Ndio hilo 'jipu' lililosemakana litapasuliwa jana!? Angalau wamesikiliza maoni yetu ingawa kwa shingo upande.
Kasheshe:
kama bodi yake mwenyewe imekataa, hiyo ni professionalism gani unayoongelea?
IDRISA NAE FACTS ZAKE NI KAMA politics!ina maana tanesco hawakujua kwamba wataface hiyo POWER DEFICIT?............
halafu mbona analazimisha sana?..........tena kwa vitisho vya kukaa gizani?kila kitu kinafanywa kama JANGA(CAKAMITIES).ni kama mtu anaefanya IMMEDIATE MEASURES katika kuyakabili maafa ambayo hakuyatarajia...........kama MAFURIKO,AU SIJUI NINI.
Dah!mzee idrisa UTAWAJIBISHWA TU IN ANY CASE
But every thing in this world needs planing, ndio maana Jeshi linakuwa na Stock ya silaha , askari , training etc.
Sasa tukirudi kwenye Tanesco iwe ni serikali mkosa au yenyewe tanesco kwa kutotekeleza kile walicho takiwa kutekeleza , kama kutoa pesa in time etc , ndio hapo tunapo taka kumjua mchawi wetu nani? kwamba moja anafanya maksudi ili aweke mazingira ya dharura, then watu watengeneze chao? at the expense ya kuuwa mtaji huo mdogo wa nchi na adha zingine. kwa sababu mradi kama huu si endelevu, ni sawa sawa na dawa ya kutuliza maumivi, wakati tiba ni chloroquine na si panadol.
Tatizo lilipo toke Mwaka 2006, Lowasa kama waziriMkuu aliwahakikishia wananchi kwamba serikali imejipanga na wasihofu (meaning pesa ipo au itatafuywa toka chanzo chochote ku-solve hiyo problem) sasa 3 year in tatizo linajirudia , na fedha kama unavyosema wewe hakuna kugharamia miradi mikuu, bali zipo za umeme wa dharura, je hii inaingia akilini?
Hivi Watanzania ni wajinga sana (mabwege au mazezeta) kiasi kwamba wababaishaji ndio wanatunukiwa nishani?? Kama mtu ameboronga huko kote kwa nini aendelee kuongoza shirika nyeti linalosimamia uhai wa Taifa kama TANESCO?
Kwa wajuvi wa sheria; ni kitu gani kama raia tunaweza kumfanya mtu huyu? Kwa hali ilivyo inaonekana aliyemteua au ambaye ana mamlaka na kitumbua chake hana shaka naye (he is very happy with his performance)!!
Kazi tunayo, tena siyo ndogo!!🙄
Phillemon Mikael,
Mku hapa tunazungumzia swala la Dowans ambalo Tanesco inahusika toka wakati wa Richmond..Hyaa ya Kinyerezi ni mada nyingine kabisa..Hivi ikiwa wao wameshindwa kuwekeza fedha walizopewa kwa mradi wa dharura wataweza vipi kumudu mradi mkubwa..
Ebu rudia tena kusoma ni fedha ngapi tunapoteza kila siku kutokana na mkataba feki wa Richmond, unataka bado kumlaumu Kikwete, hivi kweli kama Tanesco kwa miaka mitatu iliyopita wangekuwa wakipata faida tungekuwa bado tunahitaji msaada wa serikali?.. hizi bail out zitakwisha lini!..why Tanesco wali contract mashirika kama haya kutuuzia Umeme wakati waliweza kabisa kununua wao kama walivyofanya na mitambo ya Ubungo.. Si wao ndio waliweka sahihi za mikataba yote tumlaumu nani ka sio wao.. They have final say hata ktk swala hili tumeambiwa kuwa Tanesco ndio wenye sauti ya mwisho wakisema wanunue, mitambo itanunuliwa..