Siku hizi hii Dowans ni kampuni ya Manji, sio ya Rostam tena kweli wajinga ndio wali wetu!
Dowans : Hatuondoki
Faraja Mgwabati
Daily News; Friday,July 25, 2008 @00:02
Hata hivyo, alisema wananchi wasiwe na wasiwasi kwa kuwa umeme wa megawati 100 ambao ulikuwa ukitolewa na Dowans, sasa utapatikana kupitia mitambo ya Watsila ya megawati 100 ambayo inamilikiwa na shirika hilo
Nani atawapatia tena kibali cha kuuza huo umeme huko machimboni,Huyo mchawi akamatwe na asulubiwe mchana kweupe.
Kungurumweupe, ni suala la makubaliano ya kibiashara tu, mbona wasafirishaji hutumia barabara ambazo ni public goods na wanalipa ada ya barabara kupitia ushuru wa mafuta kama sikosei tanroad wanalipwa shs 90/= kwa kila lita ya diesel.
Nalishauri tanesco iwe holdings company ndani yake yaundwe mashirika matatu wazalishaji, wasafirishaji na wauzaji. Hivyo Dowans wanaweza kuzalisha umeme wakausafirisha kwa mtandao wa tanesco kwenda kwa wateja wao, pia Dowans wanaweza kununua umeme wa ziada toka tanesco na kuuza kwa wateja wao.
Miaka kadhaa iliyopita mawasiliano na watu waishio maeneo kama, Misozwe-Muheza, Nanjilinji, tandahimba, kibakwe, mgololo hawakuwa na mawasiano ya simu, lakini hivi sasa wanatesa masaa 24, unaweza kuwajulia hali bibi na babu zako hata usiku wa manane, shukrani ziwaendee mashirika ya simu za mikononi hawa jamaa wanafanya kazi kweli kweli minara yao inapanda kila kukicha, kama hadi sasa tungekuwa na TTCL pekee mambo kama haya yasingetokea ingebaki kuwa hadithi tuu, wacha yaje makampuni binafsi yaifundishe TANESCO jinsi yakusambaza umeme mpaka Misozwe-Muheza, Nanjilinji, tandahimba, kibakwe hadi mgololo..na kama DOWANS wanazosifa zinazohitajika basi nao wapewe nafasi hiyo.
Ni hayo tu.
Kwa wale mnaoifahamu bongo yaani Dsm,pale ubungo baada ya jengo la makao ya Tanesco kama unakwenda Kimara kuna mtambo mkubwa kabisa umejengwa na kampuni ya Watsila ni wa kisasa(according to them).
Lakini Watsila ndo kampuni iliyojenga mitambo ya IPTL pia. Nijuavyo mimi ni kwamba watsila ni mjenzi na mmiliki ni serikali. Sasa kama nimekosea mnisamehe na mwenye ukweli atusaidie.
Ndugu Kungurumweupe kama alivyosema ndugu malila, Watsila ni wajenzi wa mitambo ya umeme na wanawajengea TANESCO. kuna kazi moja tulifanya nao hawa jamaa. wanajenga tu na baadaye watakabidhi TANESCO itakayoiendesha mitambo hivyo.Hata mimi nimewahi kuuona huo mtambo, lakini je 'who is the owner'??