Dowans: Another Richmond in making?

Dr. Iddriss Rashid katoa Press Release LEO ambayo inaonesha kuwa mkataba huo hautokuwepo kufikia August mosi mwaka huu. Najua hii ni habari njema kwa walio wengi na mbaya kwa wachache.

Taarifa zaidi tutafahamishana hapa.

Kwa wanaoangalia TBC wanaweza kuona hii habari muda si mrefu
We believe kwamba tutafika, kwani mbio za sakafuni lazima ziishie ukingoni!!!!!!!!!

Thanks God for hearing prayers of millions of average human being in Tanzania
 
...yaani 152m per day kwa siku zote zile(almost a year) leo ndio wanakuja kukurupuka eti mkataba ni batili na mnawasifu,tumeliwa tuu hapo maana hata kisheria mkataba ndio unaisha hiyo Agost kwa hiyo wasitupige changa la macho eti wanavunja mkataba ...ni umekwisha!


Kama ile ya Balali vile !!!!!!!!!Alitimuliwa kazi wakati yeye alisha acha kazi zaidi ya miezi kadhaa.
Mkataba unavunjwa baada ya kuisha hii imetulia kweli.Hawa jamaa wanajua kuwa manipulate jf.Na watu tunatokea kifua mbele, kweli kazi bado ipo.
 
Dr. Rashid anasema mkataba unasimamishwa na anasisitiza kuwa umesimamishwa na malipo ya Milioni 152 ambayo walikuwa wanalipwa kila siku itakuwa kwenye hatua ya pili. Hatua ya kwanza ambayo na serikali imeridhia ilikuwa ni kuusimamisha mkataba huo haraka baada ya kushauriwa vema na wanasheria.

Malipo ya Capacity Charge wanalipa Hazina kwa niaba ya serikali. TANESCO inalipia gesi kila mwezi kulingana na gesi inayotumiwa.

Anasema hawataweza kuwadai matumizi ya gesi kwakuwa ilikuwa inatumiwa lakini suala la Capacity Charge ambayo ilikuwa ikilipwa kila siku ndilo wanaliangalia kwa undani.

Waziri William Ngereja pia amethibitisha jambo hili na anasema wamegundua kweli mkataba mzima ulikuwa si halali (ni batili).

Zaidi tutaendelea kupata toka vyanzo vya habari
Hehehehe! Invisible ngoja mi nijichekee na kujiimbia kawimbo haka kazuri sana

Tanzaniaaa Tanzaniaaaa!! Nakupenda kwa moyo woooteee
Nchi yangu Tanzaniaaaa Stori zako ni tamuu saanaaa!!
Nilalapo namwaza Vijisentiiii
Niamkapo Mkapa baba weee!
Tanzania Tanzaniaaaa Nakupenda na EPA zakoooooo
TANZANIA!!! TANZA NIAThe only country were footballers plays BUT they dont win!!
The only country were mzungu comes with one dollars and leaves with millions of dollars!!The only country were engineers builds but House falls down!!
The only country with Politicians who believes in voo doo!!! Attorney General!!
The only country were ufisadi is Prestige!!!The only country with many TUMEz!!
The only country were development is in Figure!!Not visible!!
The only country were politicians are richest men!!the only country were Language iz a problem!!AND
THE ONLY COUNTRY were PRESIDENT keep on SMILING despite of national difficulties! !!
THE ONLY COUNTRY WITH HANDSOME PREZZIDAAA!! ! I LAV THIS COUNTRY!!

Hapo sasa,ngoja tujipe matumaini.
 
Hivi jamani huyu Ngeleja si alikuwa wizara hii hii (wakati wa kusaini mkataba)!! sasa nini tena leo anasema "wamegundua" mkataba ulikuwa "fake", jamani huyu Ngeleja si ni yule mtaalamu wa masuala ya sheria!? Jamani hii imekaaje!

