KGM;
Ngoja niwe devil's advocate hapa. Toka mada hii inaanza hakuna aliyekuja na bei ya mitambo mbadala mpaka inakuwa installed. Tungemnyooshea Zitto kidole kama tungesema kuwa mitambo kutoka US au Malaysia yaneye ubora uleule au zaidi ni Billion 40 na ya Dowans ni Bilion 60. Ila mitambo ya kutoka nje itachukua miaka miwili. Kimahesabu Billions 20 ni nyingi. Tuagize kutaka nje.
Huo ndo uchambuzi niliokuwa nikiisubiri hapa.
Tatizo lingine ni kuwa sehemu kubwa ya umeme wetu unatokana na Maji. Je tumefanya analysis kujua kama mvua hazitanyesha mwaka huu?.
Suala zima mi naona ni siasa tupu.
Wezi watupu wote huko Sirikalini na Tanesco!
Kwa hiyo unadhani kuwa ni wewe tu mwenye haki ya kutukana watu. Sasa kwa kuwa Zitto ni mheshimiwa basi asikwambie kama ni mpuuzi hata kama madai yako ni ya kipuuzi?
omarilyas
Mzee unaweza ukatupa reference, ili tuzimwage hapa zikae kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili vione ni kwa jinsi gani tunavyokosa busara?
Mbona humu ndani bei zimeshatolewa sana tu. wewe pitia pitia tu utaona.
Tena bei zimetoka kwa wenyewe sio wababishaji kama DOWNS ambayo hata inakotokea hakujulikani au mwenzetu unajua Downs walitokea wapi na walifahamianaje/walipasianaje Dili lao la kuihujumu nchi na RICHMOND
Hata hivyo sijakuelewa kama uko upande gani. Uko upande wa Sita+Mwakiembe+Shelukindo+Wananchi au Uko na Zito+RA+IDIRSA RASHID+MAFISADI bila kumsahau OMalys
Jamani hebu niwaulizeni:
Ni wapi Zitto amekosea? Mbona tunaharakisha kumhukumu kuwa ni fisadi, ni rafiki ya Rostum, ameshapokea hongo etc.etc? Nimesoma threads zake zote hakuna mahali Zitto amesema kuwa Tanesco LAZIMA wanunue mitambo ya Dowans. Au mimi ndiye mbumbumbu?
B + Duties and VAT(if any)+commisioning costs =
Hiyo ya bei ni Usd 39 Million ni CRAP!. Tupe analysis ya gharama zote zinazofuatia.
Hope nimeeleweka.
FDR mitambo ilikuja haikuwa mipyaa, ni mmoja tuu wa 35mw ndio ulikuwa mpyaa, watu wanachouliza ni kwamba kwa nini isinunuliwe mipyaa kabisa na yenye warranty kuliko hiyo mitumba, na ukiangalia bei ya hiyo mitumba ya dowans inauzwa bei kubwa zaidi ya mpyaa, ndio maana hata mimi najiuliza kwani Mhe Zitto kaona yaani solution ni kununua mitambo ya Dowans tuu, na wakati huwa anakuja kusoma hapa na kuna mahali wameweka hata bei ya mitambo mipya na yenye warranty. Kwani anashindwa kuuliza na wakaweka hii tenda kwenye uwazi na watu wagombanie tenda na waone nani atatoa huduma nzuri ya uhakika kwa bei nzuri? Mhe Zitto anang'ang'ania hii ya Dowans tuu kuna nini? kalipwa? yaani theres no alternative in his mind? kwa sababu kuna mahali kaandika kwamba hawezi aku-back down kwenye hili! ya kweli hayaa!Wakuu kumhukumu zito eti kanunuliwa na rostam hapo tumeenda mbali sana, hoja za zito na kamati yake ziko wazi. Wa tz tunasahau kuwa siasa chafu ndio iliyotufikisha hapa tulipo na si vinginevyo, hatukuwa wakweli tangu uhuru na tunaendelea na utamaduni huu na kuwajengea watu wakweli majungu na kuwapa wasifu potofu, tunataka mitambo iliyoingizwa tz 2006-7 leo inaitwa mitumba, ninyi tanesco ndio mlioianza kuitumia sasa muendelezo wake unaitwa tayari mtumba, ufisadi n.k tuache ushabiki usio na tija.
