BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
- Thread starter
- #121
Ama Kweli Uungwana Ni Vitendo.
Yani sasa nchi ni kama hata haina Rais.
Na mwenyewe sasa yuko wapi?
Hao mambo ya ZIMBABWE SI YASHAISHA?
VIPI KUHUSU ZILE HOTUBA ZAKE SIJUI NI ZA KILA MWISHO WA MWEZI?
SALVA NAYE MBONA KIMYA?
MBONA HAKUNA ANAYEKAMATWA?
KUNA WANAOSUBIRIWA WAFE?
Watanzania tumeshachoka na hotuba zake za kila mwisho wa mwezi ambazo hazina kichwa wala miguu. Umekaa na watu wazima ndani ya chumba na meza uliyokalia wewe kuna kinyesi, na kila mtu aliyekuwepo katika chumba kile anaona kuna kinyesi. Wote wanasubiri uwaambie kinyesi kile kimefikaje pale juu ya meza na vipi utaondoa kinyesi kile maana wewe ndio mwenye nyumba. Lakini unajibaraguza baraguza kuongelea vitu ambavyo wote hawana hamu wala hawataki kuvisikia. Lakini hugusii chochoye kuhusu kile kinyesi.
Mwezi uliopita alitaka kuzungumzia mafanikio makubwa ya Sullivan Summit, bahati mbaya tukamwahi hapa JF na kusema kama angetoa hotuba basi ingekuwa ni kuhusu SS.
Mwezi huu anaweza kuzungumzia Zimbabwe wakati sisi wenyewe tuna matatizo chungu nzima. Mhishimiwa JK Watanzania tunataka kujua kinyesi juu ya meza yako kimefikaje na je utakiondoa vipi au nani mwenye jukumu la kuondoa kinyesi hicho. Tumechoka na uwongo kila kukicha. Hebu kuwa mkweli wa nafsi yako na uzungumze na Watanzania kile ambacho wengi wetu tunataka kukisikia toka kwako.