Mi binafsi sikubaliani na maelezo mepesi namna hii, ninachotaka bunge litengue kile kipengele cha sheria kisha mjadala ya Richmond urudiwe tena kujadiliwa!! Mpaka mchawi apatikane!!
Naibu waziri ni kajitu kadogo sana serikalini ni kakuamrishwa tu hasa ukifanya kazi na mtu mjanja kama karamagi.Naibu waziri kikatiba si mjumbe hata wa baraza la mawaziri,hivyo huenda naye Ngeleja huu ndio wakati wake wa kujitutumua.
 
Kuhusu suala la pesa yetu,kwa mujibu wa Idriss Rashid kaema hilola kisitisha mkataba ni la kwanza.tusubiri kitakachofuata jamani warudishe hiyo hela ni nyingi sana kila siku 152m si mchezo ati

Hawa jamaa walishauona mabwege kweli.Kwanza wametuma watu wao kuchokoza hisia kwa kuandika kuwa inawezekana mkataba wa Dowans na akina Aggreko ukaongezwa.Naamini hii ilikuwa ni makusudi ili kuwatayarisha watu kwa kuwajaza hasira ili ndugu yetu Idrisa Rashidi akija na hili watu waone kwa Serikali imefanya jambo la maana.

Mkataba tuliusoma hapa JF,mwezi wa 8 utakuwa umekwisha.Nitarudia kuusoma tena na ikiwezekana naomba Mods muuweke hapa au Muunganishe hii thread na ile Single yetu ya Richmond ili tuweze kuchambua pumba na mchele hasa kwa faida ya wanachama wapya ambao hawakuisiliza hiyo single.
 
Hawa wanfikiri watu wamelala, mkataba unaisha muda wake unavunjwaje wakati naturally umeisha. Wanataka point za bure bila kuzifanyia kazi, unaganisheni na ile CD ili wajue kuwa tumewatangulia hatua 2 mbele kuliko wanavyofikiri, hakuna points bila kuzifanyia kazi.
 
Waswahili tunasemaga hivi: Ukiaminiwa Jiaminishe; Za mwizi Arobaini; na Ukiona mwenzako ananyolewa, we tia nywele zako maji.

Watanzania tutafika tu.
 
Hawa CCM wasitufanye wajinga! Wanajua mkataba unakwisha August then wanajifanya eti wanauvunja, hili ni kosa juu ya kosa. Tafadhali MODS wekeni hiyo CD tuichambue tena.
 
Mkataba wa Richmond wafutwa
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,July 01, 2008 @00:01

Ni baada ya ushauri wa kisheria
Tanesco yasema haukuwa halali

SERIKALI imefuta mkataba kati yake na kampuni ya kutoa huduma ya umeme ya Dowans Tanzania Ltd kuanzia Agosti mosi mwaka huu. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupata ushauri wa kisheria kwamba mkataba kati ya shirika hilo na Kampuni ya Richmond ambayo mkataba wake ulihamishiwa Dowans, haukuwa halali wala haukuwa na nguvu kisheria.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk. Idris Rashid alisema jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Dar es Salaam, kuwa uamuzi huo ulifikiwa juzi katika mkutano kati ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

Dk. Rashid alisema kutokana na mkataba kati ya Richmond na Tanesco kuwa na utata, shirika hilo liliajiri kampuni ya sheria kutoa ushauri wa uhalali wa utaratibu mzima wa mkataba huo. Hakuitaja kampuni gani. Alisema kampuni hiyo ilibaini kuwa utaratibu mzima wa ununuzi wa huduma hiyo ya umeme na kuingia mkataba na Richmond Development Company LLC, ulikiuka sheria ya ununuzi namba 21 ya 2004.

“Kutokana na ukiukwaji huo, mkataba baina ya Tanesco na Richmond Development Company LLC haukuwa halali na hauna nguvu ya kisheria,” alisema Rashid. Alisema kampuni hiyo pia ilibaini kwamba iwapo mkataba husika ungekuwa halali, uhamishaji wa mkataba kutoka RDVCO badala ya Richmond Development LLC kwenda Dowans Tanzania Ltd, haukufuata msingi wa mkataba.

“Hivyo uhamishaji haukuwa halali na ifahamike kwamba mkataba ulikuwa baina ya Richmond Development Company LLC na Tanesco na siyo na REDVCO na Tanesco,” alisema.

