Uwiano Maalum;
Kwa kawaida kampuni yoyote ikileta mitambo hapa nchini inalipia Duty and VAT. Wizara ya Fedha inaweza kusamehe kodi lakini. Kwa case ya Tanesco sijui kama wana Exemption au la. Ila Tanesco ni kampuni na sio serikali; ingawa inamilikiwa 100% na serikali. Kwakuwa inauza huduma na kupata faida ndo maana inalipa kodi serikalini.
Kama mtambo uleletwa kifisadi, hilo ni nje ya mada. suala ni kuwa je Bie hiyo ni halali?, hapo ndo nikasema tulinganishe apple na apple interms of Bei.
Kutaifisha lazima uwe na good grounds. Tukishapata thamani ya mtambo mbadala na kulinganisha gharama za dowans ndo tunaweza kusema ni wa kifisadi au la.
hope nimekujibu.
Asante
FP
Uwiano Maalum; Kwa kawaida .......
...hapo ndo nikasema tulinganishe apple na apple interms of Bei.
Kutaifisha lazima uwe na good grounds. Tukishapata thamani ya mtambo mbadala na kulinganisha gharama za dowans ndo tunaweza kusema ni wa kifisadi au la.
.....
FP
Yes sir. Maamauzi yao mengi yametupeleka gizani mara kibao,hakuna busara hakuna hekima hakuna utaalamu unaotumika kwenye maamuzi ya serikali ya tanzania kwa sababu hakuna hata mmoja anayejali maamuzi kwani hakuna hukumu akifanya vizuri au reward akifanya vibaya atakuwepo tu vyovote vile.
Dr Idrisa tayari anamgao wake kutoka kwa Chenge inawezekana anao tayari mwingine kutoka kwa dowans.
Tatizo la umeme halijaanza jana wala juzi, miaka ya 1995 na kuendelea tulikuwa na tatizo kubwa la umeme na maamuzi ya wataalamu wengi yalikuwa haya
Kusafisha mabwawa
kununua turbine mpya
kuongeza ukubwa wa mabwawa na turbine
kuongeza vyanzo vingine vya umeme
Kilichofanyika ni wizi na ujambazi wameendelea kununua mitambao ya kitapeli isiyo na manufaa kwa nchi ila kwa matumbo yao.
Kamati zote ile ya Richmond na bunge ziliona richmond ni utapeli mitambo haikuwaka kwa sababu ilikuwa mibovu sasa kama leo tanesco wanasema ni mizima kwanini wawepo kazini hii ni hujuma mbaya sana. tulikaa giza tukiamini mitambo mibovu leo hii mitambo ileile imekuwa mizima.
Hakuna haja ya kuwazawadia mafisadi walitufanyia uhuni walituingiza mkenge tununue mipya.
Nilipata habari kwamba Rostam na lowasa walifanya hadaa isiwake ili waje watubamize bei naona deal limekubali na ninaamini kabisa wote wanao bebea hili swala bango wamelishwa asali.
Tuvute subira litakaa wazi.
Uwiano Maalum;
Kesi ya bwana Gire ni ya kizushi na kukurupuka kama kawaida yetu wabongo. Ameshtakiwa sio kwa kuongeza bei ya mitambo. Check your facts. Mitambo ya Dowans haiwezi kuwa michafu bali watu ndo wachafu. Mimi sisemi tuinunue au la, ila tuangalie COST BENEFIT ANALYSIS. Hii ndo msimamo wangu.
SMU;
Upo sahihi, hata Life span pia ni bora kuiangalia na present value ya future costs pia ni muhimu kuiangalia. Kwa ufupi inatakiwa analysis ya kutosha kabla ya kukurupuka na kuikataa moja kwa moja. Mie kama nilivyosema nipo neutral kwenye hili.
Vyote vinawezekana. Ila tukikaa gizani (huku tukisubiri mitambo ya kutoka nje ije)tutakuwa tumepoteza kiasi gani cha fedha kiuchumi?
Swali ndo hilo.
FP
Of all the people we appended hope to (kwamba ni mtetezi wa maslahi ya Taifa) Zitto has let his calibre slide down.Awali ya yote: HII MITAMBO MWANZONI KABISA SI TULIAMBIWA SERIKALI INAKODI TU NA SI VYINGINEVYO??
Mambo yanavyokwenda ama kweli inaonekana kuna mtu ambaye anaongoza idara / wizara kwa remote.
Of all the people we appended hope to (kwamba ni mtetezi wa maslahi ya Taifa) Zitto has let his calibre slide down.
Sisemi mimi nasupport au kupinga ununuzi wa ile mitambo ya dowans. Ninachotaka ni kwamba tusiwe gizani na ndicho nadhani Zitto anakiangalia. Now the question ya how tunatakiwa kutokuwa gizani ndo pale serikali inatakiwa kuwa na wise decision ambayo ni ya haraka. Kila mtu anaweza kuja na pendekezo lake, mfano kuna jamaa wamesema mitambo inaweza kuja mipya for $39mn unlike kununua hiyo ya dowans for more than that ... that is a good idea but nani wa kuongoza huu mchakato ni Serikali na wataalamu wake. So tusimkaange sana zitto kwani naona yeye ametanguliza maslai ya taifa. Sion sababu ya kuendelea kupoteza muda na serikali yetu hii ambayo tayari wewe umeshaichambua hapo juu uozo wake...mimi nnachotaka ni umeme wa haraka kwan what we loose kwa kutokuwa na umeme ni mara dufu ya what we loose for buying the dowan thing. Niseme tu maslai yangu Mbele.
FP, ukiuziwa apple la ambalo aliyekuuzia amelipata kitapeli, ukakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, utajitetea kwa kusema apple lile ni si chafu bali tapeli aliyekuuzia ndio mchafu?
Of all the people we appended hope to (kwamba ni mtetezi wa maslahi ya Taifa) Zitto has let his calibre slide down.
kijana bado yuko makini tusimtetereshe kwa hili ambalo wanaolipinga zaidi ni wabwatukaji na wapenda sifaa kisiasa...
kijana yuko sawa na anafuata ushauri wa kitaalamu sio hisia na SIASA ZA MAKUNDIIIIIIIIIIIIII
Sikonge;
Kumbuka mimi ni mchambuzi tu, sijaegemea upande wowote!
Regards
FP
FP,
Huo mtambo nafikiri ukiwaona Wa-Ukraine na dege lao (Antonov An-225 Myria) basi mtambo ni wiki moja unakuwa umetua Tanzania. Ukitaka kuliona hebu licheki mwenyewe hapa chini :- ANTONOV AN-225
Nimeliona hilo dege! Ni kubwa! Ila wasiwasi wangu ni kuwa litatua wapi? Uwanja wa Mwl Nyerere 😀?