leo tena. Ninafahamu wapo wale ambapo kweli walikwazika kwa sababu ya jinsi walivyo/wanavyomheshimu Zitto, lakini ninafahamu pia kuwa na wale ambao sasa wanachekelea kwamba "wamempata". Hawa wote wanataka kuona Zitto anakuwa duni, anaondolewa na kufanywa kuwa irrelevant.
Hii yote ni sehemu ya siasa, ni matumaini yangu kuwa hili halitamrudisha nyuma, atatambua political misstep that he took, he'll learn to be calculating, and he will always look into political ramification of whatever position he might take in the future. Naamini Zitto is not a typical politician, he is a technocrat who got into politics. Nadhani pole pole ataielewa siasa kuwa it is more than simple right and wrong, maslahi ya taifa au la..
So, I heard ya'll but cut the guy some slack! vinginevyo, bado tutakwazika na kina Mwakyembe, Selelii, mama Kilango, na wengine siku wakichukua maamuzi au misimamo ambayo itafutanya tukune vichwa.
..Katika maisha haya nimejifunza kuwa marafiki watakusaliti, ndugu watakukana, adui atakuwa mwokozi na wale uliowadharau watasimama kama mashujaa! Yote ni sehemu ya hili drama tunaloliita maisha. Hivyo, kweli Zitto kachukua msimamo tofauti ambao kisiasa haukuwa na hekima (kama alivyosema Halisi na wengine) lakini kufikia mahali pa kumshusha na kumfanya duni na kujaribu kumuangamiza na ati kumtaka ajiuzulu na kuomba radhi ni jazba isiyo na sababu!
Mzee Mwakijiji,
..
Mkuu hapa wala sikubaliani na wewe kabisa.. Ni mawili Aidha hao marafiki wako ni Wanafiki au wewe mwenyewe una matatizo!..
Nikirudi kwa issue ya Zitto kulingana na maneno haya - naogopa hata kufikiria ulichoandika!...
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu, kufuatia maelezo yako hapo juu...nilichosema mimi sio swala la uchaguzi..Kama ume experience mambo hayo toka kwa marafiki zako basi kuna tafsiri mbili tu..
1. Marafiki zako wanafiki au 2. Wewe mwenyewe una matatizo..
In real life marafiki wanatakiwa kinyume kabisa cha yaliyokutokea..haikutokea hivyo basi jibu umelipata..Na nikitazama upande wa issue hii naogopa sana kuwepo Uwezekano kuwa Zitto kapitia yaliyokukuta wewe..
Nilijuwa Zitto ataleta mgawanyiko mkubwa sana hapa JF...Zitto ni kweli amewaweka mashabiki wake kwenye hard times sana...Well lets wait and see, nina imani Zitto anaweza kuja na maelezo ya kina ambayo at least watu wataweza ku level na uamuzi wake ambao ulikuwa so un popular.
NBC, msnbc.com and news services
updated 10:21 p.m. ET, Tues., Feb. 3, 2009
WASHINGTON - President Barack Obama on Tuesday abruptly abandoned his nomination fight for Tom Daschle and a second major appointee who failed to pay all their taxes, telling NBC News: "I screwed up."
"I've got to own up to my mistake. Ultimately, it's important for this administration to send a message that there aren't two sets of rules - you know, one for prominent people and one for ordinary folks who have to pay their taxes," Obama said on NBC's "Nightly News with Brian Williams."
The admission came little more than 24 hours after Obama had said he was "absolutely" committed to Daschle's confirmation as secretary of health and human services, a job in which he would taken the lead in the president's ambitious plans for the nation's health care system. /
My point ni kuwa Zitto haitaji kutoa maelezo zaidi ya aliyoyatoa. Wote tunajua alichosema. Wapo ambao hawakubaliani naye na wapo wanaokubaliana naye. Mimi sijakubaliana naye, lakini kutokubaliana naye haina maana namuona fisadi, kanunuliwa au kanisaliti! Ninachukulia tu kuwa tumetofautiana kimtazamo na hasa kisiasa. Naamini position yangu ina nguvu kuliko ya kwake (bila ya shaka na yeye anaona kinyume chake). Lakini tofauti hiyo haisemi lolote kuhusu ninavyomfikiria au kumdhania kwa sababu ya kutofautiana naye.