Alisema kutokana na kasoro hizo, Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo ilizingatia na kuafiki ushauri wa kisheria na iliwasilisha mapendekezo Wizara ya Nishati na Madini na ndipo Waziri Ngeleja alikutana na Bodi hiyo na kutoa uamuzi. Dk. Rashid alisema tayari wameiarifu kampuni hiyo iliyopewa kazi ya kuzalisha megawati 100 na kuiuzia Tanesco miaka miwili iliyopita wakati wa hali ya ukame ulioikumba nchi.

Ingawa taarifa ya Dk. Rashid haikueleza matokeo ya uamuzi huo, Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alimkariri Mkurugenzi huyo akisema, “wachukue mitambo yao waende, mengine yatafuata baadaye.” Maelezo ya kampuni iliyopewa kazi na Tanesco kutoa ushauri yanafanana na ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa mwanzoni mwa mwaka huu kuchunguza mchakato mzima wa mkataba wa Richmond na Tanesco.

Kamati iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), ambako kutokana na ripoti hiyo, aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa alijiuzulu.

Wengine waliojiuzulu ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha ambaye alikuwa Waziri Wizara hiyo na kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutokana na mapendekezo ya ripoti hiyo, serikali iliahidi kuyafanyia kazi mapendekezo ya ripoti hiyo, na juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliahidi kuwa yuko tayari kutoa taarifa ya serikali kuhusu ilivyofanyia kazi mapendekezo ya Bunge.
 
Hatimaye baada ya 'kelele' za muda mrefu za Watanzania kuhusiana na mkataba wa kifisadi kati ya TANESCO na Richmond ambapo TANESCO ilikuwa inawalipa shilingi 152 millioni pamoja na kuwa walikuwa hawazalishi chochote. Watanzania popote mlipo duniani hongereni sana kwa juhudi zenu. 'Kelele' za Watanzania zinafika mpaka juu na kamwe msichoke kidogo kidogo tutaibadilisha nchi yetu kwa manufaa ya Watanzania wote na vizazi vyetu vijavyo kamwe tusikubali nchi yetu itekwe nyara na kundi dogo la mafisadi wenye ulafi wa utajiri wa kupindukia. Mungu ibariki Tanzania

Alutta Continua
 
Tanesco to halt Dowans contract
CHARLES KIZIGHA
Daily News; Tuesday,July 01, 2008 @00:01

The government has endorsed a recommendation by the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) to terminate the services of the controversial Dowans Tanzania Limited with effect from August 1, 2008, it has been learnt.

The Managing Director of Tanesco, Dr Idris Rashid, told newsmen in Dar es Salaam yesterday that he has already written a letter to Dowans informing them on the decision to de-commission their services by August 1, 2008.

He pointed out that DOWANS documents showed that its services would have officially ended on September 5, next year. Dr Rashid said that DOWANS, who now own the 100 MW generators installed at Tanesco headquarters' yard at Ubungo in Dar es Salaam, would be free to take them away after August 1.

He said that the endorsement was made in Dar es Salaam when Tanesco's board and management met the Minister of Energy and Minerals, Mr William Ngeleja, with his experts last Sunday. Dr Rashid explained that termination of DOWANS services was one among several recommendations including taking legal action against it in the light of findings drawn by a local law firm contracted to look into the marriage between Richmond Development Company (RDC) LLC and Tanesco.

He explained that Tanesco's board engaged the law firm to work to establish the legality of documents ("contract") which tied Tanesco and RDC on June 23, 2006 for a period of two years. Dr Rashid said the findings showed that the entire process of engaging RDC flouted the Public Procurement Act (PPA) rendering the contract between Tanesco and RDC illegal.

It was established that assuming the Tanesco and RDC contract was a legal one, the assigning of that contract from RDEVCO instead of RDC to DOWANS Holdings SA and subsequently DOWANS Tanzania Limited did not have the basis of the agreement hence illegal. He hinted that the law firm's findings established that DOWANS Holdings SA was registered in Costa Rica with a capital of 100 US dollars (119,000/-).

