Sasa Mwakyembe ameacha kuwa msemaji wa kamati yake ya Madini na Nishati na karukia kuwa msemaji wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya umma. Unaona sasa tatizo la ku poke his nose kila mahala? Kama uwaziri umempitia mbali basi asubiri awamu ya tano. Njia anayotumia sasa haimsaidii sana hasa kwa huyu Rais aliyopo madarakani.
Je kama mitambo ya Dowans inawezekana kutatua tatizo hili na kama bei zinazo tajwa ni anuai... ni kitu gani kinachotufanya tusite..
mkuu umesikia mahojiano waliofanya Zitto na Mwakyembe na ITV? Mwakyembe kasema live msimamo wa Zitto si wa kamati yake.....ni wake binafsi na anamshangaa kama ndio Zitto anaemfahamu.....Zitto hakubisha....
LAITI ZITTO ANGEUJUA UZITO
Wahenga walinena nasi tukatega sikio
Hoja walitoa waasisi tena nzito nzito
Ziumiazo ndizo nyasi wapiganapo tembo
Laiti Zitto angemdisi Idrisa wa Tanesko
Laiti Zitto angemdisi Idrisa wa Tanesko
Mbunge Kijana angehisi Dowani imedisko
Wala singedadisi uazizi wake mitambo
Angechukua bisi bisi aifungue wozo
Angechukua bisi bisi aifungue wozo
Kwa yake kasi angeunyofoa huo utumbo
Wanainchi ndio sisi tungelimuunga mkono
Laiti Zitto Mfanisi angejua tu wazito
Laiti Zitto Mfanisi angejua tu wazito
Asingelikuwa mwepesi wa kulitoa tamko
Sasa lafanya aonwe muasi wa wazalendo
Uwi mwokoeni na majasusi kijana Zitto
Ubalikiwe mkuu,hapa naona kuna mashujaa wa CCM wanataka kupotosha mawazo ya watu dhidi ya Zitto na wao kujijenga kisiasa.Suala lililo mbele yetu ni namna ya kupata nishati ya uhakika kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.Sasa hapa watu wanataka kuaminisha watu kuwa Zitto ndie mwenye ukiritimba wa mawazo na ni wazo lake tu ndio lichukuliwe uzito.Nashauri tu,tukitaka kuwa na consistent Debate,we must avoid childish speculation.
Kwanini tutangulize hisia za mtu kununuliwa? kwa mtindo huu,hatuwezi kuwa na mjadala wenye tija.Let us just dwell katika debate
Mkuu wangu nadhani nimekusoma... nashukuru sana kwa maelezo haya na hakika ungeyaweka mwanzoni hapa JF tungekuwa ukurasa mmoja..Huko ktk magazeti ungesema kama kamati ilivyotaka lakini hapa nyumbani ungetushtua kinachoendelea laa sivyo mkuu wangu ilionyesha wazi sio Zitto tunayemfahamu..Kumbuka mengi yaliyopita siku zote umekuwa ukitushtua kwanza hata kama sio kwa habari kamili lakini tulifahamu umesimama wapi..Lakini ktk hili mkuu wangu ulipoanza kuwa mkali na kutoa maneno mazito ya kuhoji uzalendo wa wananchi kwa sababu tunaishi nje nilishtuka sana..Nikasema huyu kweli Zitto ama mtu mwingine maanake hao wanaishi ndani ya nchi kina Yona, Mramba, Rostam, Lowassa, Karamagi, yaani baraza zima la Mawaziri waliotangulia toka Mkapa hadi Kikwete wana uzalendo gani!.Ni kitu gani kinachompa ushujaa Zitto kama sio kupambana na mafisadi walioko ndani ya nchi na sio sisi tunaoishi nje!..mkuu sikukuelewa kabisa!Hapana sijaandika barua kwa Waziri ili asupport kununua mitambo ya Dowans. Sina mamlaka ya kuingilia manunuzi ya Shirika. Shirika linapokuja kwenye Kamati yetu huwa linakuja na Bodi, ikiwakilishwa na Mwenyekiti wao wa Bodi.
Nilizungumza na Shelukindo. Nilizungumza na Mwambalaswa. Sikumpata Mwakyembe kwani huwa hapatikani kwa urahisi kwa simu na alikuwa Kahama na Mengi. Seleli sikumtafuta maana asuingeweza kusaidia. Stella Manyanya nilimtafuta.
I am always like that napokutana na suala tete. Ndio maana hata Kamati nilipoona ina sway kwa TANESCO nikasema hapana, hatuwezi kupingana na Kamati ya Nishati na Madini. Nikaatoa hoja ndani ya Kamati kwamba Kamati 2 zikutane. Wenzangu hawakutaka kukutana na kuanza kulobby kwa spika asikubali kukutana. Wakaanza kujibu kupitia press. Sikuwa na cha kufanya bali kundika barua kwa Waziri kutoa maoni ya kamati kwa majibu wa kanuni za Bunge.
I tried my level best and all documented. JF ninavyoijua itapata tu hizo documents. Walionihukumu wataona aibu tu! I am genuine, i am honest and as always i sub-ordinate my interests to those of the nation. Sijakurupuka. Wazee wanaogopa kuwa challenged na vijana.
Ahaaa, ni muongo,alipata kidogo dogo fulani !! Ana price zito asituzuge hapa,tena akitaka usalama wa chama chao ajiuzulu tu,hapo hamna short cut ya kujiosha kwa wana jamii forum.
Zitto,
Mkuu wangu nadhani nimekusoma... nashukuru sana kwa maelezo haya na hakika ungeyaweka mwanzoni hapa JF tungekuwa ukurasa mmoja..Huko ktk magazeti ungesema kama kamati ilivyotaka lakini hapa nyumbani ungetushtua kinachoendelea laa sivyo mkuu wangu ilionyesha wazi sio Zitto tunayemfahamu..Kumbuka mengi yaliyopita siku zote umekuwa ukitushtua kwanza hata kama sio kwa habari kamili lakini tulifahamu umesimama wapi..Lakini ktk hili mkuu wangu ulipoanza kuwa mkali na kutoa maneno mazito ya kuhoji uzalendo wa wananchi kwa sababu tunaishi nje nilishtuka sana..Nikasema huyu kweli Zitto ama mtu mwingine maanake hao wanaishi ndani ya nchi kina Yona, Mramba, Rostam, Lowassa, Karamagi, yaani baraza zima la Mawaziri waliotangulia toka Mkapa hadi Kikwete wana uzalendo gani!.Ni kitu gani kinachompa ushujaa Zitto kama sio kupambana na mafisadi walioko ndani ya nchi na sio sisi tunaoishi nje!..mkuu sikukuelewa kabisa!
Hata hivyo, mkuu wangu sisi binadamu tunachokiomba kwako ni kusimamia maslahi yetu iwe hata kwa gharama kubwa..