Dr. Rashid alipoichukua tanesco alifanya deal na makampuni yanayotajwatajwa kwa commitment ya dr rashid, jamaa wakatoa mapesa $300m kama mkopo wa kuifanya tanesco ijiendeshe na kuwapa assurance wadau hao huduma.
Dr.rashid anasimamia ukweli halis na siyo siasa zetu chafu.
Watz tuwe wakweli tu jamani kuwa shelukindo na mwakyembe hawasukumwi na uzalendo bali agenda yao ndani ya ccm. Spika huyo tushamjua ni mropokaji na dikteta tunamwacha hukohuko.
Tufanye kazi kwa dhati ya mioyo yetu na siyo chuki na majungu
Nilidhani zigo la serikali linakuwa tax exempted na kwamba unalipa commission kama utatumia agent. Isn't it?
Wakuu kumhukumu zito eti kanunuliwa na rostam hapo tumeenda mbali sana, hoja za zito na kamati yake ziko wazi. Wa tz tunasahau kuwa siasa chafu ndio iliyotufikisha hapa tulipo na si vinginevyo, hatukuwa wakweli tangu uhuru na tunaendelea na utamaduni huu na kuwajengea watu wakweli majungu na kuwapa wasifu potofu, tunataka mitambo iliyoingizwa tz 2006-7 leo inaitwa mitumba, ninyi tanesco ndio mlioianza kuitumia sasa muendelezo wake unaitwa tayari mtumba, ufisadi n.k tuache ushabiki usio na tija.
Dr. Rashid alipoichukua tanesco alifanya deal na makampuni yanayotajwatajwa kwa commitment ya dr rashid, jamaa wakatoa mapesa $300m kama mkopo wa kuifanya tanesco ijiendeshe na kuwapa assurance wadau hao huduma.
Dr.rashid anasimamia ukweli halis na siyo siasa zetu chafu.
Watz tuwe wakweli tu jamani kuwa shelukindo na mwakyembe hawasukumwi na uzalendo bali agenda yao ndani ya ccm. Spika huyo tushamjua ni mropokaji na dikteta tunamwacha hukohuko.
Tufanye kazi kwa dhati ya mioyo yetu na siyo chuki na majungu
Commision sio sawa na commisioning costs. ni kuwa baada ya Installations kuna kujaribu mtambo na kuhakikisha unafanya kazi vizuri, Pale wataalamu wanaofanya hiyo kazi wanatoka kampuni iliyoifunga na wanalipwa na kuna vitu vinatumika kutest mitambo.
Uwiano maalum,
Hili suala ni pana. Humu JF ni kama tunaropoka. So far hakuna analysis yoyote ya maana iliyofanyika humu!.
Ndo maana nikasema sipo upande wowote. Mimi ni positive thinker!
Regards
FP
Wakuu,
Hivi kelele zote hizi bado hakuna anayesema mtambo mpya wa kununua huu hapa?
Angalau Zitto ameonyesha hafuati upepo na yuko tayari kukosa umaarufu wa kisiasa kwa kitu anachokiamini.
Wanasiasa wote wamehamia Dar kupiga kelele za mtambo, hakuna uamuzi unachukuliwa, nchi giza totoro baada ya muda tunajiuliza eti kwanini hatuendelei?
Haya makundi yanayopingana yangeliweza kukaa pamoja na kujadiliana kwa wiki na kisha kuamua cha kufanya sio kama sasa wanasiasa wamegeuka watalaamu wa umeme.
Wacha wengine tuwajibike!