"The fact is that the contract was between Richmond Development Company LLC and Tanesco and not RDEVCO and Tanesco," he elaborated. He pointed out that RDC LLC was an assumed name in the contract and was not registered in Texas, USA for the undertaking. Dr Rashid further said that under normal circumstances Tanesco, RDEVCO and DOWANS should have signed a joint contract.

The assignment was done before informing Tanesco, he added. Messrs RDC LLC were selected among several other bidders to install 100mw generators to alleviate (then) power crisis in the country but it took several months to import the entire plant. After winning the tender, owners of the company knocked doors of several banks to get guarantee to import the engines to no avail but later managed after getting government support. However, the company imported the plant in piecemeal. The tender appeared to have been too big hence looked for another firm and assigned it.
 
Mkataba unaisha 30 july 08 ...je wataendelea kulipwa mpaka tarehe hio?....kwa nini wasivunje mkataba palepale kama imejulikana ni batili?...je fedha walizochukua wanazirudisha?...isiwe tunazugwa hapa...
 
Hatua nzuri sana, lakini vipi sasa, je pesa walizokwisha chukua zitarudishwa?
 
huu sasa wizi.... yaani wameajiri kampuni ya sheria kuwashauri kwa mambo ambayo tumeyaandika magazetini? Nadhani it is about time watugawie hiyo fee waliyowalipa hao jamaa.

Tangu siku ya kwanza tuliwaambia mkataba wa Dowans hauna msingi wa sheria na tukasema ni kwanini kweli wanaenda kuajiri mtu mwingine kuwaambia kitu ambacho kiko dhahiri?

Hii inaudhi kweli!!
 
Waungwana,

Bado kuna utata hapa. Huu mkataba ulihamishiwa Dowans kifisadi baada ya kuanza kuujadili kwamba ulikuwa umejaa ufisadi wa hali ya juu. Sasa kama ulikuwa batili baada ya kuuhamisha huo mkataba Dowans basi TANESCO ina haki ya kudai pesa zote walizolipwa hao Dowans (shilingi 152 millioni kwa siku tangu siku mkataba huo ulipohamishiwa Dowans) pamoja na riba ya pesa zote walizolipwa.

Haya makampuni ya kifisadi lazima kula nayo sahani moja ili kuyakomesha yaache wizi wa kuziangamiza nchi za Afrika. Kuna haja ya kuwatia ndani hao wakurugenzi wa Dowans kabla hawajaikimbia nchi ili kuhakikisha wanarudisha pesa zote ambazo kampuni hiyo ililipwa pamoja na kuwa ilikuwa haistahili kulipwa malipo hayo.
 
ya Richmond ilikuwa kashfa hii ya Dowans is waaaaaaaaay above that!..


....It was established that assuming the Tanesco and RDC contract was a legal one, the assigning of that contract from RDEVCO instead of RDC to DOWANS Holdings SA and subsequently DOWANS Tanzania Limited did not have the basis of the agreement hence illegal. He hinted that the law firm’s findings established that DOWANS Holdings SA was registered in Costa Rica with a capital of 100 US dollars (119,000/-).


My memory is very good:

a. mwanzo tuliambiwa Dowans ni kampuni ya Uarabuni
b. Baadaye tukaambiwa kampuni ya Dowans ni ya Afrika ya Kusini
c. Leo tunaambiwa iliandikishwa Costa Rica

you wanna bet?

Dowans iliandikishwa wiki chache kabla ya kupewa huu mkataba!!! how much you wanna bet...
 
huu sasa wizi.... yaani wameajiri kampuni ya sheria kuwashauri kwa mambo ambayo tumeyaandika magazetini? Nadhani it is about time watugawie hiyo fee waliyowalipa hao jamaa.

... kwanini kweli wanaenda kuajiri mtu mwingine kuwaambia kitu ambacho kiko dhahiri? Hii inaudhi kweli!!

Unajua nini, angalau safari hii wameajiri law firm ya Kibongo. Huwa nachukia sana ma contract wakipewa wageni.

But then again ndio unakuta ma law firm hayo hayo ya Wabunge wa CCM.

Yale yale!
 
Back
Top Bottom